Hivi Punde: Mke Mdogo wa Mzee Yusuf Amefariki Usiku Huu

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Bendi ya Jahazi Modern, Mzee Yusuf amefiwa na mkewe usiku huu. Mmoja wa Wakurugenzi wa Jahaz Modern Taarab, Mzee Juma Mbizo ameiambia Global Publishers kuwa bi Chiku, ambae alikua mke mdogo wa Mzee Yusuf amefariki dunia katika Hospitali ya Amana wakati akijifingua. Mtoto nae pia amefariki.

Marehemu bi Chiku, ambae alikua mke mdogo wa Mzee Yusuf.

Pumzika kwa amani Chiku. Pole kwa Mzee Yusuph ndugu jamaa na  marafiki.

 

Bongo Movies

Read more


Habari Zinazoendana

2 years ago

Malunde

Tanzia: MKE WA MZEE YUSUF 'BI CHIKU' AMEFARIKI DUNIA


Habari zilizonifikia muda huu kutoka Dar es salaam ni kuhusu kifo cha mke mdogo wa Mwimbaji wa zamani wa Jahazi Modern Taarabu Alhaj Mzee Yusuph Chiku amefariki usiku huu wakati anajifungua na mtoto naye amefariki. Kupitia Instagram yake Mtangazaji wa Clouds FM Geah Habib ameandika: >>>”Innalillah wainaillah rajuun mke mdogo wa Mzee Yusufu #Chiku amefariki dunia usiku huu alipokuwa akijifungua na mtoto amefariki taarifa zaidi tutaendelea kupeana!!” – Geah Habib.Chiku amekutwa na mauti leo...

 

2 years ago

Zanzibar 24

Habari Mbaya: Mke wa Mzee Yusuf afariki Dunia

Aliyekuwa mfalme wa muziki wa Taarab Alhaj Mzee Yusuf amefiwa na mke wake Chiku Khamis Tumbo.

Chiku amefariki usiku huu katika hospitali ya Amana, Ilala jijini Dar es Salaam alipokuwa amepelekwa kujifungua na kwa bahati mbaya yeye na mwanawe wamefariki.

Marehemu Chiku Khamis Tumbo

Mzee Yusuf amenukuliwa katika moja ya vyombo vya habari kuwa alimpeleka mkewe hapo Amana leo saa 10 alasiri kwaajili ya kujifungua na kwa bahati mbaya opereshini (upasuaji) iliyofanywa jioni, haikwenda salama na...

 

2 years ago

Zanzibar 24

Habari za hivi punde: Aliyekuwa Naibu Waziri wa fedha apandishwa Mahakamani mchana huu

Aliyekuwa Naibu Waziri wa fedha na mbunge wa Mkuranga, Adam Kigoma Malima amefikishwa mahakamani kujibu tuhuma za kumshambulia askari polisi.

Malima anashtakiwa pamoja na dereva wake Ramadhani Mohamed Kigwande anayekabiliwa na tuhuma za kujeruhi.

Washtakiwa wamesomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Respicious Mwijage wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Wakili wa serikali, Mwanaamina Kombakono amedai, Mei 15 mwaka huu huko Masaki katika wilaya ya Kinondoni jijini Dar es Salaam...

 

3 years ago

MillardAyo

Ukweli wa taarifa za Mzee Yusuf kuoa mke wa tatu uko hapa

Mzee Yusuf ni staa kutoka kwenye muziki wa Taarab Tanzania, moja ya stori zilizomfanya aongelewe zaidi ndani ya hizi wiki ni habari zake zilizosambaa kwamba ana mpango wa kuongeza mke wa tatu, tazama hii video hapa chini kupata info na ukweli wake. Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na […]

The post Ukweli wa taarifa za Mzee Yusuf kuoa mke wa tatu uko hapa appeared first on TZA_MillardAyo.

 

3 years ago

Bongo5

Dida wa Times FM aeleza kisa cha kutukanwa na mke mdogo wa Mzee Yussuf

page

Mtangazaji wa Kipindi cha Mitikisiko ya Pwani kupitia Times FM, Khadija Shaibu ‘Dida’ amefunguka na kuzungumzia sababu ya kutukanwa katika mtandao wa kijamii na mke mdogo wa Mzee Yussuf, Chiku.

page

Mzee Yussuf Jumanne hii aliamua kuwaondoa wake zake wawili Leyla Rashid na Chiku katika mtandao wa Instagram baada ya kuwa wanatupiana maneno machafu kupitia mtandao huo hali ambayo inadaiwa ilikuwa inamchafua mume wao.

Akizungumza na Bongo5 Ijumaa hii, Dida amedai alitukanwa na Chiku ambaye ni mke...

 

2 years ago

Mtanzania

MZEE ANAYESAKA MKE AAPA KUMPATA MWAKA HUU

MZEE Athuman Mchambua (76)

MZEE Athuman Mchambua (76)

Na FARAJA MASINDE-DAR ES SALAAM

MZEE Athuman Mchambua (76) ambaye ametoa tangazo la kutafuta mke wa kuoa, amesema anaamini atafanikiwa lengo lake kabla mwaka huu kumalizika.

Alisema hadi sasa ameshapokea simu za wanawake wa mikoa karibu yote ya Tanzania bara isipokuwa Pwani.

Akizungumza na MTANZANIA kwa simu jana, Mzee Mchambua alisema kuwa hatatumia tena njia ya kuweka madalali nchi nzima kama alivyoahidi awali, badala yake kuna mkakati mpya ambao anafikiria...

 

5 years ago

Michuzi

BREAKING NYUZZZZZ.....: MZEE SMALL AFARIKI DUNIA USIKU HUU

MUIGIZAJI MKONGWE HAPA NCHINI,SAID NGAMBA MAARUFU KWA JILA LA MZEE SMALL AMEFARIKI DUNIA USIKU WA LEO KATIKA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI ALIKOKUWA AMELAZWA AKIPATIWA MATIBABU.
AKITHIBITISHA TAARIFA YA KIFO CHA MZEE SMALL,MWANAE AITWAE MAHMOUD AMESEMA MZEE WAKE AMEFIKWA NA MAUTI HAYO MAJIRA YA SAA NNE USIKU WAKATI AKIWA HOSPITALINI HAPO AKIENDELEA KUPATIWA MATIBABU.
MIPANGO INAFANYIKA NYUMBANI KWAO TABATA NA KADRI TAARIFA ZITAKAVYOKUWA ZIKITUFIKIA TUTAENDELEA KUJULISHANA.
NI PIGO...

 

Share

Trending Now

Zinazosomwa Sasa

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani