Kocha wa Karume Boys atamba kubeba ubingwa wa CECAFA

Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Zanzibar ya soka chini ya miaka 17 (Karume Boys) Mzee Ali Abdallah amewatoa hofu Wazanzibar juu ya kikosi chao kinachotarajiwa kwenda Burundi katika Mashindano ya CECAFA ya vijana yanayotarajiwa kuanza rasmi April 14 mwaka huu.

Akizungumza mara baada ya kumaliza mazoezi mchana wa leo katika uwanja wa Amaan Kocha Mzee amesema wameamua kufanya mazoezi mchana ili kuzowea mazingira ya Burundi katika Mashindano hayo kwani katika ratiba wamepangiwa kucheza michezo mengine mchana huku akiwatoa hofu wa Wazanzibar na kusema kuwa anaamini kikosi chake kitatwaa Ubingwa wa Mashindano hayo.

“Tunashukuru Mungu mazoezi yanaendelea vizuri mana Vijana wanapokea vizuri mazoezi, tumeamua kufanya mazoezi mchana kwasababu kule Burundi ratiba ya michezo yetu siku nyengine tunacheza mchana ili tuzowee mazingira, mimi naamini vijana hawa kwa vile wanaari kubwa watabeba ubingwa na Wazanzibar wasiwe na wasi wasi wowote”.

Aidha kocha Mzee amesema hana wasi wasi kwa timu zilizomo katika kundi lao B huku akisema wao wanaamini watashinda bila ya woga wowote.

“Baadhi ya watu wanasema kundi letu B ni kundi la Kifo lakini mimi sina wasi wasi wowote wa timu zile, sisi tunajivunia vipaji na vijana wanahamasa ya kufanya vyema kama kaka zao Zanzibar Heroes”. Alisema Kocha Mzee.

Wakati huo huo kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Zanzibar (Zanzibar Heroes) na Msaidizi wa timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) Hemed Suleiman (Morocco) amesema Zanzibar ina vipaji vingi hivyo anaamini kikosi cha Karume Boys kitafika mbali katika Mashindano hayo.

“Mimi sina wasi wasi na vijana hawa kwasababu tuna program nzuri ya Vijana na pia tuna vipaji, japo tumecherewa kuanza mazoezi na vijana hawa lakini watafika mbali”. Alisema Kocha Morocco.

Mashindano hayo yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi nchini Burundi April 14 hadi 28, 2018 ambapo Zanzibar imepangwa kundi ‘B’ pamoja na ndugu zao Tanzania bara, Sudan na Uganda huku kampeni zake Zanzibar kuwania kombe hilo zitaanza kwa kucheza na Sudan April 15 katika uwanja wa Gitega majira ya saa 7:30 za mchana.

 

Na Abubakar Khatib Kisandu, Zanzibar.

The post Kocha wa Karume Boys atamba kubeba ubingwa wa CECAFA appeared first on Zanzibar24.

Zanzibar 24

Read more


Habari Zinazoendana

4 years ago

Tanzania Daima

Kocha KCC ashangaa kubeba ubingwa Zenji

KOCHA Mkuu wa timu ya KCC ya Uganda, George Nsimwa, juzi alitoa kali kwa kusema anashangazwa na timu yake kubeba ubingwa wa Kombe la Mapinduzi kwenye Uwanja wa Amaan, mjini...

 

1 year ago

MillardAyo

VIDEO: Kocha aliyeipa Ubingwa wa AFCON Ivory Coast ndio kaivua Ubingwa leo

Mabingwa watetezi wa kombe la mataifa ya Afrika timu ya taifa ya Ivory Coast usiku wa January 24 ndio siku rasmi ilivuliwa ubingwa wa mataifa ya Afrika, baada ya kuruhusu kufungwa goli 1-0 na timu ya taifa ya Morocco katika mchezo wao wa mwisho wa Kundi C. Ivory Coast ambao walikuwa Kundi C na timu za Morocco, […]

The post VIDEO: Kocha aliyeipa Ubingwa wa AFCON Ivory Coast ndio kaivua Ubingwa leo appeared first on millardayo.com.

 

2 years ago

Michuzi

JULIO ATAMBA KUCHUKUA UBINGWA MSIMU UJAO

Kocha Mkuu wa Mwadui FC Jamhuri Kihwelo'Julio'
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.KOCHA Mkuu wa Mwadui FC Jamhuri Kihwelo'Julio' amesema kuwa msimu huu wanatarajia kuja na kasi nyingine kwani wameamua kufanya marekebisho kwenye kikosi chao na wamepunguza idadi ya wachezaji na kwa maandalizi wanayoyafanya basi watakuwa Leciester City wa Tanzania na kufanya maajabu makubwa sana. Awali Mwadui ilikuwa na wachezaji takribani 33 na sasa wameamua kuwapunguza na kufikia hatua ya kufikisha wachezaji...

 

2 years ago

Bongo5

Kocha aliye zipa ubingwa wa Kombe la Afrika Zambia na Ivory Coast awa kocha mpya wa Morocco

Herve-Renard

Kocha Mfaransa, Renard, ambaye ana umri wa miaka 47, amefanikiwa kushinda Kombe la Mataifa ya Afrika mara mbili, mwanzo akiwa na Zambia mwaka 2012 na baadaye akiwa na Ivory Coast mwaka 2015, Herve Renard ameteuliwa kuwa kocha wa Morocco akirithi mikoba ya mzalendo,Badou Zaki aliyeondolewa wiki iliyopita.

Herve-Renard

Renard ameweka wazi mipango katika timu ya taifa ya Morocco mara tu baada ya uteuzi huo.

“Changamoto ya kwanza ni, kufuzu Fainali za Mataifa ya Afrika mwaka 2017, Na kufuzu kwa Kombe la...

 

3 years ago

Habarileo

Twiga imeiva, atamba kocha

KOCHA Mkuu wa timu ya soka ya taifa ya wanawake, Twiga Stars, Rogasian Kaijage amesema kikosi chake kimeiva na anachosubiri ni mechi ya kirafiki dhidi ya Kenya mwishoni mwa wiki ijayo.

 

2 years ago

Michuzi

SERENGETI BOYS YAKWEA PIPA KUWAFATA WASHELISHELI, MCHAWI MWEUSI ATAMBA

Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri wa chini ya miaka 17 ‘Serengeti Boys’ imeondoka saa 9.45 alfajiri ya leo Juni 30, 2016 kwa ndege ya Shirika la Ndege la Ethiopia kwenda Visiwa va Hame-Shelisheli kwa ajili ya kuwavaa wenyeji katika mchezo wa marudiano kuwania nafasi ya kufuzu fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika kwa vijana.
Serengeti Boys inaondoka na matumaini makubwa ya kuiondoa Shelisheli katika mbio hizo baada ya kuvuna ushindi mnono wa mabao 3-0 katika mchezo wa kwanza uliofanyika...

 

1 year ago

Habarileo

Kocha Lyon atamba kuipasua Mbao

KOCHA wa African Lyon, Charles Otieno amejigamba kuifunga Mbao FC kwenye mchezo wa Ligi Kuu utakaochezwa kesho kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.

 

2 years ago

Habarileo

Serengeti njia nyeupe, atamba kocha Shime

KOCHA wa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 ‘Serengeti boys’ Bakari Shime amesema matokeo ya sare ya bao 1-1 waliyopata dhidi ya Afrika Kusini juzi yanawapa nafasi ya kujipanga kwa mchezo ujao wa marudiano ili kufanya vizuri zaidi.

 

2 years ago

Bongo5

Kilimanjaro Queens yatwaa ubingwa wa CECAFA 2016

Timu ya Taifa ya Wanawake ‘Kilimanjaro Queens’ yaifunga Harambe Starlets ya Kenya 2-1 na kutwaa Kombe la Chalenji la CECAFA 2016 huko Jinja, Uganda leo jioni.
14390765_10154543673149339_1241431227057215031_n

Magoli ya Tanzania yamefungwa na Mwahamisi Omar dk 28, 45, Kenya limefungwa na Christina Nafula.

Tanzania walifika fainali baada ya kuwalaza wenyeji Uganda 4-1 mechi ya nusu fainali.

Jiunge na Bongo5.com sasa Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani