MGOMBEA URAIS TFF FREDRICK MWAKALEBELA AJA NA MAMBO KUMI YA KUINUA SOKA NCHINI


 Mgombea Urais katika Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini, Fredrick Mwakalebela akizungumza na waandihi wa habari jijini Dar es Salaam leo wakati wa akunadi sera zake.
Na Mwandishiwetu , Dar es Salaam
Mgombea Urais katika Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini, Fredrick Mwakalebela ametaja mambo kumi atakayo fanya katika kuinua mpira hapa nchini kama atapata ridhaa ya kuwa Rais wa TFF.

Akizungumza na Waandishi wa Habari wakati uzinduzi wa kampeni yake Mwakalebela amesema kuwa kwa kwanza ataanza na Utawala bora kwa Kuweka misingi ya wazi katika mapato na matumizi ya TFF, Kuzifanya kamati za TFF kuwa huru na kufanya kazi bila kuingiliwa,uingalia upya Agenda ya kupunguza idadi ya wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF ili tuweze kupanua wigo wa wadau wa mpira wa miguu kutuwakilisha kwa wingi katika mkutano mkuu.
Amesema kuwa pia ataweza kusimamia matakwa ya katiba ya shirikisho la mpira wa miguu Tanzania kwa kufanya vikao na mikutano inayotambuliwa kikatiba, kuwa na vyombo imara vya usimamizi ndani ya shirikisho ili kuleta matokeo chanya yenye ufanisi katika soka.

Mwakalebela amesema ataweza kusaidia Timu za Taifa ,wanaume,Wanawake na Vijana kwa Kuwa na makocha wenye viwango vya juu ikiwa ni pamoja na Kurudisha hamasa kwa watanzania kuzipenda timu za Taifa kwa kuongeza idadi kubwa za wachezaji wa ndani kucheza nje ya nchini pamoja na kucheza FIFA date zote na Kuziweka timu kambini kwa wakati
idha katika mpango huu wa pili ataweza Kuanzisha na kusimamia Academy nyingi Tanzania kwa kuhakikisha timu zinapata mechi nyingi za kirafiki na kimataifa kuandaa mashindano ya kimataifa Kuwa na mfadhili wa kugharimia mpango kazi wa timu za Taifa.

Katika mpango wake wa tatu Mwakalebela amesema atashirikiana naVilabu kwa Kupitia upya mikataba ya sasa ili kuiboresha na kuleta tija katika vilabu pia ameadhimia kuongeza idadi ya mashindano ili kuongeza ufanisi kwa wachezaji na Taifa kwa ujumla.

Ameongeza ataweza kuboresha kanuni zetu kuwa zenye tija na ufanisi hili kuongeza mapato ya vilabu kwa kuifanya Bodi ya Ligi kuwa huru nakuweza kuboresha viwanja vya mashindano pamoja na kuongeza idadi ya wadhamini kwa kufanya mpira kuwa starehe na biashara.

Katika kusaidia Vyama vya Soka vya Mikoa Mwakalebela amesema kuwa atafanikisha kupatikana kwa vitendea kazi kama mipira,kompyuta,printers na thamani za ofisini na kuwawezesha kuwapatia Wadhamini wa kudumu kwa ajili ya ofisi kujiendesha na kuwapatia ruzuki za kila mwezi kwa shughuli za chama kwa kuongeza idadi ya mashindano mikoaniKuboresha viwanja na ofisi za mikoani kuwapatia viongozi mafunzo ya kuwajengea uwezo ndani na nje ya nchi.

Katika kusaidia Vyama Shiriki Waamuzi,Tiba Michezo,Waamuzi,Tiba Michezo,Makocha,Wanawake,Sputanza kwa Kutoa Mafunzo ya ndani na nje ya nchi ili kuwajengea uwezo, Kuwapatia ruzuku kwa ajili ya shughuli za kila siku na kuwapatia wadhamini kwa kuwapatia vitendea kazi.
Katika kuboresha Sekretarieti Mwakalebela amesema atawezesha Sekretarieti kuwa na watendaji wenye weledi na uwezo katika maeneo yao ya kazi kwa Kuajiri watendaji kwa kuzingatia sifa na vigezo katika nafasi husika.

Kuongeza uadilifu katika utendaji kazi.
Kusimamia watendaji waweze kutimiza wajibu wao kwa kuzingatia uhitaji wa wadau wa soka nchini.
Kuwajengea uwezo kwa kuwapatia mafunzo ndani na nje ya nchi.
Katika Mahusiano na Wadau Mwakalebela amesema
Ili kupata mafanikio chanya katika maendeleo ya soka ni lazima kuhakikisha wadau wanashirikishwa ipasavyo, hivyo nitahakikisha natambua nafasi ya wadau na kushirikiana nao,Serikali pamoja na Vyombo vyake,Wachezaji wa sasa na wale wa zamani,Wanahabari, Taasisi, Mashirika na Kampuni mbalimbali,Mashabiki na wapenzi wa mpira,Wadhamini na wafadhili,Wamiliki wa viwanja vya michezo, Watanzania wote kwa ujumla.

Katika uwekezaji wa Kitega Uchumi Mwakalebela ametaja kuwa Mafanikio ya mpira yanahitaji rasilimali fedha, kwa kulitambua hilo, nitahakikisha kunafanyika uwekezaji wa jengo la kisasa la kitega uchumi katika uwanja wa kumbukumbu ya Karume ili kuweza kusaidia ufanikishaji .
Amesema Uwezeshaji wa ruzuku kwa wanachama wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania,Kusaidia maendeleo ya mpira wa miguu katika ngazi mbalimbali kutokana na uhitaji,Mafunzo kwa wanachama,Vitendea kazi kwa wanachama,Uboreshaji wa ofisi za TFF kuwa zakisasa zaidi.

Katika kuboresha Bodi ya ligi Mwakalebela amesema Bodi ya Ligi itakuwa huru kwa kuijengea uwezo kwa kuongeza wafadhili na Kuwa na Mpango kazi ambao utasaidia kuifanya bodi hiyo kufanya kazi kwa ufanisi pasipo kuingiliwa.

Katika kuboresha Miundombinu Mwakalebela amesema kuwa kwa Kushirikiana na wamiliki wa viwanja ataweza kuviboresha hili kuwa na nyasi bandia katika kila kanda kwa kuwa na Viwanja vyenye hadhi na sio kuta tu peke yake.

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

3 years ago

Mwananchi

Profesa Mwandosya aja na mambo 10 kuinua uchumi

>Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Kazi Maalumu), Profesa Mark Mwandosya jana alitangaza nia ya kuwania urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,  na kusema kesho atachukua fomu za kuwania nafasi hiyo.

 

1 year ago

Dewji Blog

Serikali yaunga mkono juhudi za TFF kuinua soka la vijana

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imesema kwamba inaunga mkono juhudi za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) katika programu za maendeleo ya vijana, hususani nia yake ya dhati kushiriki michuano ijayo ya Olimpiki itakayofanyika Tokyo, Japan mwaka 2020.

Mkurugenzi wa Michezo, Yusuph Omari ndiye aliyesema hayo mara baada ya kusikia program za TFF kutoka kwa Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi na Makamu Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC),...

 

3 years ago

Mwananchi

Sifa kumi za mgombea urais wa CCM

Hivi karibuni nimesaidiana kimawazo na Watanzania wenzangu katika kufanya uchambuzi wa watu wanaotajwa au waliojitangaza kuwa watawania uteule wa urais kupitia CCM na nalishukuru gazeti hili kwa kukubali kuchapisha maoni yangu.

 

3 years ago

GPL

RAIS KIKWETE ATEUA WAKUU WA WILAYA WAPYA 27, PAUL MAKONDA NA FREDRICK MWAKALEBELA NDANI

Mkuu mpya wa Wilaya ya Kinondoni, Paul Makonda. RAIS Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko ya Wakuu wa Wilaya kwa kuwateua Wakuu wapya 27, kuwahamisha vituo vya kazi 64 na wengine 42 amewabakisha kwenye vituo vyao vya kazi vya zamani. Mkuu mpya wa Wilaya ya Wanging’ombe, Fredrick Wilfred Mwakalebela. Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa OWM TAMISEMI leo mchana (Jumatano, Februari 18, 2015) Waziri Mkuu Mizengo… ...

 

2 years ago

Vijimambo

MJUE MGOMBEA WA KITI CHA URAIS WA MAREKANI NA NINI TUNACHOWEZA KUJIFUNZA KATIKA UCHAGUZI WA URAIS NCHINI TANZANIA

DONALD TRUMP
Na Mwandishi Maalum
Wakati mdahalo wa pili wa wagombea wa chama cha Republican unasubiriwa kwa hamu usiku wa Jumatano tarehe 16 Septemba, ni vyema kuandika machache kuhusu mgombea Donald Trump ambaye anaendelea kuongoza kura za maoni katika kundi kubwa la wagombea wa chama cha Republican kwenye kinyang’anyiro cha kuwania kuingia Ikulu ya Marekani mwishoni mwa mwaka kesho. Katika kuchambua harakati za Bwana Trump za kuusaka uongozi wa juu wa taifa la Marekani pia tumejaribu...

 

3 years ago

Michuzi

NEWS ALERT: RAIS KIKWETE ATEUA WAKUU WA WILAYA WAPYA 27,WAPYA WAKIWEMO SHABANI KISU,PAUL MAKONDA,FREDRICK MWAKALEBELA


*Atengua uteuzi wa Ma-DC 12, awabadilisha vituo 64, awabakiza 42 kwenye vituo vyao vya zamani.
RAIS Jakaya Kikwete amefanya mabadiliko ya Wakuu wa Wilaya kwa kuwateua Wakuu wapya 27, kuwahamisha vituo vya kazi 64 na wengine 42 amewabakisha kwenye vituo vyao vya kazi vya zamani.
Akizungumza na waandishi wa habari kwenye ukumbi wa OWM TAMISEMI leo mchana (Jumatano, Februari 18, 2015) Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema mabadiliko hayo yamesababishwa na kuwepo kwa nafasi wazi 27 ambazo zilitokana...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani