Mbowe- Matibabu ya awamu ya tatu ya Tundu Lissu yatafanyika nje ya nchi

Mwenyekiti wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Mhe. Freeman Mbowe amesema kuwa hali ya Mbunge wa Singida Mashariki  mh. Tundu Lissu sasa imezidi kuimarika na kusema atasafirishwa kwa matibabu ya awamu ya tatu siku za karibuni.

Mbowe amesema hayo leo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari kwenye Makao Makuu ya chama hicho, alipokuwa akitoa taarifa ya maendeleo ya Tundu Lissu na kusema mpaka sasa Mbunge huyo anaendelea vizuri na kudai amefanyiwa upasuaji mara 17.

“Tundu Lissu...

Zanzibar 24

Read more


Habari Zinazoendana

11 months ago

Zanzibar 24

Picha:Tundu Lissu akiwasili Ubelgiji kwa awamu ya tatu ya matibabu yake

Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Antipas Lissu amewasili katika uwanja wa ndege jijini Brussels, nchini Ubelgiji ambapo amepelekwa kwa ajili ya awamu ya tatu ya matibabu yake yatakayohusisha mazoezi ya viungo.

Tundu Lissu amewasili jijini hapo akitokea katika Hospitali ya Nairobi, nchini Kenya alikokuwa anapatiwa matibabu kwa muda wa takribani miezi minne sasa, kutokana na kushambuliwa kwa risasi.

Mbunge Tundu Lissu, ambaye pia ni Mnadhimu Mkuu wa kambi ya Upinzani Bungeni, alishambuliwa...

 

1 year ago

CHADEMA Blog

TUNDU LISSU KUSAFIRISHWA KWA MATIBABU NJE YA AFRIKA

Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu anatarajiwa kusafirishwa nje ya nchi kwa matibabu mwezi mmoja kuanzia sasa.Familia yake imesema Lissu baada ya kupata matibabu nje ya nchi amepanga kufanya mambo matano akirejea salama .Akizungumza na waandishi wa habari leo Alhamisi Novemba 23, kaka wa Tundu Lissu, Wakili Alute Mughwai alisema taratibu za kumsafirisha nje ya nchi

 

1 year ago

CHADEMA Blog

TAARIFA KUHUSU MATIBABU YA TUNDU LISSU

Chadema imetangaza kuanzisha kampeni maalumu kuchangisha fedha kwa ajili ya kumgharimia mbunge wake, Tundu Lissu anayeendelea kupata matibabu mjini Nairobi huku matibabu yake yakigharimu Sh 10 milioni kwa siku.Kutokana na ukubwa wa gharama hizo chama hicho tayari kimeziomba jumuiya za kimataifa ikiwamo Ujerumani na Jumuiya ya Umoja wa Ulaya(EU) kuangalia kama inaweza kusaidia matibabu ya

 

10 months ago

Malunde

WABUNGE WAVUTANA MATIBABU YA TUNDU LISSUMbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema amehoji sababu za Bunge kutogharamia matibabu ya Tundu Lissu aliyepo nchini Ubelgiji tangu Januari 7, 2018 akipatiwa tiba ya mazoezi.


Lema ametoa kauli hiyo leo Februari 8, 2018 bungeni mjini Dodoma wakati akichangia taarifa za utekelezaji wa shughuli za kamati za Bunge za Utawala na Serikali za Mitaa, Katiba na Sheria na Sheria Ndogo.

Lissu ambaye ni mbunge wa Singida Mashariki (Chadema) alishambuliwa kwa zaidi ya risasi 30 akiwa ndani ya gari...

 

1 year ago

RFI

Tundu Lissu asafirishwa Nairobi kupata matibabu

Mwanasiasa wa upinzani nchini Tanzania na rais wa chama cha Mawakili cha Tanganyika Tundu Lissu, amesafirishwa jijini Nairobi nchini Kenya kwenda kupata matibabu zaidi.

 

11 months ago

Zanzibar 24

Spika Ndugai azungumzia matibabu ya Mh. Tundu Lissu

Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai amesema serikali inaangalia namna gani watatakiwa kugharamia matibabu ya Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu anayeendelea kupatiwa matibabu nchini Kenya baada ya kushambuliwa kwa risasi Septemba 7 mwaka 2017 mjini Dodoma na watu wasiojulikana.

Spika Ndugai akizungumza na Azam News baada ya familia ya Lissu kulalamika kuwa pamoja na kuandika barua kwa ofisi ya Bunge hakuna hatua zozote zilizochukuliwa.

“Suala lake kidogo ni...

 

1 year ago

Malunde

TAARIFA KUTOKA KENYA HALI YA MATIBABU YA TUNDU LISSU

Mbunge wa Iringa Mjini, Peter Msigwa amesema wamefika salama Nairobi nchini Kenya na Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu anaendelea vizuri na matibabu.

Lissu alipigwa risasi jana Alhamisi nyumbani kwake Area D mjini Dodoma.
Katika ukurasa wake wa mtandao wa Twitter, Mbunge Msigwa amewataka watu waendelee kumuombea Lissu aliyesafirishwa jana usiku kupelekwa kwa matibabu katika Hospitali ya Aga Khan akitokea Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma.
 Follow
peter msigwa @MsigwaPeterTlifika salma...

 

1 year ago

CHADEMA Blog

KUTOA NI MOYO SI UTAJIRI, CHANGIA MATIBABU YA TUNDU LISSU

https://www.gofundme.com/Lissumedicalcare

 

1 year ago

Zanzibar 24

Kauli ya serikali kuhusu gharama za matibabu ya Tundu Lissu

Serikali imesema ipo tayari kugharamia gharama za matibabu ya Mbunge wa Singida Mashariki Mh. Tundu Antiphas Lissu katika hospitali yoyote duniani, iwapo familia yake itaomba serikali ishiriki kuwenye jambo hilo.

Kauli hiyo imetolewa leo na  Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu , na kusema kwamba kama familia itahitaji na ripoti ya madaktari ikionesha kuna ulazima wa Tundu Lissu kupatiwa matibabu zaidi, serikali itasimamia suala hilo.

Hivi karibuni...

 

Share

Trending Now

Zinazosomwa Sasa

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani