MAKONDA AJIBU HOJA YA YEYE KUDAIWA KUHUSIKA PIA DAWA ZA KULEVYA


Mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, Paulo Makonda ametupa jiwe gizani kwa kumjibu Wema Sepetu baada ya siku chache zilizopita kuenea kwa sauti yake mitandaoni akiwa mahabusu huku akimlalamikia mkuu huyo wa mkoa kushindwa kulitaja jina la Agness Masogange kwenye orodha ya kwanza ya watuhumiwa wa madawa ya kulevya.


Akijibu swali kutoka kwa mwandishi wa habari Jumatano hii ofisini kwake wakati akitaja orodha ya pili ya watuhumiwa wa madawa hayo, Makonda amesema, “Ukitaja jina kwanza utakuwa unaingia...

Malunde

Read more


Habari Zinazoendana

2 years ago

MillardAyo

FULL VIDEO: Awamu ya pili ya Makonda na dawa za kulevya, ajibu pia kuhusu Wema na Masogange

Mkuu wa mkoa Dar es salaam Paul Makonda amesimama tena mbele ya Waandishi wa habari Dar es salaam leo February 8 2017 kwenye sakata la ishu ya Dawa za kulevya ambapo ameiita hii ni awamu ya pili ya kuwataja. Pamoja na kuitaja orodha yenyewe, Waandishi wa habari hawakusita kumuuliza kuhusu mwigizaji Wema Sepetu kutoonekana na […]

The post FULL VIDEO: Awamu ya pili ya Makonda na dawa za kulevya, ajibu pia kuhusu Wema na Masogange appeared first on millardayo.com.

 

2 years ago

Bongo Movies

Mbowe, Gwajima Watuhumiwa Kuhusika Dawa za Kulevya

Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam leo ameingia awamu ya pili ya kupambana na dawa za kulevya na ametaja watu wanaotuhumiwa kuhusika na dawa za kulevya kwa namna moja ama nyingine.

Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe na Mchungaji Josephat Gwajima ni miongoni wa watu waliotajwa katika tuhuma hizo na kuwataka kuripoti kituo kikuu cha Polisi Dar es Salaam siku ya Ijumaa wiki hii kwa ajili ya mahojiano.

Wengine aliowataja ni pamoja na Mmiliki wa hotel ya Slip Way, Mmiliki wa MMI Wine anayefahamika...

 

2 years ago

Channelten

Freeman Mbowe Akanusha kuhusika na dawa za kulevya

Mwenyekiti wa taifa wa chama cha demokrasia na maendeleo (CHADEMA), kiongozi wa upinzani bungeni na mbunge wa Hai Freeman Mbowe amekanusha kujihusisha kwa hali yoyote na biashara ya dawa za kulevya na ameahidi kutoa ushirikiano kwa polisi, endapo sheria na taratibu zitafuatwa.

Akizungumza na waandishi wa habari bungeni mjini Dodoma, Bw. Mbowe amesisitiza kuwa hajawaHi kujihusisha kwa namna yoyote biashara hiyo ya dawa za kulevya.

Kiongozi huyo wa upinzani bungeni ameunga mkono juhudi...

 

2 years ago

Ippmedia

Askari 12 wanaotuhumiwa kuhusika na dawa za kulevya wasimamishwa kazi

Mkuu wa jeshi la polisi nchini Inspekta Jenerali wa polisi Ernest Mangu amewasimamisha kazi askari kumi na mbili ambao wametuhumiwa kuhusika na biashara ya dawa za kulevya huku uchunguzi dhidi yao ukiendelea.

Day n Time: Jumamosi saa 2:00 UsikuStation: ITV

 

2 years ago

Mwananchi

Watumishi wawili TRA washikiliwa kuhusika na dawa za kulevya

Mamlaka ya Udhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya inawashikilia watumishi wawili wa Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) kwa kuhusika kupitisha viuatilifu vya kutengeneza dawa za kulevya.

 

2 years ago

Michuzi

WALIOTAJWA KUHUSIKA NA DAWA ZA KULEVYA MKOANI KILIMANJARO HAWA HAPA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro,Kamishna Msaidizi Mwandamizi,Wilbroad Mutafungwa akitaja majina ya watu wanadaiwa kujihusisha na usafirishaji,uuzaji na matumizi ya dawa za kulevya.
Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii Kanda ya Kaskazini.
JESHI la Polisi mkoa wa Kilimanjaro limetaja majina ya watu 47 wanaotuhumiwa kuhusika katika  kusafirisha,kuuza na kutumia dawa za kulevya huku likifanikiwa kukamata misokoto 269 na miche 13 ya Bhangi,pamoja na kilogramu 32.9 za mirungi pia...

 

2 years ago

MillardAyo

VIDEO: Hemed PHD azungumzia kudaiwa kutumia dawa za kulevya

hemedi

Baada ya hivi karibuni kusambaa kwa post kwenye mitandao ya kijamii ikitaja baadhi ya wasanii wa Bongo wanaotumia dawa za kulevya, miongoni mwa wasanii waliotajwa ni pamoja na Hemedy Suleiman. AyoTV na millardayo.com imempata Hemedy Suleiman kuzugumzia madai hayo……>>>‘Nilipoiona hiyo post nilicheka kwa sababu mimi naujua ukweli, ila nilimfikiria zaidi mama yangu mzazi akisikia hizo […]

The post VIDEO: Hemed PHD azungumzia kudaiwa kutumia dawa za kulevya appeared first on...

 

2 years ago

Malunde

JINSI MANJI ALIVYOTUA POLISI BAADA YA KUTAJWA KUHUSIKA DAWA ZA KULEVYA

Mfanyabiashara maarufu nchini, Yusuph Manji amefika kituo cha Polisi cha Kati leo saa 4:54 asubuhi kwa ajili ya mahojiano baada ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda kumtaka afike polisi.
Manji amefika leo badala ya kesho ambapo yeye na wengine 64 walitakiwa kufika kituoni hapo.
Manji ambaye pia ni Mwenyekitu wa Klabu ya Yanga jana alizungumza na waandishi wa habari na kusema hatoweza kufika kituoni hapo siku ya Ijumaa.

Amewasili leo na gari aina ya Range Rover rangi nyeusi .
Manji...

 

2 years ago

Bongo5

Lulu Diva azungumzia tuhuma za kuhusika na biashara ya dawa za kulevya (Video)

Lulu Diva, mrembo anayefanya muziki wa Bongo Flava ambaye alitajwa kwenye orodha ya watu wanaodaiwa kuhusika na madawa ya kulevya amezungumzia alivyochukulia na jinsi wazazi wake walivyojisikia.

Akiongea na Bongo5, mrembo huyo amesema hakutarajia kutajwa kwenye orodha hiyo na ni kitu ambacho kiliwashtua mpaka ndugu zake kwa kuwa hajawahi kujihusisha na biashara hiyo haramu.

“Nilishtuka kwa sababu ni kitu ambacho sikuwahi kutarajia wala kutegemea kwa kuwa nilikuwa sifahamu chochote....

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani