Kipaumbele cha Fatma Karume kama Rais mpya wa TLS

Rais mpya wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), Fatma Karume ametaja mambo matano ambayo atayafanyia kasi baada ya kuchaguliwa kuongoza chama hicho, Jumamosi mjini Arusha.

Fatma Karume ambaye ni binti wa Rais Mstaafu wa Zanzibar amesema kuwa, ataendeleza yale yaliyofanywa na mtangulizi wake, Tundu Lissu, ikiwamo kusimamia demokrasia, haki, utawala bora, haki za wanasheria pamoja na kufanya uchunguzi ili kubaini sababu zinazopelekea watu kutokutaka kuifanya kazi hiyo.

Katika uchaguzi huo, Fatma alipata kura 820 akimzidi Godwin Gwilimi aliyepata kura 363, Godwin Mwalongo (12) na Godfrey Wasonga (6).

Aliongeza kuwa TLS itahoji mamlaka ya Mkurugenzi wa Makosa ya Jinai na Upelelezi (DPP), kuhakikisha wanasheria wanashirikishwa katika utungaji wa sheria na ada za uanachama wa TLS.

Baada ya kuingia katika uongozi, Fatma alisema kuwa jambo la kwanza atakalolifanya ni kubadili hali ya wanasheria nchini.

“Nataka kujua kwa nini hawataki kufanya kazi za uwakili. Kuna tatizo hapa la kwa nini wanasomea kazi hii lakini hawataki kuifanya. Nataka nitafute sababu,” alisema.

Alisema wanachama wa TLS waliofanya kzi za uwakili kwa mwaka 2016 walikuwa 2,931 lakini kwa mwaka 2018 wamepungua na kufikia 2,270.fatma ameseama kuwa TLS imepoteza wanachama 661 waliokuwa wanafanya kazi za uanasheria.

“Tukumbuke mwaka huu na mwaka jana kumetokea nini? Ofisi za (kampuni ya uwakili ya) Immma zilishambuliwa kwa bomu, ofisi za wanansheria wengine zimeshambuliwa na wengine wamewekwa selo bila makosa, lakini pia (aliyekuwa ) Rais wa TLS alipigwa risasi,” alisema.

Fatma, ambaye pia ni mwanasheria wa kampuni ya Immma, alisema hata kama serikali itasomesha vijana wengi kuwa wanasheria, kama mazingira ya kazi yatabaki kuwa ya vitisho na mashambulizi, wengi wataachia taaluma hiyo.

“Kwa maana hiyo wananchi ndio wataathirika. hii ni changamoto kubwa sana,” alisema.

Jambo la pili ambali alisema atalifanyia kazi akiwa TLS ni kuhoji namna DPP anavyotumia madaraka yake.

Alisema DPP amekuwa akiwakamata watu na baadaye kuwanyima dhamana au kuendelea kuwashikilia akidai kuwa upelelezi haujakamilika.

“Inakuwaje anawakamata watu wakati upelelezi haujakamilika? Watu wakiomba kudhaminiwa anasema wasidhaminiwe. Anaiambia mahakama hakuna kutoa dhamana, hii ina maana anatumia madaraka vibaya,” alisema.

“Mpaka sasa unajua ni wanasheria wangapi wako ndani na kesi zao hazijasikilizwa na hawajapewa dhamana?

“TLS isimamie suala hili kwa nguvu sana, kuhusu namna anavyotumia madaraka yake vibaya.”

Alisema zamani TLS ilipuuza suala hilo, lakini kwa sasa limekuwa kubwa na wameona walifanyie kazi kwa kina.

Kadhalika, Fatma amesema suala la tatu ni kuhakikisha wanasheria wanashirikishwa katika shughuli za kutunga sheria.

“Lazima tushirikishwe kwa sababu sisi ni wadau na tuna wajibu wa kutazama sheria, kuangalia hii inafaa na hii haifai, hii itamuumiza huyu,” alisema.

Kuhusu suala la ada za uanachama wa, Fatma alisema hakuna haja ya kuzishusha kwa sababu hilo si ytatizo linalosababisha  wanachama kuacha kufanya kazi za uanasheria.

“Hatutapunguza ada, baraza kuu limeamua kuwa ni bora ada kubaki vilevile. Mungu akijalia tutamaliza mwaka ssalama na ninataka kuhakikisha kwamba tunawavutia watu kuingia katika taaluma hii kwa sababu (kwa sasa) imeharibiwa,” alisema.

Kuhusu kufuata nyayo za Lissu, mwanasheria huyo alisema Mbunge huyo wa Singida Mashariki (CHADEMA) ni kiongozi aliyesimamia utawala bora, haki za wanasheria hivyo na yeye anakwenda kusimamia hayo.

Kuhusu kanuni za uchaguzi za TLS, Fatma alisema juzi  baraza Kuu la Chama hicho lilikubaliana kwamba alichokifanya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG) ni uvunjaji wa sheria.

Machi 10, 2018, TLS ilidai kuwa ofisi ya AG imeongeza masharti katika mabadiliko ya kanuni za uchunguzi wa chama hicho, yanayowanyima futsa watumishi wa umma na wanasiasa kuwania uongozi owote wa chama hicho.

Fatma alisema wanachama zaidi ya 1,500 wa baraza kuu la chama hicho walikubaliana kuwa AG alivunja sheria. Hata hivyo hawakutaka kusema hatua ambazo TLS inachukua.

Chanzo: Swahili times

The post Kipaumbele cha Fatma Karume kama Rais mpya wa TLS appeared first on Zanzibar24.

Zanzibar 24

Read more


Habari Zinazoendana

2 weeks ago

VOASwahili

Fatma Karume achaguliwa kuwa Rais wa TLS

Wakili Fatma Karume amechaguliwa kuwa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanzania (TLS).

 

1 week ago

Malunde

MBOWE AMPONGEZA FATMA KARUME KUWA RAIS WA TLS

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Kiongozi wa kambi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe amempongeza Fatma Karume kwa kuchaguliwa kuwa Rais mpya wa TLS.

“Ushindi wako umetuma ujumbe kuwa mawakili wa Tanganyika wanajua msimamo wako na wanaamini kwa dhati kuwa kwa kushirikiana na viongozi wenzako mliochaguliwa kuongoza TLS utawavusha katika kipindi hiki ambacho Taifa linapitia na kushuhudia majaribu mengi ya uvunjifu wa Katiba, sheria na kanuni mbalimbali.

"Umepokea kijiti katika...

 

(Yesterday)

Zanzibar 24

Jaji mkuu amjibu Rais wa TLS Fatma Karume

Jaji Mkuu Profesa Ibrahimu Juma, amesema Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), kinafanya kazi za umma, hakipaswi kujiingiza katika siasa wala uanaharakati, kwani kwa kufanya hivyo kinaweza kukosa ushirikiano. Kauli hiyo ya Jaji Mkuu, imekuja siku moja baada ya Rais wa TLS, Fatma Karume, kusema chombo chao si mali ya Serikali na hakuna mwenye uwezo wa kukiingilia kwa mujibu wa sheria. Akizungumza na waandishi wa habari jana, Profesa Juma, alisema na kusisitiza kutokana na majukumu ya TLS,...

 

1 week ago

Zanzibar 24

Mbowe atoa neno baada Fatma Karume kuwa Rais wa TLS

Mwenyekiti wa CHADEMA Taifa, Kiongozi wa kambi ya Upinzani Bungeni na Mbunge wa Hai, Freeman Mbowe amempongeza Fatma Karume baada ya kuchaguliwa kuwa Rais mpya wa TLS.

Soma hapa taarifa kamili.

The post Mbowe atoa neno baada Fatma Karume kuwa Rais wa TLS appeared first on Zanzibar24.

 

2 weeks ago

Malunde

FATMA KARUME NDIYO MRITHI WA TUNDU LISSU...ACHAGULIWA KUWA RAIS TLS

Wakili wa kujitegemea, Fatma Karume amechaguliwa kuwa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (Tanganyika Lawyers Society – TLS), akichukua mikoba ya aliyekuwa Rais wa Chama hicho, Tundu Lissu baada ya muda wake kumalizika.

Katika uchaguzi huo, Dkt. Rugemeleza Nshala amechaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa chama hicho.

Aidha, Ndugu Omar Shaaban amechaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar Lawyers Society.

Kwa mujibu wa katiba ya Chama hicho, Uongozi wa TLS hudumu kwa kipindi cha mwaka mmoja tu, na baada ya...

 

2 weeks ago

Zanzibar 24

Fatma Karume ashinda urais wa TLS

WAKILI wa kujitegemea, Fatma Karume amechaguliwa kuwa Rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (Tanganyika Lawyers Society – TLS), akichukua mikoba ya aliyekuwa Rais wa Chama hicho, Tundu Lissu baada ya muda wake kumalizika.

Katika uchaguzi huo, Dkt. Rugemeleza Nshala amechaguliwa kuwa Makamu wa Rais wa chama hicho.

Aidha, Ndugu Omar Shaaban amechaguliwa kuwa Rais wa Zanzibar Lawyers Society.

Kwa mujibu wa katiba ya Chama hicho, Uongozi wa TLS hudumu kwa kipindi cha mwaka mmoja tu, na baada...

 

1 month ago

Malunde

FATMA KARUME AJITOSA KUMRITHI TUNDU LISSU TLS

Wakili wa kujitegemea, Fatma Karume amejitosa kumrithi Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kwa kugombea urais wa Chama cha Mawakili wa Tanganyika (TLS), utakaofanyika Aprili 14, mwaka huu.


Lissu, ambaye aliteuliwa kugombea nafasi hiyo lakini ameshindwa kukidhi matakwa ya kamati kutokana na fomu ya uteuzi iliyowasilishwa kwa sekretarieti hiyo.

Kwa mujibu wa sheria mpya, Lissu hataweza kugombea tena nafasi hiyo kwani kifungu cha nane cha sheria hiyo, kinamzuia mtu ambaye ni kiongozi wa...

 

9 months ago

MwanaHALISI

Fatma Karume naye amvaa Rais Magufuli

FATUMA Karume, wakili wa Tundu Lissu, Mwanasheria mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) amesema kila mtu ana haki ya kumkosoa Rais, anaandika Hellen Sisya. Wakili huyo ameyasema hayo nje ya Mahakama ya Hakimu mkazi Kisutu ambapo Lissu amefikishwa siku ya leo akishtakiwa kwa kosa la kutoa lugha ya uchochezi ambayo imeleta chuki katika ...

 

2 years ago

Mwananchi

Bulembo: Fatma Karume akae pembeni

Aliyekuwa Meneja wa kampeni za mgombea urais wa CCM, Abdalah Bulembo amesema haoni dosari katika uamuzi wa kufuta uchaguzi wa Zanzibar na kumshauri mtoto wa aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Fatma Karume akae pembeni badala ya kuwachanganya wananchi.

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani