Jalada kesi ya Malinzi larudi Takukuru.

Jalada la kesi ya  utakatishaji wa fedha inayomkabili aliyekuwa rais wa (TFF), Jamal Malinzi na wenzake limerudishwa Takukuru  kwa maagizo ya kurekebisha vitu vichache ili kukamilisha iuchunguzi.

Mbali ya Malinzi, wengine ni Katibu wa TFF, Mwesigwa Selestine na Mhasibu wa shirikisho hilo, Msiande Mwanga. Wakili wa serikali kutoka Takukuru, Leornad Swai amedai hayo leo mbele ya Hakimu  Mkazi Mkuu, Wilbard Mashauri, pindi shauri hilo lilipoitishwa kwa ajili ya kutajwa.

Swai alidai jalada la kesi hiyo limesharudishwa Takukuru likitokea kwa mkurugenzi wa mashtaka  DPP na kudai wamepewa maelekezo ya kukamilisha baadhi ya uchunguzi.Hata hivyo, wakili wa Utetezi Nehemia Nkonko aliomba upelelezi dhidi ya kesi hiyo ukamilike kwa haraka kwa sababu washtakiwa wapo ndani.

Hakimu Mashauri amahirisha kesi hiyo hadi January 25, 2018 kwa ajili ya kutajwa.Washtakiwa kwa pamoja wanakabiliwa na mashitaka 28, yakiwemo ya kughushi na utakatishaji fedha ambazo ni Dola za Marekani, 375,418.

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

2 days ago

Michuzi

JALADA KESI YA MHASIBU MKUU WA TAKUKURU NA WENZAKE LAPELEKWA TAKUKURU KWA UPELELEZI ZAIDI

Na Karama Kenyunko, Glogu ya jamii, 
Upande wa mashtaka katika kesi ya utakatishaji fedha na kumiliki mali zisizoendana na kipato chake  inayomkabili Mhasibu Mkuu wa Takukuru Godfrey Gugai na wenzake watatu umeiEleza mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa jalada la kesi hiyo limepelekwa Takukuru kwa ajili ya upelelezi zaidi.
Wakili wa Serikali Simon Wankyo akisaidiana na wakili Salim Msemo ameeleza leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, wakati shauri hilo lilipofikishwa mahakamani hapo...

 

2 years ago

Habarileo

Jalada la kesi ya Kitilya na wenzake lapelekwa Takukuru

JALADA la kesi inayomkabili aliyekuwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Harry Kitilya na wenzake, limepelekwa kwenye ofisi ya Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru).

 

2 months ago

Michuzi

KESI YA JALADA LA VIGOGO WA SIMBA LAREJESHWA TAKUKURU.

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Novemba 17, imeambiwa jalada la kesi inayowakabili vigogo wa Klabu ya Simba Evans Aveva na Godfrey Nyange maarufu "Kaburu" limeisharudi kutoka kwa (DPP) na limerejeshwa TAKUKURU
Hayo yameelezwa na wakili wa Takukuru, Leonard Swai mbele ya Hakimu Mkazi, Godfrey Mwambapa, wakati shauri hilo lilipokuja kwa kwa kutajwa.Wakili Swai alidai jalada hilo lilirudishwa juzi kutoka kwa DPP ambaye ametoa maelekezo ya kukamilisha zaidi upelelezi.
Upande wa jamhuri...

 

1 year ago

Mwananchi

Jalada kesi ya Lwakatare lahitajika kortini

Upande wa mashtaka katika kesi inayomkabili Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama wa Chadema, Wilfred Lwakatare na mwenzake Ludovick Joseph umetakiwa na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kufuatilia na kupeleka jalada la shauri hilo linalodaiwa kuwapo Mahakama Kuu.

 

1 year ago

Mtanzania

‘Jalada kesi ya Masamaki liko hatua za mwisho’

b

Na Kulwa Mzee-Dar es Salaam

JALADA la kesi inayomkabili  Kamishna wa Kodi na Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Tiagi Masamaki  na wenzake, lililopelekwa kwa Manasheria Mkuu wa Serikali (AG), liko katika hatua za mwisho.

Wakili wa Serikali, Christopher Msigwa alisema hayo jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shahidi,   kesi hiyo ilipokuwa inatajwa.

Msigwa alisema  jalada la kesi hiyo liko kwa AG katika hatua za mwisho hivyo aliomba...

 

1 year ago

Habarileo

Jalada kesi ya Mpemba lipo kwa Sirro

JALADA la kesi ya kujihusisha na biashara ya meno ya tembo yenye thamani ya Sh milioni 785.6 inayowakabili watu sita akiwemo Mpemba aliyewahi kutajwa na Rais John Magufuli, Yusuf Ali Yusuf, lipo kwa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Simon Sirro.

 

10 months ago

Michuzi

JALADA KESI YA NIDA LIPO KWA DPP

Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.
Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeelezwa kuwa jalada la kesi  ya uhujumu uchumi na kusababisha hasara ya bilioni 1.16 inayomkabili aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho (NIDA), Dickson Maimu na wenzake lipo kwa  (DPP)
Mwendesha Mashtaka wa Takukuru, Leonard Swai, amesema kuwa, jalada hilo liko kwa DPP kwa ajili ya kufanyiwa tathmini ya upelelezi uliofanyika
Hakimu Mkazi Mkuu, Respicius Mwijage  ameiahirisha kesi hiyo hadi Aprili 20,2017 kwa...

 

1 year ago

Mwanaspoti

Malinzi akaliwa kooni, Takukuru waibuka

WAKATI aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Tabora, Yusuf Kitumbo akimkalia kooni Rais wa Shirikisho la Soka nchini (TFF), Jamal Malinzi, Taasisi ya Kupambana na Kuzuia Rushwa (Takukuru) imesema imekamilisha uchunguzi juu ya sakata la upangaji matokeo ya FDL na inajiandaa kuweka mambo hadharani.

 

3 years ago

Mtanzania

Jalada kesi ya Zitto laitwa kwa Jaji Kiongozi

kabweNa Mwandishi Wetu, Dar es Salam
SAKATA la kufukuzwa uanachama kwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe (Chadema), limechukua sura mpya baada ya Jaji Kiongozi, Shabani Lila kuitisha jalada la kesi yake hali inayoonyesha kupitiwa upya kwa kesi hiyo.
Wiki hii Mahakama Kuu ilitupilia mbali ombi la Zitto la kutaka Kamati Kuu ya Chadema kutomjadili na hatimaye kumfukuza uanachama wake baada ya makada wenzake, Samson Mwigamba aliyekuwa Mwenyekiti wa Mkoa wa Arusha na Profesa Kitila Mkumbo...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani