KAMPENI UCHAGUZI TFF ZAENDELEA, WALIOKATWA WAREJESHWA

Kampeni za wagombea mbalimbali katika Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika shirikisho, zinaendelea. Kwa mujibu wa kanuni 11.10 ya uchagizi wa TFF, kampeni hizo za wiki moja hadi Ijumaa wiki hii ambako Uchaguzi Mkuu utafanyika Agosti 12, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Hosteli ya Mtakatifu Gasper mjini Dodoma. Kwa mujibu wa kamati hiyo iliyokutana Jumamosi Agosti 5 2017, wagombea ambao wanawania urais ni pamoja na Wallace Karia, Imani Madega, Fredrick Mwakalebela, Ally Mayay, Shija Richard na Emmanuel Kimbe.Katika nafasi ya Makamu wa Rais wanaowania ni Mulamu Ng’hambi, Michael Wambura, Mtemi Ramadhani, Robert Selasela na Stephen Mwakibolwa. Kanda namba 1 ya Mikoa ya Kagera na Geita: waliopitishwa ni Saloum Chama, Leopold Mukebezi na Kaliro Samson wakati Kanda namba 2 inayounganisha mikoa ya Mara na Mwanza wamo Aaron Nyanda, Vedastus Lufano, Samwel Daniel na Ephraim Majinge. Kanda namba 3 (Mikoa ya Shinyanga na Simiyu) wanaowania nafasi hiyo ni Stanslaus Nyongo, Bannista Rogora na Mbasha Matutu ilihali Kanda namba 4 (Mikoa ya Arusha na Manyara) waliopitishwa ni Omar Walii, Sarah Chao na Peter Temu.  Katika Kanda namba 5 inayounganisha mikoa ya Kigoma na Tabora waliopitishwa ni John Kadutu, Issa Bukuku, Abubakar Zebo na Francis Michael wakati Kenneth Pesambili na Baraka Mazengo – wote wamepitishwa kuwania ujumbe kupitia Kanda namba 6 yenye mikoa ya Katavi na Rukwa. Kanda namba 7 inayounganisha mikoa ya Mbeya na Iringa waliopitishwa ni Elias Mwanjala, Cyprian Kuyava na Erick Ambakisye huku Kanda namba 8 yenye mikoa ya Njombe na Ruvuma waliopitishwa ni James Mhagama, Golden Sanga, Vicent Majili na Yono Kevela.  Kanda namba 9 Lindi na Mtwara ambako Athumani Kambi na Dunstan Mkundi (wamepitishwa) wakati Kanda namba 10 Dodoma na Singida waliopitishwa ni Hussein Mwamba, Steward Masima, Ally Suru na George Komba. Kanda namba 11, mikoa ya Pwani na Morogoro waliopitishwa ni Charles Mwakambaya, Gabriel Mkwawe na Francis Ndulane wakati Kanda namba 12 Kilimanjaro na Tanga waliopitishwa ni Khalid Mohamed na Godluck Moshi.  Kanda namba 13 Dar es Salaam: waliopitishwa ni Emmanuel Kazimoto, Abdul Sauko, Ayoub Nyenzi, Shaffi Dauda, Peter Mhinzi, Lameck Nyambaya, Mussa Kissoky, Said Tully, Ally Kamtande, Aziz Khalfan, Ramadhani Nassib na Saad Kawemba.  Hii sasa ni orodha ya mwisho baada ya baadhi ya wagombea kufanikiwa kushinda rufaa zao katika Kamati ya Rufaa za Uchaguzi wakipinga kuondolewa na Kamati ya Uchaguzi.  Kamati ya Uchaguzi ilipokea taarifa kutoka Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) na kueleza kuwa iliwakamata viongozi wa soka kutoka mikoa mbalimbali katika mazingira ya kuvunja sheria za nchi na kanuni za uchaguzi.  Kamati iliamua kuwaondoa wagombea hao ambao ni Shafii Dauda wa Dar es Salaam; Banista Rugora wa Shinyanga; Ephraim Majinge wa Mara na Elias Mwanjala wa Mbeya katika kuwania nafasi za Ujumbe wa Kamati ya Utendaji katika uchaguzi ujao wa TFF unatarajiwa kufanyika Agosti 12, mwaka huu kwa ukiukwaji wa Kanuni ya 14 (3) inayozungumzia kampeni kabla ya wakati.

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

2 years ago

Michuzi

KAMPENI JIMBO LA CHALINZE ZAENDELEA

Na John Gagarini, Mandela MGOMBEA Ubunge Jimbo la Chalinze kupitia Chama Cha Mapinduzi Ridhiwani Kikwete amesema kuwa endapo atafanikiwa kuchaguliwa kwenye nafasi hiyo atahakikisha zahanati inajengwa kwenye Kijiji cha Kibaoni ili kuwaondolea adha wananchi wa kijiji hicho. Aliyasema hayo jana kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika Kijijini hapo kata ya Mandela na kusema kuwa ilani ya chama anasema kila kijiji lazima kiwe na zahanati huku kila kata ikitakiwa kuwa na kituo cha afya ili...

 

10 months ago

Michuzi

TFF YAGONGA MWAMBA TRA, OFISI ZAENDELEA KUFUNGWA

TFF YAGONGA MWAMBA TRA, OFISI ZAENDELEA KUFUNGWA


Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.

Shirikisho la Mpira wa Miguu Nchini TFF limeendelea kuwa katika sintofahamu baada ya ofisi zake kufungwa na Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) baada ya kuwa na malimbikizo ya mda mrefu.

Maofisa hao kutoka kampuni ya YONO Auction Mart walipewa mamlaka na TRA ya kufungia ofisi hizo za TFF huku wakiwambia hawaruhusiwi kuendelea na kazi mpaka pale watakapomalizana na TRA.

Kwa mujibu wa deni hilo, TFF wanadaiwa deni...

 

4 years ago

Michuzi

KAMPENI ZA CCM JIMBO LA CHALINZE,ZAENDELEA LEO KATA YA LUGOBA

Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi (CCM),Nape Nnauye akiwahutubia wananchi wa kijiji cha Makombe,Kata ya Lugoba leo Machi 25,2014,wakati wa muendelezo wa Kampeni za Kumnadi Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete (hayupo pichani). Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze,Ridhiwani Jakaya Kikwete akinadi sera zake kwa wananchi wa kijiji cha Makombe,Kata ya Lugoba leo Machi 25,2014,ikiwa ni muendelezo wa Kampeni zake. Mgombea Ubunge...

 

4 years ago

Michuzi

Kampeni za uhamasishaji virutubishi kwenye chakula zaendelea Mkoani Manyara

Mwelimishaji wa masuala ya lishe kutoka mradi wa USAID Tuboreshe,Bi. Sara Luzangi akiongea na wanafunzi wa shule za msingi wilayani Babati mkoani Manyara juu ya umuhimu wa matumizi ya vyakula vilivyowekwa virutubishi katika kampeni za kutoa elimu hiyo zinazoendelea katika wilaya mbalimbali za hapa nchini. Waendeshaji wa kampeni ya kuongeza virutubishi katika chakula kutoka mradi wa USAID Tuboreshe Chakula wakiendesha kampeni ya umuhimu wa virutubishi kwa wanafunzi wa shule za msingi...

 

4 years ago

Michuzi

KAMPENI ZA CCM JIMBO LA CHALINZE ZAENDELEA KWA KASI KATIKA HATUA ZA LALA SALAMA

Mgombea Ubunge katika Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Chalinze kwa tiketi ya CCM,Ridhiwani Jakaya Kikwete akizungumza na vijana wajasiriamali wa UVCCM,Mara baada ya kufungua Shina la vijana la mshikamano Visakazi,lililopo kwenye kata ya Ubena Zomozi leo April 1,2014. Katibu wa NEC,Itikadi na Uenezi CCM,Nape Nnauye akizungumza jambo na mmoja wa wafugaji wa Kimasai wa Tawi la Kivuga kata ya Ubena Zomozi wakati wa Mkutano wa Kampeni za CCM za Ubunge jimbo la Chalinze,leo April 1,2014. Mgombea...

 

2 years ago

Channelten

Uchaguzi wa Rais na Wabunge C.A.R Kura zaendelea kuhesabiwa

_88263007_88263005

Maafisa wa uchaguzi wanaendelea kuhesabu kura baada ya Jamhuri ya Afrika ya Kati baada ya kukamilisha duru ya pili iliyocheleweshwa ya uchaguzi wa rais na wabunge.

Uchaguzi huo unatarajiwa kurejesha amani baada ya machafuko makubwa ya kidini kuwahi kushuhudiwa nchini humo tangu uhuru mwaka 1960.

Upigaji kura umefanyika jana chini ya ulinzi mkali huku maelfu ya vikosi vya kulinda amani vya Umoja wa Mataifa wakiwa wamesambazwa nchini humo. Taarifa za awali zimesema kuwa hakuna vurugu zozote...

 

4 months ago

Zanzibar 24

Sababu za kufutwa uchaguzi Kenya zaendelea kutajwa

Naibu jaji mkuu nchini Kenya Philomena Mwilu amesema IEBC kushindwa kufuata agizo la mahakama kuhusu madai yaliyoibuliwa na upinzani inaashiria na kuonesha kuwa madai ya udukuzi yalikuwa ni ya ukweli.

Jaji Mwilu amesema mahakama ilikubaliana na madai ya upinzani kuwa matokeo yalitangazwa kabla ya matokeo yote kutoka kwa vituo 40,000 kupokelewa.

“Uchaguzi haukuwa na uwazi na hatukuwa na lingine ila kuufuta,” naibu jaji huyo alisema.

The post Sababu za kufutwa uchaguzi Kenya zaendelea kutajwa...

 

7 months ago

Mwanaspoti

KUELEKEA UCHAGUZI MKUU TFF 2017: Simba yashikilia Umakamu TFF

MWANASPOTI inaendelea kukupa habari za kina kuelekea uchaguzi mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) utakaofanyika Agosti 12 mjini Dodoma. Katika uchaguzi huo nafasi zinazowaniwa ni Rais, Makamu Rais na Ujumbe.

 

7 months ago

Michuzi

UCHAGUZI TFF: IMANI MADEGA ACHUKUA FOMU YA URAIS WA TFF
Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya soka ya Yanga Seneta Imani  Maugila Madega

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.


Mwenyekiti wa zamani wa klabu ya soka ya Yanga Seneta Imani  Maugila Madega amejitokeza kuchukua fomu ya kuwania Urais wa Shirikisho la soka nchini Tanzania TFF.
Madega anakua ni mtu wa pili kuchukua fomu ya Urais baada ya Rais anaemaliza muda wake Jamal Malinzi kuchukua mapema asubuhi ya leo.

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani