Kampuni ya kigeni inapotumia mbinu chafu kuidhalilisha serikali

BIASHARA ya utalii imekuwa na ushindani mkubwa si nje bali hata ndani ya nchi yetu. Ushindani wa kibiashara unadhihirishwa na jinsi ambavyo makampuni ya ndani na nje yanavyopigana vikumbo kutafuta njia na mbinu za kuwapiku washindani wao.

Hilo ni jambo la kawaida kabisa.

Hakika pale ambako hapana ushindani basi ni wazi pia kwamba hapatakuwapo na tija kwani mama wa biashara huria ni ushindani na hilo hakuna wa kubishana. Hata hivyo, kuna mvutano ambao umeanzishwa na kampuni ya Wengert Windrose Safaris Limited, kampuni tanzu ya Friedkin Conservation Fund (Friedkin Family Tanzania) dhidi ya serikali ya Tanzania ambao hauna tija kwa pande zote mbili na ambao unahitaji kumalizwa kwa sababu umeendelea kuikosesha nchi mapato.

Kampuni nyingine ni Tanzania Game Trackers Safaris Limited na Mwiba Holdings Limited.

Kampuni hiyo imeingia katika mvutano na serikali kuanzia mwaka 2013 wakati msimu mpya wa uwindaji wa kitalii ulipoanza, hasa pale walipokosa moja ya vitalu walivyoomba katika utaratibu wa ushindani. Kitalu hicho kilijulikana kwa jina la Lake Natron Game Controlled Area (North). Baadaye kitalu hiki kilikuja kujulikana kama Lake Natron Game Controlled Area (East), ambacho kiligawiwa kwa Green Mile Safari Company Limited baada ya ushindani.

Kitalu hiki cha uwindaji wa kitalii ndicho kimekuwa luba na kufanya mahusiano kati ya kampuni hiyo na serikali kuyumba sana hadi leo takriban miaka mitatu baada ya kampuni hiyo kukosa umiliki katika mchakato wa ushindani. Katika mazingira ya kawaida kampuni ya kigeni inayofanya biashara hapa nchini kwa kutumia sheria za Tanzania haina budi kukubaliana na sheria, na kama kuna kutoridhika na chochote inatakiwa kwenda mahakamani kutafuta haki.

Hata hivyo, baada ya kampuni hiyo kwenda mahakamani mara kadhaa kutafuta haki ya kumilikishwa kitalu hicho ikashindwa kuipata imeamua kuendeleza vita dhidi ya serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia vyombo vya habari. Tena vita hiyo ambayo inaendeshwa kwa kutumia vyombo vya habari vya ndani na nje ya nchi ilihamishiwa hadi katika Baraza la Congress la Marekani.

Shehena ya bangi ikishushwa kwenye gari la Kampuni ya Wengert Windrose Safaris katika kituo cha polisi mkoani Arusha baada ya kukamatwa.

Gari la Kampuni ya Wengert Windrose Safaris likiwa limeshikiliwa kituo cha polisi mkoani Arusha baada ya kukutwa na shehena ya bangi.

Gari la Kampuni ya Wengert Windrose Safaris likiwa limeshikiliwa kituo cha polisi mkoani Arusha baada ya kukutwa na shehena ya bangi.

Baraza la Congress liliaminishwa na wamiliki wa kampuni hiyo ya Wengert ambayo ni ya Kimarekani kwamba Tanzania ni nchi ya hovyo ambayo sheria hazifuatwi hata kidogo.

Kampuni ya Wengert ikafikia hatua ya kuliaminisha Baraza hilo kwamba imetendewa ndivyo sivyo nchini kwa kunyang’anywa kitalu kinyume cha sheria na kwamba kitendo hicho kimefanyika kinyume cha sheria.

Katika kulighadhibisha Baraza hilo Wengert wakadai kwamba imenyang’anywa kitalu na kupewa kampuni nyingine ya kigeni. Hiyo ya kudai kwamba imenyang’anywa kampuni ya Kimarekani na kupatiwa kampuni nyingine ya kigeni ni katika ile ile tabia ya kutaka kuwachochea watunga sheria hao wa Marekani kwa kutumia kigezo cha kwamba wao ni bora zaidi hivyo haiyumkiniki akanyang’anywa Mmarekani halafu apewe mgeni mwingine!

Uchochezi huo ukatumika kwa malengo ambayo kampuni ya Wengert ilitaka.

Baraza la Congress la Marekani lilimwandikia Rais wa Marekani, Barack Obama, barua likiituhumu Idara ya Wanyamapori kwa kuinyanga’anya kampuni ya Wengert kitalu na kukitoa isivyo halali kwa Kampuni nyingine, jambo ambalo halikuwa kweli. Hata hivyo, ukweli ni kwamba kampuni iliyogawiwa kitalu hicho ni ya Kitanzania.

Kampuni hiyo haikutaka kusema ukweli kwamba uamuzi wa kutogawiwa  kitalu ulitokana na maamuzi ya kamati ya ugawaji wa vitalu na kamwe sio kutokana na uamuzi wa Idara ya Wanyamapori.

Vitalu hugawiwa na Waziri wa Maliasili na Utalii baada ya kushauriwa na kamati ya ugawaji wa vitalu. Tuhuma hizo za uongo zilipelekwa mbele ya Baraza la Congress baada ya rufaa yao waliyokata kupinga ugawaji wa vitalu kukataliwa. Ni wazi kabisa kwamba ushawishi uliofanywa kwa Baraza la Congress kwa kutumia mbinu chafu na uongo uliokithiri ulilenga katika kuiweka katika shinikizo serikali ya Tanzania ili iende kinyume na maamuzi yake halali yaliyofanayika kwa mujibu wa sheria.

Wengert walikwenda mahakamani mara kadhaa kupinga maamuzi hayo ya serikali na mara zote wamegonga ukuta. Wiki iliyopita walishindwa kwa mara ya nne mahakamani katika jitihada zao za kutaka kuthibitisha kwa kutumia vielelezo wanavyodai ndivyo halali kwamba kuna makosa katika ugawaji wa vitalu katika eneo la Lake Natron Game Controlled Area. Imefikia hatua kampuni ya Wengert inadai kwamba nyaraka rasmi za Serikali ya Tanzania ni batili na kwamba yenyewe ndiyo ina ramani halali na nyaraka mbalimbali kutoka serikalini.

Inachekesha sana kwamba kampuni ya kigeni inakuja nchini na kuamua kupambana na serikali yetu kwa ajili ya kulazimisha umiliki wa kitalu cha uwindaji wa kitalii kwa kila njia ikiwa ni pamoja na kuvifunga midomo vyombo vya habari kwa kutumia mbinu chafu. Kwa taarifa rasmi za kiserikali ni kwamba kampuni hiyo, pamoja na kampuni nyingine za Friedkin Family Tanzania, zimekuwa zikiwatumia watumishi wake na mawakala mbalimbali kufanya vitendo vya hujuma dhidi ya makampuni mengine ya uwindaji wa kitalii.

Aidha, kampuni hiyo pia imekuwa ikiendesha kampeni chafu dhidi ya viongozi mbalimbali wa Wizara ya Maliasili na Utalii kwa lengo la kutaka kuthibitisha kwamba viongozi hao wanafanya maamuzi yasiyozingatia sheria. Ukweli ni kwamba kampuni hizo ndiyo zimekuwa mstari wa mbele kutotii sheria za nchi.

Tabia hii ilishamiri sana wakati wa awamu iliyopita. Kumekuwapo na jitihada za kuitaka kampuni hiyo iendelee kufanya shughuli zake za kitalii katika maeneo halali iliyokabidhiwa na serikali ya Tanzania lakini kila uchao kumekuwapo na tuhuma za kila aina dhidi ya wadau wengine wa sekta ya utalii na serikali kutoka kwa kampuni hizo.

IMG-20150325-WA0002

Shehena ya bangi ikishushwa kwenye gari la Kampuni ya Wengert Windrose Safaris katika kituo cha polisi mkoani Arusha baada ya kukamatwa.

Inasikitisha kwamba kampuni hizo hazioni kwamba ni bora kuachana na malumbano yasiyokuwa na tija na badala yake kuendelea na kazi kama zinapenda kuendelea kuwekeza Tanzania vinginevyo kama zinafikiri zinaonewa ziondoke nchini kwa sababu Tanzania sio nchi pekee ambayo wanaweza kufanya biashara ya uwindaji wa kitalii. Katika kuthibitisha kwamba kampuni hizi hazina hata chembe ya ustaarabu, wamediriki kuwafuata wageni wa kampuni shindani na kuwafanyia fujo jambo ambalo liliripotiwa serikalini.

Aidha, katika kuthibitisha uwezo wake wa kufanya mambo ya hovyo upo ushahidi kwamba watumishi au mawakala wa kampuni hiyo walichimba mashimo katika kiwanja kidogo cha ndege kilichopo kwenye moja ya vitalu vya washindani wao eti tu kwa sababu uwanja huo waliutengeneza wao wakati wanamiliki kitalu hicho.

Swali kubwa linalojitokeza katika vurugu hizi za makampuni haya ya Kimarekani ni kwamba nani anayewachochea na kuwavimbisha kichwa kiasi cha kuidhalilisha serikali ya Tanzania huku wakiwa nchini? Kwa nini hadi leo hatusikii hatua za kinidhamu na hata kisheria dhidi ya kampuni hizii ambayo inaonekana kila uchao yanazidisha mapambano dhidi ya serikali yetu? Tusiruhusu mwekezaji yeyote yule kutupanda kichwani, hata kama anatoka taifa linalojigamba kuwa taifa kubwa duniani! Tunachohitaji kwa wawekezaji ni wao wanufaike na sisi pia tunufaike.

Mtuhumiwa

Mtuhumiwa ambaye ni dereva wa gari hiyo akiwa ameshikiliwa na polisi.

The post Kampuni ya kigeni inapotumia mbinu chafu kuidhalilisha serikali appeared first on DEWJIBLOG.

Dewji Blog

Read more


Habari Zinazoendana

2 months ago

Zanzibar 24

Tundu Lissu kupelekwa mahakamani kwa kuidhalilisha Serikali

Mwenyekiti wa Kampuni ya CZ International & Media Consultant LTD, Cyprian Musiba amesema kuwa yeye pamoja na baadhi ya wanasheria wamekusudia kumfikisha mahakamani Mhe. Tundu Lissu kutokana na hotuba aliyoitoa nchini Kenya kwa vyombo vya habari akiituhumu serikali ya Tanzania kushindwa kufuatilia tukio la yeye kushambuliwa kwa risasi na matukio mengine.

“Tundu Lissu aliutangazia Umma na dunia nzima kwamba Tanzania sasa si salama tena, nchi hii watu wanakufa hovyo hovyo kitu ambacho si cha...

 

3 years ago

Mtanzania

Chadema yabaini mbinu chafu

Pg 5NA SHABANI MATUTU, DAR ES SALAAM

CHAMA Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimeibua tuhuma mpya dhidi ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), kikisema kimebaini shahada zaidi ya milioni mbili za kupigia kura zinazotarajiwa kuingizwa kinyemela katika Daftari la Wapiga Kura na  kugawiwa kwa wana CCM ambao hawakujiandikisha.

Chama hicho kimedai kwamba, mbali na shahada hizo pia wakimbizi zaidi ya 70,000 mkoani Kigoma wameandikishwa katika daftari hilo kwa ajili ya kupiga kura.

Tuhuma  hizo...

 

2 years ago

Mzalendo Zanzibar

Kuna mbinu chafu za ccm hizi hapa .

Viongozi wa Chadema/UKAWA kuweni Makini sana na huu mfumo wa BVR bao la mkono liko njiani kufanikiwa. Mkipuuza mtalia kilio ambacho hatapatikana mtu wa kuwafuta machozi. Vitambulisho fake ni vingi sana na hakuna mashine ya kuvitambua […]

The post Kuna mbinu chafu za ccm hizi hapa . appeared first on Mzalendo.net.

 

11 months ago

Mwananchi

CUF chadai kubaini mbinu chafu dhidi yake

Chama cha Wananchi  (Cuf), kimewaonya vijana waliopangwa kuvamia ofisi ya makao makuu ya chama Buguruni kutothubutu kufanya hivyo.

 

3 years ago

Habarileo

Wafanyakazi kampuni za kigeni wapewa somo

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Meck SadikiWATANZANIA wanaopata ajira katika kampuni mbalimbali za wawekezaji waliopo nchini wametakiwa kubadilika na kuacha tabia ya kutisha wawekezaji hao kwa kutofanya kazi kwa bidii, uadilifu na uaminifu.

 

2 years ago

Mtanzania

Kampuni za kigeni zinavyoshindana kwenye mafuta, gesi Afrika

Maersk-Viking

Na FARAJA MASINDE,

UCHUMI wa Bara la Afrika unatajwa kukua kwa kasi zaidi katika kipindi cha miongo miwili ijayo, hali hiyo inatokana na ongezeko la watu, kukua kwa miji na kuibuka kwa tabaka la kati la uchumi likichagizwa na rasilimali zilizopo.

Kampuni zaidi ya 500 kutoka kwenye mataifa ambayo yanajihusisha na utafiti wa nishati hizo kwa sasa yamejikita zaidi kwenye nchi za Afrika.

Bara la Afrika linaelezwa kuwa awali lilikuwa na tani karibu milioni tisa za mapipa ya mafuta ambayo...

 

2 years ago

Mtanzania

Kampuni za kigeni zinavyoshindana kwenye mafuta, gesi Afrika – 2

South_Asian_Summit_on_Gas_Trading_and_Transportation

Na FARAJA MASINDE,

LEO tunaendelea kuangalia namna ambavyo kampuni za kigeni zinavyogombea mafuta na gesi barani Afrika, ambapo tunaelezwa kuwa asilimia 33 ya mafuta na gesi asilia inayozalishwa Nigeria huuzwa katika Soko la Marekani.

Kwa mujibu wa takwimu zilizopo zinaonyesha kwamba, Nigeria ndiyo nchi pekee ya Afrika yenye kampuni nyingi zainazomilikiwa na wazawa ambazo zinajihusisha na utafiti pamoja na uchimbaji wa mafuta na gesi ambapo kati ya kampuni 70 zilizopo, 38 ni za wazawa ama...

 

2 years ago

Mtanzania

Kampuni za kigeni zinavyoshindana biashara mafuta, gesi Afrika – 4

1395182180739

NA FARAJA MASINDE,

SAFARI ya kampuni hizi zaidi ya 500 zinazowania nishati barani Afrika inaendelea ambapo leo tunaangalia nchini, Morocco, ambako huko kuna kampuni kubwa ya ndani ya Akwa Group S.A. ikiwa na makao makuu yake katika mji wa Casablanca.

Akwa Group ambayo ilianzishwa mwaka 1959Afriquia SMDC, ukiacha masula ya Nishati pia iko kwenye Nyanja za Utalii, hoteli, mawasiliano, majengo makubwa, huku ikiwa na kampuni nyingine zinazojihusisha na mazao ya gesi.

Ukiacha hiyo pia kuna...

 

1 year ago

Bongo5

Kampuni ya China kuboresha miundo mbinu Dodoma

Mwenyekiti wa kampuni ya ujenzi (CRCC) China, Fengchao Meng, ameahidi kuwekeza kwa kuisaidia serikali katika kuboresha miundo mbinu ya mkoa wa Dodoma.

tumblr_m4r9oa3hm01r67lwjo1_1280

Ameyasema hayo Jumatatu hii jijini Dar es Salaam, alipokutana na waziri mkuu, Kassim Majaliwa na kusema kampuni hiyo itaungana na serikali katika kuboresha miundo mbinu ya Dodoma.

“Kampuni yangu itaungana na serikali katika kuboresha makao makuu ya serikali, tunatarajia kutuma wataalamu wetu mkoani Dodoma kuangalia maeneo ya wawekezaji”,...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani