KILI STARS YAJIFUA TAYARI TAYARI KUWAVAA NDUGU ZAO ZANZIBAR HEROS

Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’, Ammy Ninje leo Jumanne Desemba 5, 2017 ameanza mazoezi maalumu ya kurekebisha upungufu wote uliojitokeza kwenye kikosi chake katika mchezo uliopita.Stars Mazoezi ya kuruka
Kilimanjaro Stars, ilicheza mchezo wa kwanza dhidi ya Libya Jumapili Desemba 3, mwaka huu kwenye Uwanja wa Kenyatta na matokeo yakawa sare tasa katika mfululizo wa mechi za michuano ya Cecafa.
Katika mazoezi yaliyofanyika Uwanja wa Machakos Academy leo asubuhi, Kocha Ninje ameanza kufanyia kazi namna ya kukaba wakati mpira unapokuwa kwa adui au timu inapopoteza mpira.
Stars Nelson Juma (kulia) na Kelvin Yondani (kulia) wakimzuga Shizza Kichuya.
Baada ya mazoezi hayo Kocha Ninje ameoneshwa kufurahishwa na namna wachezaji walivyoelewa na kufanya kile alichowaelekeza kukifanya ambapo amesema inaonesha dalili nzuri ya kumaliza tatizo hilo lililoonekana kwenye mchezo wa kwanza na Libya.
Katika mazoezi hayo pia walifanya mazoezi ya namna ya kufanya mashambulizi na kupandisha timu.
Stars_ Boniface Maganga (kushoto) akimkabili Amani Kaita (katika) huku Yohanna Mkomola akiwa tayari kutoa msaada.
Kesho wataendelea tena na mazoezi kujiandaa na mchezo unaofuata utakaochezwa Alhamis kwenye Uwanja wa Kenyatta, Machakos dhidi ya timu ya Taifa ya Zanzibar.
Stars_ Elias Maguli (kushoto) akipiga hesabu za kumtoka Jonas Mkude
Kilimanjaro Stars ipo kundi A pamoja na timu za Rwanda, Zanzibar, Libya na wenyeji Kenya ambapo kabla ya michezo ya leo katika kundi hilo – Harambee Stars inaongoza kwa kupata pointi 3 katika mchezo wa mwanzo, wakifuatiwa na Libya na Kilimanjaro Stars wenye pointi 1 kila mmoja wakati Zanzibar na Rwanda wakiwa hawana pointi.

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

2 years ago

Michuzi

TWIGA STARS TAYARI KUWAVAA ZIMBABWE KESHO

Kikosi cha timu ya Taifa ya Wanawake ya Mpira wa Miguu (Twiga Stars), leo kimefanya mazoezi ya mwisho tayari kwa kuwakabili timu ya Taifa ya Wanawake kutoka Zimbabwe (Mighty Warriors) katika mchezo wa kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa ya Afrika kesho Ijumaa katika uwanja wa Azam Complex Chamazi jijini Dar es salaam.
Twiga Stars inayonolewa na kocha mzawa mwanamke, Nasra Juma imekamilisha ratiba yake leo asubuhi kwa kufanya mazoezi mepesi katika uwanja wa Karume ofisi za TFF, huku kocha...

 

2 years ago

Michuzi

MKWASA ASEMA STARS IPO TAYARI KUWAVAA NIGERIA KESHO

Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) inayodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro, Charles Mkwasa (pichani) amesema kikosi chake kipo tayari kwa mchezo wa kesho dhidi ya Nigeria kuwania kufuzu kwa Fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 2017.Akiongea na waandishi wa habari leo katika ukumbi wa mikutano wa TFF uliopo Karume, Mkwasa amesema vijana wake wapo katika hali nzuri kuelekea kwenye mchezo huo wa kesho ambao ni muhimu kwa Taifa Stars.“Tumefanya mazoezi kwa takribani siku kumi,...

 

1 week ago

Zanzibar 24

Zanzibar Heroes wapo tayari kuwavaa Rwanda kesho

Kikosi cha Timu ya Taifa ya Soka ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) kipo tayari kwa ajili ya mchezo wao wa awali kesho Disemba 5 wa kombe la CECAFA SENIOR CHALLENGE CUP dhidi ya Rwanda katika uwanja wa Kenyatta uliopo Machakos nchini Kenya, pambano litakalopigwa majira ya saa 8:00 za mchana.

Zanzibar Heroes wanashuka dimbani huku kikosi kizima kikiwa katika hali nzuri ambapo ripoti ya Kocha imesema kwamba hakuna mchezaji yoyote ambaye ana majeraha yatakayomzuia kucheza mchezo huo muhimu...

 

2 years ago

Vijimambo

TAIFA STARS YAWASILI ZANZIBAR TAYARI KUWAKABILI WAGANDA JUMAMOSI

Kocha wa Timu ya Taifa Stars alipowasili bandarini Zanzibar pamoja na Timu ya taifa Taifa StarsWachezaji wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars walipowasili bandarini Zanzibar wakisubiri usafiri kuwapeleka hoteliniWachezaji wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars wakiwasili visiwani Zanzibar leo tayari kwa mchezo dhidi ya Uganda Jumamosi Uwanja wa Amaan, kuwania kufuzu Fainali za Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN), michuano inayoshirikisha wachezaji wanaocheza ligi za...

 

2 years ago

Global Publishers

Yanga Walivyotua Songea, Tayari Kuwavaa Majimaji

Yanga (1) Yanga (2) Yanga (3) Yanga (4) Yanga (5) Yanga (6)

Wachezaji na viongozi wa Yanga wakati wakiwasili katika Hoteli ya Top One Inn, Songea wakiwa tayari kuwakabili Majimaji.

Mabingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara msimu wa 2015/16 ambao tayari wamekabidhiwa kombe lao Yanga leo watakuwa ugenini katika Uwanja wa Majimaji, Songea mkoani Ruvuma kuwavaa Majimaji.

Mechi hiyo ni mojawapo ya mechi nane zitakazopigwa leo zikiwa ni za kufunga msimu. Mechi nyingine za leo ni pamoja na Simba Vs JKT Ruvu, Azam FC Vs Mgambo JKT, Kagera Sugar Vs Mwadui,...

 

9 months ago

Michuzi

YANGA TAYARI KUWAVAA KILUVYA KESHO KOMBE LA FA

Na Zainab Nyammka, Globu ya Jamii
Msafara wa mabingwa wa watetezi wa ligi kuu Tanzania bara  Yanga SC , umewasili salama jijini Dar es salaam ukitokea Morogoro walipokwenda kucheza na Mtibwa Sugar kwa matokeo ya sare ya 0- 0.
Msafara huo umeelekea moja kwa moja kambini kwa maandalizi ya michezo miwili muhimu itakayofanyika kesho machi 7, 2017 dhidi ya Kiluvya United uwanja wa Taifa na machi 11, klabu bingwa Afrika dhidi ya Zanaco FC.
Timu imeendelea na mazoezi jioni ya leo kwa ajili ya...

 

9 months ago

Michuzi

NGOMA, TAMBWE WAREJEA MAZOEZINI TAYARI KUWAVAA ZANACO

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii
KOCHA Msaidizi wa Yanga Juma Mwambusi amesema kuwa timu inaendelea na mazoezi na wachezaji wote wapo katika hali nzuri na wale waliokuwa majeruhi wamejiunga na wenzao katika mazoezi kuanzia jana tayari kwa kuwavaa Zanaco toka nchini Zambia siku ya Jumamosi..
Mwambusi amesema kuwa Donald Ngoma, Thaban Kamosoku na Amisi Tambwe wameanza mazoezi jana na wenzao ila mpaka sasa bado haijajulikana kama maamuzi ya benchi la ufundi kuwatumia katika mchezo wa Jumamosi wa...

 

10 months ago

Michuzi

AZAM YATIA KAMBI MKOA WA PWANI TAYARI KUWAVAA RUVU SHOOTINGNa Zainab Nyamka, Globu ya Jamii


Timu ya Azam FC, imetia nanga mkoani Pwani, tayari kabisa kwa ajili ya mchezo wa kesho wapinzani wao Ruvu Shooting utakaofanyika kesho katika Uwanja wa Mabatini mkoani humo.

Mchezo huo nunaotarajiwa kupigwa majira ya saa 10 Alasiri utakuwa wanushindani mkubwa sana hasa baada ya Azam kukumbuka sare ya mechi ya awali iliyomalizika kwa goli 2-2.
Kikosi cha Azam FC kimeondoka jana kikiwa na morali kubwa ya kufanya vizuri kwenye mchezo huo kutokana na mazoezi makali...

 

8 months ago

Michuzi

SERENGETI BOYS WAJIFUA TAYARI KUWAVAA BURUNDI LEO UWANJA WA KAITABA, BUKOBA


Timu ya Taifa ya mpira wa miguu ya vijana wenye umri wa miaka 17 maarufu kwa jina la Serengeti Boys Leo Jamatano wamefanya mazoezi kujiweka tayari na mchezo wao wa kesho na Timu ya U17 ya Burundi.Serengeti Boys itakuwa kambini Bukoba hadi Aprili 2, mwaka huu ambako inatarajiwa kucheza michezo miwili ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya timu vijana ya Burundi kwenye Uwanja wa Kaitaba, mjini Bukoba mkoani hapa Kagera. Michezo hiyo itaanza kuchezwa Machi 30, 2017 na kurudiana Aprili mosi, mwaka...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani