Mawaziri Tanzania wazuru meli za uvuvi Zanzibar

Naibu waziri wa mifugo na uvuvi wa Tanzania Abdallah Khamis Olega akikagua meli ya kampuni ya xinshiji iliyofika zanzibar kwa ajili ya kuomba leseni ya uvuvi wa bahari, kuu nchini Tanzania.

Mawaziri wa uvuvi Zanzibar, Tanzania wakagua meli zinazoomba leseni kwa mujibu wa Utaratibu wa kusajiliwa kwa meli za kigeni hapa Tanzania kwa ajili ya kuendesha shughuli za uvuvi, ni miongoni mwa njia zitakazotoa fursa za ajira kwa Watanzania.

Waziri wa Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Mhe. Hamad Rashid Mohammed, amesema pia kwamba utaratibu huo utasaidia kuimarisha uchumi kwa kukuza pato la taifa.

Waziri wa kilimo, maliasili, mifugo na uvuvi wa zanzibar Hamad Rashid Mohammed, akizungumza na mwakilishi wa kampuni ya Intrechick Zanzibar huko bandarini Unguja.

Akiwa katika ziara ya kuitembelea meli ya uvuvi ya kampuni ya XINSIJI No. 83 kutoka Jamhuri ya Watu wa China iliyofika bandarini Zanzibar, Waziri huyo alisema, Tanzania itapata mabalozi wazuri ikiwa vijana wake wataajiriwa katika meli za aina hiyo.

Meli hiyo ipo kisiwani Unguja kwa ajili ya kufanyiwa ukaguzi ikiwa ni utaratibu wa kawaida na kisheria kabla kupewa leseni ya kuendesha shughuli za uvuvi hapa nchini.

Aidha alisema, kuongezeka kwa meli hizo zinazovua katika bahari kuu samaki wenye viwango, kutawanufaisha wananchi wa Zanzibar pamoja na wageni wanaofika nchini kwa ziara za kitalii ambao hoteli wanazofikia zina mahitaji makubwa ya samaki.

“Meli kama hizi ni muhimu kwa visiwa vyetu pamoja na Tanzania, kwani kuna uhakika wa kupatikana samaki wenye sifa na viwango vinavyokubalika kiafya kwa usalama wa mlaji,” alisema Waziri huyo.

Kwa upande wake, Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Abdallah Hamis Olega, amesema kuwepo kwa meli za uvuvi kutahakikisha rasilimali za nchi hazipotei.

Alisema katika wakati huu ambapo Tanzania iko safarini kuelekea kuwa nchi ya viwanda na uchumi wa kati, kupatikana samaki kwa wingi na wenye kiwango kizuri, kutahamaisha uwekezaji katika viwanda vya  kusindika samaki.

Olega, alisema pia kwamba hatua hiyo inaleta matumaini makubwa kwa vijana wa Kitanzania kufaidika na fursa za ajira, na kuondoa mazoea ya kutokuajiriwa kwa wazalendo katika meli zilizojikita katika uvuvi wa bahari kuu.

Waziri wa kilimo, maliasili, mifugo na uvuvi Zanzibar Hamad Rashid Mmohammed na naibu waziri wa mifugo na uvuvi Tanzania Abdallah Khamis Olega wakipakia samaki katika gari bandarini mjini Zanzibar.

Ziara ya viongozi hao kutembelea meli zilizomo katika hatua ya kuomba leseni za uvuvi wa bahari kuu ni ya kwanza, ambapo kwa sasa meli 17 zimeomba leseni ili kuanza kuvua samaki.

Na: Kijakazi Abdalla Maelezo.

The post Mawaziri Tanzania wazuru meli za uvuvi Zanzibar appeared first on Zanzibar24.

Zanzibar 24

Read more


Habari Zinazoendana

2 years ago

Dewji Blog

Mawaziri wa Kilimo wa Tanzania Bara na Zanzibar wafanya mkutano wa pamoja na watendaji wa Uvuvi bahari kuu

Waziri wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi wa Tanzania Bara na  Zanzibar wamekutana na kufanya mkutano na watendaji wa Mamlaka ya Uvuvi wa Bahari Kuu katika mkutano wa pamoja na watendaji wa Mamlaka hiyo,  uliofanyika Fumba, Zanzibar.

DSC_0025Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo, Maliasili, Mifugo na Uvuvi Zanzibar Juma Ali Juma akiwakaribisha Mawaziri wanaoshughulikia Uvuvi wa Tanzania Bara na Zanzibar katika Mkutano wa pamoja uliozungumzia mikakati ya kuimarisha Uvuvi wa Bahari Kuu Tanzania uliofanyika Mamlaka ya...

 

10 months ago

Zanzibar 24

Meli mpya ya kudhibiti uvuvi harama yawasili Zanzibar

Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imesema itahakikisha inasimamia azma yake ya kudhibiti uvuvi haramu Bahari kuu ili kuweza kufaidika na uchumi unaotokana na mazao ya baharini.

Akizungumza mara baada ya kuwasili kwa meli ya doria hapa Zanzibar inayotoka Madagaska ambayo inaelekea  katika ukanda wa bahari kuu kwaajili ya doria  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya kusimamia Uvuvi haramu wa Bahari mkuu Hosea Gonza Mbilinyi amesema kutokana na hasara inayopatikana  wamejipanga kikamilifu...

 

10 months ago

Zanzibar 24

Zanzibar ipo katika hatua za mwisho za kukodi meli ya Uvuvi

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe,Dkt Ali Mohammed Shein amesema kuwa mashirikiano ya pamoja na nchi ya Djibouti  yatasaidia  kuimarisha a uchumi wa Zanzibar .

Hayo aliyasema wakati alipokuwa akizungumza na Waandishi wa Habari huko Uwanja wa Ndege wa Zanzibar  mara tu aliporudi katika ziara yake ya siku tatu nchini Djibouti.

Alisema katika mazungumzo yao  na Rais wa Djibouti Ismail Omari Guelleh ambae alimualika rasmi kutembelea katika nchi yake walikubaliana...

 

1 week ago

BBCSwahili

Tanzania kutaifisha meli ya uvuvi ya China

Kwa mujibu wa Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amesema meli hiyo ilikamatwa mwishoni mwa mwezi Januari.

 

3 years ago

BBCSwahili

Meli ya uvuvi ya Urusi yazama

Boti ya uvuvi ya Urusi imezama katika visiwa vya Kamchatka,ikiwa na mabaharia wapatao hamsini na wanne ambao wamekufa maji wote.

 

4 years ago

Tanzania Daima

Bandari kudhibiti meli za uvuvi yaja

WIZARA ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi ipo mbioni kujenga bandari ili kuhakikisha meli zinazofanya uvuvi nchini zinakaguliwa na kufuata sheria zote za uvuvi. Kauli hiyo ilitolewa jijini Dar es...

 

4 months ago

BBCSwahili

Korea Kaskazini yaiwachilia huru meli ya uvuvi ya K Kusini

Korea Kaskazini inasema kuwa itaiachilia meli ya uvuvi ya Korea Kusini ilioikamata siku sita zilizopita kwa kuingia katika himaya yake kinyume cha sheria, chombo cha habari kimesema

 

1 year ago

Michuzi

MAWAZIRI UGANDA NA TANZANIA WATEMBELEA ENEO LITAKAPOJENGWA GATI ITAKAYOTUMIKA KUPAKIA MAFUTA KUTOKA UGANDA KWENYE MELI

Waziri wa Nishati na Madini wa Tanzania, Profesa Sospeter Muhongo na Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini wa Uganda, Mhandisi Irene Muloni wametembelea eneo la Chongoleani mkoani Tanga ambako kutajengwa hifadhi ya mafuta pamoja na gati itakayotumika kupakia mafuta kwenye Meli mbalimbali ili kusafirishwa. 
Mafuta hayo yatapakiwa kwenye Meli hizo baada ya kusafirishwa na Bomba kutoka Hoima nchini Uganda kwa ajili ya kusafirishwa nje ya nchi. 
Akiwa katika eneo hilo Waziri wa Nishati na...

 

2 years ago

StarTV

Wavuvi watahadharishwa kuepuka  kutega vyavu za uvuvi njia za meli.

 

Kampuni ya huduma za meli MSC inayotoa huduma zake katika ziwa Victoria imewatahadhariasha wavuvi wanaofanyia shughuli zao ndani ya ziwa hilo kuacha kutega nyavu kwenye maeneo ya njia za meli kwa ajili ya usalama wao na meli.

Tahadhari hiyo imetolewa kufuatia Meli ya Mv Serengeti iliyosimama kutoa huduma zake tangu Januari 08 mwaka huu kutokana na kupata hitilafu katika mfumo wa shafti na majembe upande wa kulia ikiwa safarini kuelekea Bandari ya Bukoba Januari 06 mwaka huu ikitokea Mwanza...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani