KUTOKA AMBONI TANGA POLISI YATOA TAMKOA HALI NI SHWARI

Baadhi ya magari ya Polisi yakiwa kwenye moja ya barabara ya kuelekea Mapango ya Amboni, wakati wa Doria maalum iliyoanza jana baada ya eneo hilo kuvamiwa na waliodaiwa kuwa ni Magaidi wa Al- Shabaab. Hata hivyo Polisi Mkoa wa Tanga leo imetoa tamko kuwa hali katika mapango hayo ni shwari baada ya kufanikiwa kuwatimua watu hao walioonekana kutimkia mpakani mwa nchi ya Kenya.Sehemu ya mawe ya Msitu wa Amboni...Baadhi ya askari Polisi wakiwa katika doria, ambapo imeelezwa kuwa jumla ya askari wanne wamejeruhiwa katika tukio hilo.Source:Sufianimafoto

Vijimambo

Read more


Habari Zinazoendana

3 years ago

Mtanzania

Polisi: Waliovamia Amboni, Tanga ni wahuni

Na Amina Omari na Oscar Assenga, TANGA
KAIMU Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tanga, Juma Ndaki, amesema watu waliopambana na askari polisi na wale wa Jeshi la Wananchi (JWTZ) ni kikundi cha wahuni.
Harakati za mapambano baina ya polisi na wahalifu hao zilidumu kwa takribani saa 48, huku Mkuu wa Mkoa huo, Said Magalula akikiri kwamba wameshindwa kuwakamata watu hao.
Jana Ndaki aliwaambia waandishi wa habari kuwa, jeshi hilo linawashikilia watu kadhaa kutokana na tukio la majambazi kushambiliana na...

 

3 years ago

Michuzi

WAFANYAKAZI KISSA PHARMACY LTD WATEMBELEA MAPANGO YA AMBONI TANGA(AMBONI CAVES)


Wafanyakazi wa Kissa Pharmacy Ltd  Pharmaceuticals Whole Sale And Retali Mbeya Tz wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuwasili katika eneo la mapango ya Amboni (AMBANI CAVES ) kwa lengo la kujifunza mambo mbalimbali ya kihistoria ndani ya Mapango hayo sanjali na kuhamasisha utalii wa ndani.Picha na Emanuel Madafa Baba JJ
Wafanyakazi Kissa Pharmacy wakisikiliza kwa makini maelezo ya mmoja wa watoa huduma katika mapango hayo Ndugu Allan Yohana kabla ya kuanza rasmi shughuli ya...

 

3 years ago

Mwananchi

Taharuki yakumba Jiji la Tanga Polisi wakipambana na majambazi mapango ya Amboni

Hali tete na taharuki imezuka katika jijini la Tanga kwa siku mbili kuanzia jana na leo baada ya kusikika milio ya mabomu na risasi zilizokuwa zikirushwa wakati vikosi vya jeshi la polisi na JWTZ vikishambuliana na kundi linalodaiwa kuwa ni la majambazi.

 

2 months ago

Michuzi

POLISI WAIMARISHA ULINZI KUELEKEA PASAKA, LASEMA HALI YA USALAMA WA NCHINI SHWARI

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii
JESHI la Polisi nchini limesema hali ya usalama nchini ni shwari na matukio makubwa ya uhalifu wa kutumia silaha yamepungua kwa kiasia kikubwa huku likieleza kipindi hiki cha kuelekea Sikukuu ya Pasaka linawahakikishia wananchi kuwa limejipanga kikamilifu
Taarifa iliyotolewa leo jijii Dar es Salaam na Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini ,IGP Simon Sirro ameshukuru ushirikiano ambao wananchi wanautoa kwa jeshi hilo ambao umesaidia kupunguza matukio ya uhalifu na nchi...

 

3 years ago

Mtanzania

‘Gaidi’ wa Amboni Tanga mbaroni

NA OSCAR ASSENGA, HANDENI
JESHI la Polisi mkoani Tanga, limedai kufanikiwa kumkamata mmoja wa watuhumiwa aliyehusika kwenye tukio lenye sura ya kigaidi katika mapango ya Amboni.
Zaidi Jeshi hilo limemuhusisha mtuhumiwa huyo na tukio la uporaji silaha kwa askari waliokuwa doria eneo la barabara ya nne na tano Mtaa wa Makoko jijini Tanga, Januari 26 mwaka huu.
Takribani mwezi mmoja uliopita, tukio hilo la Amboni ambalo msingi wa kujulikana kwake ulitokana na kuporwa kwa silaha hizo,...

 

3 years ago

Michuzi

Mwandani wa: Mapango ya Amboni mkoani Tanga

Na Sultani Kipingo Mapango maarufu ya Amboni mkoani Tanga ni eneo kubwa kuliko yote lenye majabali ya chokaa katika Afrika Mshariki. Yapo takriban kilomita nane hivi Kaskazini mwa mji wa Tanga, njia ya kuelekea huko ikichepuka toka barabara mkuu ya Tanga-Mombasa. Kumbukumbu zilizopo zinaonesha mapango hayo yalizuka kiasi cha miaka milioni 150 iliyopita, katika zama za mijusi wakubwa wajulikanao kama Jurassic age. Eneo lake lina kiloita za mraba 234, na kwa mujibu wa watafiti, eneo hilo...

 

3 years ago

Mwananchi

Uhalifu wa Amboni Tanga unatufunza nini?

Katika masuala ya usalama, watu wanaweza kukaa eneo moja kwa muda mrefu wakipanga kufanya matukio ya uhalifu.

 

3 years ago

CloudsFM

Watanzania watakiwa kutembelea mapango ya Amboni,Tanga

Watanzania wametakiwa kutembelea kutembelea (kutalii) kwenye mapango ya Amboni yaliyopo nje kidogo ya mji wa Tanga,kwani idadi imepungua kutokana na vyombo vya habari hasa magazeti kupotosha kuwa matukio ya kigaidi yaliyotokea hivi karibuni yalitokea maeneo hayo ya mapango.

Muongozaji wa Watalii katika mapango hayo aliyejulikana kwa jina la Bw.Tabu akizungumza na mtangazaji wa kipindi cha Power Breakfast cha Clouds FM,Saidi Bonge alipotembelea katika mapango hayo alisema kuwa tangu magazeti...

 

2 years ago

Michuzi

JESHI LA POLISI MKOA WA MWANZA YATOA TATHMINI YA HALI YA UHALIFU MKOANI HUMO.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi.
Na Mwandishi wetu. MKOA wa Mwanza  kwa kipindi chaa mwezi Juni  mwaka huu umekuwa shwari ikilinganishwa na ya mwezi mei mwaka huu. katika matukio ya uhalifu.
Kwa mujibu wa taarifa ya Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza, Ahmed Msangi  amesema kuwa pamoja na kuwa usalama kulikuwepo na baadhi ya matukio makubwa ya jinai kama mauaji,unyang’anyi wa kutumia silaha, unyang’anyi wa kutumia nguvu, uvunjaji,kubaka na wizi wa mifugo.
Amesema licha ya...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani