Dkt. Shein afurahishwa na uhusiano uliopo kati ya Zanziba na India 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, amesema kuwa utekelezaji wa hati ya makubaliano (MOU) kati ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) na Chuo Kikuu cha Teknolojia (VIT) cha nchini India ni muendelezo wa uhusiano na ushirikiano wa kihistoria uliopo kati ya Zanzibar na India.

Dk. Shein aliyasema hayo leo Ikulu Mjini Zanzibar wakati alipokuwa na mazungumzo na Mkuu wa Chuo Kikuu cha Teknolojia (VIT) cha nchini India  Dk. Govindasamy Viswanathan akiwa na  wenyeji wake uongozi wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA), ukiongozwa na Makamu Mkuu wa chuo hicho Profesa Idris Ahmada Rai.

Katika maelezo yake Dk. Shein alitoa pongezi kwa uongozi wa Chuo Kikuu cha (VIT) kwa kufika Zanzibar kwa lengo la kuimarisha uhusiano na ushirikiano kati ya chuo hicho na chuo Kikuu cha (SUZA), hatua ambayo inazidi kujenga udugu na uhisiano kati ya Zanzibar na India.

Dk. Shein alieleza kuwa Zanzibar ina mambo ya kujifunza kutoka India hasa katika  masuala ya Teknolojia ya kisasa ambayo nchi hiyo imeweza kupiga hatua na kupata mafanikio makubwa.

Aliongeza kuwa licha ya chuo Kikuu cha SUZA kuwa kichanga lakini kimeweza kupiga hatua kubwa na kupata mafanikio, hivyo kuendeleza uhisnao na vyuo vikuu ulimwenguni kikiwemo chuo Kikuu cha VIT kutakisaidia chuo hicho kupanua wigo wa maendeleo sambamba na kujenga uwezo wa wafanyakazi kitaaluma.

Aidha, Dk. Shein alisisitiza kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar inathamini ushirikiano wan chi rafiki hivyo hatua ya chuo hicho kusaini hati ya mashirikiano kati yake na chuo kikuu cha SUZA kinaipa Serikali kuendelea kutilia mkazo suala hilo pamoja na kuendelea kutekeleza azma yake ya kuimarisha sekta ya elimu hapa nchini.

Pamoja na hayo, Dk. Shein alimueleza Mkuu huo wa Chuo Kikuu cha VIT alieongozana na Mkurugenzi wa Uhusiano wa Kimataifa wa chuo hicho Dk. C. VijayKumar kuwa azma na malengo ya nchi zote za Jumuiya ya Umoja wa Afrika (AU) ikiwemo Tanzania ni kuimarisha sekta ya viwanda.

Hivyo, alisisitiza kuwa hatua ya ushirikiano huo utaimarisha zaidi uanzishwaji wa vituo vya ubunifu na ujasiriamali kupitia Teknolojia ya kisasa na hatimae kuisaidia Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kutekeleza azma ya kuanzisha viwanda vikiwemo vidogo vidogo na vya kati kutokana na rasilimali zake zilizopo.

Alieleza kuwa hatua hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza soko la ajira kwa wananchi wa Zanzibar huku akisisitiza haja ya kutilia mkazo suala zima la utafiti kwa chuo kikuu cha (SUZA) jambo ambalo limo katika hati ya makubaliano (MoU) ya vyuo vikuu hivyo.

Kuhusu utafiti wa bahari Dk. Shein alieleza haja ya kuendeleza utafiti wa bahari ili Zanzibar iweze kufaidika na bahari hasa ikizingatiwa kuwa maeneo yake yote ya visiwa vya Zanzibar yamezungukwa na bahari.

Nae Mkuu wa chuo Kikuu cha (VIT), Dk. Govindasamy Viswanathan alimueleza Dk. Shein kuwa chuo chake kimekusudia kuimarisha uhusiano na mashirikiano zaidi na Chuo Kikuu cha (SUZA) kwa manufaa ya pande zote mbili.

Alieleza kuwa Chuo chake kiko tayari kuyatekekeza yale yote yaliotiwa saini katika hati ya mashirikiano na kusisitiza kuwa tokea kuanzisha mashirikiano yao mwaka 2013 kumekuwa na mafanikio makubwa.

Alieleza kuwa Chuo cha (VIT) ni miongoni mwa vyuo maarufu sana nchini India na kwa upande wa vyuo binafsi ni chuo kinachoongoza nchini humo ambacho kimeweza kupata mafanikio makubwa ndani na nje ya nchi hiyo hasa katika masuala ya Teknolojia ya kisasa.

Mapema Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) Profesa Idris Rai alimueleza Dk. Shein kuwa mnamo mwaka 2013 vyuo hivyo vilisaini hati ya makubaliano (MoU) na kukubaliana kushirikiana katika maeneo ya kadhaa yakiwemo kubadilishajna wafanyakazi, kubadilishana wanafunzi na kufanya tafiti za pamoja.

Aidha, alieleza mashirikiano mazuri na mahusiano yaliopo kati ya Chuo Kikuu cha (SUZA) na chuo cha (VIT) huku akieleza matumaini makubwa wanayotarajia katika mahusiano hayo hasa ikizingatiwa kuwa chuo hicho kimepiga hatua kubwa katika masuala ya Teknolojia.

Aliongeza kuwa mpaka hivi sasa tayari (SUZA) imeshasomesha walimu wa TEHAMA wawili katika ngazi ya Shahada ya Uzamili na mmoja anaendelea na masomo na wamekwua wakipata mashirikiano mazuri na chuo cha (VIT) katika mafunzo hayo.

Alieleza kuwa moja ya dhamira za ziara ya Mkuu huyo wa Chuo Kikuu cha (VIT) ni kuweka saini nyongeza ya Hati ya Makubaliano (MoU), itayowezesha kuanza kwa masomo ya TEHAMA mwaka ujao pamoja na dhamira ya kufanya mazungumzo juu ya uanzishwaji wa kituo cha Ubunifu na Ujasiriamali kupitia (TEHAMA) zoezi ambalo lilifanyika hapo jana huko katika ukumbiw a Chuo Kikuu cha (SUZA) Tunguu.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 

 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

The post Dkt. Shein afurahishwa na uhusiano uliopo kati ya Zanziba na India  appeared first on Zanzibar24.

Zanzibar 24

Read more


Habari Zinazoendana

3 years ago

Michuzi

UHUSIANO ULIOPO KATI YA PUNYETO NA TATIZO LA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME

 UKOSEFU  ama  upungufu  wa  nguvu  za  kiume, ni  tatizo  linalo  wakabili  mamilioni  ya  wanaume  duniani. 
 Zipo  sababu  nyingi  zinazo  sababisha  tatizo  la  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume, Miongoni  mwa  sababu  hizo  ni  pamoja  na  maradhi  kisukari, presha,shinikizo  la  damu, moyo, figo, matatizo  kwenye  mishipa  ya  ubongo  &  mishipa  ya  uti  wa mgongo, matatizo  kwenye  mishipa itumikayo  kusafrisha damu  mwilini, maradhi  ya  ngiri,  pamoja  na   upigaji  punyeto  kwa  muda ...

 

3 years ago

Michuzi

UHUSIANO ULIOPO KATI YA PUNYETO NA TATIZO LA UKOSEFU / UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME.

 Ukosefu  na/ama  upungufu  wa  nguvu  za  kiume, ni  tatizo  linalo  wakabili  mamilioni  ya  wanaume  duniani.  Zipo  sababu  nyingi  zinazo  sababisha  tatizo  la  ukosefu  wa  nguvu  za  kiume.  Miongoni  mwa  sababu  hizo  ni  pamoja  na  maradhi  kisukari, presha,shinikizo  la  damu, moyo, figo, matatizo  kwenye  mishipa  ya  ubongo  &  mishipa  ya  uti  wa mgongo, matatizo  kwenye  mishipa itumikayo  kusafrisha damu  mwilini, maradhi  ya  ngiri,  pamoja  na   upigaji  punyeto ...

 

3 months ago

Zanzibar 24

Dkt. Shein afurahishwa na jitihada zinazotolewa Umoja wa Mataifa

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, amelipongeza Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu Duniani (UNFPA), kwa kuendelea kuiunga mkono Zanzibar katika kuhakikisha huduma za jamii zinaimarika zikiwemo huduma za afya.

Dk. Shein aliyasema hayo leo Ikulu Mjini Zanzibar wakati alipokuwa na mazungumzo na Mwakilishi mpya wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Idadi ya Watu Duniani (UNFPA), Bibi Jacqueline Mohan.

Katika maelezo yake Dk. Shein alisema kuwa...

 

3 years ago

Michuzi

FAHAMU UHUSIANO ULIOPO KATI YA UNENE & UZITO ULIOZIDI (OBESITY & OVERWEIGHT ) NA TATIZO LA UKOSEFU/UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME

Unene  na  uzito  uliozidi  ( Obesity )  ni  miongoni  mwa  vyanzo  na  visababishi  vikuu  vya  tatizo  la  ukosefu  na  upungufu  wa  nguvu  za  kiume.
Kwa   mujibu  wa  tafiti  mbalimbali  za  kitabibu, asilimia  kubwa  ya  wanaume  wenye   unene  na  uzito  uliozidi, wanakabiliwa  na  tatizo  la  ukosefu  na  upungufu  wa  nguvu  za  kiume.
KWANINI  WANAUME  WENYE  UNENE  NA  UZITO  ULIOZIDI  WANAKABILIWA  NA  HATARI  KUBWA  YA  KUPATWA  NA  TATIZO  LA  UKOSEFU  NA  UPUNGUFU  WA  NGUVU  ZA...

 

4 years ago

GPL

UHUSIANO ULIOPO UNA MANUFAA MAISHANI MWAKO?

ILI jambo lolote liwe na maana ni lazima liwe na manufaa. Hakuna mtu anayeweza kufanya jambo ambalo halina faida kwake. Marafiki, kwa bahati mbaya sana, wapo ambao wanakuwa kwenye uhusiano bila ya kuwa na mipango yoyote ya maana. Ndugu zangu, huwezi kukwepa mapenzi katika maisha, lakini jiulize, upo kwa sababu gani na huyo mwenzi wako? Umempenda au unataka kupoteza muda?
Anayefanya mambo bila kutazama faida na hasara zake siyo...

 

4 years ago

GPL

UHUSIANO ULIOPO UNA MANUFAA MAISHANI MWAKO?-3

ILI uhusiano wako uwe na maana lazima uangalie mara mbili na ujiridhishe kuwa una manufaa na wewe. Kuna mengi tumezungumza katika matoleo yaliyopita lakini leo tunafikia ukingoni. Marafiki, uhusiano usio na amani, kuharibu fedha kwa anasa hauna maana katika maisha yako. Sanasana unazidi kujiongezea matatizo tu. Kwa mfano, si utaratibu mzuri kutumia fedha nyingi kwa kulipia nyumba za wageni, taksi na mahitaji mengine kwa ajili ya...

 

2 years ago

Michuzi

DKT SHEIN ANOGESHA MKUTANO WA MABALOZI WILAYA YA KATI, PONGWE, UNGUJA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dkt.Ali Mohamed Shein akizungumza na wanachama cha Mapinduzi CCM na Viongozi wa Wilaya ya kati Mkoa wa Kusini Unguja leo wakati alipokua akiwapongeza wanachama hao na kuwashukuru baada ya ushindi wa Uchaguzi marudio uliomalizika mwezi wa Machi mwaka huu,mkutano ulifanyika leo katika ukumbi wa Azao Resort &SPA Zanzibar Pongwe Wilaya ya Kati,(kulia) Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai.

 

1 year ago

Michuzi

DKT SHEIN KUWA MGENI RASMI KONGAMANO LA KIBIASHARA KATI YA TANZANIA NA COMORO

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii.
RAIS wa Zanzibar Dk. Ali Mohamedi Shein anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika Kongamano la kibiashara la Tanzania Comoro (Trade Forum) lenye lengo la kuboresha fursa za kiuchumi baina ya nchi za Tanzania na Comoro.
Kongamano hilo ambalo linatarajiwa kuhudhuriwa na wafanyabiashara zaidi ya 150 wanatakao shiriki katika kongamano.
Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Mratibu wa Kongamano hilo kutoka Chemba ya Wafanyabiashara wenye Viwanda na Kilimo (TCCIA, Anna...

 

3 years ago

Michuzi

DKT. SHEIN AENDELEA NA ZIARA YA KUIMARISHA CHAMA,AKUTANA NA MABALOZI WILAYA KATI,UNGUJA

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Viongozi wa Ngazi mbali mbali za Chama cha Mapinduzi alipofika katika viwanja vya Tamarind Hotel Kijiji cha Uroa Wilaya ya Kati Unguja alipofika kuzungumza na Mabalozi na Wenyeviti wa Maskani katika Mkutano maalum wa mwendelezo wa ziara zake za kumarisha Chama.Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani