DStv kuonyesha London Marathon Mubashara!

Dar es Salaam, Ijumaa Aprili 21, 2017; Jumapili 23 April 2017 saa tano asubuhi, Macho na masikio ya watanzania yataelekezwa jijini London, kumshuhudia mwanariadha wetu pekee anayeshiriki mashindano ya London Marathon akifanya vitu vyake. 
Haya ni moja ya mashindano maarufu zaidi ya riadha ulimwenguni na yanashirikisha wanariadha wa viwango vya kimataifa kutoka nchi mbalimbali kikiwemo Kenya na Ethiopia ambazo zina sifa kubwa katika ulingo wa riadha.
Mashindano hayo yataonekana Mubashara kupitia king’amuzi cha DStv  katika chaneli namba 209 ya SuperSport (SS9) kuanzia saa tano asubuhi kwa saa za Afrika Mashariki.
Mkurugenzi Mtendaji wa Multichoice Tanzania Maharage Chande amesema kuwa kupitia king’amuzi maarufu cha DStv kitaonyesha mashindano hayo mubashara hivyo watanzania wataweza kushuhudia wenyewe na wala siyo kwa kuhadithiwa.
“Wakati wote DStv imekuwa kinara katika kuwahakikishia watanzania wengi uhundo wa aina yake hususan katika ulingo wa michezo na burudani na kwa mara nyingine tena tunauwezesha umma wa watanzania kushuhudia tukio hili muhimu ambapo balozi wetu Alphonce Simbu anatuwakilisha katika mashindano makubwa ya riadha” akisema Maharage.
Alphonce, ambaye ni Balozi maalum wa DStv, ni Mtanzania wa kwanza kushinda medali ya dhahabu katika mashindano maarufu ya Standard Chartered Mumbai Marathon na anatarajiwa kuwapa wakati mgumu manguli wa riadha ulimwenguni wanaoshiriki mbio hizi za London.
Multichoice Tanzania inamdhamini Simbu kwa muda wa mwaka mzima kwa lengo la kufanikisha maandalizi yake ya kushiriki katika mashindano ya Dunia yatakyofanyika jijini London mwezi wa nane mwaka huu. Udhamini huu ulianza tangu mwaka 2016 ambapo Multichoice humpatia Alphonce posho ya kujikimu pamoja na kusaidia kambi yake ya mazoezi

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

2 years ago

Global Publishers

DStv kuonyesha live mechi 300 Premier League

REFILE - CORRECTING BYLINE Chelsea's Branislav Ivanovic (R) challenges Arsenal's Kieran Gibbs during their English Premier League soccer match at Stamford Bridge in London October 5, 2014. REUTERS/Stefan Wermuth (BRITAIN - Tags: SPORT SOCCER TPX IMAGES OF THE DAY) NO USE WITH UNAUTHORIZED AUDIO, VIDEO, DATA, FIXTURE LISTS, CLUB/LEAGUE LOGOS OR "LIVE" SERVICES. ONLINE IN-MATCH USE LIMITED TO 45 IMAGES, NO VIDEO EMULATION. NO USE IN BETTING, GAMES OR SINGLE CLUB/LEAGUE/PLAYER PUBLICATIONS. FOR EDITORIAL USE ONLY. NOT FOR SALE FOR MARKETING OR ADVERTISING CAMPAIGNS

Wilbert Molandi, Dar es Salaam

KAMPUNI ya Multchoice Tanzania, juzi ilizindua rasmi msimu wa Ligi Kuu ya England ‘Premier League’ ambayo inatarajiwa kuanza rasmi kesho Jumamosi.

Wakati wa uzinduzi huo kupitia DStv, Mkurugenzi wa Multchoice Tanzania, Maharage Chande, alisema mechi 300 kati ya 380 zitaonyeshwa ‘live’.

Maharage amesema pamoja na kuongeza mechi za live, sasa hadi wenye king’amuzi wanaolipia shilingi 23,500 nao wataona live mechi 100 za ligi hiyo. “Hii ni asilimia 80 ya mechi za...

 

12 months ago

TheCitizen

Simbu fifth at London Marathon

Tanzania’s long distance athlete Alphonce Simbu came close to giving Tanzanians an ideal weekend gift yesterday after finishing fifth at the 2017 London Marathon.

 

3 years ago

BBC

VIDEO: London Marathon's fantastic four

Meet the women deemed Kenya's 'fantastic four,' Edna Kiplagat, Florence Kiplagat, Mary Keitany and Priscah Jeptoo.

 

4 years ago

BBCSwahili

Wakenya watamba London Marathon

Wakenya walishinda nafasi za kwanza mbili katika mbio za wanaume na zile za wanawake huko London.

 

4 years ago

BBC

Farah eighth in London Marathon

Kenyan athletes come first and second at the London marathon in both men's and women's races, with Mo Farah eight.

 

1 year ago

Habarileo

Simbu kushiriki London marathon

MWANARIADHA wa Kimataifa wa Tanzania, Alphonce Felix Simbu atashiriki London Marathon zitakazofanyika Aprili 23 mwakani, imeelezwa.

 

1 year ago

Mwananchi

London Marathon wamwaga mamilioni

Bingwa wa mashindano London Marathon atajinyakulia dola 100,000 msimu huu. hii.

 

12 months ago

BBC

Keitany record at London Marathon

Mary Keitany breaks Paula Radcliffe's women's-only world record to win the London Marathon, while Daniel Wanjiru takes victory in the men's race.

 

3 years ago

BBCSwahili

Je washindi wa London Marathon walitumia dawa ?

Washindi mara saba wa mbio za marathon za London walikuwa na matokeo ya kutatanisha baada ya damu yao kupigwa msasa.

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani