Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi azindua Kituo cha Zimamoto na Uokozi cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ametahadharisha kwamba uzembe wa aina yoyote  unaoweza kufanywa  na Kikosi cha Zimamoto na Uokozi wakati inapotokea dharura kwa bahati mbaya unaweza kukimbiza huduma za ndege za Kimataifa zinazotumia uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar.Alisema  umuhimu wa Kikosi hicho kuwepo katika maeneo ya Viwanja vya ndege hata Bandarini kwa ajili ya kutoa huduma za uokozi wa masuala ya dharura ni muhimi na mkubwa kwa Uchumi wa Taifa hili.
Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo wakati wa ufunguzi wa Kituo cha Zimamoto na Uokozi cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume ikiwa ni miongoni mwa shamra shamra za maadhimisho ya sherehe za kutimia miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar ya Mwaka 1964.
Balozi Seif alisema  Serikali imekuwa ikichukuwa jitihada mbali mbali za kukiimarisha Kikosi hicho cha Zimamoto ili kiende sambamba  na Teknalojia  ya kisasa pamoja na kufikia  kutoa huduma zenye viwango vya  Kimataifa.Alisema Idara ya  Zimamoto na uokozi  ni nyenzo muhimu katika Taifa lolote Duniani, hivyo ni vyema kwa watendaji wa Taasisi hiyo   wakaandaliwa utaratibu muwafaka wa kupatiwa mafunzo ya mara kwa mara  ndani na nje ya nchi.
  Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikagua gari jipya la zimamoto baada ya  kuzindua rasmi Jengo la Kituo cha kikosi cha zimamoto na uokozi cha uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Aman Karume Zanzibar ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya sherehe za miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar. Gari jipya la Kikosi cha zimamoto na Uokozi likiwa ni moja  miongoni mwa magari Manne yaliyonunuliwa na Serikali Kuu kwa ajili ya Kikosi cha zimamoto na Uokozi Zanzibar. Kamishna wa Kikosi cha Zimamoto na Uokozi Zanzibar Kamishna Ali Abdulla Malimus akitoa Taarifa ya ujenzi wa Kituo cha Zimamoto cha Uwanja wa Ndege wa Zanzibar. Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa, Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ  Bibi Radhia Rashid Haroub akizungumza kwenye uzinduzi wa Jengo la Kituo cha Zimamoto na Uokozi cha Uwanja wa Ndege wa Zanzibar.Balozi Seif Ali Iddi  kati kati waliokaa akiwa katika picha ya pamoja na Baadhi ya Mawaziri wa SMZ, Viongozi wa  Taasisi zinazosimamiz sekta ya mawasiliano pamoja  na Maafisa wa Kikosi cha Zimamoto na Uokozi mara baada ya uzinduzi wa jengo la Kikosi cha Zimamoto Uwanja wa Ndege wa Zanzibar. Picha na – OMPR – ZNZ.Kupata taarifa kamili BOFYA HAPA

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

1 year ago

Zanzibar 24

Balozi Seif : ufunguzi wa Kituo cha Zimamoto na Uokozi cha Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Karume

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alitahadharisha kwamba uzembe wa aina yoyote  unaoweza kufanywa  na Kikosi cha Zimamoto na Uokozi wakati inapotokea dharura kwa bahati mbaya unaweza kukimbiza huduma za ndege za Kimataifa zinazotumia uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar.

Amesema  umuhimu wa Kikosi hicho kuwepo katika maeneo ya Viwanja vya ndege hata Bandarini kwa ajili ya kutoa huduma za uokozi wa masuala ya dharura ni muhimi na mkubwa kwa Uchumi wa Taifa hili.

 

1 year ago

Michuzi

BALOZI SEIF - KUKAMILIKA KWA UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA ABEID AMAN KARUME KUTAKUZA UCHUMI WA NCHI

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema kumalizika kwa ujenzi wa uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Aman Karume  ni mwanzo wa safari ndefu ya mafanikio  kwa Zanzibar katika azma yake ya kuitumia Sekta ya Utalii kuwa muhimili wa Uchumi Mkuu wa Visiwa vya Zanzibar.
Alisema azma hiyo ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imelenga kutafuta njia nyengine mbadala za kukuza uchumi wake na mapato ya Taifa ambayo kwa sasa yanaendelea kutegemea zao moja tu la karafuu.

Balozi...

 

3 years ago

Michuzi

Balozi Seif Ali Idd akagua ujenzi wa Jengo jipya la Abiria wa usafiri wa Anga katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, Zanzibar

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi wa Tatu kutoka kushoto akikagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la Abiria { Terminal 11 } katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar wa Abeid Amani Karume akiwa pamoja na uongozi wa Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar. Kushoto ya Balozi Seif ni Katibu Mkuu Wizara ya Miundombinu na Mawasiliano Zanzibar Dr. Juma Malik Akio na Msimamizi wa ujenzi wa jengo la Abiria katika uwanja wa ndege wa Zanzibar upande wa Serikali ya...

 

1 year ago

Michuzi

MAKAMU WA PILI RAIS ZANZIBAR BALOZI SEIF ALI IDDI AZINDUA JENGO LA MAABARA YA SKULI YA KITOPE

Picha na – OMPR – ZNZ.                             Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliitahadharisha Jamii  kuelewa kwamba maendeleo kwa wana Taaluma wa Fani ya Sayansi iwe Maskulini au vyuoni  yataendelea kuwa ndoto iwapo  hakutakuwa na mipango imara ya  kuimarisha miundombinu kwenye Majengo ya Maabara katika maeneo husika.

Alisema Wazazi kwa kushirikiana na Kamati za Maskuli na vyuo kupitia usimamizi wa Wizara inayosimamia masuala ya Elimu bado wana jukumu la...

 

3 years ago

Vijimambo

NDEGE KUBWA ZAANZA KUTUA UWANJA WA KIMATAIFA WA ABEID AMAN KARUME ZANZIBAR

Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Abeid Amani Karume, ikitowa huduma za ndege kubwa baada ya kumalizika kwa ujenzi wake wa maegesho ya ndege na barabara ya kuondokea, hivi karibuni kama inavyoonekana picha ndege mbili kubwa za Ethiopian airline na Oman Air zikiwa katika uwanja huo kwa wakati mmoja zikitowa huduma ya kusafirisha abiria kupitia uwanja huo' Zanzi News

 

4 years ago

Michuzi

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ahitimisha Mkutano wa 12 wa Chama cha Majaji Wanawake Duniani jijini Arusha

 Makamu wa Kwanza wa Rais wa Mahakama ya Kimataifa Jaji Sanji Mmasenono Monageng Raia wa Jamuhuri ya Botswana akifurahia Tuzo Maalum aliyokabidhiwa na Mwenyekiti wa Chama cha Majaji Wanawake Duniani Jaji Eusebia Munuo kushoto yake kwenye Tafrija ya Wajumbe wa Mkutano huo iliyofanyika Mkoani Arusha.Pembeni yao kulia ni Mkurugenzi  Mkuu wa Chama cha Majaji Wanawake Duniani      { IAWJ } anayefanya kazi zake  Makuu ya Chama hicho Mjini Washington Marekani Jaji J. Winship.  Jaji Mkuu wa...

 

3 years ago

Michuzi

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi awahimiza Watanzania kuitumia fursa inayotolewa na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania

 Mkamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akitia saini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili Makao Makuu ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania yaliyopo Bungo Kibaha Mkoa wa Pwani kwa ajili ya mahafali ya 26  ya chuo hicho.Aliyesimama ni Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania ambae pia ni Waziri wa Katiba na Sheria Tanzania Dr. Asha – Rose Migiro. Balozi Seif akisalimiana na baadhi ya wahitimu wa shahada, stashahada na vyeti wa chuo Kikuu huria cha Tanzania ambao wametokea ...

 

2 months ago

Michuzi

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akutana na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi

 Makamu wa Rais wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano  wa Tanzania Mh. Samia Suluhu Hassan  Kushoto akisalimiana na Kumkaribisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ofisini kwake Ikulu Jijini Dar es salaam.Mh. Samia Suluhu Hassan Kulia akizungumza na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi katika Mikutano na Vikao vya kawaida vya kubadilishana mawazo ya kiutendaji  Serikalini kati ya Viongozi wa ngazi ya Juu ya Serikali za SMT na SMZ. Picha na – OMPR –...

 

4 years ago

Michuzi

Balozi Seif Ali Iddi autaka Uongozi wa Mamlaka ya uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Zanzibar { ZIA } kuwa wabunifu

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ameuagiza Uongozi pamoja na Watendaji wa Mamlaka ya uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Zanzibar { ZIA } kuwa wabunifu katika kuandaa utaratibu mzuri unaokwenda na wakati ambao utaondoa usumbufu kwa wasafiri wanaotumia uwanja huo.
Alisema watendaji hao pia wanapaswa kubadilika na kwenda na wakati kulingana na huduma wanazotoa kwa wasafiri hasa wakizingatia kwamba uwanja huo hivi sasa unaendelea kuimarishwa katika hadhi na kiwango cha...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani