IGP Sirro azungumzia tukio la kushambuliwa kwa Tundu Lissu

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amewataka wananchi kutoa ushirikiano wa kutosha ili kufanikisha kuwatia mbaroni wahalifu waliohusika kumshambulia kwa risasi Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu.

IGP Sirro ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari na kudai usalama wa nchi upo vizuri na jeshi la polisi limeongeza nguvu ya upelelezi mjini Dodoma ili kuhakikisha linawapata watu ambao wamefanya uhalifu wa kumpiga risasi mbunge Tundu Lissu , huku akiwataka...

Zanzibar 24

Read more


Habari Zinazoendana

1 year ago

Zanzibar 24

IGP Sirro upelelezi tukio la Tundu lissu umekwama

Kutokuwepo kwa dereva wa Lissu nchini, ambaye anapewa matibabu ya kisaikolojia Jijini Nairobi, kumesababisha kukwama kwa upelelelzi wa polisi kuhusiana na tukio la kushambuliwa kwa risasi Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.

Mkuu wa Jeshi la polisi (IGP), Simon Sirro aliyasema hayo jana Jumatano, Oktoba 4 na kueleza kuwa Polisi wanamsubiria dereva wa Tundu Lissu ili aweze kuwasaidia katika kukamilisha uchunguzi kuhusiana na tukio hilo lililotokea Septemba 7, mwaka huu, wakati mbunge...

 

2 years ago

Channelten

Kushambuliwa kwa Mbunge Tundu Lissu, Chadema walaani tukio hilo

CHADEMA

Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA kimesema hali ya mwanasheria mkuu wa chama hicho ambae pia Rais wa chama cha mawakili Tanganyika TLS TUNDU LISSU inaendelea vizuri akiwa anapatiwa matibabu mjini Nairobi Kenya.

Bwana Tundu Lissu alishambuliwa jana na watu wasiojulikana akiwa nyumbani kwake eneo la Area D mjini Dodoma ambapo inaelezewa kuwa takribani risasi tano zilimpata mwilini mwake na kulazimika kufikisha hospitali ya mkoa wa Dodoma kwa ajili ya matibabu ya awali.

Akizungumza na...

 

2 years ago

CHADEMA Blog

MAELEZO YA MBUNGE WA ROMBO MHESHIMIWA JOSEPH SELASINI KUHUSU TUKIO LA KUSHAMBULIWA TUNDU LISSU

Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini ameeleza jinsi Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu alivyopigwa risasi nyumbani kwake mjini Dodoma.Selasini amesema kuwa maelezo aliyopata ni kuwa alikuwa akifuatiliwa na gari tangu anatoka bungeni na dereva wake alilishtukia. Amesema kuwa alivyoona wanamfutilia alipofika nyumbani, dereva alimsihi Lissu asishuke ndani ya gari."Hao watu walipoona hawashuki

 

2 years ago

Zanzibar 24

Tundu Lissu amfungukia mkuu wa majeshi IGP Sirro.

Rais wa chama cha Wanasheria Tanzania (TLS) na Mwanasheria Mkuu wa chama cha CHADEMA, Tundu Lissu amewata wakuu wa vyombo vya usalama nchini wawaelekeze watumishi wao kazi za kufanya na siyo kupoteza muda na rasilimali za nchi.

Lissu amesema hayo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano uliyoitishwa na CHADEMA wenye lengo la kuzungumzia namna nchi inavyoenda kufilisika na ndipo alipomtaka Mkuu wa Idara ya Usalama wa Taifa Kamanda Modestus Francis Kipilimba na Mkuu wa...

 

1 year ago

Malunde

IGP SIRRO: BADO TUNA SHIDA NA DEREVA WA TUNDU LISSU

 
Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Simon Sirro amesema wanaendelea na upelelezi wa tukio la kushambuliwa na kujeruhiwa kwa risasi Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu.IGP Sirro akizungumza leo Jumatano akiwa ziarani mkoani Mtwara amemtaka dereva wa Lissu kulisaidia jeshi hilo katika kukamilisha upelelezi.Lissu ambaye anapata matibabu katika Hospitali ya Nairobi nchini Kenya, alishambuliwa na kujeruhiwa kwa risasi Septemba 7 nyumbani kwake Area D mjini Dodoma na watu...

 

1 year ago

Malunde

WAKILI WA CHADEMA AMVAA IGP SIRRO KUZUIA MJADALA KUHUSU TUNDU LISSU

Wakili wa CHADEMA, John Malya amefunguka na kuzungumzia juu ya kauli ya IGP Sirro kuhusu kuzuia wanasiasa kuzungumzia sakata la Lissu na kusema IGP hana mamlaka hayo kuzuia wananchi kuzungumzia jambo lolote na kufanya hivyo ni kuvunja sheria.

John Malya amesema hayo jana alipokuwa akiongea na waandishi wa habari Makao Makuu ya chama hicho yaliyopo Kinondoni na kusema kuwa Sirro anapaswa kukaa kimya sasa na kuendelea na uchunguzi wa sakata hilo ila hana mamlaka ya kuzuia wananchi wasitoe...

 

Share

Trending Now

Zinazosomwa Sasa

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani