MAKAMU WA RAIS AFANYA MAJUMUISHO YA ZIARA YAKE MKOANI IRINGA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka Viongozi wa mkoa wa Iringa kushirikiana ili kuweza Kuwasaidia wananchi.Makamu wa Rais ameyasema hayo wakati wa kutoa majumuisho ya ziara yake ya kuhamasisha shughuli za maendeleo mkoani Iringa.
Makamu wa Rais alitembelea wilaya ya Iringa, Kilolo na Mufindi ambako kote alishiriki shughuli za kimaendeleo ikiwa kuzindua Vituo vya Afya Kising’a wilaya Iringa, Jengo la Utawala na Madarasa katika Shule ya Sekondari Kilolo, Pia aliweka jiwe la msingi katika Ujenzi wa Maabara na Madarasa katika shule ya sekondari Mgololo na kuweka jiwe la Msingi katika upanuzi wa Kituo cha Afya cha Ihongole kilichopo Mafinga.  Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongoza kikao wakati wa majumuisho ya ziara yake mkoani Iringa, Wengine pichani ni Mkuu wa mkoa wa Iringa Bi. Amina Masenza (kushoto) na Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Bw. Salim Abri Asas. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais). Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza wakati wa kikao cha majumuisho ya ziara yake mkoani Iringa. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi mbalimbali mara baada ya kumaliza kikao cha majumuisho ya ziara yake mkoani Iringa.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

1 week ago

Michuzi

MAKAMU WA RAIS AANZA ZIARA YA SIKU NNE MKOANI IRINGA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo ameanza ziara ya siku nne mkoani Iringa ikiwa na lengo la kuhamasisha shughuli mbalimbali za maendeleo na kuzindua mradi wa kuendeleza utalii ukanda wa kusini mwa Tanzania – REGROW.

Mara baada ya kuwasili mkoani Iringa , Makamu wa Rais alifungua wodi mpya katika Zahanati ya Kising’a ambapo aliwaomba wananchi wote wajiunge na mfuko wa bima ya Afya ili waweze kunufaika na huduma bora za afya.“niwaombe sana...

 

3 years ago

GPL

RAIS KIKWETE AHITIMISHA ZIARA YA MKOA WA MOROGORO, AFANYA MAJUMUISHO

Rais Kikwete akiongoza kikao cha majumuisho baada ya kutembekea Mkoa wa Morogoro. Rais Kikwete akiongea kwenye kikao hicho. Kulia ni Mbunge wa Mvomero na Naibu Waziri wa Maji Mhe Amos Makalla akifuatiwa na Mbunge wa Morogoro kusini ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa huo Mh Innocent…

 

3 years ago

Dewji Blog

Rais Kikwete ahitimisha ziara ya mkoa wa Morogoro, afanya majumuisho na watendaji

Rais Jakaya Mrisho Kikwete akilakiwa na Mbunge wa Morogoro kusini ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM wa mkoa huo Mh Innocent Kalogeris  alipowasili katika ukumbi wa shule ya msingi Gairo ya kwenye kikao cha majumuisho na watendaji wa mkoa huo baada ya kuhitimisha ziara yake ya mkoa wa Morogoro. Rais Kikwete akisalimiana na Mbunge wa Mvomero na Naibu Waziri wa Maji Mhe Amos Makalla Rais Kikwete akiwashukuru wafadhili wa miradi ya afya ya mama na mtoto mkoani Morogoro. Watendaji wa kada...

 

2 years ago

Michuzi

MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AENDELEA NA ZIARA YAKE MKOANI MOROGORO LEO

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akitembelea Hospitali ya Rufaa Mkoa wa Morogoro leo April 17,2016, wakati alipowasili Hospitalini hapo kwa ajili ya kuangalia huduma zinazotolea kwa Jamii katika Hospitali hiyo. Makamu wa Rais yupo Mkoani Morogoro kwa ziara ya kikazi ya siku tatu. kulia Daktari Mfawizi wa Hospitali hiyp Dr. Rita Lyamuya.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akimfariji Bibi Fausta Andreas na...

 

1 year ago

Ippmedia

Makamu wa Rais Mhe Mama Samia Suluhu Hassan aanza ziara yake ya kikazi mkoani Dodoma

Makamu wa Rais Mhe Samia Suluhu Hassan ameanza ziara yake ya kikazi mkoani Dodoma ambapo pamoja na mambo mengine ameiagiza mamlaka ya ustawishaji makao makuu kuacha urasimu na kufanya kazi kwa mazoea katika ugawaji wa ardhi kwa ajili ya ujenzi wakati Dodoma inatarajia kupokea ugeni mkubwa unaotokana na serikali kuhamia mkoani humo.

Day n Time: Jumapili saa 2:00 usikuStation: ITV

 

3 years ago

GPL

WAZIRI LUKUVI AFANYA ZIARA MKOANI IRINGA KUTATUA MIGOGORO YA ARDHI

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mh. William Lukuvi akizungumza na watendaji wa Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) na wale wa sekta ya ardhi na Sekretarieti ya Mkoa wa Iringa ambapo alisisitiza Shirika la Nyumba nchini kuhakikisha kuwa linaboresha mazingira ya Manispaa ya Iringa kwa kuhakikisha kuwa linajenga nyumba bora, pia aliagiza Shirika hilo kufanya utafiti ili liweze kujenga nyumba za gharama nafuu zaidi ili...

 

3 years ago

Michuzi

WAZIRI wa Ardhi William LUKUVI AFANYA ZIARA mkoani IRINGA KUTATUA MIGOGORO YA ARDH

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Mhe. William Vangimembe Lukuvi ameanza ziara ya siku tatu Mkoani Iringa ambapo aliongea na watendaji wa Mkoa wa Iringa kuhusiana na migogoro ya ardhi inayoukumba Mkoa huo . Aidha, Waziri Lukuvi alipata fursa ya kukagua shughuli za Shirika la Nyumba la Taifa na kusikiliza migogoro ya ardhi inayowakabili wananchi wa Manispaa ya Iringa na wilaya za jirani za Kilolo na Mufindi.  Katika ziara hiyo, Waziri Lukuvi amerejea kauli yake aliyoitoa katika...

 

7 months ago

Michuzi

WAZIRI NDALICHAKO AFANYA ZIARA YA KUZITEMBELEA SHULE ZENYE UHITAJI MAALUM MKOANI IRINGA

 Waziri wa elimu na mafunzo ya Ufundi Prof. Joyce Ndalichako alifanya ziara ya ghafla katika shule Mkoani Iringa. Alitembelea shule zinazo fundisha watoto wenye mahitaji maalum za Makala Wilaya ya Mfundi, Shule ya viziwi Mtwivila, Shule ya sekondari ya wasichana Mtwivila na shule ya sekondari ya Lugalo.
 Nia ya ziara hiyo ni pamoja na kukagua vifaa vya kufundishia ambavyo serikali imetoa. Pia alipta fursa ya kusalimia wanafunzi na walimu. Katika ziara hiyo aliongzana na Mkuu wa Mkoa wa Iringa...

 

11 months ago

Michuzi

KAIMU MKURUGENZI MKUU NIDA AFANYA ZIARA KUKAGUA SHUGHULI ZA USAJILI VITAMBULISHO VYA TAIFA MKOANI IRINGA


Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Ndugu Andrew W. Massawe yuko mkoani Iringa kukagua maendeleo ya zoezi la Usajili na Utambuzi wa watu; ambapo pamoja na mambo mengine anatazamiwa kushuhudia sherehe za uzinduzi wa utoaji Vitambulisho vya Taifa kwa wananchi wa Wilaya ya Mufindi na kuzinduliwa kwa kampeni ya Usajili wa wananchi na wageni wenye umri wa miaka 18 na kuendelea wanaoishi mkoani humo.Katika ziara yake; leo amekutana na Mkuu wa Wilaya ya Mufindi Mhe....

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani