Man United yasonga nusu fainali Europa League, Samatta hoi njiani

Usiku wa jana (Alhamisi) zilichezwa mechi nne katika viwanja tofauti kwenye kombe la ligi ya Europa. Timu ya Manchester United imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya ligi hiyo baada ya kufanikiwa kuifunga Anderlecht ua Ubelgiji kwa mabao 2-1 na kufanya kufuzu katika hatua hiyo kwa jumla ya magoli 3-2.

Nayo Ajax ya Uholanzi imefuzu katika hatua hiyo japo ilifungwa kwa mabao 3-2 na Schalke 04 ya Ujerumani, lakini katika matokeo ya Jumla yanaifanya timu hiyo kusonga mbele kwa jumla ya magoli 4-3.

Katika mechi nyingine iliyochezwa usiku huo klabu ya Olympique Lyonnais, imeungana na timu nyingine katika hatua ya nusu fainali baada ya kuitoa Beşiktaş kwa njia ya mikwaju ya penalty ambao walishinda kwa 7-6. Katika dakika 120 za mchezo huo Beşiktaş ilishinda 2-1 na kufanya timu hizo kufungana jumla ya mabao 3-3, ambapo katika mchezo wa kwanza Lyon ilishinda kwa mabao 2-1.

Wakati huo huo timu ya KRC Genk anayoichezea Mbwana Samatta kutoka Tanzania, iliondolewa katika mashindano hayo na Celta de Vigo ya Hispania japo zilitoka sare ya kufungana bao 1-1. Katika mchezo wa mwanzoni, Genk walifungwa mabao 3-2 na kufanya jumla ya matokeo yote kuwa 4-3.

Droo ya timu zitakazo kutana katika hatua hiyo ya nusu fainali inatarajiwa kupangwa leo.

Jiunge na Bongo5.com sasa Usipitwe!! Jiunge nasi kupitia Facebook, Twitter na Instagram ili kupata habari zote za town! Usikose kujiunga na Youtube kuangalia video zote kali kutoka Bongo5!Share on Whatsapp

Bongo5

Read more


Habari Zinazoendana

2 years ago

Zanzibar 24

Europa league: Pogba afanya kweli Man United ikiua, Genk ya Samatta yaiadhibu Bilbao

Paul pogba amefunga magoli mawili, Manchester United ikiibuka na ushindi mnono wa magoli 4 kwa 1 dhidi ya Fenerbahce na kusogea mpaka katika nafasi ya pili katika kundi A.

pogba_fenerbahce

Timu ya Genk ambayo anaichezea Mtanzania Mbwana Samata iliibuka na ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Atletico Bilbao na kukusanya pointi tatu wakiutumia vyema uwanja wao wa nyumbani Cristal Arena, Samatta aliingia dakika ya 56 kipindi cha kuchukua nafasi ya Thomas Buffel.

genk-vs-bilbaoMbwana Samatta kazini

Matokeo ya mechi zote za Europa...

 

2 years ago

Global Publishers

Nusu Fainali ya Uefa Europa League

3330EE6C00000578-0-image-a-15_1460716219507

Droo ya Nusu Fainali ya Uefa Europa League imefanyika na tayari timu nne zilizoingia katika hatua hiyo zimepangwa jinsi zitakavyokutana.

Villarreal imepangwa kuanza mechi ya kwanza ya hatua hiyo kwa kuikaribisha Liverpool wakati ambapo Shakhtar Donetsk itacheza dhidi ya Sevilla.

Nusu fainali ya kwanza inatarajiwa kuchezwa Aprili 28 wakati ambapo mechi za marudio za hatua hiyo zitachezwa Mei 5, 2016.

Fainali ya michuano hiyo inatarajiwa kuchezwa Mei 18, 2016 kwenye Uwanja wa St. Jakob-Park...

 

2 years ago

MillardAyo

Yamenifikia majibu ya droo ya nusu fainali ya UEFA Europa League 2016

uefa-europa-league-trophy

Najua tayari umepata majibu ya droo ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, ila UEFA wametoa tena majibu ya droo ya UEFA Europa league iliyokuwa inahusisha timu za Liverpool, Villarreal, Sevilla na Shakhtar Donetsk. Majibu haya hapa baada ya UEFA kumaliza kuchezesha droo hiyo. Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa […]

The post Yamenifikia majibu ya droo ya nusu fainali ya UEFA Europa League 2016 appeared first on TZA_MillardAyo.

 

2 years ago

Bongo5

Liverpool,Sevilla, Shakhtar Donetsk na Villarreal zatinga nusu fainali Europa League

Michuano ya Europa hatua ya Robo fainali imeendelea tena usiku wa Alhamisi kwa michezo minne, ambapo Liverpool imefanikiwa kutinga hatua ya nusu fainali kufuatia ushindi wa mabao 4 -3 dhidi ya Borrussia Dortmund.

article-3540569-3330FB9C00000578-854_964x384

Magoli ya Liverpool yamefungwa na wachezaji Divock Origi, Philippe Coutinho, Mamadou Sakho na Dejan Lovren.

Na magoli ya Dortmund yamefungwa na Henrikh Mkhitaryan, Pierre-Emerick Aubameyang na Marco Reus .

Sevilla imeiondoa Athletic Bilbao kwa changamoto ya penalti 5-4 kufuatia...

 

2 years ago

Global Publishers

Makundi ya Europa League Haya Hapa, Samatta Awakwepa Man U

CqyHu9sWAAA5eyz.jpg large

Makundi ya Klabu ambazo zitacheza Europa League ikiwemo timu anayoichezea Mtanzania Mbwana Samatta, KRC Genk ya Ubelgiji yamepangwa huku matarajio ya Watanzania wengi ilikuwa ni kumuona pengine Genk ya Samatta wakipangwa kundi moja na Manchester United wanayoichezea Zlatan Ibrahmovic na Paul Pogba.

Genk na Man U wamekwepana kwa Man U kupangwa Kundi A huku Genk wakiwa wamepangwa Kundi F. Endapo akina Samatta watafuzu kwenye kundi lao pia Man U nayo ikafuzu huenda wakakutana hatua yeyote ya...

 

1 year ago

BBCSwahili

Man Utd yaingia robo fainali ya Europa League

Yaichapa Rostov ya Urusi 2-1. Genk ya Samatta nayo yaingia robo fainali

 

2 years ago

Dewji Blog

Man United yaikosa UCL na kuangukia Europa League

Nafasi ya Manchester United kucheza Ligi ya Mabingwa Ulaya UEFA kwa msimu ujao imemalizika katika mchezo wa Bournemouth baada ya kuibuka na ushindi wa goli 3-1 na ikiwa inahitaji kupata magooli 19 ili kuipita Manchester City ambayo walikuwa na alama sawa wakiwa na tofauti ya magoli.

Magoli ya Man United katika mchezo huo wa Bournemouth yalifungwa na Wayne Rooney, Marcus Rashford na Ashley Young na goli pekee la Bournemouth akijifunga beki wa Man United, Chris Smalling baada ya kupigwa mpira...

 

2 years ago

MillardAyo

Hatimae Man United wapata ushindi wa kwanza Europa League

38eeeba200000578-0-image-m-11_1475182540366

Baada ya kuanza vibaya kwa klabu ya Man United katika mchezo wake wa kwanza wa Europa League dhidi ya Feyenoord nchini Uholanzi, usiku wa Septemba 29 Man United walishuka tena dimbani kucheza mchezo wao wa pili wa Kundi A Europa League dhidi ya Zorya. Man United ambao mchezo wa kwanza walipoteza kwa goli 1-0 dhidi […]

The post Hatimae Man United wapata ushindi wa kwanza Europa League appeared first on millardayo.com.

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani