MKUU WA MKOA WA ARUSHA AMPA WIKI MBILI MKURUGENZI WA JIJI KUHAKIKISHA WALIMU WOTE WANAODAI SEREKALI WALIOPO NDANI YA JIJI LA ARUSHA WANALIPWA FEDHA ZAO


MKUU wa mkoa Arusha Mrisho Gambo amemuagiza mkurugenzi wa jiji la
Arusha, Athumani Kihamia kulipa madeni yote wanayodai walimu ya
milioni 154 ndani ya wiki mbili ambayo wamekuwa wakidai serikali
kuu kwa muda mrefu bila kulipwa na hivyo kusababisha walimu hao
kukata tamaa ya ufundishaji wanafunzi .

Gambo alitioa agizo hilo jana alipokuwa akizungumza na walimu wote wa
shule za msingi 48 zilizopo ndani ya Halmashauri ya jiji la Arusha ,waratibu elimu,wakaguzi elimu pamoja na maafisa elimu kata katika mkutano wa kujua changamoto zinazowakabili walimu hao ili zipatiwe ufumbuzi.

Alisema kuwa walimu wamekuwa wakifundisha katika mazingira magumu na kwamba hadi sasa wapo walimu wa shule za msingi wanaoadai madeni ya likizo na mengineyo yenye gharama ya milioni 154 ambapo serikali kuu
ndio inayopaswa izilipe na hadi sasa hawajalipwa jambo ambalo
linawafanya walimu hao kupoteza muda wa kufundisha na kufuatilia kila
siku madeni hayo.

“mkurugenzi nakupa muda wa wiki mbili deni hili la milioni 154 kwa
ajili ya walimu akikisha zinalipwa haraka iwezekanavyo wakishalipwa
ndio upambane na serikali kuu ufidie hapo zilikotolewa kwani
haiwezekani walimu wapoteze muda kila siku wakifuatilia tu madeni huku
wakiwa wameacha vipindi bila kufundisha wanafunzi wetu”alisema Gambo.

Mkurugenzi wa halmashauri ya jiji hilo,Athumani Kihamia akijibu agizo
hilo alilopewa na mkuu wa mkoa alisema kuwa fedha hizo ambazo ni
madeni hayo zinapaswa zitokee serikali kuu na kwamba atahakikisha
kuwa ndani ya muda wa wiki mbili atazilipa kupitia fedha za ndani za
halamshauri hiyo ili zikija zirejeshwe.

Alifafanua kuwa deni hilo atalipa kutoka kwenye fedha alizoziokoa
ambazo zilikuwa zinalipwa kinyume cha sheria kwa madiwani ambapo
kiasi cha milioni 130 zilizokuwa zinatumika kuwalipia madiwani
mafuta ,simu pamoja na nauli zitaelekezwa kulipa walimu hao madai
yao ili waweze kujikimu na hali wanayokabiliana nayo.

‘‘Fedha ambazo zimeokolewa kwa ajili ya mafuta ni milioni 40.8,fedha
za simu za madiwani milioni 61.2,nauli iliyookolewa milioni 28 ambapo
jumla ni milioni 130 ambazo zimelipwa kinyume hivyo fedha hizi
zinaelekezwa kwa walimu wa msingi na sekondari ikiwa ni madeni
wanayodai halmashuri hii ambapo fedha zinasubiriwa serikali kuu lkni
tumeona tuwatangulizie hizi fedha ili wajikimu na waweze kufundisha
watoto wetu vizuri”alisema Kihamia .

Kihamia alisema kuwa watatanguliza fedha hizo kwa walimu hao wakati
wakiwa wanasubiria fedha toka serikali kuu ili waendelee kujikimu
kwani zimeokolewa katika mianya ambayo zilikuwa zinateketea hivyo
zitaongeza ufanisi kwa walimu katika kufundisha wanafunzi na akili
zao na kufanya akili zao kuzielekeza kwa wanafunzi ili wapate elimu
bora.

Baadhi ya walimu hao wakieleza kero zao walisema kuwa wanakabiliwa na
tatizo la kutopandishwa madaraja kwa waliokaa kazini muda mrefu huku
wengine walioingia kazini muda mfupi wakiwa wanapandishwa madaraja
bila kujua vigezo hivvyo kumwomba mkuu wa mkoa kuingilia swala hilo.

MKUU wa mkoa Arusha Mrisho Gambo akiongea na walimu wote wa shule za msingi 48 zilizopo ndani ya Halmashauri ya jiji la Arusha ,waratibu elimu,wakaguzi elimu pamoja na maafisa elimu kata .
Mkuu wa wilaya ya Arusha Mhe. Gabriel Daqarro akiwa anaongea na walimu waliohuthuria mkutano huo.Habari picha na Woinde Shizza,Arusha.

wa kwanza kushoto ni mkurugenzi wa jiji la ArushaAthumani Kihamia akiwa anasikiliza kwa makini malalamiko ya walimu hao.
picha ya juu na chini ni walimu waliouthuria mkutano huo wa mkuu wa mkoa uliofanyika katika ukumbi wa kimataifa wa mikutano wa AICC uliopo mkoani Arusha.Habari picha na Woinde Shiza-Arusha.

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

2 years ago

Michuzi

MKUU WA MKOA WA ARUSHA AMPA WIKI MBILI MKURUGENZI WA JIJI KUHAKIKISHA WALIMU WOTE WANAODAI SERIKALI WALIOPO NDANI YA JIJI LA ARUSHA WANALIPWA FEDHA ZAO

Habari picha na Woinde Shizza,Arusha  MKUU wa mkoa Arusha Mhe Mrisho Gambo amemuagiza mkurugenzi wa jiji la Arusha Athumani Kihamia kulipa madeni yote wanayodai walimu ya milioni 154 ndani ya wiki mbili ambayo wamekuwa wakidai serikali kuu kwa muda mrefu bila kulipwa na hivyo kusababisha walimu hao kukata tamaa ya ufundishaji wanafunzi. Mhe. Gambo alitioa agizo hilo jana alipokuwa akizungumza na walimu wote wa shule za msingi 48 zilizopo ndani ya Halmashauri ya jiji la Arusha ,waratibu...

 

2 years ago

Michuzi

MKURUGENZI WA JIJI LA ARUSHA AMSIMAMISHA KAZI AFISA MAENDELEO YA JAMII WA JIJI KWA KUSHINDWA KUTEKELEZA MAJUKUMU YAKE


Mkurugenzi wa Jiji la Arusha Ndg. Athumani J. Kihamia amempuzisha kutekeleza majukumu yake Afisa Maendeleo ya Jamii wa Jiji Bi. Mwantumu Dosi kwa tuhuma za kushindwa kutekeleza majukumu yake hivyo kukiuka kanuni za Utumishi wa Umma za mwaka 2003.
Mkurugenzi Kihamia ametoa taarifa hiyo leo tarehe 27.08.2016 baada ya kukamilisha mbio za Mwenge wa Uhuru na kufanya tathmini ya miradi iliyopitiwa na Mwenge na kugundulika kwa dosari zilizojitokeza katika moja ya mradi ambao uko chini ya Idara...

 

3 years ago

GPL

MWANAHARAKATI AVAA GUNIA NA KUTINGA OFISI ZA JIJI KUMDAI MKURUGENZI WA JIJI LA MWANZA AMLIPE FEDHA ZAKE

Mwanaharakati John Masweta akiwa kwenye geti kuu la Makao Makuu ya Jiji la Mwanza.…

 

4 years ago

Michuzi

MKUU WA MKOA ARUSHA AZINDUA WIKI YA NENDA KWA USALAMA BARABARANI, KITAIFA JIJINI ARUSHA LEO.

Washiriki wa maonesho, wananchi mbalimbali wakiwa katika maandamano ya kuadhimisha Wiki ya Nenda kwa Usalama Barabarani iliyozinduliwa katika Kiwanja cha Mpira wa Amri Abeid jijini Arusha leo. Mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mrongo aliyazindua maonesho hayo huku akiwataka madereva nchini wawe makini kwa kufuatia sheria za barabarani ili kuepuka ajali. Kauli mbiu ya Maadhimisho ya mwaka huu ni “Maamuzi yako Barabarani Hatma Yetu-Fikiri Kwanza”. Mgeni rasmi Mkuu...

 

4 years ago

Habarileo

Fedha zakwamisha miradi Jiji la Arusha

HALMASHAURI ya Jiji la Arusha, inakabiliwa na changamoto kubwa ya ufinyu wa fedha za kukamilisha miradi mbalimbali ya barabara kwa wakati na hivyo kusababisha mtandao wa mawasiliano kuwa mgumu.

 

2 years ago

Michuzi

MKURUGENZI WA JIJI LA ARUSHA AAHIDI KUKOMESHA UVAMIZI WA MAENEO YA WAZI

Mkurugenzi wa halmashauri ya Jiji la Arusha(CD),Athuman Juma akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo juu ya mipango kamambe ya kukomesha wavamizi wa maeneo ya wazi ambayo yametambuliwa kuwa ni viwanja 52.Mkurugenzi wa halmashauri ya Jiji la Arusha(CD),Athuman Juma akizungumza namna jinsi walivyojipana kukusanya mapato kwa njia za kieletroniki na mashine za EFD's kuhakikisha mapato hayapotei.Afisa Habari Mwandamizi wa Jiji la Arusha,Nteghenjwa Hoseah akizungumza jambo baada ya...

 

1 year ago

Raia Mwema

Mkurugenzi Jiji la Arusha: Tumeboresha mfumo wa usimamizi, ukusanyaji mapato

Mkurugenzi  wa Jiji la Arusha Athuman Kihamia

Mkurugenzi  wa Jiji la Arusha Athuman Kihamia

MKURUGENZI  wa Jiji la Arusha Athuman Kihamia kipaumbele  cha Halmashauri ya Jiji hilo kwa sasa ni kijiimarisha katika ukusanyaji wa mapato na matumizi yake  ili  kurahisisha maendeleo kwa wananchi wa jiji hilo.

“Kwa kuzingatia umuhimu huo Halmashauri ya Jiji la Arusha kwa sasa imeboresha mfumo wake wa usimamizi na ukusanyaji mapato ikiwamo kusimamia sheria ndogo ndogo za Jiji”alisema Kihamia.

“Hii ni pamoja na kuwakumbusha wananchi wajibu...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani