Mfaume kuzihukumu Yanga na Simba kesho

Nusu fainali za kombe la Mapinduzi zitasukumwa kesho katika Uwanja wa Amaan ambapo kamati ya Waamuzi tayari imeshawaweka hadharani Waamuzi watakaosimamia sheria 17 za soka katika michezo hiyo.

 

Nusu fainali ya kwanza itakayopigwa majira ya saa 10:15 za jioni kati ya Azam na Taifa ya Jang’ombe itachezeshwa na Muamuzi wa kati Mohammed Kassim “Edi” akisaidiwa na washika vibendera Nassor Salum Mohd (Line 1), Mustafa Khamis Hasira (Line 2), huku Muamuzi wa akiba akiwa ni Shehe Suleiman Humud na Kamisaa wa mchezo huo ni Issa Ahmada Hijja (Jogoo).

 

Nusu fainali ya pili itakayopigwa majira ya saa 2:15 usiku Derby ya Kariakoo kati ya Simba na Yanga itasimamiwa na Muamuzi wa kati Mfaume Ali Nassor (Wa FIFA) akisaidiwa na washika vibendera Mgaza Ali Kinduli (Line 1 wa FIFA), Haule Mbaraka Haule (Line 2), huku Muamuzi wa akiba akiwa ni Waziri Sheha Waziri na Kamisaa wa mchezo huo ni Ramadhan Nassor Mohd.

The post Mfaume kuzihukumu Yanga na Simba kesho appeared first on Zanzibar24.

Zanzibar 24

Read more


Habari Zinazoendana

3 years ago

Mtanzania

Nkongo kuzihukumu Yanga, Azam

nkongoNA MWALI IBRAHIM NA JULIET MORI (TUDARCO)

MWAMUZI Israel Nkongo anayetambulika na Shirikisho la Soka Duniani (FIFA), anatarajiwa kuamua mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya Azam na Yanga, utakaochezwa Jumamosi hii, Uwanja wa Taifa Dar es Salaam.

Nkongo ana historia kubwa na mechi hiyo kwani aliwahi kuchezesha mechi ya ligi ya miamba hiyo Machi 2012, lakini mchezo huo ulioishuhudia Azam ikitoka kifua mbele kwa kushinda 3-1, ulimalizika kwa Nkongo kupata mkong’oto kutoka kwa wachezaji wa Yanga,...

 

4 years ago

Mwananchi

Wasomali, kuzihukumu Yanga, Azam

Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limeteua waamuzi kutoka Somalia na Sudan kuchezesha mechi ya  Ligi ya Mabingwa Afrika kati ya Yanga na Komorozine na ile ya Kombe  la ShirikishoAfrika kati ya  Azam FC dhidi ya Ferroviario Da Beira.

 

1 year ago

Habarileo

Simba leo, Yanga kesho

MZUNGUKO wa kwanza wa Ligi Kuu Tanzania Bara unafikia tamati leo na kesho.

 

1 year ago

Michuzi

MABONDIA MOHAMED MATUMLA NA MFAUME MFAUME WASAINI KUZIPIGA FEB 5 UWANJA WA NDANI WA TAIFA

Mratibu wa mpambano wa ngumi Jocktan Masasi katikati akiwainuwa mikono juu mabondia Mfaume Mfaume kushoto na Mohamed Matumla Baada ya kusaini mkataba wa kuzipiga feb 2 katika ukumbi wa uwanja wa ndani wa Taifa jijini Dar es salaam.
Mmoja wa Viongozi wa TPBC Joe Anena  katikati akiwainuwa juu mikono mabondia Mfaume Mfaume kulia na Mo0hamed Matumla wakati wa utambulisho wa mpambano wao utakaofanyika Feb 5 katika uwanja wa ndani wa Taifa. kulia kabisa ni mmoja wa wajumbe wa TPBC Chese Masanja 

 

1 year ago

Bongo5

Baada ya kumtwanga Matumla jr, huyu ni bondia mwingine ambaye Mfaume Mfaume anamtaka ulingoni

Takribani wiki mbili zikiwa zimekatika toka lilipofanyika pambano la masumbwi la round 8 lisilo la ubingwa lililofanyika February 5 mwaka huu katika uwanja wa ndani wa Taifa ambapo bondia Mfaume Mfaume alifanikiwa kumtwanga mpinzani wake Matumla jr kwa knockout katika round ya saba na kumsababishia majeraha ya kichwa.

Baada ya pambano hilo kupita hatimaye mbabe huyo anayechipukia kwa kasi katika mchezo wa ndondi mwenye uzito wa kilo 62 ameibuka na kudai kuwa kwa sasa anamhitaji zaidi...

 

3 years ago

Michuzi

SIMBA NA YANGA KUKIPIGA DUBAI KESHO

kesho jumatatu katika jiji la Dubai kutakuwa na mtanange wa kukata na shoka kati ya Wapenzi na washabiki wa timu za Simba na Yanga katika mpambano wa kunogesha bonanza la nyama choma kwenya uwanja wa Al Ahli Stadium saa nne usiku. Utakuwa ni mpambano wa kukata ma shoka kila timu ikijigamba kuondoka na ushindi..... mtoto hatumwi dukani hapo

 

2 years ago

BBCSwahili

Dabi ya Simba na Yanga kupigwa kesho

Ligi kuu ya Tanzania bara itaendelea tena hapo kesho kwa jumla ya michezo sita kuchezwa.

 

1 year ago

Mtanzania

SIMBA, YANGA KUUMANA VIKALI KESHO

*Ni nusu fainali Kombe la Mapinduzi

simba-na-yangaNa MWANDISHI WETU-ZANZIBAR

VIGOGO wa soka nchini Simba na Yanga, kesho wataumana vikali katika pambano la kukata na shoka kwenye hatua ya nusu fainali ya mashindano ya Kombe la Mapinduzi yanayotarajiwa kumalizika Januari 12, mwaka huu.

Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa saa 2:15 usiku katika Uwanja wa Amaan, Zanzibar baada ya Simba kufanikiwa kuongoza Kundi B kwa kufikisha pointi 10 kutokana na ushindi wa mabao 2-0 waliopata jana dhidi ya Jang’ombe...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani