KIGOGO WA TRA KUGOMBEA URAIS TFF

Na Agness Francis, Globu ya Jamii.

Mgombea wa Urais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania (TFF) Shija Richard ameanza rasmi harakati za kufungua kampeni yake ya kuwania nafasi ya urais wa shirikisho hilo hapa nchini. 
Shija amezungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam nia na madhumuni ni kufungua rasmi zoezi la kampeni yake ambayo imejikita  kuzungumzia sera zaidi ya TFF  badala ya  maswala ya kiutendaji
Mgombea huyo amesema kuwa atahakikisha  kunakuwepo na sport Academi katika kanda sita hapa nchini, hii itaongeza vipaji vingi vya kabumbu na  kuwashawishi  wazazi wanapeleka watoto wao wenye vipaji katika  shule hizo za mafunzo ya mpira.
Hata hivyo Shija amesema kumekuwa na tatizo kubwa kwa klabu kukosa kuwa na uwanja, na hilo pia husababisha kutofanya vizuri kimataifa hivyo amesema atahakikisha anatafuta wadhamini kujikita katika swala zima la miundo mbinu ili kila klabu kujengewa kiwanja chake
Amesema ili kucheza mpira kwa amani na utulivu bila kupendelea upande mmoja wa timu  ataweka mkakati kwa kushirikiana na vyama vingine vya michezo duniani kote ili kuleta ufanisi kwenye mchezo huo hapa nchini.
Uchanguzi huo unatarajiwa kufanyika tarehe 12 Agosti  mwaka huu mjini Dodoma ambapo wagombea hao wa  kiti cha urais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania (TFF) ni Shija Richard, Wallace Karia, Iman Madega, Ally Mayay,  na Emmanuel Kimbe.Mgombea urais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini Tanzania (TFF), Shija Richard akizungumza na waandishi wa habari kuhusu namna atakavyofanya kampeni zake alizozizundua leo rasmi na akiahidi maendeleo ikiwemo na kujenga shule za akadeni ya kabumbu katika kanda sita 6 nchini.

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

8 months ago

Michuzi

Kigogo TRA ajitosa urais TFF

MBIO za kuwania uongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), zimezidi kushika kasi baada ya Ofisa wa juu Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Shija Richard kujitosa kuwania urais wa shirikisho hilo.
Shija ambaye ni Meneja ndani ya Mamlaka ya Mapato Tanzania, amechukua fomu hiyo leo Jumatatu katika ofisi za TFF Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, ingawa hakuzungumza lolote kwa maelezo kuwa muda wa kampeni bado. 
“Ni kweli nimechukua fomu kuwania urais wa TFF, wengi mtataka kujua mengi kuhusu mimi na...

 

8 months ago

Mwanaspoti

Kigogo TRA ajitosa kuwania urais wa TFF

Mbio za kuwania uongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), zimezidi kushika kasi baada ya Ofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Shija Richard kujitosa kuwania urais wa shirikisho hilo.

 

8 months ago

Michuzi

ofisa wa TRA kugombea urais wa TFF

MBIO za kuwania uongozi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), zimezidi kushika kasi baada ya Ofisa wa juu Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Shija Richard kujitosa kuwania urais wa shirikisho hilo.Shija ambaye ni Meneja ndani ya Mamlaka ya Mapato Tanzania, amechukua fomu hiyo leo Jumatatu katika ofisi za TFF Uwanja wa Karume, Dar es Salaam, ingawa hakuzungumza lolote kwa maelezo kuwa muda wa kampeni bado. “Ni kweli nimechukua fomu kuwania urais wa TFF, wengi mtataka kujua mengi kuhusu mimi na...

 

8 months ago

Malunde

ZITTO KABWE AGOMA KUGOMBEA URAIS TFF

Ijumaa ya Aprili 21, mwaka huu, gazeti la michezo na burudani nchini, Mwanaspoti, liliandika habari kwenye ukurasa wake wa kwanza yenye kichwa: "Zitto ajitosa Urais TFF, Rage amkubali."

Upande wangu, licha ya kwamba habari hiyo ilichapishwa bila kupata maoni yangu, lakini haikuwa ngeni. Hii ni kwa sababu kabla ya habari hiyo nilikuwa nimeshapokea maombi kutoka kwa watu mbalimbali, wakiwemo viongozi wakubwa wakinitaka nigombee Urais TFF.

Baada ya habari hiyo kuchapishwa na kupata umaarufu...

 

8 months ago

Mwanaspoti

Mwamanda ampa tano Mayay kwa kuamuzi wa kugombea urais wa TFF

Wakati hekaheka za wadau kuchukua fomu za kuwania nafasi mbalimbali katika uchaguzi mkuu wa TFF zikipamba moto, beki wa zamani wa Yanga na Taifa Stars Samson Mwamanda amesema anamuunga mkono Ally Mayay kugombea urais.

 

8 months ago

Mwanaspoti

Mshua wa TRA autaka urais TFF

HARAKATI za kuwania uongozi wa Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF), zimezidi kushika kasi baada ya Ofisa wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Shija Richard, kujitosa kuwania urais.

 

3 years ago

GPL

Vijana wapiganie sasa haki ya kugombea urais, Vijana wasisubiri wazee wawaruhusu kugombea urais

Patrice Lumumba. Julius Nyerere. Na Walusanga Ndaki
IJUMAA moja ya alasiri na kiangazi jijini Dar es Salaam, mwandishi wa makala hii ambaye sasa ana umri wa miaka 60 alikuwa akifanya mzaha wa kupiga danadana mpira wa miguu nje ya ofisi yao kabla ya kwenda kwenye mechi ya soka kati ya timu ya ofisi yake na taasisi moja ya habari. Mwandishi huyo alifanya hivyo kwa umahiri mkubwa kwa kama dakika tano mbele ya wafanyakazi wenzake...

 

4 months ago

Malunde

KIGOGO TRA APANDISHWA KIZIMBANI

Afisa Msaidizi wa Forodha wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Jennifer Mushi amepandishwa kizimbani kwenye Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na kosa la kumiliki mali ambazo ni magari 19 na kuishi maisha ya kifahari kinyume na mshahara wake
Mshtakiwa amesomewa makosa yake mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shahidi na Wakili wa Serikali, Vitalis Peter ambaye alidai mshtakiwa ana makosa mawili.Alidai kuwa kati ya March 21, 2016 na June 30, 2016 katika maeneo tofauti ya Jiji la Dar es...

 

2 years ago

Vijimambo

Mgombea Urais wa Chama cha ACT Mhe Khamis Iddi Lila Arejesha fomu ya Kugombea Urais wa Zanzibar Tume ya Uchaguzi ZEC.

Mgombea Urais wa ACT Mhe Khamis Iddi Lila akiwasili katika viwanja vya Afisi ya Tume ya Uchaguzi ziliko katika hoteli ya Bwawani Zanzibar kwa ajili ya kurejesha famu yake ya kugombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama cha ACT. Mgombea Urais kupitia Chama cha ACT Mhe Khamis Iddi Lila akiwa na mkoba wake wa fomu ya kugombea Urais wa Zanzibar akishindikizwa na Viongozi wa Chama hicho wakiwasili katika Afisi za Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC bwawani Zanzibar. Mgombea Urais wa Zanzibar kupitia Chama...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani