Kesi ya Mbowe Vs RC Makonda, Sirro na Kamanda Wambura Yaanza Kuunguruma Mahakama Kuu

DAR ES SALAAM: Kesi ya kupinga kukamatwa kwa Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Taifa, Freeman Mbowe dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, Kamanda wa Jeshi la Polisi Dar, Kamishna Simon Sirro na Mkuu wa Upelelezi wa Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Camilius Wambura imeanza kusikilizwa leo katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam.

Katika kesi hiyo, Mbowe anapinga kukamatwa na Jeshi la Polisi Dar kufuatia wito wa RC Makonda aliyemtaja kwa tuhuma za...

Global Publishers

Read more


Habari Zinazoendana

2 years ago

Global Publishers

Sakata la Madawa: Makonda, Kamanda Sirro Kamanda Wambura Waitwa Mahakamani Leo

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam (RC), Paul Makonda, Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu Dar es Salaam (ZPC), Kamishna Simon Sirro na Mkuu wa Upelelezi wa kanda hiyo (ZCO), Camilius Wambura, wamepelekewa barua za mwito za kuwataka wafike Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam leo. Viongozi hao wamepelekewa mwito huo kutokana na kesi ya Kikatiba iliyofunguliwa na Mwenyekiti wa Chadema Taifa, Freeman Mbowe dhidi yao. Mbowe amefungua kesi hiyo kupinga Makonda kumtaja katika orodha yake ya watuhumiwa...

 

2 weeks ago

Michuzi

KESI YA MBOWE NA WENZAKE YAENDELEA KUUNGURUMA MAHAKAMA YA KISUTU

Na Karama Kenyunko, Michuzi TvSHAHIDI wa Tatu katika kesi ya uchochezi inayowakabili viongozi Tisa wa Chadema, ameieleza mahakama kuwa alimshuhudia Mwenyekiti wa Chama hicho, Freeman Mbowe akichukua kipaza sauti  na kutoa tamko la kuwashinikiza  viongozi wenzie na wafuasi wa Chadema kuandamana kuelekea katika ofisi ya Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni kuchukua barua.
Shahidi huyo, E 6976 Koplo Rahimu Msangi, ameeleza hayo leo, Mei 15, 2019 mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba wa ...

 

3 years ago

Channelten

Kesi ya Kubenea na Makonda Mahakama yaanza kusikliza ushahidi

IMG-20151214-WA0051

Mahakama ya Kisutu jijini Dar es salaam imeanza jana imeanza kusikiliza ushahidi wa Kesi inayomkabili Mbunge wa Ubungo Said kubenea dhidi Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Paul Makonda ambapo Kubenea ameshitakiwa kwa kosa la kutoa lugha ya matusi na dharau kwa Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni bwana Paul Makoda Desemba 14 mwaka jana.

Mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Kisutu jijini Dar es salaam Thomas Simba, mpaka sasa mashahidi watatu tayari wameshapanda kizimbani kwa ajili ya kutoa Ushahidi...

 

3 years ago

Zanzibar 24

Mahakama kuu yatupilia mbali kesi ya Mbowe Hotels dhidi ya NHC

Mahakama Kuu ya Tanzania Divisheni ya Ardhi imefuta kesi iliyofunguliwa na Mbowe Hotels Ltd. dhidi ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) ,kuwa Shirika hilo liliitoa kampuni hiyo katika jengo lake jijini Dar es salaam kwa kufuata taratibu zote na kuzishikilia mali zake kihalali. Uamuzi huo umetolewa asubuhi hii na Jaji Sivangilwa Mwangesi, ambaye amesema madai ya Mbowe kwamba aliingia mkataba na NHC hayana mashiko na kwamba mkataba huo haukuwahi kutekelezwa.

Mlalamikaji alikuwa wakidai kwamba...

 

2 years ago

CHADEMA Blog

KESI YA KIKATIBA ILIYOFUNGULIWA NA MH FREEMAN MBOWE IMEENDELEA LEO MAHAKAMA KUU

MAHAKAMA Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imetupilia mbali maombi yaliyowasilishwa na Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe ya kutaka asikamatwe hadi kesi yake ya kikatiba dhidi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda itakapomalizika.Maombi hayo yalitupwa kwa sababu kifungu cha sheria kilichotumika kuyafungua si sahihi na kwamba hutumika pale ambapo sheria

 

1 year ago

Michuzi

UAMUZI KESI MBOWE, WENZAKE KUPELEKWA MAHAKAMA KUU AU LAA KUJULIKANA MEI 15


Na Ripota Wetu, Globu ya jamii
UAMUZI wa kesi inayowakabili viongozi 9 wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo(Chadema) akiwemo Mwenyekiti wao Freeman Mbowe ya kufanya maandamano/mkusanyiko usio halali unatarajiwa kutolewa Mei 15 mwaka huu kama iende Mahakama Kuu au laa.
Hatua hiyo inatokana na mvutano wa hoja za kisheria zilizotolewa jana katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na Wakili wa utetezi, Peter Kibatala kisha kujibiwa leo na Wakili wa Serikali Mkuu, Faraja Nchimbi mbele ya Hakimu...

 

5 years ago

Uhuru Newspaper

Kesi ya Madabida yaanza kuunguruma


NA MWANDISHI WETU
MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu, imeelezwa kuwa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), ilikagua na kugundua dawa za kupunguza makali ya Ukimwi (ARVs) zilizotengenezwa na Kiwanda cha Tanzania Pharmacentical Ltd (TPL), kinachomilikiwa na Ramadhani Madabida kuwa ni bandia.
Hayo yalidaiwa jana na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Osward Tibabyekomya, mbele ya Hakimu Mkazi, Nyigulila Mwaseba, wakati akiwasomea maelezo ya awali Madabida na wenzake.
Madabida, ambaye ni Ofisa...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani