Hatma ya janga la Dawa za Kulevya Zanzibar limo mikononi mwa Tume kufanyiwa kazi

Makamu wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alitahadharisha kwamba hatma ya Zanzibar kuhusiana na janga la Dawa za Kulevya limo mikononi mwa Tume ya Kitaifa ya kuratibu na kudhibiti madawa ya kulevya iliyoundwa kwa lengo la kukabiliana na janga hilo.

 

Alisema wakati Wajumbe wa Tume hiyo wakijipanga kuingia kwenye vita hivyo  waelewe kwamba wanaingia katika vita vikali vya kupambana na wenye fedha nyingi na mtandao wa siku nyingi.

Akiizindua rasmi Tume hiyo ya Kitaifa ya kuratibu na kudhibiti dawa za kulevya hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar akiwa yeye ndie Mwenyekiti wa Tume hiyo  Balozi Seif Ali Iddi alisema mafanikio ya Tume hiyo yatategemea zaidi jinsi wajumbe wake watakavyojipanga vizuri kwa kushirikiana  kwa karibu zaidi na wadau wengine katika kukabiliana na uingizwaji wa dawa hizo Nchini.

Balozi Seif alisema hali ya utumiaji na usambazaji wa dawa za kulevya nchini kote sio mzuri hali iliyopelekea Serikali zote mbili kulivalia njuga tatizo hilo sugu la Dawa za kulevya lenye kuiangamiza jamii hasa Vijana ambao ndio nguvu kazi kubwa ya Taifa.

Alisema kwa kuwa wanaojishughulisha na dawa za kulevya baadhi yao wanaeleweka na wanaishi pamoja na jamii Mitaani. Hivyo ni vyema jukumu la Wajumbe wa Tume hiyo likaelekeza zaidi nguvu zake katika uzuiaji wa uingizaji wa dawa hizo hapa nchini sambamba na kutoogopa kuwachukulia hatua za kisheria wahusika hao.

Balozi Seif alisisitiza kwamba kwa kuwa suala la dawa za kulevya linazikumba pembe zote za Dunia, mafanikio ya vita hivyo yatahitaji mashirikiano ya Taasisi za ndani na nje ya nchi ambazo zinajihusisha moja kwa moja na dawa hizo thakili.

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alimshukuru Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar Dr. Ali Mohamed Shein mwa imani aliyokuwa nayo kwake  kwa kumteua kuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo.

Aidha Balozi Seif aliwapongeza Wajumbe wote walioteuliwa kushirikiana naye katika utekelezaji wa jukumu hilo zito ambalo anaimani kwamba kila mjumbe analiweza licha ya uzito uliopo mbele yao.

Balozi Seif  aliwakumbusha Wajumbe wa Tume hiyo  wajibu wao kwa Mujibu wa Kifungu cha 4 {1} cha Sheria  wa kusimamia mambo Tisa akiyataja baadhi yake kuwa ni pamoja na kuandaa na kusimamia utekelezaji wa mpango wa Taifa za Udhibiti wa Dawa za kulevya.

Nyengine alisema ni kupitia sheria na kanuni za Udhibiti wa dawa za kulevya, kuimarisha na kuendeleza jitihada za kuzuia matumizi ya dawa za kulevya, kuanzisha mfumo wa ukusanyaji na uchambuzi wa Taarifa za matumizi na biashara haramu ya dawa za kulevya.

Kwa mujibu wa sheria nambari 9 ya mwaka 2009  kifungu cha 4 {1} Tume ya Kitaifa ya Kuratibu na Kudhibiti Dawa za Kulevya  Wajumbe wake wana wajibu wa kukutana Mara Mbili kwa Mwaka.

The post Hatma ya janga la Dawa za Kulevya Zanzibar limo mikononi mwa Tume kufanyiwa kazi appeared first on Zanzibar24.

Zanzibar 24

Read more


Habari Zinazoendana

1 year ago

Zanzibar 24

Mbowe mikononi mwa polisi kwa tuhuma za kujihusisha na dawa za kulevya

Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe amekamatwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam kufuatia kukaidi wito wa jeshi hilo alipotakiwa kufika Kituo cha Polisi cha Kati kwa ajili ya mahojiano kufuatia tuhuma za kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro amethibitisha taarifa hizo kuwa wanamshikilia kiongozi huyo.

Kwa mujibu wa msemaji wa CHADEMA Boniface Makene, amesema...

 

1 year ago

Channelten

Kubaliana na dawa za kulevya Zanzibar, Tume ya kuratibu na kudhibiti dawa hizo yazinduliwa

madawa-ya-kulevya

 

Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi amesema hatma ya Zanzibar katika kukabiliana na matumizi ya dawa za kulevya, ipo mikononi mwa Tume ya kitaifa ya serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya kuratibu na kudhibiti dawa za Kulevya iliyoundwa hivi karibuni ambayo ameitaka kujipanga katika kupambana vikali na wenye fedha na mtandao wa muda mrefu.

Balozi Seif Ali Iddi ametoa kauli hiyo, muda mfupi baada ya kuizindua rasmi Tume ya Kitaifa ya Kuratibu na...

 

2 years ago

Dewji Blog

Matumizi ya dawa za kulevya ni janga linaloathiri vijana wengi Zanzibar- Dk. Mahmoud

Matumizi ya dawa za kulevya ni janga linaloathiri vijana na kupoteza mwelekeo ambao hupelekea kufanya maamuzi yasiyo sahihi na kupoteza kumbukumbu jambo ambalo linarejesha nyuma maendeleo ya Taifa.

Akitoa mafunzo kwa watendaji wa Chuo cha Mafunzo  Kaimu Mkurugenzi Tume ya Taifa ya Kudhibiti na Kupambana na Madawa ya Kulevya Dkt Mahmoud Ibrahim Mussa katika shamra shamra za kuadhimisha siku ya kudhibiti madawa ya kulevya.

Amesema mtumiaji wa madawa ya kulevya huathirika ubongo ambao hawezi...

 

3 years ago

Dewji Blog

Hatma ya CCM ipo mikononi mwa vijana

-Shirikisho lina Wajumbe 683

-Wanachama 31,000

-Vijana wafurahi kupiga picha pamoja na Nape

 Wanafunzi kutoka vyuo vya elimu ya juu nchini wakifurahi kupiga picha na Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnauye.

 Kila mwanafunzi alipenda apate ukumbushokwa kupiga picha na na Katibu wa NEC Npe Nnauye.

 Wajumbe kutoka mikoa mbali mbali wakiimba na kucheza nyimbo za hamasa.

 Mwenyekiti wa CCM Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza meza kuu kuimba wakati wa kufungua kwa mkutano wa Shirikisho la...

 

3 years ago

Mwananchi

Hatma ya Miss Tanzania mikononi mwa Basata

Hatma iwapo mashindano ya Miss Tanzania yataendelea au yatasitishwa kwa muda, itategemea majibu ya tathmini iliyofanyika mwishoni mwa wiki jana yanayotarajiwa kutolewa na Baraza la Sanaa la Taifa (Basata) wiki chache zijazo.

 

11 months ago

Mwananchi

Hatma ya Rais Zuma mikononi mwa mahakama

Dar es Salaam. Mahakama ya kikatiba nchini Afrika Kusini inatarajiwa kutoa uamuzi kama wabunge wanaweza kupiga kura ya siri ya kutokuwa na imani na Rais Jacob Zuma au la.

 

5 months ago

RFI

Hatma ya Kenya mikononi mwa Mahakama Kuu

Tangu Jumatano, Novemba 15, majaji wa Mahakama Kuu ya Kenya wanachunguza rufaa mbili ambazo zinaomba kufutwa kwa uchaguzi mpya wa Rais Uhuru Kenyatta.

 

2 years ago

Dewji Blog

Hatma ya Griezmann kujiunga Man United yasalia mikononi mwa Simeone

Kwa siku za karibuni katika michezo ya kimataifa kumekuwepo na taarifa ambazo zinamhusu mshambuliaji wa Atletico Madrid na timu ya taifa ya Ufaransa, Antoine Griezmann kuwa anaweza kujiunga na Manchester United baada ya msimu wa 2016/2017 kumalizika.

Taarifa kutoka mtandao wa The Manchester United News, zimeeleza kuwa staa huyo amewambia Man United kuwa kama wanamhitaji basi wafanye mazungumzo na kocha wa klabu yake, Diego Simeone kwani ndiye ambaye anajua hatma yake ya soka klabuni...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani