Kampuni ya Reli Tanzania TRL leo imezindua Treni maalum ya kubeba mizigo

1 (1)

Kwa mara nyingine Kampuni ya Reli Tanzania TRL leo imezindua Treni maalum ya kubeba mizigo(BLOCK TRAIN)Itakayokuwa inatumika kusafirisha mizigo mbalimbali iikiwemo mizigo ya Shirika la Mpango wa Chakula Duniani WFP kutoka bandari ya Dar es salaam na kuelekea ghala kuu ya Chakula ya Shirika hilo iliyopo Kizota Mkoani Dodoma.

Akizungumza wakati wa hafla hiyo ya uzinduzi uliofanyika jijini Dar es salaam Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Masanja Kadogosa amesema lengo la uanzishwaji wa Usafirishwaji...

Channelten

Read more


Habari Zinazoendana

3 years ago

Michuzi

UONGOZI WA KAMPUNI YA RELI TANZANIA (TRL) LASITISHA HUDUMA YA TRENI YA JIJI MAARUFU KAMA TRENI YA MWAKYEMBE.

Shimo katika tuta la reli  eneo la Buguruni kwa Mnyamani  ambalo limesababishwa na mvua inayoendelea kunyesha hapa nchini ambapo ukarabati wa eneo hilo unaendelea ili kufanikisha usafiri kurejea hapo kesho.

KAMPUNI YA RELI TANZANIA(TRL) Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) umetangaza kusitishwa huduma ya treni ya jiji maarufu kama Treni ya Mwakyembe awamu ya jioni ya leo Februari 09, 2016. 
Taarifa imefafanua kuwa hatua hiyo imechukuliwa kutokana na maji ya mvua kuchimba shimo kubwa...

 

2 years ago

Ippmedia

Abiria wa treni inayotumia reli ya kati wakwama Morogoro baada ya reli kuzibwa na treni ya mizigo.

Mamia ya abiria wa treni inayotumia reli ya kati kutoka Dar es Salaam kuelekea mikoa ya Dodoma, Tabora, Mwanza, Kigoma na mikoa mingine ya bara wamekwama mjini Morogoro na kushindwa kuendelea na safari, baada ya reli hiyo kuzibwa na treni ya mizigo iliyoharibika katika eneo la Mkata wilayani Kilosa.

Day n Time: jumatatu saa 2:00 usikuStation: ITV

 

2 years ago

Channelten

TRL imezindua rasmi huduma maalumu ya usafirishaji wa shehena kwa njia ya reli kutoka DSM – Burundi

maxresdefault

Kampuni ya Reli Tanzania imezindua rasmi huduma maalumu ya usafirishaji wa shehena kwa njia ya reli kutoka dar es salaam kwenda Burundi kwa kutumia train nzima(Block Train).

 

Akizungumza muda mfupi kabla ya kuanza safari kwa treni hiyo , kaimu mkurugenzi mtendaji TRL Shaban Kiko amesema treni hiyo yenye mabehewa 20 ambazo zina uwezo wa kubeba tani 40 kila behewa, imebeba mzigo wa malighafi ya chuma ambao utasafirishwa kwa siku tatu hadi kuingia mkoani kigoma na siku moja kuwasili mjini...

 

2 years ago

MillardAyo

Asubuhi hii Mafundi wa TRL waliokesha wakitengeneza reli palipoanguka Treni

Shirika la reli Tanzania TRL jana usiku lilifanya mahojiano na AyoTV na millardayo.com ambazo zimeweka kambi kwenye eneo la tukio ilikopata ajali Treni ya abiria ya Express ikitokea Kigoma kuelekea Dar es salaam. Kwenye mahojiano hayo ilitamkwa kwamba reli hiyo iliyoharibika ni lazima itengenezwe ili kuruhusu Treni za Mizigo na abiria ziendelee na shughuli zake kama […]

The post Asubuhi hii Mafundi wa TRL waliokesha wakitengeneza reli palipoanguka Treni appeared first on...

 

4 years ago

Michuzi

TRL YASITISHA SAFARI ZA TRENI YA ABIRIA KWENDA BARA KUANZIA LEO

Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania – TRL umetangaza kusitishwa huduma za safari ya treni abiria kuanzia leo Ijumaa Machi 06, 2015 kufuatia eneo la tuta la reli kati ya stesheni za Kilosa na Kidette kuharibika kwa mafuriko ya mvua inayonyesha hivi  sasa katika eneo hilo.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo Wahandisi na Mafundi wa TRL wako katika eneo la tukio wakifanya tathmini ya jinsi zoezi la ukarabati utakavyofanyika na kwa muda gani.
Ikifafanua zaidi taarifa imeeleza kuwa tathmini ya mafundi hao...

 

3 years ago

Mwananchi

Treni ya mizigo yaanguka, abiria 1,000 wa treni wakwama Dodoma

Zaidi ya abiria 1,000 waliokuwa wakisafiri kwa treni ya Kampuni ya Reli Tanzania (TRL) kutoka jijini Dar es Salaam kwenda mikoani ya Kigoma na Mwanza wamekwama mkoani hapa baada ya treni ya mizigo kuanguka kati ya Kituo cha Itigi na Kitalaka.

 

3 years ago

Dewji Blog

Treni TRL ya Pugu kufanya safari za majaribio bure leo, vituo vipo hapa

Huduma ya 2 ya treni ya Jiji kutoka Pugu kwenda kituo kikuu cha Dar es Salaam kuanza kwa majaribio siku ya leo ya Jumatatu Agosti 01, 2016  kuanzia majira ya saa 12 asubuhi.

Aidha taarifa Uongozi wa Kampuni ya Reli Tanzania (TRL ) inafafanua huduma hiyo ya majaribio ya siku 2 Jumatatu na Jumanne itakuwa bure kwa Wakazi wa vituo husika ambavyo ni pamoja na Pugu stesheni ni Mwisho wa Lami, Gongo la mboto, FFU Mombasa, Banana (Njia panda Segerea) na Karakata.

Vingine ni pamoja na Vingunguti...

 

4 years ago

Michuzi

Abiria wa Treni ya Reli ya Kati wakwama katika Stesheni ya Uvinza,Kigoma leo

 Taarifa iliyoifikia Globu ya Jamii hivi sasa kutoka Mkoani Kigoma,inaeleza kuwa Abiria waliokuwa wakisafiri kwa Treni ya Reli ya Kati kutokea jijini Dar es salaam kuelekea Kigoma wamekwama wa katika Stesheni ya Uvinza mara baada ya kutokea kwa hitilafu kwenye Treni ya mizingo iliyokuwa ikitokea mkoani Kigoma kuelekea Dar es salaam.
Ripota wa Globu ya Jamii ambaye ni mmoja wa abiria hao,amezungumza na stesheni masta wa wa Uvinza na kumueleza kuwa ameshatuma wataalam kwenda eneo la tukio...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani