KIGWANGALA : SITAKI KUONA ASKARI MWENYE KITAMBI

WAZIRI wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamis Kigwangala ametuma salamu kwa majangilli wanaojihusisha na uwindaji haramu wa wanyama kwenye Hifadhi za Taifa ikiwemo Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA).


Amesema Serikali na wadau wengine wamejipanga kuhakikisha rasilimali za nchi zinalindwa kwa kudhibiti ujangili wa wanyama na viumbe hai vyote vinavyotokana na maliasili yetu ya asili kwenye hifadhi za Taifa.

Dkt. Kigwangala alituma salamu hizo kupitia Mbio za Ngorongoro Marathon zilizofanyika jana Aprili 21, 2018 kwa kuanzia Lango Kuu la kuingilia Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro na kuishia Uwanja wa Mazingira Bora mjini Karatu mkoani Arusha.

Pamoja na kuwa mgeni rasmi kwenye mbio hizo, Dkt. Kigwangala pia alikimbia kilomita 21 kuanzia saa 3.30 asubuhi na kumaliza saa 6.20 mchana, na kusema hiyo ni ishara tosha ya kujipanga na kukabiliana na majangili. 

Dkt. Kigwangala alisema kwa kumaliza mbio hizo, sio tu anawatishia majangili kuwa yupo vizuri kukabiliana nao, bali anataka askari wote wa wanyama pole wawe wakakamavu na asimuone askari yeyote mwenye kitambi.

“Moja ya malengo ya mbio za Ngorongoro Marathon kwa mwaka huu ni kupambana na ujangili na majangili. Na sikumaliza mbio hizi za kilomita 21 kwa bahati mbaya, bali ni kuwadhihirishia majangili na watu wote wenye nia mbaya na rasilimali zetu kuwa nipo fiti.

“Lakini sio kwa majangili, hata kwa askari wetu, nataka kuwaeleza kuwa kuanzia sasa sitaki kuona askari anakuwa na kitambi. Hatuwezi kupambana na majangili kama askari wetu wana vitambi na wapo legelege… Na nataka kuwaeleza askari kama wanataka twende nao pamoja kwenye hili basi wajipange” alisema Kigwangala.

Dkt. Kigwangala alisema nia nyingine ya NCAA kudhamini mbio hizo ni kutangaza shughuli za utalii ndani na nje ya nchi, kwani anaamini kupitia waandishi wa habari na washiriki wa mashindano hayo kutokea ndani na nje ya nchi, itawezesha kuongeza watalii na hifadhi hiyo kujulikana zaidi.
Naye Rais wa Chama cha Riadha nchini (RT) Anthony Mtaka, alisema moja ya mambo yanayotushinda nchini ni kujitangaza, lakini hapo hapo kushindwa kupenda vya kwetu, kwani pamoja na kuwa Mlima Kilimanjaro upo Tanzania, lakini matangazo yake mengi yapo Kenya.

Mtaka ambaye pia ni Mkuu wa Mkoa wa Simiyu alisema amefurahishwa na uongozi wa NCAA kudhamini mashindano hayo, kwani yatawezesha Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro kufahamika duniani kote.

“Kwenye Serikali ukiwa na mtu kama Dkt. Fred Manongi (Mhifadhi Mkuu wa Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro) mambo yatakwenda vizuri. Tumempa taarifa wiki mbili kabla ya mashindano kumuomba atudhamini, lakini akawa amekubali na mambo yamekwenda vizuri.

“Hiki cha kukubali kudhamini mashindano haya ni kikubwa sana. Sasa anatufanya Watanzania tuanze kujitangaza na kupenda vya kwetu. Hili tatizo la kushindwa kujitangaza ni kubwa ndiyo maana kila siku kuna malalamiko kuwa Kenya wanajitangaza Mlima Kilimanjaro ni wa kwao. Sisi sasa tujitoe na kuonesha rasilimali hizi za utalii ni za kwetu” alisema Mtaka.

Malunde

Read more


Habari Zinazoendana

3 years ago

Michuzi

FAHAMU JINSI KITAMBI KINAVYO PATIKANA NA JINSI DAWA ASILIA YA MKATAA KITAMBI INAVYO ONDOA KITAMBI

Kitambi  ni  ile  hali  ya  tumbo  kuwa kubwa  na  kuchomoza  kwa  mbele  na  wakati mwingine  kufikia  hatua  ya  kunin’ginia. JINSI  KITAMBI  KINAVYO  PATIKANAKwa  mujibu  wa  tafiti  mbalimbali  za  kitaalamu, mwili wa binadamu una seli kati  ya bilioni 50  hadi 200 za mafuta zilizogawanyika katika  sehemu  mbalimbali  za  mwili wa binadamu. Kwa wanawake  seli hizo  zipo sana katika maeneo ya matiti, kwenye  nyonga, kiunoni na kwenye makalio.
Kwa upande  wa  wanaume seli  hizo...

 

2 years ago

Raia Mwema

Trump: Sitaki kuwa mtu mwenye sauti ya upole

WASHINGTON, MAREKANI

DONALD Trump siku ya Jumapili (Novemba 13,2016) aliwataka wafuasi wake kuacha kuwanyanyasa Wamarekani wa jamii za wachache, katika mahojiano yake ya kwanza ya televisheni tangu aukwae urais wa Marekani.

“Nimesikitishwa kusikia hizo taarifa,” Trump alimwambia mwendeshaji wa mahojiano hayo, Leslet Stahl wa kituo cha CBS pale alipomweleza kuwa Walatino na Waislamu wananyanyaswa. “Na ninasema, acheni. Kama kauli yangu inaweza kusaidia, nasema hivi, na nitasema mbele...

 

3 years ago

Vijimambo

JUSSA MWANASIASA MWENYE KUONA MBALI

Na Swahilivilla. Blog Washington  Waziri Majivuno wa Kusadikika alisema: "Hekima ni kitu adimu kupatikana kwa mtu asiye na mvi...". Pia Waswahili wanasema: "Akili ni nywele"Mshitakiwa Karama aliipinga hoja ya Waziri Majivuno kwa kusema: "....Elimu ilipokuwa haijulikani hapa duniani, mvi zilizingatiwa kuwa ni ishara ya hekima..."Nimekuwa nikiyatafakari mafungu hayo matatu ya maneno ili kuona kama yana uhalisia wowote katika maisha yetu ya leo.Pichani Ndugu  Saidi Mwamende akimuliza swali  ...

 

3 years ago

Vijimambo

Mwanaume Mwenye Hips Kubwa na za Kuvutia jitiririshe kuona picha zake na takubari mwenyewe

Uwezi Kuamini Kama Huyu ni Mwanaume wa Shoka Kabisa na sio Shoga ila ana Hips Balaa , Tena hips ambazo Wanawake wengi huzitamani mpaka kwenda kuzitafuta kwa Operation na Kumeza madawa ya kichina...Anaitwa Micah ni Kijana Mwanamuziki wa mwenyeji wa Chicago ..Leo ametupia picha nyingine kwenye account yake ya Instagram kama anavyoonekana hapo juuu kiasi cha Midume mingine kucomment na kuacha number zao za simu ..Check out more cuts…
I know a lot of women out there will be super jealous of this...

 

8 months ago

Malunde

IGP SIRRO : NI AIBU KWA MWANASIASA KUTAKA KUMFUNDISHA KAZI ASKARI....SITAKI MALUMBANO

Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP), Simon Sirro amesema hataki malumbano na hana majibu kuhusu shinikizo linalotolewa na Chadema na familia ya mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kuruhusu vyombo vya nje kufanya uchunguzi wa tukio la kushambuliwa na kujeruhiwa kwa risasi kwa mbunge huyo.

IGP Sirro amesema hayo jana Jumapili jijini hapa, akiwa katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mbeya alipojibu maswali ya waandishi wa habari waliotaka kujua kauli yake baada ya familia ya Lissu na viongozi wa...

 

2 years ago

Mtanzania

Kizimbani kwa kutangaza kuoa askari mwenye KY

mahakamaNA KULWA MZEE, DAR ES SALAAM

MFANYABIASHARA Christon Mbalamula, amefikishwa mahakamani kwa tuhuma za kulidhalilisha Jeshi la Polisi kwa kudai anatangaza ndoa na askari watakaomhudumia kama mume, huku akihoji kama wameshanunua mafuta ya kilainishi maarufu KY.

Mshtakiwa huyo alifikisha katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana akikabiliwa na shtaka la kutumia huduma ya mtandao wa kijamii wa ‘WhatsApp’ kulidhalilisha jeshi hilo.

Akisomewa mashtaka mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Dk. Yohana...

 

4 years ago

Michuzi

Jeshi la Polisi Mkoani Lindi lamsaka askari Mwenye tuhuma za kujihusisha na biashara haramu ya Meno ya Tembo

Jeshi la polisi mkoani Lindi linamtafuta askari wake mmoja mwenye namba F6508 Detective Constable JOSEPH YONA MASANJA mwenye Umri wa miaka 34 mzaliwa wa Wilaya ya ILEMELA Mkoani MWANZA Abae alikuwa akifanya kazi kituo cha polisi KILWA kwa tuhuma za kuhusika na wizi wa vipande 62 vya meno ya tembo vyenye uzito wa kilo 568 yaliyokuwepo kituoni hapo kama Vielelezo.
Hayo yamebainishwa na Kamanda wa polisi mkoa wa Lindi,Kamishna Msaidizi Renatha Mzinga alipokuwa Akitoa taarifa kwa waandishi...

 

11 months ago

Mwanaspoti

Nimesema sitaki, sitaki mkome!

SOSHIOLAITI maarufu nchini Huddah Monroe kafunguka ya moyoni kwa kudai kuwa  amechoshwa na usumbufu wa ma-ex wake wanaoshinda kumtafuta kila wakati kwa kuwa hawataki kukubalia kuwa waliachana.

 

1 year ago

Malunde

ASKARI POLISI MWENYE MKE AJINYONGA TABORA KISA 'MCHEPUKO WAKE' KUWA NA MCHEPUKO MWINGINEAskari aliyekuwa akifanya kazi kituo kidogo cha polisi tarafa ya Igurubi wilayani Igunga mkoani Tabora, amejiua kwa kujinyonga kwa kutumia shuka kutokana na kinachodaiwa kuwa ni wivu wa mapenzi.

Askari aliyejiua ametambulika kwa jina la G.4185 PC Geofrey Mwenda (32 ) ambaye inadaiwa hawara yake mpya ndiyo chanzo cha kuchukua maamuzi ya kutoa uhai wake.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, Hamisi Issa alisema tukio hilo limetokea juzi saa tatu usiku.

Akisimulia tukio hilo, Kamanda Issa alieleza...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani