MAAMUZI YA KAMATI YA NIDHAMU YA TFF

Kamati ya nidhamu iliyokutana Januari 1, 2018 ilipitia ripoti mbalimbali za mchezo kati ya Kagera Sugar na Tanzania Prisons uliochezwa Uwanja wa Kaitaba Novemba 2, 2017 na ule kati ya Azam Fc na Mbeya City uliochezwa Uwanja wa Chamazi Oktoba 27, 2017.

Kwenye mchezo kati ya Kagera Sugar na Tanzania Prisons,Meneja wa timu ya Tanzania Prisons Erasto Ntabahani alipelekwa kwenye kamati hiyo ya nidhamu kwa kosa la kumshambulia muamuzi wa akiba,kamati imejiridhisha kuwa Ntabahani alimshambulia kwa maneno muamuzi huyo wa akiba na hivyo imemfungia miezi miwili(2) na kulipa faini kwa mujibu wa kanuni ya 40(2) ya udhibiti wa viongozi.
Kamati pia ilipitia suala la golikipa wa Mbeya City Owen Chaima kudaiwa kumpiga mshambuliaji wa Azam FC Yahya Mohamed.
Chaima alikiri kumpiga Yahya na Kamati kupitia kanuni ya 35(7b) ya udhibiti wa wachezaji imemfungia kucheza mechi 4 na faini.

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

2 years ago

Channelten

KESI YA KUPANGA MATOKEO Kamati ya Nidhamu TFF kutoa maamuzi wiki ijayo

 

tff

Kamati ya nidhamu ya shirikisho la soka nchini imeahirisha kutoa hukumu ya kesi ya upangaji matokeo ya mechi za ligi ya daraja la kwanza kufuatia mapungufu kadhaa ikiwemo kukosekana kwa mashahidi muafaka, na baadhi ya watuhumiwa wa vitendo hivyo kutofika ambapo mwenyekiti wa kamati hiyo Tarimba Abbas Tarimba amesema uamuzi utatolewa Alhamisi ijayo.

 

3 years ago

Michuzi

2 years ago

Michuzi

HAYA NDIO MAAMUZI YA KAMATI YA NIDHAMU KWA TIMU ZILIZOPANGA MATOKEO

Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) chini ya Makamu Mwenyekiti Wakili, Jerome Msemwa leo imetoa maamuzi ya shauri la upangaji wa matokeo wa kundi C kwa Ligi Daraja la Kwanza (StarTimes League).
Akisoma hukumu hiyo baada ya kumaliza kuwahoji viongozi wa vilabu na wenyeviti wa vya vyama vya mpira wa miguu vya mikoa jana, Wakili Msemwa amesema adhabu hizo zimetolewa kwa kufuata Kanuni za Nidhamu za TFF, na nafasi ya kukata rufaa kwa wahusika juu ya maaamuzi hayo ziko...

 

3 years ago

Michuzi

KAMATI YA NIDHAMU TFF YAWAADHIBU JUMA NYOSO NA AGGREY MORRIS


Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imewafungia kati ya mechi tatu na nane wachezaji Juma Nyoso wa Mbeya City na Aggrey Morris wa Azam kutokana na makosa ya kinidhamu waliyoyafanya wakiwa uwanjani.

Nyoso ambaye alilalamikiwa na TFF kwa kumfanyia vitendo vya udhalilishaji mshambuliaji Elias Maguri wa Simba amefungiwa mechi nane za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL). Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Ibara ya 57 na Ibara ya 11 (f) ya Kanuni za Nidhamu za TFF Toleo la...

 

9 months ago

Michuzi

SALUM MKEMI KIKAANGONI APRIL 30,AITWA KAMATI YA NIDHAMU YA TFF

Mjumbe wa kamati ya Utendaji wa Yanga Salum Mkemi (kulia) akiwa sambamba na Katibu Mkuu wa Yanga Charles Boniface Mkwasa.

Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
Mjumbe wa kamati ya Utendaji wa Yanga, Salum  Mkemi ameitwa mbele ya kamati ya nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF) kujibu tuhuma zinazomkabili dhidi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPBL).
Kwa mujibu wa barua hiyo, Mkemi anakabiliwa na tuhuma za kuishutumu bodi ya ligi na kuidhalilisha kamati ya utendaji na usimamizi wa kanuni...

 

1 year ago

Habarileo

Kamati yatengua maamuzi ya TFF

KAMATI ya Rufani za Uchaguzi Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), imetengua maamuzi ya Kamati ya Uchaguzi ya TFF kuhusu uchaguzi wa Chama cha Soka cha Kinondoni, (KIFA) na kudai kamati hiyo imekiuka Katiba ya TFF.

 

2 years ago

Bongo5

Figisufigisu za kamati ya nidhamu ya TFF katika issue ya upangaji matokeo FDL

advctMsemwa

Mwishoni mwa msimu wa 2015/2016 skendo kubwa ya upangaji wa matokeo ya mechi iliikumba ligi kuu ya soka nchini Italia(Serie A) ikivihusisha vilabu vikubwa nchini humo ambavyo ni Juventus ambao walipata ubingwa msimu huo pamoja na AC Milan,Lazio,Fiorentina na Reggina.Upangaji huu wa matokeo ulitokana na vilabu hivi kuhonga waamuzi(chama cha waamuzi)ili wawe wanapangiwa waamuzi wanaowahitaji wao katika michezo yao huku kinara wa mpango huu akiwa ni aliyekua mkurugenzi wa klabu ya Juventus kwa...

 

9 months ago

MillardAyo

VIDEO: Adhabu aliyopewa Haji Manara wa Simba na kamati ya nidhamu ya TFF

Leo April 23 2017 hukumu ya mkuu wa idara ya habari na mawasiliano wa Simba Haji Manara imetangazwa rasmi na kamati ya maadili ya TFF, baada ya mtuhumiwa Haji Manara kushindwa kufika katika kamati ya maadili kujieleza kwa madai amepata dharura na kusafiri kwenda Zanzibar katika matatizo ya kifamilia. Manara wa Simba aliitwa na kamati […]

The post VIDEO: Adhabu aliyopewa Haji Manara wa Simba na kamati ya nidhamu ya TFF appeared first on millardayo.com.

 

6 months ago

Malunde

HAJI MANARA AACHIWA HURU NA KAMATI YA NIDHAMU TFF KUITUMIKIA SIMBA SC
Wote wanaofatilia soka mnajua kwamba Mkuu wa kitengo cha Habari wa Simba SC Haji S. Manara alipewa kifungo kama adhabu na TFF siku zaidi ya 70 zilizopita lakini leo imekuja habari mpya kuhusu kifungo hicho.

Habari yenyewe ni kwamba Haji Manara ameachiwa huru na kamati ya nidhamu ya TFF na sasa ataendelea na majukumu yake kama kawaida.
Simba SC imethibitisha taarifa hiyo kwa kusema “Kamati ya nidhamu ya TFF imemuachia huru mkuu wa kitengo cha Habari wa klabu ya Simba Haji Manara sasa kuendelea...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani