Jeshi la Polisi kanda Maalum Dsm limetoa siku tatu Sheikh Ponda Issa Ponda kujisalimisha Polisi

b2

Jeshi la Polisi kanda Maalum Dsm limetoa siku tatu kwa katibu wa kutetea haki za waislam nchini Sheikh Ponda Issa Ponda kujisalimisha Polisi kanda Maalum ili ahojiwe kwa tuhuma za kutoa lugha za Uchochezi wakati akizungumza na waandishi wa habari jana.

Kamanda wa Polisi kanda Maalum dsm Lazaro mambosasa akizungumza na waandishi wa habari jijini dsm amesema wanamtafuta sheikh Ponda kumhoji kutokana na kauli zake wanazodai za Uchochezi ambapo jana katika hotel ya Iris polisi walishindwa kumtia mbaroni baada ya kutoweka katika eneo hilo wakati polisi walipofika kumkamata ingawa baadhi ya wanahabari waliokuwapo katika mkutano huo walishikiliwa kwa muda,kuhojiwa na baadae kuachiwa.

Katika kupambana na Matukio ya uhalifu jeshi hilo limefanikiwa kuwauwa majambazi wawili katika majibizano ya risasi waliokuwa na bunduki aina ya SMG eneo la mbezi wakati wakipanga njama za kuvamia duka na kutaka kufanya uporaji,ambapo jeshi hilo pia limetoa ilani kwa wahalifu kuwa hawatakuwa salama ikiwa wataendelea na uhalifu.

Share on: WhatsApp

The post Jeshi la Polisi kanda Maalum Dsm limetoa siku tatu Sheikh Ponda Issa Ponda kujisalimisha Polisi appeared first on Channel Ten.

Channelten

Read more


Habari Zinazoendana

4 months ago

MwanaHALISI

Sheikh Ponda kimenuka, apewa siku tatu kujisalimisha Polisi

JESHI la Polisi kanda Maalum ya Dar es Salaam limemtaka Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislam Tanzania, Sheikh Issa Ponda kujisalimisha mikononi mwa Polisi ndani ya siku tatu kuanzia leo, anaandika Hamisi Mguta. Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa amesema Sheikh Ponda ametenda makosa ...

 

4 months ago

BBCSwahili

Sheikh Ponda apewa siku 3 kujisalimisha kwa polisi Tanzania

Maafisa wa polisi nchini Tanzania wamempatia katibu mkuu wa baraza la mashirika ya kiislamu siku tatu kujisalimisha kwa madai ya kutoa matamshi ya uchochezi

 

10 months ago

Channelten

Jeshi la Polisi Kanda maalum ya DSM limetoa taarifa ya watu wawili kufariki dunia kutokana na Mvua

4bkc9489eee9c6kab4_800C450

Jeshi la Polisi Kanda maalum ya DSM limetoa taarifa ya watu wawili kufariki dunia kutokana na Mvua zinazoendelea kunyesha jijini DSM akiwemo mmoja aliyetumbukia katika shimo lililojaa maji eneo la Golani Kimara Suka na mwingine akiangukiwa na ukuta katika eneo la Kimbiji.

Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dsm Kamishna Simon Siro akizungumza na waandishi wa habari, amewataja watu hao kuwa ni Msichana Alice Gerald na Zakaria Charles ambapo ametoa wito kwa wananchi kuchukua tahadhari kutokana...

 

1 year ago

Channelten

Jeshi la Polisi kanda maalum Dsm limewahakikishia hili wananchi wa DSM

siro

Jeshi la Polisi kanda maalum Dsm limewahakikishia wananchi wa jiji la dsm litaendelea kwa nguvu kubwa kupambana na majambazi au wahalifu wanaotumia silaha na kuwataka wananchi kutoa taarifa sahihi na ushirikiano ili kukabiliana na vitendo vya uhalifu jijini Dsm.

Kamishna wa Polisi kanda Maalum Simon Sirro akizungumza na waandishi wa habari amesema katika mwaka 2016 unaisha matukio ya uhalifu yalipungua kulingana na mwaka 2015 ingawa kulitikiswa na matukio makubwa ikiwemo kuuwawa kwa askari...

 

8 months ago

Channelten

Jeshi la Polisi kanda maalum Dsm linawashikilia watu wanane wanaodaiwa kuwa Vinara wa wizi wa magari DSM

IMG_2851

Jeshi la Polisi kanda maalum Dsm linawashikilia watu wanane wanaodaiwa kuwa Vinara wa wizi wa magari katika jiji la dsm ambapo pia wamekuwa wakiyasafisha magari hayo katika mikoa mbali mbali nchini.

Akizungumza na waandishi wa habari Kaimu kamanda wa Polisi kanda maalum Dsm Lucas Mkondya amesema watuhumiwa hao ambao wanadaiwa kuwa na mtandao mkubwa wa wizi huo walikamatwa eneo la kongowe nje kidogo ya jiji la dsm.

Aidha jeshi hilo linawashikiliwa watuhumiwa 250 wa makosa mbali mbali ya...

 

1 year ago

Channelten

Jeshi la Polisi kanda maalum Dsm linawashikilia watuhumiwa 325

Screen Shot 2017-01-13 at 3.59.48 PM

Jeshi la Polisi kanda maalum Dsm linawashikilia watuhumiwa 325 wa matukio mbali mbali ya uhalifu katika msako mkali unaoendelea jijini dsm ambapo pia jeshi hilo limepiga marufuku uuzwaji wa silaha za kienyeji barabarani yakiwemo mapanga,Visu,pinde mikuki na manati .

Kamishna wa Polisi kanda Maalum Dsm Simon Sirro akizungumza na waandishi wa habari amesema watuhumiwa waliokamatwa ni pamoja na wanaojihusisha na Unyang’anyi wa kutumia nguvu,makundi ya uvamizi katika nyumba maarufu kumi nje...

 

4 months ago

Zanzibar 24

Mkutano wa Sheikh Ponda wavamiwa na Polisi

Jeshi la Polisi limevamia na kuzuia mkutano wa Sheikh Issa Ponda uliokuwa amepangwa kuzungumza na vyombo vya habari kuhusu tukio la kushambuliwa kwa risasi, Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, mara baada ya Sheikh Ponda kurejea kutoka Nairobi ambako alikutana na kuzungumza na Lissu.

Mkutano huo ulikuwa umepangwa kufanyika katika Hoteli ya Iris, iliyopo eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam leo asubuhi.

Mwenyekiti wa Kamati ya Uongozi ya Chama cha Wananchi (CUF), Julius Mtatiro...

 

4 months ago

Channelten

Jeshi la Polisi Kanda maalum DSM, Lafanikiwa kuua majambazi watatu

MAMBO SASA

Jeshi la polisi kanda maalum ya Dsm limefanikiwa kuwaua majambazi watatu katika eneo la Msongola manispaa ya Ilala jijini Dar es salaam baada ya majibizano ya risasi wakati majambazi hao wakiwa katika pikipiki ambapo walikutwa na Mabomu saba ya kijeshi ya kurusha kwa mkono, bunduki moja ya SMG ikiwa na risasi 16 na bastola Moja.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dsm SACP- Lazaro Mambosasa amesema Majambazi hao wakiwa katika pikipiki isiyokuwa na namba walikuwa mbioni kwenda kufanya Uporaji...

 

4 months ago

Malunde

SHEIKH PONDA AACHIWA POLISI KWA DHAMANA

Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limemwachia kwa dhamana Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Ponda Issa Ponda.
Pondà ameachiwa leo Jumamosi jioni baada ya kushikiliwa na Jeshi hilo tangu jana Ijumaa asubuni akituhimiwa kutoa lugha za kichochezi katika mkutano wake na waandishi wa habari Jumatano iliyopita.
Msemaji wa Jumuiya hiyo, Sheikh Rajabu Katimba amesema: "Sheikh Ponda ameachiwa kwa dhamana na atatakiwa kuripoti tena polisi."
Awali, Kamanda wa Kanda...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani