MAKAMU WA RAIS MHE. SAMIA AWEKA JIWE LA MSINGI KATIKA MRADI WA UJENZI WA NYUMBA 252 ZA MAKAZI MBWENI ZANZIBAR


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimwa Samia Suluhu Hassan ameuagiza uongozi Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) uchangamkie fursa za uwekezaji wa ujenzi wa nyumba za makazi Tanzania Bara hasa kwenye Makao Makuu ya nchi Dodoma hatua ambayo itauwezesha mfuko huo kuongeza maradufu mtaji wake kwa uuzaji wa nyumba hizo.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ametoa kauli hiyo wakati anaweka jiwe la msingi katika mradi mkubwa wa ujenzi wa nyumba 252 za makazi katika eneo la MBWENI kisiwani Unguja ikiwa ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Makamu wa Rais amesema kutokana na kazi kubwa na nzuri inayofanywa na mfuko huo wa ZSSF hasa ujenzi wa nyumba za makazi ya wananchi ni muhimu kwa mfuko huo kuangalia namna bora ya kwenda kuwekeza katika mikoa mbalimbali ya Tanzania bara kutokana maeneo mengi kuwa na mahitaji makubwa ya nyumba za makazi.

Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan amesema ujenzi wa nyumba za makazi Tanzania Zanzibar ulitokana na fikra na ahadi za hayati mzee Karume kupitia ASP wakati wa haraka za kudai uhuru za kuhakikisha wananchi wanapata makazi bora ya kuishi katika kisiwa cha Pemba na Unguja kutokana na idadi kubwa ya wananchi katika kipindi hicho kuishi katika mazingira yasiyoridhisha.

“Miradi yote hii ni katika kuenzi utekelezaji wa kauli ya Mapinduzi Daima yanayotaka kuleta maendeleo yanayoonekana kwa wananchi kila uchao hususani kipindi hiki tunapotimiza miaka 53 ya Mapinduzi yetu ya Matukufu ya Zanzibar”

Makamu wa Rais pia amewahimiza wananchi wote wachangamkie fursa za kununua na kumiliki nyumba kwa bei nafuu na zenye miundombinu ya kisasa na huduma zote za kijamii ikiwemo viwanja vya michezo.

Kuhusu umiliki wa nyumba kwa Watanzania wanaoishi nje ya nchi, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameziagiza Wizara zinazoshughulika na masuala ya ardhi Tanzania Bara na Zanzibar kutoa ufafanuzi au tafsiri sahihi ya sheria zinazoongoza masuala ya ardhi na umiliki wa nyumba ili kuondoa sintofahamu iliyopo kuhusu wana diaspora kumiliki nyumba.

Amesisitiza kuwa Serikali zote mbili zimekuwa zikisisitiza wana diaspora kuchangia maendeleo ya nchi na kutumia fursa mbalimbali zilizoko nyumbani ikiwemo kununua nyumba zinazojengwa na mifuko na mashirika mbalimbali hivyo ni muhimu kwa wizara zinazoshughulikia masuala ya ardhi kutoa maelekezo haraka ili kuondoa sintofahamu iliyopo kwa sasa kuhusu wana diaspora kulimiki nyumba kwa ajili ya makazi.

Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan amesema ni muda muafaka sasa hivi kwa mifuko hiyo kuwekeza katika sekta ya viwanda hasa kwenye miradi yenye tija kwani viwanda vitatoa fursa kwa vijana wengi kuajiriwa na kuongeza kipato na kuongeza huduma za kijamii na kupunguza umaskini kwa wananchi.

Kwa upande wake, Waziri wa Fedha na Mipngo wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Dkt Khalid Salum Mohamed amemhakikishia Makamu wa Rais kuwa Serikali hiyo inaendelea kumuezi Mzee Karume kwa vitendo kwa kujenga nyumba za makazi na kukarabati nyumba zilizopo ili kuhakikisha wananchi katika Kisiwa cha Pemba na Unguja wanapata makazi bora ya kuishi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akiweka jiwe la msingi kwenye mradi wa ujenzi wa nyumba 252 za makazi zinazojengwa na Shirika la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) zilizopo Mbweni, Zanzibar ikiwa moja ya maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi.Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akihutubia mara tu alipoweka jiwe la msingi kwenye mradi wa ujenzi wa nyumba 252 za makazi zinazojengwa na Shirika la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) zilizopo Mbweni, Zanzibar ikiwa moja ya maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akiwa ndani ya moja ya nyumba hizo 252 mara baada ya kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa nyumba hizo za Shirika la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) zilizopo Mbweni, Zanzibar ikiwa moja ya maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akiangalia ramani ya ujenzi wa nyumba 252 za makazi zinazojengwa  na Shirika la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) zilizopo Mbweni, Zanzibar ikiwa moja ya maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi.

Pichani ni Nyumba za makazi zinazojengwa na Shirika la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) zitakazokuwa na nyumba 252, Viwanja vya Michezo kwa Watoto,Sehemu ya kuogelea na Ukumbi mkubwa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu  Hassan akfurahia jambo na wanafunzi waliojitokeza kushuhudia uwekaji wa  jiwe la msingi la ujenzi wa nyumba 252 za makazi zinazojengwa na Shirika la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) zilizopo Mbweni, Zanzibar ikiwa moja ya maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi.

BOFYA HAPA KWA PICHA ZAIDI

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

1 year ago

CCM Blog

MAMA SAMIA AZINDUA MRADI WA UJENZI WA NYUMBA 252 ZA MAKAZI MBWENI, ZANZIBAR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiweka jiwe la msingi kwenye mradi wa ujenzi wa nyumba 252 za makazi zinazojengwa na Shirika la Mfuko wa Hifadhi ya Jamii Zanzibar (ZSSF) zilizopo Mbweni, Zanzibar ikiwa moja ya maadhimisho ya miaka 53 ya Mapinduzi. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutubia mara tu alipoweka jiwe la msingi kwenye mradi wa ujenzi wa nyumba 252 za makazi zinazojengwa na Shirika la...

 

3 years ago

Michuzi

MHE. LUKUVI AWEKA JIWE LA MSINGI MRADI WA NYUMBA MPYA ZA MAKAZI ZA NHC MJINI SUMBAWANGA

Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi wa tatu kulia na Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Eng. Stella Manyanya wa kwanza kushoto wakikagua mradi wa ujenzi wa nyumba 20 za makazi zinazojengwa na Shirikia la Nyumba la Taifa (NHC) katikati ya Manispaa ya Sumbawanga tarehe 26/03/2015. Kwa mujibu wa Mkurugenzi Mkuu wa shirika hilo Ndugu Nehemia Mchechu nyumba hizo ambazo ni za ghorofa moja zitauzwa baada ya kukamilika ujenzi wake kwa njia ya fedha taslimu na njia ya Mikopo ya...

 

1 year ago

CCM Blog

RAIS DK. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA NYUMBA ZA MAKAZI MAGOMENI KOTA, DAR ES SALAAM, LEO

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli  na muwakilishi wa wananchi  wakifunua pazia  kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi kuanza rasmi ujenzi wa nyumba za makazi eneo la Magomeni Kota jijini Dar es salaam leo
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe na viongozi wengine na muwakilishi wa wananchi  kuashiria kuanza rasmi ujenzi wa nyumba za makazi eneo la Magomeni Kota jijini Dar es salaam leo.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa...

 

1 year ago

Michuzi

RAIS DKT MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI LA UJENZI WA NYUMBA ZA MAKAZI MAGOMENI KOTA JIJINI DAR ES SALAAM LEO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akihutubia wananchi wakati wa sherehe za uwekaji wa jiwe la msingi kuashiria kuanza rasmi ujenzi wa nyumba za makazi eneo la Magomeni Kota jijini Dar es salaam leo.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe na viongozi wengine na muwakilishi wa wananchi kuashiria kuanza rasmi ujenzi wa nyumba za makazi eneo la Magomeni Kota jijini Dar es salaam leo.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt....

 

3 years ago

Michuzi

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA MRADI WA VITUO VYA MAPUMZIKO NA VYOO VYA WASAFIRI KATIKA BARABARA KUU NCHINI, KATIKA KIJIJI CHA IDETERO, MUFINDI-IRINGA.

 Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohamed Mgimwa, akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Makamu wa Rais Dkt. Bilal, kuhutubia wananchi wa Kijiji cha Idetero Wilaya ya Mufindi Mkoa wa Iringa, wakati wa hafla ya uwekaji Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Mradi wa Vituo vya Mapumziko na Vyoo vya Wasafiri katika Barabara Kuu nchini, leo Okt 17, 2015. Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akifunua kitambaa kuweka Jiwe la Msingi la wa Mradi wa Vituo vya...

 

3 years ago

Vijimambo

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA MRADI WA VITUO VYA MAPUMZIKO NA VYOO VYA WASAFIRI KATIKA KIJIJI CHA IDETERO, MUFINDI-IRINGA.

Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Mohamed Mgimwa, akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi Makamu wa Rais Dkt. Bilal, kuhutubia wananchi wa Kijiji cha Idetero Wilaya ya Mufindi Mkoa wa Iringa, wakati wa hafla ya uwekaji Jiwe la Msingi la Ujenzi wa Mradi wa Vituo vya Mapumziko na Vyoo vya Wasafiri katika Barabara Kuu nchini, Okt 17, 2015. Picha na OMRMakamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wananchi wa Kijiji cha Idetero Wilaya ya...

 

1 month ago

Michuzi

MAKAMU WA RAIS AWEKA JIWE LA MSINGI WA UJENZI WA NYUMBA 36 ZA JESHI LA POLISI MFIKIWA CHAKE CHAKE PEMBA

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu akiweka jiwe la msingi la ujenzi wa nyumba za polisi 36 Mfikiwa Chake Chake Pemba. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu akipeana mikono na Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro mara baada ya kuweka  jiwe la msingi la ujenzi wa nyumba za polisi 36 Mfikiwa Chake Chake Pemba. kuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro akizungumza mara baada ya Makamu wa...

 

2 years ago

Michuzi

MAKAMU WA RAIS AWEKA JIWE LA MSINGI UJENZI WA WODI ZA WAZAZI KATIKA HOSPITALI TATU JIJINI DAR ES SALAAM.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akihutbia kwenye hafla fupi ya uwekaji jiwe la msingi ujenzi wa wodi tatu za wazazi na watoto katika Hospitali za Rufaa za Mkoa wa Dar es salaam leo Octoba 11,2016.

Kampuni ya Amsons Gropu imefadhili ujenzi wa wodi za wazazi katika hospitali ya Wananyamala, Amana-Ilala na Temeke, wodi za kisasa zitakuwa vitanda 150 na ujenzi wake utagharimu bilioni 4.5 mpaka ukamilike.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa...

 

2 years ago

Michuzi

RAIS DKT. MAGUFULI AWEKA JIWE LA MSINGI KATIKA MRADI WA UJENZI WA HOSTELI ZA WANAFUNZI WA CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kabla ya kuweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa Hosteli za Wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Wengine katika picha ni Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Mhandisi John Kijazi watatu kutoka (kulia), Waziri wa Elimu Sayansi Teknolojiana Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako wanne kutoka (kulia) watatu kutoka kushoto, Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli, Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam Profesa...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani