Kubaliana na dawa za kulevya Zanzibar, Tume ya kuratibu na kudhibiti dawa hizo yazinduliwa

madawa-ya-kulevya

 

Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi amesema hatma ya Zanzibar katika kukabiliana na matumizi ya dawa za kulevya, ipo mikononi mwa Tume ya kitaifa ya serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ya kuratibu na kudhibiti dawa za Kulevya iliyoundwa hivi karibuni ambayo ameitaka kujipanga katika kupambana vikali na wenye fedha na mtandao wa muda mrefu.

Balozi Seif Ali Iddi ametoa kauli hiyo, muda mfupi baada ya kuizindua rasmi Tume ya Kitaifa ya Kuratibu na Kudhibiti dawa za kulevya, katika hafla fupi iliyofanyika ofisini kwake eneo la Vuga, visiwani hapa.

Balozi Seif amesema mafanikio ya Tume hiyo yatategemea zaidi juhudi za wajumbe wake namna watakavyojipanga vizuri kwa kushirikiana na wadau wengine, na kuwakumbusha kuwa wanaojishughulisha na biashara hiyo baadhi yao wanaeleweka na kuishi pamoja na jamii, na kuitaka Tume hiyo kutoogopa kuwachukulia hatua za kisheria wahusika wote.

Balozi Seif Ali Iddi amemshukuru Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Ali Mohamed Shein kwa kumteua kuwa Mwenyekiti wa Tume hiyo, na kuahidi kushirikiana na wajumbe wote walioteuliwa kwa kuandaa na kusimamia utekelezaji wa mpango wa Tume hiyo.

Matumizi ya dawa za kulevya visiwani Zanzibar yanaendelea kuongeza na yameathiri vijana wengi licha ya kufunguliwa kwa vituo vya ushauri nasaha maarufu kama Sober House, kutokana na udhibiti wa uingiaji na usambazaji kuwa mdogo.

Channelten

Read more


Habari Zinazoendana

10 months ago

Channelten

Vita dhidi ya dawa za Kulevya Waathirika wa dawa hizo wanena

Ikiwa ni wiki moja tangu Serikali ianze mapambano kamili dhidi ya dawa za kulevya, madhara kwa watumiaji wa dawa hizo tayari yameanza kuonekana, baada ya watumiaji hao kujitokeza hadharani na kudai serikali iwasaidie njia mbadala ya kupambana na maumivu yanayotokana na kukosa dawa hizo yajulikanayo kama Arosto.

Wakizungumba na Channel Ten kwenye maeneo tofauti ya jiji la Dar es salaam, baadhi ya watumiaji wa dawa hizo ambao walikuwa tayari kuzungumza wamesema wao wenyewe wanaunga mkono...

 

8 months ago

Zanzibar 24

Hatma ya janga la Dawa za Kulevya Zanzibar limo mikononi mwa Tume kufanyiwa kazi

Makamu wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alitahadharisha kwamba hatma ya Zanzibar kuhusiana na janga la Dawa za Kulevya limo mikononi mwa Tume ya Kitaifa ya kuratibu na kudhibiti madawa ya kulevya iliyoundwa kwa lengo la kukabiliana na janga hilo.

 

Alisema wakati Wajumbe wa Tume hiyo wakijipanga kuingia kwenye vita hivyo  waelewe kwamba wanaingia katika vita vikali vya kupambana na wenye fedha nyingi na mtandao wa siku nyingi.

Akiizindua rasmi Tume hiyo ya Kitaifa...

 

4 years ago

Michuzi

UZINDUZI WA KAMATI YA KITAALAMU YA TUME YA KURATIBU NA UDHIBITI WA MADAWA YA KULEVYA ZANZIBAR


Na Ramadhan Ali-Maelezo ZANZIBAR  Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Fatma Abdulhabib Ferej (pichani) amesema juhudi za Serikali ya kuwasogezea wananchi maendeleo hazitokuwa na tija iwapo wimbi la vijana wa Zanzibar watatumika kusafirisha dawa za kulevya na wataendelea kuwa wahanga wa matumizi ya dawa hizo.   Amesema hatma ya maendeleo ya Taifa itategemea zaidi vijana wenye mwelekeo mzuri wa tabia na waliojiepusha na matumizi ya mihadharati ambayo inahatarisha afya...

 

9 months ago

Michuzi

MASAUNI ATEMBELEA BANDARI YA ZANZIBAR, AAGIZA JESHI LA POLISI KUSHIRIKIANA NA UONGOZI WA BANDARI KUDHIBITI UINGIAJI WA DAWA ZA KULEVYA

 Naibu Waziri Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni, akizungumza wakati wa ziara ya kutembelea Bandari ya Zanzibar,  ikiwa na lengo la kukagua mifumo ya udhibiti wa uingizwaji wa Dawa za Kulevya huku akiliagiza Jeshi la Polisi Zanzibar kushirikiana na Uongozi wa Bandari,  kuhakikisha ukaguzi wa mizigo unafanyika ili kukomesha uingiaji wa dawa hizo ambazo humaliza nguvu kazi ya Taifa. Wakwanza kushoto ni Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano wa Serikali ya...

 

9 months ago

Habarileo

Posta kudhibiti dawa za kulevya

KATIKA kupambana na uhalifu wa dawa za kulevya, Shirika la Posta Tanzania (TPC), linasimika mfumo wa kisasa utakaogharimu Sh. Milioni 200 wa kudhibiti usalama na kurahisisha utambuzi wa vitu na matukio hatarishi na haramu yanayopitishwa au kujitokeza kupitia mtandao wa shirika hilo.

 

10 months ago

Michuzi

TID AWAOMBA RADHI WATANZANIA KWA UTUMIAJI WA DAWA ZA KULEVYA,AKIRI KUUNGA MKONO JUHUDI ZA KUPAMBANA NA DAWA ZA KULEVYA

Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii

Msanii wa Bongo fleva Khalid Mohamed (TID) amesema kuwa hawezi kufumbia macho wala kuwaonea aibu kwa kuwataja watu wote ambao wanafanya biashara ya dawa za kulevya.

TID amesema hayo jijini Dar es Salaam katika mkutano wa mkuu wa mkoa na waandishi wa habari juu ya mapmbano dhidi ya dawa za kulevya kwa mara ya tatu.

“Mimi mnyama na mkuu wa mkoa kaonesha unyama katika kupambana na madawa ya kulevya, hivyo namshukuru sana kwa hatua ngumu aliyoamua...

 

7 months ago

Malunde

Utafiti: HISIA ZA MAPENZI ZINAMSAIDIA MUATHIRIKA WA DAWA ZA KULEVYA AACHE KUTUMIA DAWA ZA KULEVYA

Wanasayansi kutoka Chuo Kikuu cha St George’s London wamegundua jinsi hisia za mapenzi zinavyoweza kumsaidia muathirika wa dawa za kulevya kupambana na hali ya arosto na kutaka kurudia matumizi ya dawa hizo iwapo aliacha kwa kipindi fulani.
Kwa mujibu wa utafiti huu binadamu huzalisha homoni inayoitwa Oxytocin ambayo humsaidia kuwa na hali ya furaha na raha ,homoni hii ambayo huzalishwa kwenye ubongo, itazalishwa kwa wingi iwapo mtu atampata mpenzi anayempenda.
Wanasayansi wanalinganisha raha...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani