Magufuli afanya mikutano ya kampeni wilaya ya Busega, Bariadi, Itilima na Meatu mkoani Simiyu leo

 Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli aliyenyanyua kofia (katikati) akiwasili katika uwanja wa  CCM mjini Bariadi kwa ajili ya kuwahutubia kwenye mkutano wa kampeni mkoani Simiyu.
 PICHA NA MICHUZI JR-SIMIYU.

 Wananchi wakishangilia kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni mjini Bariadi.  Wananchi wa Nanga wilaya ya Itilima wakishangilia ujio wa Mgombea Urais wa CCM,Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akipita kuwasalimia  Umati wa wakazi wa kijiji cha Mwanhunzi wilaya ya Meatu wakiwa wamekusanyika kwenye mkutano wa kampeni za CCM mjini Meatu,mkoani Simiyu jioni ya leo  Wananchi wakimsiliza Mgombea Urais wa CCM,Dkt John Pombe Magufui alipokuwa akiwahutubia mjini Meatu jioni ya leo.Dkt Magufuli leo ametembelea wilaya ya Busega,Bariadi,Itilima pamoja na wilaya ya Meatu mkoa wa Simiyu Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha Mapinduzi, Dk.Magufuli akiwahutubia wakazi wa mji wa Mwanhunzi jioni ya leo mjini Meatu mkoani Simiyu,Dkt Magufuli alisema kuwa atakapokuwa Rais atakuwa karibu na wananchi wanyonge na kuwa yeye anatoka katika familia ya watu maskini na anajua nini maana ya umaskini,Alisema anatoka kwenye familia ya wakulima na wafugaji  hivyo anajua nini ambacho anatakiwa kufanya kuboresha maisha ya makundi hayo mawili na kwenye hilo atahakikisha anaweka mazingiza mazuri ya matumizi bora ya ardhi.

Alisema Serikali yake kwa sehemu kubwa itakuwa upande wa wananchi wanyonge ili hatimaye wawe na maisha yenye neema na kwenye hilo ana uhakika atafanya kazi nzuri maana kwake yeye ni kazi tu na hakuomba kuwa Rais ili awe mwanasiasa bali anaomba nafasi hiyo kwa kujua anajua namna ambavyo amejipanga kufanya kazi kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania wote.“Nitakuwa upande wenu wananchi wanyonge.Serikali yangu ni marufuku watu wa bodaboda kushikwa na polisi.Serikali yangu haitakuwa ya kunyanyasa mama ntile na kudaiwa kodi za hovyo.Hivyo sitakuwa tayari kuona mama ntile wanatozwa kodi.Najua nitaimarisha ukusanyaji wa kodi kwenye serikali yangu lakini nitawabana wafayabiashara  wakubwa ambapo baadhi yao hawalipi kodi,”alisema Dk.Magufuli.

Aliwataka wananchi kumuamini kwa yale ambayo amekuwa akiyasema kwenye mikutano yake ya kampeni na kuongeza anachoahidi ndicho ambacho atakitekeleza kwenye serikali yake na kwenye maisha yake huwa hataki kutoa ahadi za uongo.

Dk.Magafuli aliweka wazi anapenda mabadiliko yenye tija na kwamba Serikali yake itasimamia nidhamu kwa watumishi wa umma ili wafanye kazi ya kuwatumikia waanchi usiku na mchana na ndio maana atawalipa vizuri na kuongeza hapendi watu wavivu kwenye kazi.

Umati wa wakazi wa kijiji cha Mwanhunzi wilaya ya Meatu wakiwa wamekusanyika kwenye mkutano wa kampeni za CCM mjini Meatu,mkoani Simiyu jioni ya leo.

 Wananchi wa Mwanhunzi mjini Meatu wakifautilia mkutano huo wa hadhara wa kampeni.  Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwanadi wagombea Ubunge na Madiwani kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni  Mwanhunzi,mjini Meatu jioni ya leo mkoani Simiyu.

Wakazi wa Lamadi ndani ndani ya wilaya ya Busega,Mkoani Simiyu wakishangilia jambo kwenye mkutano wa kampeni za CCM zilizofanyika mjini humo leo.

Mgombea Ubunge wa Jimbo la Busega,Raphael Chegeni akiwahutubia wananchi wa Busega mapema leo mchana kwenye mkutano wa hadhara wa Kampeni, katika uwanja wa mpira wa Nyamijashi-Lamadi mkoani Simiyu.

Mwenyekiti wa Wazazi CCM Taifa Ndugu Abdallah Bulembo akimkaribisha mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli kuwahutubia wananchi wa Busega,mapema leo mchana kwenye mkutano wa hadhara wa Kampeni,katika uwanja wa mpira wa Nyamijashi-Lamadi mkoani Simiyu.

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli akisisitiza jambo wakati alipokuwa akiwahutubia wananchi wa Busega mapema leo mchana kwenye mkutano wa hadhara wa Kampeni,katika uwanja wa mpira wa Nyamijashi-Lamadi mkoani Simiyu.

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wananchi wa Busega mapema leo mchana kwenye mkutano wa hadhara wa Kampeni,katika uwanja wa mpira wa Nyamijashi-Lamadi mkoani Simiyu.Dkt Magufuli aliwaomba wananchi hao kuitunza amani waliyonayo na kuwa kuwapuuza wale wote wenye maneno ya kuleta ufarakanishi katika nchi yetu.

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia tiketi ya chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akiwahutubia wakazi wa kijiji cha Mkula,alipokuwa akipita kuwasalimia wananchi hao akielekea Wilayani Busega kwenye mkutano wa hadhara.

 Maandalizi ya kumpokea Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli ndani ya uwanja wa CCM mjini Bariadi yalikuwa kama hivyo pichani.
Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwaaga wananchi wa Mwanhunzi,alipomaliza kuwahutubia kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika jioni ya leo mjini Mwanhunzi,Wilayani Meatu mkoani Simiyu.

Dewji Blog

Read more


Habari Zinazoendana

3 years ago

Michuzi

MAGUFULI AFANYA MIKUTANO YA KAMPENI WILAYA YA BUSEGA,BARIADI,ITILIMA NA MEATU MKOANI SIMIYU LEO.

 Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli aliyenyanyua kofia (katikati) akiwasili katika uwanja wa  CCM mjini Bariadi kwa ajili ya kuwahutubia kwenye mkutano wa kampeni mkoani Simiyu. Wananchi wakishangilia kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni mjini Bariadi  Wananchi wa Nanga wilaya ya Itilima wakishangilia ujio wa Mgombea Urais wa CCM,Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akipita kuwasalimia  Umati wa wakazi wa kijiji cha Mwanhunzi wilaya ya Meatu wakiwa wamekusanyika kwenye mkutano wa kampeni...

 

1 year ago

Michuzi

RAIS DKT. MAGUFULI AWASILI BARIADI MKOANI SIMIYU, AWEKA JIWE LA MSINGI HOSPITALI YA RUFAA YA SIMIYU PIA AFUNGUA BARABARA YA BARIADI-LAMADI (KM 71.8)

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono wakati alipowasili Bariadi kwa ajili ya kuifungua rasmi barabara ya Bariadi-Lamadi yenye urefu wa kilometa 71.8. Wengine katika picha ni Mkuu wa mkoa wa Simiyu Antony Mtaka na Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame MbarawaRais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipunga mkono wakati alipowasili Bariadi kwa ajili ya kuifungua rasmi barabara ya Bariadi-Lamadi yenye urefu wa...

 

3 years ago

Vijimambo

LOWASSA AENDELEA NA ZIARA ZAKE ZA KAMPENI, BARIADI MKOANI SIMIYU LEO

Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akiwapungia mkono wananchi wa Mji wa Bariadi (hawapo pichani) wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Mpira wa Halmashauri Wilaya ya Bariadi Mkoani Simiyu, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni zake, anazoendelea kuzifanya katika Majimbo mbali mbali ya Uchaguzi hapa nchini. Katika ziara hiyo, Mh. Lowassa aliambatana na Waziri Mkuu wa Zamani, Mh. Fredrick Sumaye pamoja na Mwanasheria wa CHADEMA,...

 

1 year ago

Michuzi

RAIS DKT. MAGUFULI AFUNGUA RASMI BARABARA YA BARIADI-LAMADI KM 71.8 BARIADI MKOANI SIMIYU


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 11 Januari, 2017 ameanza ziara ya siku mbili mkoani Simiyu kwa kuwataka wananchi wa mkoa huo na Tanzania kwa ujumla kuwapuuza  watu wanaoendesha siasa alizozitaja kupitwa na wakati kwa kutumia baadhi ya vyombo vya habari kutangaza kuwa Tanzania inakabiliwa na njaa badala ya kuwahamasisha wananchi kufanya kaziDakta Magufuli amesema hayo wakati akizungumza na wananchi katika uwanja wa Shule ya Msingi Somanda mara...

 

2 years ago

Michuzi

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AFANYA ZIARA ITILIMA MKOANI SIMIYU

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua ujenzi wa Maabara katika shule ya Sekondari ya Budalabugija wilayani Itilima akiwa katika ziara ya mkoa wa Simiyu Machi 4, 2016. Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akifungua Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu Machi 4, 2016. (P:icha na Ofisi ya Waziri Mkuu)Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akikagua bwawa la umwagiliaji na maji ya kunywa la kijiji cha Mkoma na Mwalushu wilayani Itilima akiwa katika ziara ya mkoa wa Simiyu, Machi 4, 2016. (Picha...

 

1 year ago

CCM Blog

RAIS DK MAGUFULI AENDA MKOANI SIMIYU KUZINDUA BARABARA YA BARIADI-LAMADI LEO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akiwasalimia wakazi wa Kisesa mkoani Mwanza wakati akiwa njiani kuelekea mkoani Simiyu kwa ajili ya ufunguzi wa barabara ya Bariadi-Lamadi.  Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe magufuli mara baada ya kushuka kwenye kivuko cha Mv Misungwi wakati akitokea Chato mkoani Geita. PICHA NA IKULU

 

2 months ago

Michuzi

MAKAMU WA RAIS AFANYA ZIARA WILAYANI MEATU MKOANI SIMIYU

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akikata utepe kwenye ujenzi wa mradi wa bwawa la maji kwa ajili ya matumizi ya binadamu na mifugo la Mwanjolo wilayani Meatu mkoani Simiyu. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa mradi wa bwawa la maji kwa ajili ya matumizi ya binadamu na mifugo la Mwanjolo wilayani Meatu mkoani Simiyu. (Picha na Ofisi ya Makamu...

 

11 months ago

Channelten

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu awaonya watendaji

e

Mkuu wa Wilaya ya Bariadi mkoani Simiyu, FESTO KISWAGA amewataka watendaji wa Halmashauri ya Bariadi Mjini na Vijijini kuhakikisha fedha zote za makusanyo ya ndani zinazokusanywa na kikosi kazi zinaingizwa kwenye akaunti sahihi kabla ya kufanyiwa matumizi ya aina yoyote ili kudhibiti matumizi yasiyorasmi na unadhirifu wa fedha za umma.

Mkuu huyo wa Wilaya alitoa agizo hilo katika kikao cha Baraza la madiwani kilichofanyika mjini Bariadi, ambapo amesema Serikali wilayani humo kupitia kamati...

 

3 years ago

Michuzi

MAGUFULI AENDELEA NA MIKUTANO YAKE YA KAMPENI WILAYA YA SIKONGE,KALIUA,ULYANKULU NA URAMBO MKOANI TABORA

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kupitia chama cha CCM Dkt Magufuli akiwahutubia wakazi wa mji wa kaliua alipokuwa akiwahutubia wakazi hao katika uwanja wa Kolimba,kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.   Wakazi wa mji wa Kaliua wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM,Dkt Magufuli alipokuwa akiwahutubia. Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akimkabidhi Ilani ya CCM Mgombea Ubunge wa jimbo la Kaliua kupitia chama cha CCM Prof.Juma Kapuya  Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akisalimiana...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani