MBUNGE MLATA AHAMASISHA MICHEZO MASHULENI

MBUNGE wa viti maalumu Mkoa wa Singida,Marther Mlata amesema ili kukabiliana na utoro mashuleni pamoja na kusuasua kwa elimu,walimu hawana budi kutafuta namna ya kuwavutia watoto kupenda shule kupitia njia ya michezo.Mbunge Mlata alitoa ushawishi huo alipokuwa akiongea na wanafunzi,wazazi na walezi wa watoto wa shule ya sekondari ya Mtakatifu Vincent iliyopo katika Mji mdogo wa Mitundu,wilayani Manyoni,Mkoani Singida. “Ni lazima walimu mtafute namna ya kuwavutia watoto kupenda shule,kwa mfano michezo mtu mwingine anaweza akaenda shule kwa ajili ya michezo tu anasema shuleni huwa kuna mpira,huwa wanacheza ngoja niende”alifafanua Mlata ambaye pia ni Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Singida.Kwa mujibu wa Mlata mwanafunzi pindi anapokwenda shuleni kwa lengo la kushiriki katika michezo,inakuwa ni rahisi pia kumpata kwenye masomo darasani.Aidha Mbunge huyo aliweka bayana kwamba ili kuhakikisha michezo mashuleni inawezekana kuwepo kwa kipindi chote,alitumia hafla hiyo kukabidhi mipira kumi na jezi pea kumi kwa ajili ya kugawa katika shule zilizopo katika kata ya Mitundu.“Mimi sikuwa najua kwamba mmeongoza mmewafunga wanyiramba sisi wakimbu tumewafunga wale wanyiramba goli 3- 0 kwa hiyo nakuja kuhimiza michezo mashuleni”alibainisha Mbunge huyo mpenda michezo.Hata hivyo aliweka bayana kwamba ndiyo maana utoro mashuleni na kusuasua kwa elimu kunakochangiwa na wanafunzi kutembea umbali mrefu kufuata masomo alilazimika kumuagiza Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Itigi kuhakikisha anazisajili shule ambazo bado hazijasajiliwa ili kuwapunguzia watoto adha ya kutembea umbali huo mrefu.Ni Baadhi ya vifaa vya michezo vilivyotolewa msaada na Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Singida,Marther Mlata kwa ajili ya kuhamasisha michezo katika shule zilizopo katika kata ya Mitundu,tarafa ya Itigi,wilayani Manyoni,Mkoani Singida wakati wa sherehe za Juma laa Taaluma lililoandaliwa na kata hiyo.(Picha Na Jumbe Ismailly)

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

4 years ago

GPL

YALIYOJIRI KWENYE MAZISHI YA BABA WA MBUNGE MARTHA MLATA JANA

Mbunge Martha Mlata akifarijiwa na waliohudhuria mazishi ya baba yake mzazi. Kushoto ni Katibu Mwenezi wa Chama cha Muziki wa Injili Tanzania ‘CHAMUITA,’ Stella Joel na mwakilishi wa wasanii wa filamu, Dokii. Baadhi ya wabunge na ndugu wakiwa katika picha ya pamoja mbele ya kaburi la baba mzazi wa Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Singida ambaye pia… ...

 

3 years ago

Dewji Blog

Mbunge wa viti maalumu (CCM) mkoa wa Singida, Bi Martha Mlata achangia ujenzi wa vyoo vya shule ya Kilimani

SAM_2399

Mbunge wa viti maalumu (CCM) Mkoa wa Singida,Bi Marther Mosses Mlata (aliyesimama kwenye jukwaa) akiwaongea na wananchi wa Kijiji cha Ibaga,tarafa ya Kirumi ,Mkoani Singida wakati wa ziara yake ya siku moja wilayani hapa yenye lengo la kukiimarisha chama.

SAM_2404

Mbunge wa viti maalumu (CCM) Mkoa wa Singida,Bi Marther Mosses Mlata(wa pili kutoka kushoto) akikabidhi vifaa vya michezo kwa timu za soka za kata ya Ibaga.

SAM_2415

Katibu wa CCM wilaya ya Mkalama,Bwana Amosi Shimba (wa pili kutoka kushoto)...

 

2 years ago

Dewji Blog

Mbunge wa viti maalum mkoa wa Singida, Mlata ashiriki zoezi la usafi Manispaa ya Singida

IMG_1128

Mbunge wa viti maalum mkoa wa Singida, Martha Mosses Mlata, akishiriki kutekeleza agizo ya rais Dk. John Pombe Magufuli la Watanzania wote kufanya usafi katika maeneo yao, kama sehemu ya maadhimisho ya sherehe za Uhuru kutimiza miaka 54, kwa kufanya usafi kwenye chuo cha wasioona cha mjini hapa. Pamoja na kufanya usafi chuoni hapo, Mlata alitoa msaada wa vifaa mbalimbali ikiwemo viti vya plastiki 150.Thamani ya msaada huo, ni zaidi ya shilingi 6.3  milioni. IMG_1124 IMG_1132 IMG_1142 Mbunge wa viti maalum...

 

1 month ago

Zanzibar 24

Picha: Uzinduzi Mpango wa Mradi wa Michezo Mashuleni Sport 55

Baadhi ya Walimu pamoja na Wanfunzi wao waliohudhuria katika Uzinduzi wa Mpango wa Mradi wa Michezo Mashuleni Sport 55 hafla iliofanyika Baraza la Wawakilishi la Zamani Kikwajuni Wilaya ya Mjini unguja.

 

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,Ali Hassan Mwinyi akisalimiana na Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Michezo Mashuleni Mhe,Balozi Mohammed Ramia mara baada ya kuwasili baraza la Wawakilishi la Zamani kwaajili ya Kuzindua Mpango wa Mradi wa Michezo Mashuleni Sport...

 

2 years ago

Mtanzania

Mlata mwenyekiti mpya CCM Singida

mlataNA SEIF TAKAZA, SINGIDA

MBUNGE wa Viti Maalumu, Martha Mlata, amechaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Singida kuziba nafasi ya Mgana Msindai aliyetimkia Chadema mapema mwaka jana.

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo uliofanyika   mjini hapa jana, Katibu wa Halmashauri Kuu Oganizesheni ya CCM, Dk. Muhammad Seif Khatib, alimtangaza Mlata kuwa mshindi kwa kupata kura 433 (asilimia 50) huku wapinzani wake Mohamed Misanga  akipata kura 261, Juma Kilimba kura 90 na...

 

3 years ago

Vijimambo

MARTHA MLATA AMWAGA SOLA SEKONDARI YA MKALAMA

Na mwandishi wetu
KERO ya maji safi na salama katika Shule ya Sekondari ya Nduguti wilayani Mkalama, imeanza kupatiwa ufumbuzi baada ya Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Singida, Martha Mlata, kubeba jukumu la kusaidia.

Martha, ambaye amekuwa akishiriki kwenye kusaidia huduma za kijamii kuhususan elimu na afya, ametosa sh. Milioni tatu katika kuhakikisha kero hiyo inapatiwa ufumbuzi.

Awali, wanafunzi walikuwa wakilazimika kukatisha masomo kwa saa 40 kwa mwezi ili kufuata maji umbali mrefu hivyo...

 

1 year ago

Michuzi

MBUNGE VENNANCE MWAMOTO AGAWA VIFAA VYA MICHEZO KATIKA JIMBO LA KILOLO


Na Fredy Mgunda,Iringa.

Mbunge wa Jimbo la Kilolo Vennance Mwamoto amegawa vifaa mbalimbali vya michezo kama alivyowahidi kwa Vijana na timu za Jimbo hilo kwa lengo la kukuza vipaji vya wanamichezo na kuwandeleza ili wawe wachezaji bora hapo baadae.
Mwamoto ametekeleza ahadi hiyo katika Vijiji mbalimbali vinanvyounganisha Jimbo hilo la Kilolo katika ziara yake inayoendelea ya kuwashukuru wananchi wake kwa kuweza kumchagua kwa kura nyingi na kwenda kuwaakilisha Bungeni.
Akielezea wakati wa kutoa...

 

3 years ago

Michuzi

Mhe. MARTHA MLATA AMWAGA SOLA SEKONDARI YA MKALAMA, SINGIDA


Na mwandishi wetu
KERO ya maji safi na salama katika Shule ya Sekondari ya Nduguti wilayani Mkalama, mkoani Singida, imeanza kupatiwa ufumbuzi baada ya Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa huo Mhe. Martha Mlata, kubeba jukumu la kusaidia.
Mhe Mlata, ambaye amekuwa akishiriki kwenye kusaidia huduma za kijamii kuhususan elimu na afya, ametosa sh. Milioni tatu katika kuhakikisha kero hiyo inapatiwa ufumbuzi.Awali, wanafunzi walikuwa wakilazimika kukatisha masomo kwa saa 40 kwa mwezi ili kufuata maji...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani