Ligi Daraja la Pili kuanza Oktoba 7, kuchezwa makundi manne ya timu sita sita nyumbani na ugenini

Kwa kuzingatia marekebisho ya Kanuni ya Ligi Daraja la Pili (SDL) yaliyofanywa na Kamati ya Utendaji ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) hivi karibuni, SDL kwa msimu wa 2015/2016 itachezwa katika makundi manne ya timu sita sita kwa mtindo wa nyumbani na ugenini.
Timu itakayoongoza kundi itacheza Ligi Daraja la Kwanza (FDL) msimu wa 2016/2017 wakati ya mwisho katika kila kundi itarudi kucheza Ligi ya Mkoa wake kwa msimu wa 2016/2017. Makundi ya SDL ni kama ifuatavyo; Kundi A ni...

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

3 years ago

Michuzi

LIGI YA MKOA KUFIKIA TAMATI JUNI 06, TIMU SITA KUPANDA DARAJA LA PILI TAIFA.

MICHUANO ya Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) msimu wa 2015/2016 inaendelea vizuri katika vituo vinne vya Kagera, Morogoro, Singida na Njombe ambapo itafikia tamati Juni 6 mwaka huu.
Timu sita zitapanda daraja kucheza Ligi Daraja la Pili (SDL) msimu wa 2016/2017. Timu hizo ni zile zitakazoongoza kila kundi, na washindwa bora (best losers) wawili kutoka makundi mawili tofauti.
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeweka waangalizi wake katika kila kituo, na litawachukulia hatua watu wote...

 

2 years ago

Habarileo

Ligi daraja la pili kuanza Oktoba 29

LIGI daraja la pili inatarajiwa kuanza Oktoba 29 ikishirikisha timu 24 zilizogawanywa kwenye makundi manne.

 

2 years ago

Bongo5

Ligi daraja la pili kuanza Oktoba 29, 2016

Timu 24, zinatarajiwa kupambana katika michuano ya Ligi Daraja la Pili msimu wa 2016/17 kuanzia Oktoba 29, mwaka huu, imefahamika.

wambura

Timu hizo zimepangwa katika makundi manne yenye timu sita kwa kuangalia zaidi jiografia au kanda ambako timu imetoka – lengo likiwa kupunguza gharama kwa timu shiriki hasa ikizingatiwa kuwa michuano hiyo haijapata mdhamini hadi sasa.

Kundi A lina timu za Mashujaa ya Kigoma, Mirambo ya Tabora, Mji Mkuu ya Dodoma, Green Warriors ya Pwani, Bulyanhulu na Transit...

 

3 years ago

Bongo5

TFF yataja makundi ya timu zitakazoshiriki ligi daraja la pili

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), limetoa orodha ya makundi manne na timu zitakazoshiriki ligi daraja la pili ((SDL) inayotarajiwa kuanza baadaye, mwaka huu.

wambura

Kwa mujibu wa Bodi ya Ligi (TPLB), chombo maalumu cha kusimamia michezo inayoendeshwa na TFF makundi na timu hizo ni kama ifuatavyo.

Kundi A

Bulyanhulu FC- Shinyanga

Geita Gold SC- Geita

Mashujaa FC- Kigoma

Milambo SC- Tabora

Polisi Tabora FC- Tabora

Transit Camp FC- Shinyanga

Kundi B

AFC- Arusha

Green Warriors- Dar es...

 

1 year ago

Zanzibar 24

Mitihani ya Darasa la nne, sita na kidatu cha pili kuanza wiki hii Zanzibar

Mitihani ya darasa la nne, la sita na mitihani ya sekondari ya awali (kidatu cha pili) inatarijiwa kuanza tarehe 20 Novemba mwaka huu hadi tarehe 5 Disemba 2017 ambapo jumla ya watahiniwa 124,190 wamesajiliwa kufanya mitihani hiyo ambapo ni sawa na ongezeko la asilimia 25.49 ukilinganisha na watahiniwa wa mwaka 2016.

Akitowa taarifa kwa vyombo vya Habari ofisini kwake Mazizini  Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar Riziki Pembe Juma amesema  Jumla ya watahiniwa  40,201 wamesajiliwa...

 

3 years ago

Zanzibar 24

Mlandege mpya ya kamal manji kuanza kazi kesho ligi daraja la pili wilaya ya mjini

Mlandege mpya ya kamal manji kuanza kazi kesho ligi daraja la pili wilaya ya mjini

Pazia la Ligi Daraja la Pili Wilaya ya Mjini linatarajiwa kuanza rasmi kesho kwa kusukumwa michezo miwili katika uwanja wa Amaan.

Saa 8 mchana wataanza Small Renger dhidi ya Muembe Makumbi na saa 10 za jioni watasukumana kati ya timu mpya ya Mlandege ilionunuliwa na Kamal Manji zamani ilikuwa Kidongo Chekundu watacheza na New Generation.

 

Na: Abubakar Khatib “Kisandu” Zanzibar.

The post Mlandege mpya ya kamal...

 

3 years ago

Channelten

Utata wa Matokeo Ligi Daraja la Kwanza, TFF yasusa kutangaza timu itakayopanda daraja Ligi Kuu Bara.

Usajili

Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limesema kuwa halitatangaza timu iliyopanda Ligi Kuu msimu ujao kutoka Kundi C, mpaka itakapoamuliwa na vyombo husika vya TFF baada ya michezo ya kundi hilo.

TFF imefikia hatua hiyo ili kupata nafasi ya kupitia taarifa za michezo kati ya JKT Kanembwa na Geita Gold na Polisi Tabora na JKT Oljoro iliyochezwa jana jioni katika mikoa ya Kigoma na Tabora.

Taarifa hiyo imeeleza kwamba michezo hiyo inasubiriwa taarifa kutoka kwa wasimamizi husika na...

 

4 years ago

Michuzi

DRFA yataja makundi ya timu zitakazoshiriki kucheza hatua ya 18 bora (hatua ya pili) ya ligi ya mkoa wa Dar es salaam

Chama cha soka mkoa wa Dar es salaam DRFA, kimetaja makundi ya timu zitakazoshiriki kucheza hatua ya 18 bora (hatua ya pili) ya ligi ya mkoa wa Dar es salaam,inayotarajia kuanza kutimua vumbi mapema mwezi huu.Katika kundi (A) limepangwa kuwa na timu za Simba U20,Red Coast,Sifa UTD,Shababi,Ukonga UTD,Zakhem,Ugimbi,Beirahotspurs na Pan Africa.Katika kundi (B) litakuwa na timu za Yanga U20,Stakishari,FFU,New Kunduchi,Sinza Stars,Changanyikeni,Tuamoyo,Sifapilitan na Azania Unga.
Ligi hiyo ya mkoa...

 

2 years ago

Mwananchi

Ndanda yapania pointi sita ugenini

 Ndanda inataka pointi sita za Kanda ya Ziwa ili ziwaweke salama kwenye msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara kabla ya kuangalia mipango mingine.

 

Share

Trending Now

Zinazosomwa Sasa

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani