JESHI LA POLISI LAMTUNISHIA MISULI WAZIRI WA MAMBO YA NDANI MWIGULU NCHEMBA...PF3 NI LAZIMA

Baada ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba kutoa taarifa kupitia ukurasa wake wa Facebook kuwa kuanzia sasa majeruhi, mahututi asiyeweza kutoroka atatibiwa kwanza ndipo ashughulikie fomu ya polisi namba 3 (PF3), Jeshi la Polisi limetolea ufafanuzi  zaidi  wa taarifa hiyo.
Katika taarifa ya Waziri Nchemba alisema, “Tumeamua, majeruhi, mahututi asiyeweza kutoroka,na mtu mwenye majeraha yasiyo na utata wapewe matibabu kwanza bila PF3.”
Aliendelea kueleza zaidi kwamba, “Hatua za kufuata PF3 zianze mara moja wakati akiendelea kupewa matibabu, hii tunalenga kuokoa maisha yao kwanza. Utaratibu huu unajicho la karibu kutoka kwenye vyombo vyetu vya usalama ili kubaini ukweli jeraha la mhusika.”
Kwa upande wa Jeshi la Polisi kupitia kwa msemaji wake, Msemaji wa Jeshi la Polisi, Advera Bulimba-ACP ameeleza umma wa Watazania kwamba, fomu hiyo ni ya lazima kwa mtu yeyote aliyepata majereha kabla ya kutibiwa na itaendelea kutumika kwa mujibu wa sheria.
“Fomu ya Polisi namba 3 ijulikanayo kama PF.3 hutolewa kwa mtu baada ya Polisi kupata taarifa kutoka kwa mlalamikaji au muathirika kwa matukio yenye madhara mwilini, ajali au matukio yenye kuleta mashaka kuhusu vyanzo vyake kama vile kipigo, kujeruhi, ubakaji, kulawiti,  kunywa sumu na mengineyo.
“Ieleweke wazi kwamba matumizi ya PF3 ni ya lazima na yanaendelea kama kawaida  kwa mujibu wa sheria. Fomu hiyo inapaswa kutumika katika kila aina ya tukio tajwa hapo juu ili muathirika aweze kupata matibabu katika vitu vya afya na hatua za kiupelelezi kwa Jeshi la Polisi ziweze kuendelea.”
Aidha, ACP Bulimba aliongeza kuwa, “Katika mazingira mengine hali ya muathirika yaweza kuwa mbaya, hivyo huduma za kuokoa maisha (huduma ya kwanza) inaweza kuendelea kutolewa wakati watoa huduma wakiijulisha Polisi ili kuharakisha upatikanaji wa PF.3”

Malunde

Read more


Habari Zinazoendana

5 months ago

Zanzibar 24

Waziri wa mambo ya ndani Mwigulu Nchemba alamba PHD

The post Waziri wa mambo ya ndani Mwigulu Nchemba alamba PHD appeared first on Zanzibar24.

 

2 years ago

Michuzi

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI MWIGULU NCHEMBA ZIARANI MKOA WA KIGOMA

Na Abel Daud wa Globu ya Jamii, KigomaWaziri wa Mambo ya ndani Mh.Mwigulu Nchemba ameutaka Mkoa wa Kigoma kuendelea kukusanya silaha haramu zinazoingia nchini na kufanya shughuli za kihalifu.Hayo ameyasema wakati akizungumza na kamati ya ulinzi na usalama ya Mkoa wa Kigoma pamoja na maofisa mbalimbali wa Mkoani hapa katika ziara aliyoifanya hii leo ambayo inatarajiwa kumalizika hiyo kesho.Akisoma taarifa kwa Waziri Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kigoma ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Kigoma Bw.Samson...

 

2 years ago

Michuzi

ZIARA YA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI MH:MWIGULU NCHEMBA KISIWANI UNGUJA


 Mwigulu akisalimiana na baadhi ya viongozi wa jeshi la polisi waliopo visiwani Zanzibar. Waziri wa mambo ya ndani ya nchi akiongoza kikao cha ndani kilichohusisha viongozi wa juu wa jeshi la polisi Zanzibar. Mh:Mwigulu Nchemba akikagua moja ya majengo chakavu yanayohitaji ukarabati ndani ya eneo la Makao makuu ya jeshi la polisi Unguja.Mwisho,Waziri wa mambo ya ndani amekutana na askari wa jeshi la polisi waliostaafu kwaajili ya kusikiliza ushauri wao katika kuimarisha utendaji kazi wa...

 

2 years ago

MillardAyo

PICHA 7: Kitwanga alivyokabidhi ofisi kwa Waziri wa mambo ya ndani Mwigulu Nchemba

????????????????????????????????????

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba amekabidhiwa ofisi rasmi na  aliyekuwa Waziri wa Wizara hiyo, Charles Kitwanga kwenye ofisi ya Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, jijini Dar es salaam leo. ULIKOSA HII YA SIKU WAZIRI KITWANGA AKIJIBU MASWALI BUNGENI NA KUDAIWA AMELEWA? UNAWEZA KUANGALIA VIDEO HAPA CHINI Unataka kutumiwa MSG […]

The post PICHA 7: Kitwanga alivyokabidhi ofisi kwa Waziri wa mambo ya ndani Mwigulu Nchemba appeared first on MillardAyo.Com.

 

1 year ago

Malunde

KAULI YA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI MWIGULU NCHEMBA KUPOTEA KWA ROMA MKATOLIKI

Usiku wa April 5 2017 taarifa za kukamatwa kwa msanii wa hip hop Roma Mkatolikia zilianza kuenea katika mitandao ya kijamii kwa kuandikwa kuwa Roma Mkatoliki na Moni wakiwa studio za Tongwe Records walikuja kukamatwa na watu wasiojulikana na kuwapeleka kusikojulikana.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mwigulu Nchemba ambaye ndio anahusika na usalama wa raia, ametumia ukurasa wake wa instagram kuonesha kuguswa na tukio la kutekwa kwa Roma Mkatoliki na Moni, Waziri Nchemba ameeleza kuwa...

 

7 months ago

Malunde

CHADEMA WAMPINGA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI MWIGULU NCHEMBA KUHUSU TUNDU LISSU

Chadema imesema haitabadili msimamo wake wa kutaka wataalamu kutoka nje kuchunguza shambulio dhidi ya mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu.
Juzi, Waziri wa Mambo ya Ndani, Mwigulu Nchemba alisema hakuna haja ya kuhangaika kutafuta wachunguzi kutoka nje kwa kuwa mazingira watakayofanyia kazi ni yaleyale na hivyo kuitaka Chadema kuviamini vyombo vya ndani vya uchunguzi.
Lakini jana, Chadema imeeleza kuwa haioni kinachoendelea na hata kama ni mazingira yaleyale, wachunguzi kutoka nje ndiyo...

 

2 years ago

Dewji Blog

Breaking News: Rais Magufuli amteua Mwigulu Nchemba kuwa Waziri wa Mambo ya ndani

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 11 Juni, 2016 amefanya mabadiliko madogo katika Baraza la Mawaziri ambapo amemteua Mbunge wa Buchosha Dkt. Charles John Tizeba kuwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi.

Kufuatia uteuzi huo, aliyekuwa Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba ameteuliwa kuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

Mhe. Mwigulu Lameck Nchemba anachukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi...

 

2 years ago

CCM Blog

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI MWIGULU NCHEMBA AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA CHINA HAPA NCHINI

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (katikati), akimkaribisha Mwakilishi Mkazi wa Jamhuri ya Watu wa China, Lin Zhiyong, kwa ajili ya mazungumzo juu ya  masuala ya ushirikiano katika sekta ya ulinzi na  usalama kati ya Tanzania na China. Kulia ni Balozi wa China nchini Tanzania, Dkt. Lu Youqing. leo, jijini Dar es Salaam. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba(kushoto), akimsikiliza Balozi wa China nchini Tanzania Dkt. Lu Youqing (katikati), wakati wa mazungumzo juu...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani