MAMBO MANNE YANAYOATHIRI MALEZI YA MTOTO

KATIKA malezi ya mtoto ya kila siku zipo changamoto ambazo zinachangia kumjenga katika makuzi na nyingine zinaweza zikamuharibu.
Changamoto zote hizi zinapaswa kutatuliwa ili mtoto aweze kukua katika utaratibu mzuri unaoleweka.
Makuzi ya mtoto/watoto ni jukumu la muhimu sana kwa mzazi yo yote katika jamii.Katika tafiti mbalimbali za kisayansi makuzi anayopata mtoto kuanzia umri wa miaka sifuri hadi 12 yanaakisi tabia atakayokuwa nayo katika utu uzima wake.
Kutokana na hali hiyo kuna mambo manne ambayo mzazi unapaswa kuyaangalia ili kuepuka kuathiri makuzi ya mtoto.
Moja ni kumuaibisha,hatua za kinidhamu unazochukua dhidi ya mtoto wako huathiri malezi yake.
Wataalam wa malezi ya watoto wanashauri malezi yetu yawe shirikishi kwa maana ya kwamba kila unapomkataza mtoto kufanya jambo fulani kama vile kutukana watu, utoro shuleni, ugomvi n.k ni vizuri zaidi ukawa unamfahamisha ni kwa nini haifai kufanya jambo fulani.
Lengo ni kumpatia nafasi ya kuhoji/kutafakari/kuelewa badala ya kumshurutisha tu kutekeleza maagizo.
Kwa kufanya hivyo, unampa uwezo wa kupambanua, kuelewa na kujiamini katika maamuzi mbalimbali. Pia hatua kali za kinidhamu kama vile kumchapa mtoto zinaweza kusababisha hofu kwa watoto wako, ambayo huathiri uwezo wao wa kuwasiliana na wewe, walimu na wezake.
Hata hivyo, pia haitakiwi kuwa mpole mno kwa sababu watoto wanaweza kuendelea kwa wakosefu wa nidhamu na kuathiri mwenendo wao katika jamii na shuleni.
Jambo la pili ni mazingira,neno mazingira kwa tafsiri fupi ni vitu vyote vinavyotuzunguka hewa, miti, majengo, watu, wanyama, shule, nyumba za ibada .n.k.
Mazingira ya mtoto yanaathiri ya moja kwa moja kwa mtoto hasa ya nyumbani na shuleni. Muda mwingi wa makuzi ya watoto hutumika nyumbani na shuleni.
Mtoto anayetoka kwenye nyumba ambayo wazazi wake wako katika hali ya ugomvi kila mara, umasikini, utajiri n.k. mambo hayo umuathiri moja kwa moja kimtazamo wa kimaisha.
Jambo la tatu la kuangalia ni mawasiliano,mtoto anapaswa kushirikishwa katika baadhi ya maamuzi ya kifamilia kama vile masuala ya chakula, vinywaji, maongezi n.k.
Ninaposema kushirikishwa katika suala ya chakula ni katika hali ya kujenga tabia ya ushirikishwaji na kumpa uhuru wa maamuzi kumuuliza mtoto leo unataka kula nini mama/baba ni kuonyesha kuthamini mawazo yake.
Pia katika maongezi nina maana mtoto akisema jambo lolote ni muhimu kumsikiliza na siyo vizuri kumpuuza au kumkaripia kwamba anapiga kelele.
Tabia hiyo, itamsaidia kwa kumpatie uwezo wa kujieleza na kujisikia kuthaminiwa na wazazi wake.
Mbali na hayo mfumo wa malezi pia unaweza kumjenga mtoto wako au kumuharibu.
Kuweka ratiba ya kukaa na watoto na kuongea nao na kusikiliza mawazo hayo huwajengea hali ya kujisikia kuathaminiwa na kupendwa na wazazi/walezi na hivyo kuwaongezea furaha na amani.
Pia tabia hii huwajengea hali ya kujiamini na uhuru wa kueleza hisia zao nyumbani na shuleni bila hofu kwa sababu ya Imani ya kupendwa imejengwe kwenye akili zao.
Wazazi tuna jukumu kubwa katika kujenga watoto wetu kisaikologia katika akiwa mdogo,kumjenga ukubwani ni vigumu kwakuwa akili inakuwa imeshakomaa.
NA AZIZA MASOUD-MTANZANIA

Malunde

Read more


Habari Zinazoendana

1 year ago

Mtanzania

MAMBO YA KUZINGATIA UNAPOMPELEKA MTOTO KITUO CHA MALEZI

SONY DSC

Na CHRISTIAN BWAYA,

WATAFITI wa malezi ya watoto wamejaribu kuangalia namna gani huduma za malezi ya kituoni – day care yanavyoweza kuboreshwa. Moja wapo ya watafiti maarufu katika eneo hili ni Taasisi ya Marekani ya Mtandao wa Afya ya Mtoto na Maendeleo ya Utafiti wa Malezi ya Watoto (NICHD).

Maswali ya msingi yanayojaribu kujibiwa na tafiti hizi ni ikiwa kuna uhusiano wa ubora wa huduma zinazotolewa na vituo hivi na makuzi ya mtoto katika nyanja za kiakili, kihisia, kimwili na kistadi;...

 

1 year ago

Mtanzania

MAMBO YA KUZINGATIA UNAPOMPELEKA MTOTO KITUO CHA MALEZI -2

10

Na Christian Bwaya,

MAKALA iliyopita tulizungumzia vigezo vitatu muhimu katika kuboresha huduma za malezi ya watoto vituoni, yaani day care. Tuliona kuwa ni muhimu idadi ya walezi (walimu) iendane na idadi ya watoto wanaonufaika na huduma inayotolewa. Pendekezo la jumla ni kuwa kituo kiwe na walezi wanaoweza kuwatazama watoto wachache kuwasaidia kujua mahitaji yao.

Pia tuliona ni muhimu walezi wawe na mafunzo maalumu ya makuzi na malezi ya watoto kuwawezesha kujua mahitaji mahususi ya...

 

3 months ago

Zanzibar 24

Diamond na Mobeto mambo safi kesi ya malezi ya mtoto

Msanii wa Mwanamuziki wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul maarufu Diamond Platnumz amesema kuwa mazungumzo katika kesi ya malezi ya mtoto wake na Hamisa Mobeto yaliyofanyika leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu katika kitengo cha watoto yamemalizika vizuri kwa wao kufikia maamuzi kuhusu namna ya kumlea mtoto wao.

Diamond amesema yeye na Mobeto hawana shida yoyote, ila kuna watu wa pembeni waliokuwa wakizungumza maneno na kumchochea Mobeto.

“Ikitokea kuna mtafaruku baina ya mtoto, kila mtu...

 

3 years ago

Mwananchi

Lowassa: Mambo manne ya mabadiliko

Mgombea urais wa Chadema, anayeungwa mkono na Ukawa, Edward Lowassa ametaja mambo manne atakayoshughulikia endapo wananchi watamchagua kuongoza Taifa akisema mambo hayo ndiyo msingi wa mabadiliko.

 

2 years ago

Mwananchi

Wataja mambo manne kuongeza kodi

Wakati Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) ikivunja rekodi kwa kukusanya kiasi kikubwa cha mapato mwezi huu ikilinganishwa na mingine iliyopita, wachumi nchini wametaja mambo manne yanayotakiwa kufanywa na Serikali ili kukusanya mapato mengi zaidi.

 

3 years ago

Mwananchi

Mambo haya manne, shemeji atatuachaje?

Neno ‘shemeji’ lilitawala zaidi katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi yaliyofanyika kitaifa mkoani Mwanza baada ya walimu kubeba bango lenye maandishi yanayosomeka “Shemeji unatuachaje?”. Maandishi hayo yalimlenga Rais Jakaya Kikwete.

 

3 years ago

Mwananchi

Kafulila: Mambo manne yalinitia nguvu

Mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila ametaja mambo manne yaliyompa ujasiri wa kulikomalia suala la ukwapuaji wa fedha kwenye akaunti ya Tegeta Escrow hadi kufikia hatua aliyosema imempa faraja katika maisha yake.

 

2 years ago

Mwananchi

Fursa imebeba mambo makuu manne

Semina za Fursa 2016 zilizozinduliwa rasmi wiki iliyopita mkoani Dodoma, leo hii zimehamia jijini Mwanza kwa lengo la kuwanoa wakazi wa jiji hilo.

 

1 year ago

Mwananchi

Bashe: Mambo manne yanayoisumbua CCM

CCM ina miaka 39 tangu izaliwe na imekuwa madarakani wakati wote huo, lakini mbunge wa Nzega  Mjini, Hussein Bashe anaona chama hicho kinasumbuliwa na matatizo manne ambayo kama mwenyekiti wake, John Magufuli atayaondoa, kitakuwa imara zaidi.

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani