Jumuiya ya Watanzania wa London (Tanzania Association- London) yapata viongozi

Jumuiya ya Watanzania wa London (Tanzania Association- London) imepata viongozi baada ya kufanyika uchaguzi huru wa kidemokrasia siku ya Jumamosi ya tarehe 15 July 2017 katika jiji la London. Mgeni rasmi alikua ni Mwenyekiti wa TZUK (Great Britain & Northern Ireland) Ndg. Abraham Sangiwa.Viongozi waliochaguliwa ni: Dada Lynne Kimaro (Mwenyekiti), Ndg. Omwami George Ndibalema (Makamu Mwenyekiti), Ndg. Lazaro Matiku (Katibu), Dada Halima Yusuph (Naibu katibu), na Dada Edith Kimaro (Mweka Hazina)Kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania Diaspora Community United Kingdom of Great Britain & NI, kila jumuiya za matawi zinatakiwa kuchagua wawakilishi wawili (2) katika Baraza (The Council) la Tanzania Diaspora UK. Wajumbe watachaguliwa hapo baadae. Napenda kutumia nafasi hii kuwapongeza sana katika hatua hio kubwa na ya muhimu katika ujenzi wa Umoja wa Watanzania UK  Asanteni, Uongozi Tanzania Diaspora Community/Association United Kingdom of Great Britain & Northern IrelandMwenyekiti wa TZUK (Great Britain & Northern Ireland) Ndg. Abraham Sangiwa (wa pili kulia) akiwa na uongozi wa Jumuiya ya Watanzania wa LondonMwenyekiti wa TZUK (Great Britain & Northern Ireland) Ndg. Abraham Sangiwa akimpongeza Mwenyekiti wa Jumuiya ya Watanzania London Dada Lynne KimaroMwenyekiti wa TZUK (Great Britain & Northern Ireland) Ndg. Abraham Sangiwa akiwa katikia picha ya pamoja na wanachama na uongozi wa Jumuiya ya Watanzania London. Picha kwa hisani ya  TZUK

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

1 year ago

Mwananchi

KUTOKA LONDON : Jumuiya ya Waingereza na watanzania ilivyowakaribisha mabalozi wapya London

Chumba kimejazana watu utadhani senene. Wazungu, Waafrika na Wahindi. Vijana kwa wazee. Baadhi ya vikongwe waliopitisha miaka themanini walifanya kazi zamani Tanzania.

 

1 year ago

Mwananchi

Waziri Mkuu awaeleza Watanzania London lisilo kawaida kusemwa na viongozi

Tumezoea kusikia wanasiasa wakija, tunapiga makofi, anatabasamu, akipunga mikono. Anatuashiria tukae. Anapiga porojo zake, weeee. Tunamshangilia. Walio karibu naye zaidi wanakenua meno wakijipendekeza pendekeza. Taswira hii iko kila mahali duniani. Siasa na uongozi vimegeuzwa mchezo wa kuigiza. Tamthiliya inayodhalilisha na kuhadaa wananchi. Kiasi kikubwa cha wanadamu duniani ni maskini wanaohangaika kama sisimizi waliomwagiwa mafuta ya taa. Wanasiasa wajibu na kazi yao kuhahakikisha hali...

 

3 years ago

TheCitizen

A CHAT FROM LONDON: London welcomes, supports anti-FGM push in Tanzania

>Wednesday, October 15, 2014...A tiny delegation of well educated women; modest and intelligent, will be welcomed into one of the most powerful rooms in the northern hemisphere. First is Mrs Rhobi Samwelly (pictured), mother of four children, hailing from Butiama, Mara Region.

 

2 years ago

TheCitizen

A CHAT FROM LONDON: Wet afternoon, junkie hobbling on a London street

It is a cold wet winter afternoon, a few days after the Paris and Bamako terrorist attacks. As I stroll down a major street in East London, a man is melodically hollering:“Evening Standard! Evening Standard!”

 

2 years ago

Mwananchi

KUTOKA LONDON: Fab Moses- Mtabiri wa London aliyetunga wimbo wa kushinda Magufuli

Wakati kampeni za uchaguzi zikiendelea miezi kadhaa iliyopita, Mtanzania mmoja mkazi London alikuwa na mtazamo tofauti. Mwanamuziki na mcheza sarakasi huyu  anaitwa Fab Moses.

 

2 years ago

Mwananchi

KUTOKA LONDON : Wakenya wakutana London kuitangaza nchi yao inayozidi kupendwa majuu

“Kenya and Friends in the Park” – yaani Kenya na marafiki zao kukutana kiwanjani ilihamasishwa na dada mcheza ngoma, mwanatamthiliya na mwanahabari Lydia Olet. Bango lenye taswira ya Simba na Mmasai aliyevaa lubega la miraba; kifua wazi na mkuki mkononi. Maneno yalisema burudani itakuwa Jumamosi tarehe 29 Agosti kuanzia tano asubuhi hadi mbili usiku. Kiingilio bure.

 

1 year ago

TheCitizen

A CHAT FROM LONDON: London man, his dogs and the midnight conversationalist

The man ties his three dogs under the lamppost. It is normal in London. Dogs rarely roam around without a leash.

 

10 months ago

Raia Mwema

Naona bora tubadilishe Bk kuwa UK na mji wa Bukoba uitwe London au hata half London ili watu wajali

Kwa Waziri wa Mikiki na Makeke,

Uzitoni Street,

Bongo.

 

Mpenzi wangu Frank,

U hali gani switiii?  Mzima kabisa?  Mimi kawaida ni mzima ndani ya nchi ya wazimu. 

Na kweli ni wazimu.  Juzi bosi alirudi na kumkuta Binti Bosi anataka kumwuliza kuhusu hali ya Bukoba.

‘Inakuhusu nini?’

‘Jamani baba, si ni Watanzania wenzetu.  Tena darasani kwangu kuna vijana watatu wanaotoka huko.  Wanahaha kwa wasiwasi.’

‘Sawa lakini yaliyotokea yametokea.  Inasikitisha sana lakini...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani