JUKWAA LA HAKI JINAI LATEMBELEA MAGEREZA NA VITUO VYA POLISI IRINGA,NJOMBE NA RUVUMA

Timu ya wataalamu kutoka Jukwaa la Haki Jinai nchini ikiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome inatembelea Magereza katika mikoa ya Iringa, Njombe  na Ruvuma ili kujionea changamoto zinazowakabili  wafungwa na mahabusu nchini katika kupata haki zao wakiwa vizuizini au magerezani na kuangalia namna ya kuzitatua. Akizungumza katika siku ya kwanza ya ziara hiyo mjini Iringa, Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof.Mchome amesema utekelezaji wa mradi huo pia unalenga kuziongezea  uwezo taasisi zinazoshughulika na utoaji haki na kusimamia haki za binadamu nchini ili ziweze kutoa huduma stahiki kwa watanzania ya utoaji haki na ulinzi wa haki za binadamu. Amesema ni matarajio ya Serikali kuwa ziara hiyo itawezesha taasisi zinazosimamia utoaji haki nchini kuchukua hatua katika kuhakikisha wafungwa na mahabusu wanapata haki zao kwa wakati.

Ujumbe huo wa jukwaa  la haki jinai unamshirikisha Mkurugenzi wa Mashitaka nchini (DPP) Biswalo Mganga, Naibu Mkurugenzi Upelelezi Makosa ya Jinai nchini (DDCI) Charles Kenyela, Ofisi ya Msajili wa Mahakama ya Tanzania, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Magereza na Jeshi Polisi.

Ujumbe huo umetembelea Gereza la wilaya ya Iringa,  Selo iliyoko katika kituo cha Polisi Iringa mjini, Gereza la Wilaya Njombe na selo iliyoko katika kituo cha Polisi Njombe na kujionea mazingira yaliyopo na kusikiliza kero zinazowakabili wafungwa na mahabusu walioko katika vituo hivyo vya polisi na magereza hayo katika kupata haki zao.

Wananchi hao waliomba kupata msaada katika maeneo ya kufikishwa mahakamani kwa wakati, uchunguzi wa tuhuma zinazowakabili kufanywa kwa wakati, kupatiwa nakala za hukumu kwa wakati   ili wawahi muda wa kukata rufaa na mashitaka yao kusikilizwa kwa wakati ikiwa ni pamoja na kusikilizwa kwa rufaa zao.  Ziara hiyo ni utekelezaji wa mradi wa upatikanaji haki na ulinzi wa haki za binadamu nchini unaoendeshwa kwa pamoja kati ya Serikali ya Tanzania na Mpango wa Maendeleo wa Umoja wa Mataifa –UNDP.

 Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Christopher Ole Sendeka akiongea na wataalamu wa Jukwaa la haki jinai nchini ambao walioongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof Sifuni Mchome  walipoanza ziara ya kutembelea magereza na vituo vya polisi mkoani humo.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Amina Masenza akiwakaribisha ofisini kwake  wataalamu wa Jukwaa lahaki jinai nchini ambao walioongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof Sifuni Mchome mjini Iringa walipoanza ziara ya kutembelea magereza na vituo vya polisi mkoani humo juzi.
 Wataalamu kutoka taasisi zinazosimamia utoaji haki nhini ikiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof Sifuni Mchome wa pili kulia waliosimama mbele wakiwa na Mkuu wa Mkoa wa Njombe Mhe. Christopher Ole Sendeka wapili kushoto waliosimama mbele Wataalamu hao walikwenda kumsalimia Mkuu wa Mkoa  wa Njombe kabla ya na kutembelea gereza la wilaya ya Njombe na kituo cha Polisi cha wilaya hiyo na kuzungumza na wafungwa na mahabusu walioko kizuizini katika maeneo yao na kutatua changamoto zinazowakabili. Timu ya wataalamu kutoka Jukwaa la Haki Jinai nchini ikiongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. SifuniMchome katika picha ya pamoja na askari magereza nje ya gereza la wilaya ya njombe baada ya kutembelea gereza hilo na kuzaungumza na wafungwa na mahabusu walioko katika gereza hilo mjini Njombe janailikujionea changamoto zinazowakabili  wafungwa na mahabusu nchini katika kupata haki zao wakiwa vizuizini au magerezani na kuangalia namna ya kuzitatua. Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Amina Masenza (katikati waliosimama mbele) katika picha ya poamoja na wataalamu wa Jukwaa la haki jinai nchini ambao walioongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof Sifuni Mchome baada ya kutoka kumsalimia Mkuu huyo wa mkoa Ofisini kwake mjini Iringa walipoanza ziara ya kutembelea magereza na vituo vya polisi mkoani humo juzi.

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

4 months ago

Michuzi

JUKWAA LA HAKI JINAI LAFANYA ZIARA MKOANI RUVUMA

Timu ya wataalamu kutoka Jukwaa la Haki Jinai iliyoko mkoani RUVUMA imetembelea magereza ya KITAI na MBINGA pamoja na Kituo cha Polisi Wilaya ya MBINGA. 
Timu hiyo ya wataalamu inayoongozwa na Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome imekutana na kuzungumza na mahabusu na wafungwa walioko katika magereza hayo kuhusiana na changamoto wanazokabiliana nazo wakiwa ndani ili kuweza kupata haki zao kwa wakati.
Timu hiyo imetumia nafasi hiyo kutoa huduma na ushauri kwa wafungwa na...

 

4 years ago

Michuzi

VIONGOZI NA WATENDAJI WAKUU WA TAASISI ZINAZOUNDA JUKWAA LA HAKI JINAI WAKUTANA MJINI BAGAMOYO KWA MKUTANO WA SIKU MBILI.

Habari katika Picha:Viongozi na Watendaji wakuu wa Taasisi zinazounda Jukwaa la  Haki Jinai wakiwa katika Picha ya pamoja,mara baada ya ufunguzi wa  Mkutano wa siku mbili. Mkutano huo umefunguliwa na Mkurugenzi Mkuu wa Uendeshaji wa Mashtaka (DPP) Dr E.Feleshi.Pamoja na mambo mengine mkutano huo utaangalia Haki za Watoto walio katika Mgongano na Sheria za Jinai.Walio kaa Kwenye viti,wa kwanza kushoto ni Kamishna Jenerali wa Magereza (CGP) John C Minja, wa pili kushoto ni Mkrugenzi wa...

 

12 months ago

Michuzi

TPDC WATOA MAFUNZO KWA WAANDISHI WA HABARI WA MIKOA YA IRINGA,NJOMBE NA RUVUMA

Na Fredy Mgunda,Iringa.
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mh. Richard Kasesela amelipongeza Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kwa kuendesha mafunzo maalum kwa waandishi wa Habari wa Mikoa ya Arusha, Iringa,Ruvuma na Njombe ameyasema hayo wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya siku moja ambayo yamefanyika mwezi wa pili tarehe ishirini na moja mwaka huu(21 / 02 /2017) katika ukumbi wa Chuo cha VETA mkoani Iringa.
“Ingawa mafunzo ni mafupi lakini napenda kulipongeza Shirika letu la Mafuta la Taifa...

 

3 years ago

Vijimambo

MWIGULU NCHEMBA ADHAMINIWA MKOA WA NJOMBE,RUVUMA NA IRINGA,WANACCM WAENDELEA KUONESHA IMANI NAYE

Mwigulu Nchemba akizungumza na WanaCCM waliojitokeza kumdhamini Mkoani Iringa.Kubwa ameendelea kusisitiza kuwa awamu ya tano ni awamu ya Kufanya mabadiliko kwa Vitendo kwenye Utendaji kazi,Kukomesha mazoea kwenye Utumishi wa Umma.Mwigulu Nchemba akisaini kitabu kuthibitisha kuwa amefika Mkoani Iringa kwaajili ya kutafuta wadhamini.Mwigulu Nchemba akisalimiana na Wadhamini wake kuelekea Safari ya Urais Mwaka 2015 kuwania kuteuliwa ndani ya CCM awezekupeperusha Bendera ya Chama.Mwigulu Nchemba...

 

1 year ago

Michuzi

DK MEDARD KALEMANI AFANYA ZIARA MIKOA YA RUVUMA, NJOMBE, IRINGA NA MOROGORO KUKAGUA MIRADI YA UMEME

 Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani (katikati) akizungumza na wananchi wa Kata ya Ulaya wilayani Kilosa, Mkoa wa Morogoro, kuhusu utekelezaji wa miradi ya umeme vijijini (REA II na REA III), wakati wa ziara yake wilayani humo hivi karibuni. Diwani wa Kata ya Ulaya wilayani Kilosa, Matokeo Kenedi (kushoto), akimweleza Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dk Medard Kalemani (kulia) mahitaji ya umeme kwa wananchi wa Kata yake, wakati wa ziara ya Naibu Waziri kukagua miradi ya...

 

11 months ago

Michuzi

MASAUNI AWATAKA MAAFISA MAGEREZA KUONGEZA KASI YA UZALISHAJI NCHINI, AFUNGUA MKUTANO WA WAKUU WA VITUO VYA MAGEREZA TANZANIA BARA, JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (aliyevaa suti) akiongozwa na Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini, (CGP) Dkt. Juma Malewa (mbele), kuingia ukumbini kwa ajili ya kufungua Mkutano wa Maafisa Waandamizi kutoka Makao Makuu ya Jeshi la Magereza pamoja na Wakuu wa Vituo vya Magereza Tanzania Bara, uliofanyika Bwalo Kuu la Maafisa wa Jeshi hilo, Ukonga, jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake ya ufunguzi, Masauni aliwataka Maafisa wa Jeshi hilo,...

 

2 years ago

Michuzi

Waziri wa Mambo ya Ndani auagiza uongozi wa Magereza ya mkoa wa Iringa kuanza mchakato wa kuhamisha magereza ya Manispaa ya Iringa

WAZIRI wa mambo ya ndani ya nchi, Mwigulu Nchemba ameagiza uongozi wa Magereza ya mkoa wa Iringa kuanza mchakato wa kuhamisha magereza ya Manispaa ya Iringa ili eneo hilo kutumika kupanua Hospitali ya rufaa ya mkoa wa Iringa.

Nchemba ametoa agizo hilo leo baada ya kutembelea eneo hilo ambalo limekuwa likiombwa kwa muda mrefu na viongozi wa serikali ya mkoa wa Iringa ili litumike kwa ajili ya matumizi ya Hospitali hiyo ya Rufaa ya mkoa wa Iringa .
Akizungumza baada ya kutembelea eneo la...

 

2 years ago

Michuzi

JAJI MKUU WA TANZANIA AFANYA ZIARA YA KUTEMBELEA MAHAKAMA KATIKA MIKOA YA IRINGA, NJOMBE NA RUVUMA, AISIFU MAHAKAMA KANDA YA SONGEA KWA KUFANYA VIZURI.

Na Mwandishi Wetu, Mahakama ya Tanzania.
Mahakama ya Tanzania ni moja kati ya Taasisi iliyopo katika mchakato wa kuboresha huduma zake. Katika kufanikisha azma hii jitihada/maboresho mbalimbali yameendelea kufanyika ili kuwezesha Mhimili huu muhimu kuwa na mazingira rafiki ya utoaji haki kwa wananchi.

Hivi karibuni Jaji Mkuu wa Tanzania, Mhe. Mohamed Chande Othman alitembelea katika Mahakama za mikoa ya Iringa, Njombe pamoja na Ruvuma, lengo la ziara ikiwa ni kukagua na kujionea hali ya...

 

3 months ago

Channelten

Msaada wa vifaa tiba kwa Polisi, Ni kusaidia vituo vya Afya 26 vya polisi

SIRRO

Jeshi la Polisi nchini limepokea msaada wa vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi bilioni 2 kwa ajili ya hospitali na vituo vya afya 26 vinavyomilikiwa na jeshi hilo nchini.

Msaada huo umetolewa na Marekani kupitia shirika lake la misaada ya USAID ni Vitanda vya hospitali, Vifaa vya upasuaji, mashine za Ultra sound na vifaa vinavyohusika kwenye chumba cha upasuaji.

Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP SIMON SIRRO amepokea msaada huo na kueleza kuwa utapunguza tatizo la vifaa tiba kwenye...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani