Habari Mbaya: Mke wa Mzee Yusuf afariki Dunia

Aliyekuwa mfalme wa muziki wa Taarab Alhaj Mzee Yusuf amefiwa na mke wake Chiku Khamis Tumbo.

Chiku amefariki usiku huu katika hospitali ya Amana, Ilala jijini Dar es Salaam alipokuwa amepelekwa kujifungua na kwa bahati mbaya yeye na mwanawe wamefariki.

Marehemu Chiku Khamis Tumbo

Mzee Yusuf amenukuliwa katika moja ya vyombo vya habari kuwa alimpeleka mkewe hapo Amana leo saa 10 alasiri kwaajili ya kujifungua na kwa bahati mbaya opereshini (upasuaji) iliyofanywa jioni, haikwenda salama na...

Zanzibar 24

Read more


Habari Zinazoendana

2 years ago

Malunde

Tanzia: MKE WA MZEE YUSUF 'BI CHIKU' AMEFARIKI DUNIA


Habari zilizonifikia muda huu kutoka Dar es salaam ni kuhusu kifo cha mke mdogo wa Mwimbaji wa zamani wa Jahazi Modern Taarabu Alhaj Mzee Yusuph Chiku amefariki usiku huu wakati anajifungua na mtoto naye amefariki. Kupitia Instagram yake Mtangazaji wa Clouds FM Geah Habib ameandika: >>>”Innalillah wainaillah rajuun mke mdogo wa Mzee Yusufu #Chiku amefariki dunia usiku huu alipokuwa akijifungua na mtoto amefariki taarifa zaidi tutaendelea kupeana!!” – Geah Habib.Chiku amekutwa na mauti leo...

 

3 years ago

MillardAyo

Ukweli wa taarifa za Mzee Yusuf kuoa mke wa tatu uko hapa

Mzee Yusuf ni staa kutoka kwenye muziki wa Taarab Tanzania, moja ya stori zilizomfanya aongelewe zaidi ndani ya hizi wiki ni habari zake zilizosambaa kwamba ana mpango wa kuongeza mke wa tatu, tazama hii video hapa chini kupata info na ukweli wake. Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na […]

The post Ukweli wa taarifa za Mzee Yusuf kuoa mke wa tatu uko hapa appeared first on TZA_MillardAyo.

 

2 years ago

Bongo Movies

Hivi Punde: Mke Mdogo wa Mzee Yusuf Amefariki Usiku Huu

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Bendi ya Jahazi Modern, Mzee Yusuf amefiwa na mkewe usiku huu. Mmoja wa Wakurugenzi wa Jahaz Modern Taarab, Mzee Juma Mbizo ameiambia Global Publishers kuwa bi Chiku, ambae alikua mke mdogo wa Mzee Yusuf amefariki dunia katika Hospitali ya Amana wakati akijifingua. Mtoto nae pia amefariki.

Marehemu bi Chiku, ambae alikua mke mdogo wa Mzee Yusuf.

Pumzika kwa amani Chiku. Pole kwa Mzee Yusuph ndugu jamaa na  marafiki.

 

 

4 years ago

GPL

MKE WA NOORAH AFARIKI DUNIA

Msanii wa Bongo Fleva Noorah akiwa na mke wake Anna Kingwalu siku ya ndoa yao. Mke wa msanii wa Bongo Fleva Noorah, Anna Kingwalu, amefariki leo nyumbani kwao Morogoro amethibitisha Dark Master. Noorah na Anna walifunga ndoa Juni 8, 2013 nyumbani kwao Shinyanga.…

 

2 years ago

Mwananchi

Mke wa Mwakyembe afariki dunia

Mke wa Waziri wa Habari,  Utamaduni, Sanaa na Michezo ,Dk Harisson Mwakyembe  amefariki usiku wa kuamkia leo  jijini Dar es Salaam.

 

1 year ago

Zanzibar 24

Mke wa Kingunge afariki dunia

Mke wa mwanasiasa mkongwe nchini, Kingunge Ngombale Mwiru, Peras Kingunge amefariki dunia leo Alhamisi katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili.

Mtoto wa Kingunge, Kinje Ngombale amethibitisha taarifa hizo na kwamba kifo cha mama yake kimetokea wakati baba yake pia ni mgonjwa.

“Ni kweli mama amefariki na baba amelala kwa sababu ndio kwanza ametoka chumba cha upasuaji aling’atwa na mbwa. Tutamwambia akiamka,” amesema

The post Mke wa Kingunge afariki dunia appeared first on...

 

1 year ago

Channelten

Ajali mbaya nchini Kenya, Gavana wa kaunti ya Nyeri afariki dunia

download

Gavana wa kaunti ya Nyeri nchini Kenya Wahome Gakuru amefariki mapema leo kufuatia ajali mbaya ya gari aliyoipata katika eneo la Kabati katika barabara kuu ya Thika-Sagana katika kaunti ya Murang’a nchini humo.

Gavana huyo alikimbizwa katika Hospitali ya Thika Level 5 kwa matibabu ya dharura lakini akaaga dunia baada ya kudaiwa kuwa aliumia vibaya katika mwili wake ambapo kamishna wa kaunti hiyo Murang’a John Elungata amethibitisha kifo hicho.

Kamishna huyo amesema kwamba kabati ni eneo...

 

4 years ago

GPL

MZEE OJWANG AFARIKI DUNIA

MWIGIZAJI nguli raia wa Kenya, Benson Wanjau 'Mzee Ojwang' amefariki dunia jana jioni akiwa Hospitali ya Taifa ya Kenyatta, alipokuwa amelazwa akisumbuliwa na ugonjwa wa homa ya mapafu (Pneumonia). Mzee Ojwang atakumbukwa katika Vipindi vya Televisheni kama Vitimbi, Vioja Mahakami, Vituko na Kinyonga. Amefariki akiwa na umri wa miaka 78.

 

5 years ago

GPL

MZEE GURUMO AFARIKI DUNIA

Maalim Muhidin Gurumo enzi za uhai wake. MKONGWE wa Dansi nchini, Maalim Muhidin Gurumo aliyekuwa akitumikia Bendi ya Msondo Ngoma ‘Baba ya Muziki’ kabla ya kustaafu mwaka jana, amefariki  dunia. Kwa mujibu wa habari tulizozipata kupitia chanzo chetu, Mwanamuziki huyo amefariki alasiri hii katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa amelazwa kwa matibabu. Mpaka sasa sababu ya kifo cha Mzee Gurumo bado haijajulikana na...

 

Share

Trending Now

Zinazosomwa Sasa

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani