IGP simon sirro awataka askari wa FFU kuwa na nidhamu

Mkuu wa Jeshi la Polisi  Tanzania IGP Simon Sirro amekitaka kikosi cha kutuliza ghasia FFU  kanda  ya Zanzibar kuwa na nidhamu ya kazi hasa  katika kulinda mali na fedha za jeshi zinazopatikana  kuzitumia kwa malengo.

Akizungumza na Askari  wa FFU wa Mikoa mitatu  katika ziara yake aliyoifanya Zanzibar amesema kikosi cha kutuliza ghasia kina kazi kubwa katika mapambano mbalimbali nchini hivyo ni vyema  kujipanga na kuongeza kasi ya mapambano ili kukabiliana na matukio yanayotokea.

Amesema  kikosi hicho bado kina kabiliwa na matatizo mengi ikiwemo ufinyu wa vitendea kazi na kuwaahidi kuwapatia magari matano makubwa  ya kufanyia kazi pamoja na gari ndogo la kusaidia katika kituo cha afya.

IGP sirro  baada ya mazungumzo na askari hao pia alitembelea  kambi za askari wa mikoa mitatu Zanzibar pamoja kukagua eneo linalotarajiwa kujengwa kambi ya kikosi cha  FFU huko matemwe.

Amina Omar 

The post IGP simon sirro awataka askari wa FFU kuwa na nidhamu appeared first on Zanzibar24.

Zanzibar 24

Read more


Habari Zinazoendana

5 months ago

Channelten

IGP Simon Sirro awapomgeza askari, azungumza na wananchi Kibiti

1-45

Wananchi wa Kibiti mkoani Pwani wametakiwa kuendelea na shughuli zao za kimaendeleo na kijamii ikiwemo kushiriki katika ibada misikitini na makanisani kutokana na kuimarika kwa hali ya ulinzi na usalama mkoani humo.

Hayo yamesemwa na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro alipokwenda kuwatembelea baadhi ya wananchi mkoani humo kufuatia kuuawa kwa wahalifu 13 katika eneo la Gari Bovu, kijiji cha Chamiwaleni, Kata ya Mchukwi, Wilaya ya Kibiti, Mkoa wa Kipolisi Rufiji.

IGP Sirro pia...

 

4 months ago

Michuzi

IGP SIMON SIRRO AFANYA MAZOEZI NA MAOFISA NA ASKARI WA MAKAO MAKUU YA POLISI

 Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro akiongoza maofisa na askari wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi leo jijini Dar es Salaam katika mazoezi ya pamoja ambayo hufanyika kila mwisho wa mwezi. IGP amewahimiza Makamanda wa Polisi wa Mikoa yote kuhakikisha wanafanya mazoezi ya pamoja ili kuendelea kuboresha afya za maofisa na askari. 

Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP Simon Sirro akiongoza maofisa na askari wa Makao Makuu ya Jeshi la Polisi leo jijini Dar es Salaam katika mazoezi ya pamoja ambayo...

 

2 months ago

Michuzi

Inspekta Jenerali wa Polisi IGP Simon Sirro akagua utendaji kazi wa askari mkoa wa pwani

 Inspekta Jenerali wa Polisi, IGP Simon Sirro akikagua askari wa Mkoani Pwani alipofanya ziara mkoani humo kukagua utendaji kazi wa askari. IGP amewasisitiza askari wa Mkoa wa Pwani kuendelea kufanya kazi kwa weledi ili kuendelea kutoa huduma bora kwa wananchi wa Mkoa huo. Askari wa kikosi maalum cha Mkoani Pwani cha kupambana na majambazi kwenye majengo makubwa wakifanya zoezi baada ya IGP kuwasili mkoani humo kukagua utendaji kazi wa askari. Askari wa kikosi maalum cha Mkoani Pwani cha...

 

8 months ago

Zanzibar 24

Rais Magufuli amuapisha Simon Sirro kuwa IGP mpya

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Magufuli amemwapisha aliyekua Kamishna wa Polisi Simon Sirro kuwa Mkuu wa Jesho la Polisi Tanzania (IGP).

IGP Sirro ameteuliwa kushika nafasi hiyo jana May 28 ambapo  amechukua nafasi ya Ernest Mangu ambaye imeelezwa kuwa atapangiwa kazi nyingine.

The post Rais Magufuli amuapisha Simon Sirro kuwa IGP mpya appeared first on Zanzibar24.

 

8 months ago

Mwananchi

Simon Sirro: Huyu ndiye IGP aliyetamani kuwa Padri

Ilikuwa Juni, mwaka 2016 siku niliyopata fursa ya kufanya mahojiano maalumu na aliyekuwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro.

 

3 months ago

Michuzi

IGP Simon Sirro atembelea njombe, awataka wanasiasa kutoliingilia Jeshi la Polisi ili liendelee na kazi zake

 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akiwasili uwanja wa ndege wa Njombe, kwa ziara ya kikazi ya siku moja akitokea mkoani Ruvuma, ili kuzungumza na maafisa na askari wa Jeshi hilo pamoja na kuona changamoto wanazokutana nazo wanapotekeleza majukumu yao na namna ya kuwasaidia. 
 Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akikagua gwaride maalumu lililoandaliwa kwa ajili yake alipowasili mkoa Njombe, kwa ziara ya kiazi ya siku moja Wajumbe wa kamati ya Ulinzi na Usalama ya...

 

8 months ago

MillardAyo

VIDEOFupi: Simon Sirro alivyoapishwa kuwa IGP mpya na Rais JPM

Leo May 29, 2017 Rais Magufuli amemwapisha Simon Sirro kuwa Mkuu wa Jesho la Polisi Tanzania (IGP), baada ya kuteuliwa kushika nafasi hiyo May 28. IGP Sirro amechukua nafasi ya Ernest Mangu ambaye imeelezwa atapangiwa kazi nyingine. Simon Sirro alivyaapa mbele ya Rais Magufuli leo kuwa Mkuu wa Jeshi la Polisi IGP, baada ya kuteuliwa […]

The post VIDEOFupi: Simon Sirro alivyoapishwa kuwa IGP mpya na Rais JPM appeared first on millardayo.com.

 

4 weeks ago

Michuzi

MKUU WA JESHI LA POLISI, IGP SIMON SIRRO AFANYA ZIARA YA KIKAZI MKOANI LINDI KWA AJILI YA KUONGEA NA ASKARI.

 IGP Simon Sirro  akisalimiana na Kaimu Mkuu wa Mkoa  ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Lindi Mh Shaibu Ndemanga baada ya kuwasili mkoani Lindi katika ziara ya siku moja ya kuongea na Askari.  Picha na Jeshi la Polisi.Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro (katikati) akiwa na Askari wa Mkoa wa Lindi baada ya kumaliza kukagua  mazoezi ya ukakamavu na utayari yaliokuwa yameandaliwa na kikosi cha kupambana na uhalifu mkoani  humo.  Picha na Jeshi la Polisi.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP...

 

8 months ago

Michuzi

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani