Klopp aanza kuchonga Liverpool

Jurgen Klopp amesema ana kikosi kizuri kinachoweza kuifunga timu yoyote duniani kwa sasa baada ya kuichapa Manchester City kwa mabao 2-1 ugenini kwenye Uwanja wa Etihad na kusonga mbele kwa ushindi wa jumla wa magoli 5-1.

Mohamed Salah alifunga bao lake la 39, msimu huu akiwa na jezi ya Liverpool, pia Misri huyo alitegeneza bao la pili lililofungwa na Roberto Firmino na kukujihakikishia ushindi mnono wa mabao 2-1 ugenini.

Pep Guardiola alicheza kamari katika mchezo huo wa marudiano kwa kuwaanzisha washambuliaji saba, na kufanikiwa kupata bao la mapema dakika 11 lililofungwa na Gabriel Jesus, lakini mambo yalibadilika kipindi cha pili katika dakika 11 za mwisho.

Kauli hiyo ya kocha huyo wa Liverpool imekuja muda mfupi baada timu  hiyo kutinga nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya juzi usiku.

 “Nadhani nina kikosi bora cha aina yake ambacho kinaweza kufunga timu yoyote duniani. Tulijua tutashinda na kusonga mbele katika mchezo wa marudiano,” alisema Klopp.

Kocha huyo wa zamani wa Borussia Dortmund alisema kipigo hicho kimemvunja nguvu Pep Guardiola.

Klopp alisema ana furaha baada ya kuivusha timu hiyo kucheza nusu fainali na mkakati wake ni kuanza maandalizi mapema.

Kocha huyo Mjerumani alisema dunia imetulia baada ya ushindi wa Liverpool.

The post Klopp aanza kuchonga Liverpool appeared first on Zanzibar24.

Zanzibar 24

Read more


Habari Zinazoendana

2 years ago

Mtanzania

Pluijm aanza kuchonga

Pluijm1NA OSCAR ASSENGA, TANGA

KOCHA Mkuu wa Yanga, Hans van der Pluijm ameanza kuchonga kutokana na ushindi waliopata dhidi ya African Sports juzi ambapo amesema umesaidia kuwapa nguvu ya kuendeleza kasi yao katika mechi zinazofuata na kuendelea kubaki kileleni.

Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara, juzi waliibuka na ushindi wa bao 1-0 ugenini dhidi ya African Sports katika mchezo uliopigwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Bao la pekee lililofungwa dakika za lala salama na kiungo Mzimbabwe,...

 

2 years ago

Habarileo

Julio aanza kuchonga

KOCHA mkuu wa timu ya soka ya Mwadui, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ ameipongeza timu yake kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbao Fc na kutamba ushindi zaidi unakuja.

 

2 years ago

Mtanzania

Klopp aanza kwa kumsajili Grujic

Marko-GujicLIVERPOOL, ENGLAND

KOCHA wa klabu ya Liverpool, Jurgen Klopp, ameanza mwaka kwa kumsajili kiungo wa Serbia, Marko Grujic, kwa kitita cha pauni milioni 5.1.

Mchezaji huyo ambaye alikuwa anakipiga katika klabu ya Red Star Belgrade ya nchini Serbia, alikuwa anaitumikia timu ya Taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 21.

Mkataba huo na klabu ya Liverpool, utamfanya aitumikie hadi kiangazi mwaka 2020, ambapo Klopp anaamini kuwa mchezaji huyo atakuza kiwango chake na kutoa mchango kwa klabu...

 

3 years ago

BBCSwahili

Liverpool wawasiliana na Jurgen Klopp

Liverpool imewasiliana na wawakilishi wa Jurgen Klopp ikimtaka achukue nafasi ya meneja aliyefutwa kazi Brendan Rodgers.

 

2 years ago

Mtanzania

Klopp: Liverpool ilikosa bahati

jurgen-kloppLONDON, ENGLAND

BAADA ya Liverpool kupokea kichapo cha mabao 3-1 ya mikwaju ya penalti dhidi ya Manchester City, kocha wa klabu hiyo, Jurgen Klopp, amedai kwamba timu yake ilikosa bahati ya kutwaa ubingwa wa michuano hiyo.

Katika mchezo huo wa Kombe la Capital One, dakika 90 zilimalizika huku timu hizo zikiwa zimefungana bao 1-1, lakini Liverpool walikuja kutolewa katika matuta 3-1, na Klopp akidai kwamba walikosa bahati.

Mabao ya awali yaliwekwa wavuni na Philippe Coutinho kwa upande wa...

 

3 years ago

BBCSwahili

Jurgen Klopp kutua Liverpool Ijumaa?

Klabu ya soka ya Liverpool imetangaza kuwa ina matumaini ya kumteua Jurgen Klopp kuwa meneja mpya wa klabu hiyo ifikapo siku ya ijumaa wiki hii.

 

3 years ago

BBCSwahili

Jurgen Klopp apewa kandarasi Liverpool

Jurgen Klopp amekubali kandarasi ya miaka mitatu kuwa mkufunzi wa kilabu ya Liverpool.

 

3 years ago

BBCSwahili

Klopp:Kuifunza Liverpool ni changamoto kuu

Mkufunzi mpya wa timu ya Liverpool Jurgen Klopp ameitaja kazi yake mpya katika kilabu hiyo ya Anfield kuwa changamoto kubwa katika kandanda duniani.

 

3 years ago

Mwananchi

Klopp ana ndoto ya kuifufua Liverpool

Kocha Jurgen Klopp anatarajiwa kutambulishwa leo kama mrithi wa kiti cha Brendan Rodgers huku akiwa na ndoto kichwani.

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani