MKE WA TUNDU LISSU AFUNGUKA KWA MARA KWANZA....DEREVA WA LISSU ASEMA HANA KUMBUKUMBU TUKIO LA KUPIGWA RISASI

Nairobi. Kwa mara ya kwanza, Alicia Magabe ambaye ni mke wa Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amezungumzia tukio la mumewe kushambuliwa kwa risasi na kudokeza kwamba haliwezi kuwa limetokana na sababu nyingine isipokuwa kazi ambazo amekuwa akizifanya.
Pia amezungumzia kuhusu afya yake na kueleza kuwa bado siyo nzuri na kuwaomba Watanzania waendelee kumuombea.
Mbali ya Alicia ambaye pia ni mwanasheria, dereva wa Lissu naye amezungumza akisema ameathiriwa kwa kiasi kikubwa na...

Malunde

Read more


Habari Zinazoendana

2 years ago

CHADEMA Blog

PICHA ZA TUKIO LA KUPIGWA RISASI GARI LA MHE TUNDU LISSU

Gari la Tundu Lissu lililopigwa risasi na kumjeruhi Picha za matundu ya risasi zilizoshambulia gari la Tundu Lissu na kumjeruhi Dereva wa Tundu Lissu aliyeshika nguo na viatu baada ya tukio la kushambuliwa kwa risasi gari ya mheshimiwa Tundu Lissu Mwenyekiti wa chadema mheshimiwa Freeman Mbowe akiwa na dereva wa Tundu Lissu

 

2 years ago

Malunde

KAULI YA JESHI LA POLISI KUHUSU TUKIO LA TUNDU LISSU KUPIGWA RISASI


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Gilles Muroto amezungumzia tukio la kupigwa risasi mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Lissu, akiwaomba wananchi wenye taarifa kulisaidia jeshi hilo.

Muroto amesema leo Alhamisi kuwa wanaendelea na uchunguzi wa tukio hilo na wameshafika eneo la tukio nyumbani kwa Lissu.
“Tunaomba mwananchi wenye taarifa atusaidie. Jeshi la Polisi tumeanza uchunguzi, tumefika eneo la tukio na tunaendelea,” amesema.
Kamanda Muroto amesema taarifa za awali zinaonyesha kuna gari...

 

1 year ago

Malunde

MAREKANI : TUPO TAYARI KUCHUNGUZA TUKIO LA TUNDU LISSU KUPIGWA RISASI
Wakati mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu akiwa amewasili nchini Ubelgiji kwa matibabu zaidi, ubalozi wa Marekani nchini umesema uko tayari kusaidia uchunguzi dhidi ya shambulio lake iwapo utaombwa.

Mbali na ubalozi huo, Umoja wa Ulaya (AU) nao umesema unategemea kuona maendeleo mazuri kutokana na uchunguzi wa tukio hilo unaoendelea.

Familia ya Lissu na chama chake cha Chadema vimekuwa vikisisitiza haja ya uchunguzi wa shambulio dhidi ya Lissu lililofanywa na watu wasiojulikana...

 

1 year ago

Malunde

TUNDU LISSU ASIMAMA KWA MARA KWANZA TANGU APIGWE RISASI..ATUMA UJUMBE BOXING DAY


 Kwa mara ya kwanza baada ya miezi mitatu, mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu amesimama.

Mwanasheria huyo wa Chadema, alishambuliwa na kujeruhiwa kwa risasi akiwa ndani ya gari kwenye makazi yake mjini Dodoma Septemba 7,2017 na tangu wakati huo amekuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Nairobi nchini Kenya.

Picha iliyotumwa kwenye mitandao ya kijamii leo Jumanne Desemba 26,2017 inamuonyesha mbunge huyo akiwa amesimama kwa msaada wa madaktari wa mazoezi.

Baadaye Lissu...

 

1 year ago

Malunde

MBUNGE WA CHADEMA AOMBA MBUNGE WA CCM ACHUNGUZWE TUKIO LA TUNDU LISSU KUPIGWA RISASI

Mbunge wa Rombo (Chadema), Joseph Selasini ameomba Mbunge wa Ulanga (CCM), Goodluck Mlinga ahusishwe katika uchunguzi wa tukio la kushambuliwa Tundu Lissu.

Selasini ametoa ombi hilo bungeni mjini Dodoma jana Alhamisi Novemba 9,2017 jioni akichangia mjadala wa mapendekezo ya mpango wa maendeleo wa Taifa kwa mwaka 2018/19 na mwongozo wa maandalizi ya mpango na bajeti kwa mwaka 2018/19.

Mbunge huyo wa Rombo akichangia alisema mbunge huyo alishahusishwa na mauaji ya mpenzi wa mpenzi wake, hivyo...

 

2 years ago

CHADEMA Blog

TUNDU LISSU ASEMA ANAWAFAHAMU WALIOMSHAMBULIA KWA RISASI

Ni waliomshambulia kwa risasiDereva wake aeleza kila kituNa Mwandishi Wetu MBUNGE wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Antipas Lissu ambaye amelazwa hospitalini Nairobi, nchini Kenya anakopata matibabu ya majeraha ya risasi, amesema “ninawafahamu walionishambulia.”Akizungumza kwa taabu akiwa kitandani kwake, jijini Nairobi, Kenya – Jumamosi iliyopita, Lissu amesema, “ninawajua. Nimekutana nao

 

2 years ago

Malunde

TUNDU LISSU APELEKWA KENYA KWA AJILI YA MATIBABU BAADA YA KUPIGWA RISASI


Tundu Lissu akipandishwa kwenye ndege usiku huu***Mbunge wa Singida Mashariki Tundu Lissu ambaye ni mwanasheria mkuu wa CHADEMA na rais wa Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS) amesafirishwa kwenda Nairobi nchini Kenya kwa ajili ya matibabu usiku huu wa kuamkia Ijumaa Septemba 8,2017 baada ya kupigwa risasi akiwa Dodoma nchini Tanzania.

Ndege ya 5H-ETG iliyombeba Tundu Lissu imetoka katika uwanja wa ndege Dodoma saa sita na robo kwa ajili ya matibabu katika hospitali ya Agha Khan jijini...

 

Share

Trending Now

Zinazosomwa Sasa

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani