- 1 HAYA HAPA MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI APRILI 22,2017
- 2 Mke Wa Chameleon Adai Talaka Mahakamani
- 3 MAGAZETI YA LEO JUMAMOSI APRIL 22,2017
SIKU KAMA YA LEO
Apr 22, 2017POPULAR ON YOUTUBE
Kiongozi mstaafu wa CCM auwawa kwa risasi
WATU wasiojulikana wamemuua kwa kumpiga risasi Mwenyekiti mstaafu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wa kijiji cha Muyui, wilaya ya Kibiti, mkoani Pwani, Iddi Kirungi (60).
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa kwa vyombo vya habari, kamanda wa Polisi mkoani humo, Onesmo Lyanga alisema kuwa Kirungi alipigwa risasikatika bega la kulia pia walimjeruhi kwa risasi ya tumbo mwanawe, Nurdin Kirungi (18) kisha kutoweka kusikojulikana.
Lyanga alisema kuwa tukio hayo kwa pamoja yalitokea Mei 17, saa 1:40 usiku huko Muyui kata ya Mtunda wilayani Kibiti
Aidha alisema kuwa majeruhi alikimbizwa kwenye Hospitali ya Misheni ya Mchukwi kwa matibabu zaidi huku taratibu za mazishi zikiandaliwa kwa ajili ya kumzika mwenyekiti huyo mstaafu.
“Hadi sasa chanzo cha mauji hayo bado hakijafahamika na hakuna mtu aliyekamatwa na jitihada za kuwatafuta wauaji hao zinaendelea ili waweze kuchukuliwa hatua za kisheria,” alisema Lyanga.
The post Kiongozi mstaafu wa CCM auwawa kwa risasi appeared first on Zanzibar24.
Zanzibar 24
Habari Zinazoendana
11 months ago
Michuzi
NEWS ALERT: KATIBU WA CCM KATA YA BUNGU WILAYANI KIBITI AUWAWA KWA RISASI

11 months ago
Malunde
KIONGOZI MWINGINE WA CCM AUAWA KWA KUPIGWA RISASI KIBITI

Kaimu Mkuu wa Wilaya ya Kibiti Juma Njwayo,ambaye pia ni Mkuu wa Wilaya ya Rufiji amethibitisha kutokea mauaji hayo.
Amesema marehemu alipigwa risasi akiwa kwake wakati akijaribu kukimbia.
Njwayo amesema kabla ya kuuawa kwa mwenyekiti huyo, pia wauaji hao walianza kumjeruhi kwa kumpiga risasi ya tumboni mtoto wa marehemu aliyetajwa kwa jina la...
1 year ago
Bongo515 Dec
Mtoto wa Rais auwawa kwa kupigwa risasi
Mtoto wa kike wa Rais wa zamani nchini Msumbiji, Armando Guebuza, Valentina Guebuza ameripotiwa kupigwa risasi na kuuawa katika mji mkuu wa Maputo. Mumewe, Zofino Muiuane amekamatwa na polisi kufuatia tukio hilo lililofanyika Jumatano.
Bi Guebuza alikua na umri wa miaka 36 na imeripotiwa alipigwa risasi mara kadhaa nyumbani kwake na kufariki dunia kutokana na majeraha wakati akipelekwa hospitalini.Mumewe alikamatwa katika moja wapo ya maeneo ya burudani mjini Maputo, kwa mujibu wa gazeti...
1 year ago
Zanzibar 2420 Dec
Balozi wa Urusi auwawa kwa kupigwa risasi
Balozi wa Urusi, Andrey Karlov ameuawa kwa kupigwa risasi wakati akihutubia hafla maalum. Urusi imeyahusisha mauaji hayo na tukio la kigaidi.
Muuaji alikuwa akimshambulia kwa risasi huku akisema “God is great. Don’t forget Syria” (Mungu ni Mkubwa! Usisahau Syria). Baadhi ya wachambuzi wanasema huenda Uturuki ikaingia kwenye mgogoro mkubwa na Urusi na kusababisha vita kati ya nchi hizo mbili.
Msemaji wa wizara ya mambo ya kigeni mjini Moscow amesema Uturuki wamehakikishiwa kwamba kutakuwa...
3 years ago
CloudsFM13 Nov
MTUHUMIWA NAMBA 1 WA ‘WESTGATE’ KENYA AUWAWA KWA RISASI
Mtuhumiwa namba 1 wa kesi ya mashambulizi ya jengo la Westgate,Samantha Lewthwaite ameuawa kwa kupigwa risasi.
Taarifa zinasema mtuhumiwa huyo ambaye alikuwa akifahamika kama “White Widow” ameuawa Ukraine katika mapambano ambapo alikuwa akipambana upande wa kikosi cha wapiganaji wa Aidar.
Samantha amekuwa akituhumiwa kuhusika na matukio kadhaa ya mashambulizi ikiwemo la Westgate Kenya 2013, japo mengi ya matukio hayo haikuwahi kuthibitika juu ya ushiriki wake katika matukio hayo.
12 months ago
Zanzibar 2404 May
Waziri mdogo zaidi Somalia auwawa kwa risasi
Waziri mwenye umri mdogo zaidi nchini Somalia Abas Abdullahi Sheikh Siraji ameuawa kwa kupigwa risasi mjini Mogadishu karibia na ikulu ya Rais.
Abas Abdullahi Sheikh Siraji aliyekuwa na miaka 31 Alikuwa waziri wa masuala ya jamii na kazi nchini Somalia pia alikua mbunge anaeiwakilisha Jubbaland Bungeni.
Amewahi kuishi katika kambi ya wakimbizi ya Dadaab iliyopo nchi jirani ya Kenya akiwa mtoto na kisha kurejea nchini mwake mwaka jana alipokwenda kwa ajili ya uchaguzi mkuu.
Waziri wa habari...
1 year ago
Bongo502 Nov
Mmoja auwawa kwa kupiga risasi akipora abiria kwa kutumia silaha
Mtu mmoja anayesadikiwa kuwa ni jambazi alijeruhiwa kwa kupigwa risasi na askari Polisi kisha kufariki dunia wakati akipelekwa katika hospitali ya Monduli kwaajili ya matibabu.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Naibu Kamishna Charles Mkumbo, alisema tukio hilo lilitokea usiku maeneo ya Makuyuni barabara ya Arusha-Makuyuni wilayani Monduli.
“Mara baada ya kulisimamisha gari hilo wakaanza kumpora abiria mmojawapo aliyejulikana kwa jina la Victor Pius (46)...
1 year ago
Mtanzania20 Dec
BALOZI WA URUSI AUWAWA KWA KUPIGWA RISASI NCHINI UTURUKI

Askari huyo aliyejulikana kwa jina la Mevlut Mert Altintas aliuliwa pia na polisi katika mapambano yaliyodumu kwa muda wa dakika 15 na katika tukio hilo, watu wengine watatu waliumizwa.
Tukio la kuuwawa kwa Karlov ambaye alikuwa balozi wa Urusi nchini Uturuki, wengi wamelihusisha na maswala ya kigaidi kwani haikujulikana dhahiri kuwa nia yake...
1 year ago
Michuzi
Waziri wa mazingira nchini Burundi auwawa kwa kupigwa risasi

Polisi nchini wamethibitisha kutokea kwa tukio hilo kwa kusema amepigwa risasi alipokuwa akielekea nyumbani kwake eneo la Rohero.
Rais wa Burundi Pierre Nkurunziza, ameapa kuchukua hatua kali za kisheria kwa atakayepatikana na hatia ya kuhusika katika mauaji hayo.
Mamia ya watu , wakiwemo maafisa wa ngazi za juu katika jeshi...