Dkt. Shein awaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein  leo amewaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni kushika nyadhifa mbali mbali katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Hafla hiyo, ilifanyika Ikulu mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Serikali ambapo viongozi walioapishwa ni Lulu Mshamu Abdalla kuwa Naibu Waziri wa Wizara ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Joseph Abdalla Meza kuwa Kamishna wa Bodi ya Mapato ya Zanzibar (ZRB).

Dk. Shein amewaapisha Makatibu Wakuu ambao ni Ali Khalil Mirza kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati, Omar Hassan Omar aliapishwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Idrissa Muslim Hija ameapishwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali.

Pia, Dk. Shein amemuapisha Khadija Bakari Juma kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale, Juma Ali Juma ameapishwa kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Biashara na Viwanda,

 Aidha, Dk. Shein amemuapisha Maryam Juma Abdalla Saadalla kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi, Shaaban Seif Mohamed kuwa Katibu Mkuu katika Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais.

Kwa upande wa Naibu Makatibu Wakuu, walioapishwa ni Tahir Mohammed Khamis Abdulla kuwa Naibu Katibu Mkuu katika   Wizara ya Ardhi, Nyumba, Maji na Nishati, Ali Khamis Juma kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Biashara na Viwanda, Ahmad Kassim Haji kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi.

Pia, Dk. Shein amemuapisha Dk. Amina Ameir Issa kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale anaeshughulikia masuala ya Utalii na Mambo ya Kale, Mwanajuma Majid Abdulla ameapishwa kuwa Naibu Katibu Mkuu katika Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wazee, Wanawake na Watoto anaeshughulikia masuala ya Wazee, Wanawake na Watoto.

Wengine ni Maua Makame Rajab ameapishwa kuwa Naibu katibu Mkuu Wizara ya Kazi, Uwezeshaji, Wanawake na Watoto anaeshughulikia masuala ya Kazi na Uwezeshaji, Amour Hamil Bakari kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo,Dk. Saleh Yussuf Mnemo kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Utalii na Mambo ya Kale anayeshughulikia masuala ya habari.

Viongozi mbali mbali walihudhuria katika hafla hiyo akiwemo Spika wa Baraza la Wawakilishi Zubeir Ali Maulid, Jaji Mkuu wa Zanzibar  Omar Othman Makungu, Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Said Hassan Said, Mawaziri na Manaibu Mawaziri.

Viongozi wengine waliohudhuria ni Mkuu wa  Mkoa wa Mjini Magharibi Ayoub Mohamed Mahmoud, Meya wa Manispaa ya Mji wa Zanzibar Khatib Abrahman Khatib, Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabih,Kadhi Mkuu wa Zanzibar Sheikh Khamis Haji, Washauri wa Rais wa Zanzibar pamoja na viongozi wengine wa Serikali.

Nao viongozi hao walioapishwa waliahidi kuendelea kumsaidia Rais Dk. Shein katika kuhakikisha Zanzibar inazidi kupata maendeleo endelevu na kusisitiza ushirikiano katika utendaji wa kazi ili malengo yote yaliokusudiwa yaweze kufikiwa ikiwa ni pamoja na kuwatumikia wananchi na kuwasogezea huduma zote muhimu za kijamii.

Kufuatia mabadiliko ya Wizara za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yaliofanyika hivi karibuni, Rais Dk. Shein alifanya uteuzi na kuwabadilisha wadhifa baadhi ya watendaji wakuu katika taasisi mbali mbali za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Rajab Mkasaba, Ikulu Zanzibar

Postal Address: 2422 Tel.:0777427449. Fax: 024 2231822 

 E-mail: rajabmkasaba@yahoo.co.uk

 

The post Dkt. Shein awaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni appeared first on Zanzibar24.

Zanzibar 24

Read more


Habari Zinazoendana

1 year ago

Zanzibar 24

Dkt. Shein awaapisha Manaibu Waziri aliowateua hivi karibuni

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mhe,Mihayo Juma Nhunga, katika hafla iliyofanyika leo Ikulu Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] 10/11/2016.Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamo wa Pili wa Rais Mhe,Mihayo Juma Nhunga, katika hafla iliyofanyika leo Ikulu Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] 10/11/2016.

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Mhe,Shamata Shaame Khamis katika hafla iliyofanyika leo Ikulu Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.] 10/11/2016.Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Idara Maalum za SMZ Mhe,Shamata Shaame Khamis katika hafla iliyofanyika leo Ikulu Mjini Unguja,[Picha na Ikulu.]...

 

1 year ago

Zanzibar 24

Dk. Shein awaapisha viongozi aliwateua hivi karibuni

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein leo amewaapisha viongozi aliowateua hivi karibuni kushika nyadhifa mbali mbali katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Viongozi walioapishwa na Rais Dk. Shein katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar ni Dk. Sira Ubwa Mamboya ambaye anakuwa Mjumbe wa Baraza la Mapinduzi na Waziri asiekuwa na Wizara Maalum.

Wengine ni Bi Zainab Omar Mohammed ambaye anakuwa Mshauri wa Rais wa Masuala ya Jamii, Wazee, Wanawake na...

 

2 years ago

CCM Blog

RAIS MAGUFULI AWAAPISHA LEO MAWAZIRI WAPYA ALIOWATEUA HIVI KARIBUNI

Mawaziri wapya wakisubiri kuapishwa leo Ikulu jijini Dar es Salaam.Mawaziri wapya wakiimba wimbo wa Taifa kabla ya kuapishwa leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli (kushoto) akimuapisha Mhe. Profesa Jumanne Maghembe (kulia) kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii,  leo Ikulu Jijini Dar es Salaam.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli (kushoto) akimuapisha Mhe. Dkt. Joyce Ndalichako (kulia) kuwa ...

 

1 year ago

Michuzi

MWENYEKITI WA CCM TAIFA RAIS DKT. MAGUFULI AKUTANA NA VIONGOZI WAPYA WA CHAMA ALIOWATEUA HIVI KARIBUNI NA DC MTEULE WA UBUNGO

Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Dkt John Pombe Magufuli akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Ubungo Mteule Mhe. Kisare Makori akishuhudiwa na viongozi wapya wa CCM aliowateua hivi karibuni. Kutoka kulia ni Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Humphrey Polepole, Katibu NEC Siasa na Uhusiano wa Kimataifa Kanali Ngemela Eslom Lubinga na Naibu Katibu Mkuu wa CCM Bara Ndg. Rodrick Mpogolo walipoenda kujitambulisha Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 20, 2016.Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Dkt John...

 

2 years ago

Michuzi

RAIS JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI AWAAPISHA MAWAZIRI ALIOWATEUA HIVI KARIBUNI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli (kushoto) akimuapisha Mhe. Profesa Jumanne Maghembe (kulia) kuwa Waziri wa Maliasili na Utalii, leo Ikulu Jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. John Pombe Joseph Magufuli (kushoto) akimuapisha Mhe. Dkt. Joyce Ndalichako (kulia) kuwa Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi. (Ni baada ya kumteua kuwa Mbunge), leo Ikulu Jijini Dar es Salaam. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,...

 

2 years ago

Zanzibar 24

Rais Dk Shein awaapisha viongozi aliowateua Ikulu leo

HassanRais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha Nd,Hassan Khatib Hassan kuwa Naibu Katibu Mkuu, Wizara ya Kazi,Uwezeshaji,Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto,atayeshuhulikia masuala ya Wazee,Vijana,Wanawake na Watoto,katika hafla iliyofanyika ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leoSidaRais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (kushoto) akimuapisha ACP Sida Mohamed Himid kuwa Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais,Tawala za...

 

3 weeks ago

Zanzibar 24

Dkt.Shein awaapicha viongozi wapya aliowateua jana

 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein  leo amewaapisha viongozi aliowateua hapo jana kushika nyadhifa mbali mbali katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Hafla hiyo, ilifanyika Ikulu mjini Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi mbali mbali wa Serikali ambapo viongozi walioapishwa ni Waziri wa Biashara na Viwanda Balozi Amina Salim Ali, Waziri wa Vijana, Utamaduni, Sanaa na Michezo Balozi Ali Abeid Karume, Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Usafirishaji...

 

1 year ago

Zanzibar 24

Rais Magufuli awaapisha Viongozi wa NEC, Secretarieti ya maadili na majaji wa rufani aliowateua

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli,  leo tarehe 23 Desemba, 2016 amewaapisha viongozi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma na Majaji wa Mahakama ya Rufani aliowateua jana tarehe 22 Desemba, 2016.

Hafla ya kuwaapisha viongozi hao imehudhuriwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa, Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora Mhe. Anjellah Kairuki, Mwanasheria Mkuu wa...

 

2 years ago

Michuzi

DKT. SHEIN AWAAPISHA VIONGOZI KATIKA TAASISI MBALI MBALI ZANZIBAR LEO

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Nd,Salmin Amour Abdalla kuwa Naibu Katibu wa Baraza la Mapinduzi katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi.Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimuapisha Nd,Asaa Ahmada Rashid kuwa Mwenyekiti wa Tume ya Maadili ya Viongozi wa Umma katika hafla iliyofanyika Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi.Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani