Kikosi cha Taifa Stars chatajwa, Watano wa Zanzibar Heroes waitwa

KOCHA Mkuu wa timu ya taifa ya soka ya Tanzania, Taifa Stars, Salum Mayanga ameteua wachezaji 23 kwa ajili ya michezo miwili ya kujipima nguvu dhidi ya timu za Algeria na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) mwezi huu, safari hii akimuacha kipa Peter Manyika wa Singida United na kumchukua kinda, Ramadhani Kabwili wa Yanga SC.
Katika mkutano na Waandishi wa Habari leo makao makuu ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Mayanga amewaita kikosini wachezaji wote wanaocheza nje, akiwemo Nahodha mshambuliaji Mbwana Ally Samatta wa KRC Genk ya Ubelgiji.
Amewaita pia Simon Msuva wa Difaa Hassan El Jadida ya Morocco, Hamisi Abdallah wa Tusker FC ya Kenya, Farid Mussa CD Teneriffe B ya Hispania na Thomas Ulimwengu ambaye hana timu kwa sasa.

Kikosi kamili cha Taifa Stars ni; Makipa; Aishi Manula (Simba SC), Abdulrahman Mohammed (JKU), Ramadhan Kabwili (Yanga SC), mabeki; Shomary Kapombe (Simba SC), Hassan Kessy (Yanga SC), Gardiel Michael (Yanga SC), Kelvin Yondan (Yanga SC), Abdi Banda (Baroka FC/Afrika Kusini), Erasto Nyoni (Simba SC).
Viungo ni Hamisi Abdallah (Tusker/Kenya), Mudathir Yahya (Singida United), Said Ndemla (Simba SC), Faisal Salum (JKU), Abdulaziz Makame (Taifa Jang’ombe), Farid Mussa (CD Teneriffe B/Hispania), Thomas Ulimwengu (Huru), Ibrahim Ajib (Yanga SC), Shiza Kichuya (Simba SC),na Mohammed Issa ‘Banka’ (Mtibwa Sugar).
Washambuliaji ni Mbwana Samatta (KRC Genk/Ubelgiji), Simon Msuva (Difaa Hassan El Jadida/Morocco), John Bocco (Simba SC) na Yahya Zayed (Azam FC). Kikosi kinatarajiwa kuingia kambini Machi 18 mwaka huu kwenye hoteli ya SeaScape iliyopo Kunduchi mjini Dar es Salaam kabla ya kwenda Algeria Machi 19.
Taifa Stars inatarajia kucheza michezo miwili ya kirafiki iliyo katika kalenda ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA) mwezi huu, ikianzia ugenini nchini Algeria Machi 22 dhidi ya wenyeji, The Greens kabla ya kurejea nyumbani, Dar es Salaam kuwakaribisha The Leopards Machi 27 Uwanja wa Taifa.
Mara ya mwisho Taifa Stars iliteremka uwanjani Novemba 1 na kulazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na wenyeji, Benin katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa l’Amitie, au Urafiki mjini Cotonou.
Katika mchezo huo uliochezeshwa na marefa wa nchini humo, Ligali Praphiou aliyesaidiwa na Bello Razack na Koutou Narcisse, hadi mapumziko wenyeji The Squirrels, walikuwa mbele kwa bao 1-0.
Bao hilo lilifungwa dakika ya 33 kwa penalti na mkongwe mwenye umri wa miaka 33, Nahodha, Stephane Sessegnon anayechezea klabu ya Montpellier ya Ufaransa.
Hata hivyo, ilikuwa ni penalti ya mashaka, kwani mchezaji aliyeugusa mpira huo kwa mkono alikuwa ni wa Benin, Khaled Adenon lakini refa akadhani ni mchezaji wa Tanzania.
Sessegnon akamtungua kipa namba moja wa Tanzania, Aishi Manula kufunga bao lake la 21 timu ya taifa katika mechi ya 68.
Wachezaji wa Tanzania wakamlalamikia refa kwa kutowapa penalti dakika ya 32 kufuatia, winga Simon Msuva kuangushwa kwenye boksi baada ya kusukumwa.
Kipindi cha pili, Tanzania ilikianza kwa nguvu na kasi zaidi wakishambulia kutokea pembeni na hatimaye kufanikiwa kupata bao la kusawazisha.
Alikuwa ni mshambuliaji wa zamani wa Simba ya Tanzania na Dhofar SC ya Oman, Elias Maguri aliyefunga bao hilo akimalizia krosi ya winga Shiza Kichuya kutoka upande wa kushoto dakika ya 50.
Matokeo haya yanamaanisha Benin ilishindwa kulipa kisasi kwa Tanzania, kwani mara ya mwisho, zilipokutana Oktoba 12, mwaka 2014 Taifa Stars ilishinda 4-1, mabao ya Nahodha wa wakati huo, beki Nadir Haroub ‘Cannavaro’ dakika ya 16, kiungo Amri Kiemba dakika ya 39, Thomas Ulimwengu dakika ya 49 na Juma Luizio, wakati la Benin lilifungwa na Suanon Fadel dakika ya 90.
Kwa sasa Tanzania inashika nafasi ya 146 kwenye viwango vya FIFA, wakati DRC ni ya 39 na Algeria ni ya 60.

The post Kikosi cha Taifa Stars chatajwa, Watano wa Zanzibar Heroes waitwa appeared first on Zanzibar24.

Zanzibar 24

Read more


Habari Zinazoendana

2 years ago

BBCSwahili

Kikosi kipya cha Taifa Stars chatajwa Tanzania

Kocha Mkuu wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars Charles Boniface Mkwasa ametangaza kikosi kitakachomenyana na Harambee Stars ya Kenya.

 

2 years ago

Bongo5

Hiki ndo kikosi kipya cha Taifa Stars chatajwa Tanzania

Kocha Mkuu wa timu ya Soka ya Tanzania, Charles Boniface Mkwasa ameita kikosi cha wachezaji 27 watakaounda Taifa Stars ambacho kinajiandaa kucheza Misri Juni 4, 2016 katika mchezo wa kuwania kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON-2017).

160328085051_taifa_stars_tanzania_640x360_tff

Mkwasa maarufu kama Master, alitangaza kikosi cha timu hiyo leo Mei 18, 2016 mbele ya Kocha Msaidizi, Hemed Morocco na waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume, Ilala...

 

4 months ago

Zanzibar 24

Taifa ya Jang’ombe, JKU zaipiku Yanga ndani ya kikosi cha Zanzibar heroes

Timu ya Taifa ya Jang’ombe na JKU zimeongoza kutoa idadi kubwa ya wachezaji ndani ya kikosi cha timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) baada ya kutoa wachezaji wanne kila timu ndani ya kikosi hicho chenye wachezaji 30.

 

Wachezaji wanne wa Taifa ya Jang’ombe waliyoitwa katika kikosi hicho nahodha wao ambae ni mlinda mlango Ahmed Ali “Salula”, mlinzi wa kati kinda Ibrahim Abdallah, kiungo Abdul Aziz Makame pamoja na mshambuliaji Ali Badru.

 

JKU ambayo nao wametoka idadi ya wachezaji...

 

1 year ago

Zanzibar 24

Kikosi cha Zanzibar kitakachokwenda Cecafa U-17 Uganda chatajwa

Kocha mkuu wa timu ya taifa ya Zanzibar ya vijana chini ya umri wa miaka 17 Abdulmutik Haji “Kiduu” ametangaza kikosi cha wachezaji 26 kitakachokwenda nchini Uganda katika Mashindano ya Vijana U-17 kwa nchi za Afrika mashariki na kati yaliyoandaliwa na CECAFA mwezi Disemba mwaka huu.

 

Mbali na kutangaza kikosi cha wachezaji 26, Kiduu ametaja vipao mbele vyake kwenye timu hiyo ambavyo amezingatia katika kuteua majina ya wachezaji hao.

 

Amesema kitu pekee ambacho wameangalia ni uwezo wa...

 

5 months ago

Zanzibar 24

Kikosi cha zanzibar heroes na zanzibar queens kutangazwa kesho

Kocha Mkuu wa timu ya mpira wa miguu ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) , Hemed Suleiman (Morocco)  kesho Jumapili Novemba 5, 2017 saa 10:00 za jioni atatangaza majina ya wachezaji watakaounda kikosi hicho. Zanzibar Heroes, inajiandaa kushiriki Mashindano ya Chalenj Cup ambayo yanaandaliwa na CECAFA kwa kushirikisha nchi za Afrika Mashariki na Kati na mwaka huu yatafanyika nchini Kenya kuanzia Novemba 25 huku nchi zinazotarajiwa kushiriki ni Kenya, Uganda, Tanzania Bara, Rwanda, Burundi, Sudan,...

 

4 months ago

Zanzibar 24

Kikosi cha Zanzibar Heroes Chaendelea na mazoezi

Kikosi cha timu ya Taifa ya Soka ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) kinaendelea na mazoezi yake kujiandaa na Mashindano ya CECAFA Chalenj CUP yanayotarajiwa kufanyika Novemba 25 na kumalizika Disemba 9, 2017 huko nchini Kenya.

Mazoezi hayo yanayosimamiwa na kocha mkuu wa kikosi hicho Hemed Suleiman (Morocco) yanaendelea kila siku kuanzia saa 2:00 za asubuhi katika uwanja wa Amaan Mjini Unguja.

Mpaka sasa wachezaji waliyoanza mazoezi ni wale ambao vilabu vyao vya Unguja huku ikiwa bado makundi...

 

3 months ago

Zanzibar 24

KIKOSI CHA ZANZIBAR HEROES DHIDI YA KENYA

Kocha wa Mkuu wa timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) Hemed Suleiman “Morocco” ametangaza kikosi chake kitakachocheza leo kwenye Mashindano ya CECAFA SENIOR CHALLENGE CUP kati ya Zanzibar na Kenya katika uwanja wa Kenyatta uliopo Machakos nchini Kenya, pambano litakalopigwa majira ya saa 10:00 za jioni.

ZANZIBAR HEROES

1.  Mohd Abrahman (Wawesha) 18

2.  Ibrahim Mohd (Sangula) 15

3.  Haji Mwinyi Ngwali 16

4.  Abdulla Kheri (Sebo) 13

5.  Issa Haidar Dau (Mwalala) 8

6.  Abdul azizi...

 

2 years ago

Dewji Blog

Kikosi cha Taifa Stars kitakachoshuka dimbani dhidi ya Harambee Stars leo

Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inatarajiwa kushuka dimbani jioni ya leo  kucheza mchezo wa kirafiki wakimataifa na timu ya Taifa Kenya (Harambee Stars)  Jijini Nairobi, Kenya. Awali vikosi vyote vilikuwa kwenye mazoezi yha kujiandaa na mchezo huo.

Vikosi vitakavyoshuka dimbani katika mchezo huo jioni ya leo ni kama ifuatavyo:

The post Kikosi cha Taifa Stars kitakachoshuka dimbani dhidi ya Harambee Stars leo appeared first on DEWJIBLOG.

 

5 months ago

Zanzibar 24

Morocco atangaza kikosi cha Zanzibar Heroes, Ninja wa Yanga ndani

Kocha mkuu wa timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes),Hemed Suleiman (Morocco) ametangaza kikosi cha wachezaji 30 kwa ajili ya maandalizi ya kujiandaa ma Mashindano ya CECAFA Chalenj CUP yanayotarajiwa kufanyika Novemba 25 hadi Disemba 9, 2017 nchini Kenya. WALINDA MLANGO Ahmed Ali “Salula” (Taifa ya Jang’ombe) Nassor Mrisho (Okapi) Mohammed Abdulrahman “Wawesha” (JKU) WALINZI Abdallah Haji “Ninja” (Yanga) Mohd Othman Mmanga (Polisi) Ibrahimm Mohammed “Sangula” (Jang’ombe Boys) Adeyum...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani