Kujeruhiwa risasi Mbunge Tundu Lissu, Jeshi la Polisi lakanusha askari wake kuhusishwa

Screen Shot 2017-09-13 at 11.35.41 AM

Jeshi la Polisi nchini limekanusha taarifa zinazosambaa katika mitandao mbalimbali ya kijamii kuhusiana na kuhusishwa kwa Askari mmoja wa Jeshi hilo akidaiwa kuonekana jijini Nairobi akifuatilia tukio, lilitokea la kujeruhiwa Risasi kwa Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu lililotokea hivi karibuni mjini Dodoma, na kudai kuwa taarifa hizo sio za kweli na kuwataka wananchi kuzipuuzia kwani zina lenga kulichafua Jeshi hilo.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Msemaji wa Jeshi la Polisi Makao Makuu ya Polisi ACP Barnabas Mwakalukwa amesema , kuhusiana na Askari huyo ni kweli alikuwa nchini Kenya kwa kozi za kimafunzo kuanzia tarehe 04/09/2017 lakini akarejea nchini siku ya tarehe 08/09/2017 huku tukio la mkasa wa Tundu Lissu wa kujeruhiwa na risasi ukitokea tarehe 07/09/2017 na kusafirishwa kwenda Nairobi usiku wa kuamkia tarehe 08/09/2017.Amesema sababu za Askari huyo kutiliwa shaka ni uwepo wa Tundu Lissu katika Hospitali Mjini Nairobi na kusababisha picha za Askari huyo wa Jeshi la Polisi kusambaa kwa kasi katika mitandao ya kijamii.

Jeshi la Polisi linakemea vikali na kuionya Jamii kutojihusisha kutumia mitandao ya kijamii kwa ajili ya kusambaza taaifa ambazo sio za kweli, na kwamba Jeshi hilo kupitia kitengo cha Upelelezi wa makosa ya jinai( CYBER CRIME INVESTIGATION UNIT)linaendelea na uchunguzi ili kuwabaini wale waliohusika na kusambaza taarifa hizo za uongo ili hatua kali za kisheria zichukuliwe dhidi yao.

Share on: WhatsApp

The post Kujeruhiwa risasi Mbunge Tundu Lissu, Jeshi la Polisi lakanusha askari wake kuhusishwa appeared first on Channel Ten.

Channelten

Read more


Habari Zinazoendana

2 weeks ago

Malunde

KAULI YA JESHI LA POLISI KUHUSU TUKIO LA TUNDU LISSU KUPIGWA RISASI


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto amezungumzia tukio la kupigwa risasi mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, akiwaomba wananchi wenye taarifa kulisaidia jeshi hilo.

Muroto amesema leo Alhamisi kuwa wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na wameshafika eneo la tukio nyumbani kwa Lissu.
“Tunaomba mwananchi wenye taarifa atusaidie. Jeshi la Polisi tumeanza uchunguzi, tumefika eneo la tukio na tunaendelea,” amesema.
Kamanda Muroto amesema taarifa za awali zinaonyesha kuna gari...

 

2 weeks ago

Malunde

TAARIFA YA JESHI LA POLISI MAKAO MAKUU KUHUSU TUNDU LISSU KUPIGWA RISASI 32


Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Sirro amefunguka na kusema watu ambao wamefanya uhalifu wa kumpiga risasi Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu wanaweza patikana ikiwa wananchi watasaidia jeshi hilo kupata taarifa za wahalifu hao.

IGP Sirro amesema hayo leo alipokutana na waandishi wa habari akielezea hali ya usalama wa nchi na kudai usalama wa nchi upo vizuri na kuwa mpaka sasa jeshi la polisi limeongeza nguvu ya upelelezi mjini Dodoma ili kuhakikisha linawapata watu...

 

2 weeks ago

Malunde

MSIGWA AMPINGA MKUU WA JESHI LA POLISI TANZANIA IGP SIRRO SAKATA LA TUNDU LISSU KUPIGWA RISASI

Mbunge wa Iringa Mjini (CHADEMA) Mchugaji Peter Msigwa amefunguka na kuonyesha kutoridhishwa na kauli ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Nyakoro Sirro kusema Tundu Lissu hakuwahi kutoa taarifa juu ya watu wanaomfuatilia.

Mbunge Msigwa ambaye sasa yupo nchini Kenya kwenye matibabu ya Tundu Lissu ameonyesha kusikitiswa na taarifa hiyo ya IGP ambayo aliitoa Septemba 8, 2017 katika mkutano wa waandishi wa habari na kusema kiongozi huyo hakuwahi kutoa taarifa yoyote polisi juu ya gari...

 

2 weeks ago

Malunde

MBUNGE ASIMULIA JINSI TUNDU LISSU ALIVYOPIGWA RISASI TUMBONI,MGUUNI NA MKONONI

Mbunge wa Rombo, Joseph Selasini ameeleza jinsi Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu alivyopigwa risasi nyumbani kwake mjini Dodoma.
Selasini amesema kuwa maelezo aliyopata ni kuwa alikuwa akifuatiliwa na gari tangu anatoka bungeni na dereva wake alilishtukia. 
Amesema kuwa alivyoona wanamfutilia alipofika nyumbani, dereva alimsihi Lissu asishuke ndani ya gari. 
"Hao watu walipoona hawashuki walijifanya kuna kitu wanaangalia walivyoona kuna utulivu walisogeza gari lao ambalo ni tinted na...

 

2 weeks ago

Michuzi

NEWS ALERT: MBUNGE TUNDU LISSU ASHAMBULIWA KWA RISASI MJINI DODOMA LEO

Taarifa iliyotufikia hivi punde, inaeleza kuwa Mbunge wa Singida Mashariki na Rais wa Chama cha Mawakili cha Tanganyika (TLS), Tundu Antipus Lissu ameshambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana alipokuwa akitoka nyumbani kwake Area D Dodoma na kujeruhiwa vibaya na kukimbizwa katika Hosiptali ya Mkoa wa Dodoma kwa matibabu. 
Taarifa zaidi zitawafikia kadri tutakavyokuwa tukizipa.

 

1 week ago

BBCSwahili

Hali ya mbunge Tundu Lissu baada ya kushambuliwa kwa risasi Dodoma wiki iliyopita

Bwana Lissu anaendelea kupokea matibabu katika hospitali ya Nairobi nchini kenya, baada ya kupigwa risasi na watu wasiojulikana mjini Dodoma wiki iliyopita.

 

1 week ago

Malunde

JESHI LA POLISI DODOMA LASIKITISHWA NA KITENDO CHA DEREVA WA TUNDU LISSU KUTOFIKA POLISI

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto ameeleza kusikitishwa kwao na kitendo cha dereva wa Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu kutokufika polisi na kutoa maelezo yake.

Kamanda Muroto amesema hayo leo Jumatano wakati akijibu swali la upelelezi unaendeleaje kuhusu tukio hilo.

Amesema upepelezi unaendelea kuhusu tukio la Lissu kupigwa risasi na watu mbalimbali wanaendelea kuhojiwa wakiwemo wamiliki nane wa gari aina ya Nissan ambazo zilikamatwa kuhusiana na shambulizi...

 

9 months ago

Global Publishers

Tundu Lissu Akamatwa na Jeshi la Polisi

lissuDAR ES SALAAM: Mbunge wa Singida Mashariki kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Tundu Lissu anashikiliwa na Jeshi la Polisi katika Kituo Kikuu, Kanda Maalum ya Dar es Salaam kwa madai ya uchochezi.

“Nashikiliwa na polisi hapa Kituo Kikuu kutokana na ile press conference (mkutano na waandishi wa habari) kuhusu kupotea kwa Ben Saanane,” Lissu alimweleza mwandishi mmoja wa habari mapema leo kupitia simu.

Hivi karibuni, Lissu alifanya mkutano na waandishi wa habari Makao...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani