MWENYEKITI UVCCM PWANI ATOA NENO KWA VIJANA

Na Elisa Shunda, KibitiMWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani (UVCCM),Charangwa Makwiro amewataka vijana wa mkoa huo kutojihusisha na mambo ambayo hayana tija kwa Taifa huku pia akipokea wanachama wapya 60 ambao wameamua kujiuna na umoja huo mkoani Pwani.
Wanachama hao wamejiunga leo wakati wa ziara yake ambayo aliongoza na wajumbe wa baraza kuu la UVCCM Mkoa wa Pwani  wakati anazungmza na wajumbe wa baraza la wilayani Kibiti.
Akizungumza baada ya kuwapokea vijana hao, Mwenyekiti Charangwa Makwiro amewatahadharisha vijana hao kutokubeba ajenda ambazo hawazielewi kwa undani wake kwa kuwaeleza wasifanye jambo ambalo halina faida kwao wala kwa Taifa.
"Serikali ya Awamu ya Tano na Mwenyekiti wetu wa CCM Taifa na Rais Magufuli ana imani kubwa na  vijana,unapokuwa kijana wa CCM unapaswa kuwa mzalendo,uwe na adabu na heshim.Kataa rushwa na kubwa zaidi tufanye kazi kwa bidii.
"Linapotokea jambo tusishabikie pasipo kuelewa undani wa jambo hilo kwani hakuna kitu kibaya kama watu wasioitakia mema nchi yetu kutaka kukuingizia wewe kijana katika ajenda zao ambazo wewe huzifahamu kwa ajili ya kuharibu amani,"amesema.
Makwiro amewakumbusha vijana kutambua wao ndo nguvu na jeuri ya CCM katika kufanikisha mambo yote yanayopaswa kufanyika katika chama hicho na kueleza kujiandaa na uchaguzi wa Serikali za mitaa unaotarajia kufanyika mwaka ujao.
"Tuhakikishe tunajiandaa kwenye uchaguzi huo mapema na vijana mnayo nafasi ya kuwania nafasi za uongozi kwenye Serikali za mitaa.Hivyo ni jukumu letu vijana wa CCM kuanza kujipanga mapema ili tushinde kwa kishindo,"ameongeza.
Pia amekumbusha umuhimu wa vijana kuchangamkia fursa ya mikopo na kwamba Serikali kutoa fedha mikopo kwa vijana wote ili kufanya shughuli za kimaendeleo na kuwashauri vijana kutengeneza vikundi ili kufanya ujasiriamali.
"Itapendeza pia kama mtakuwa na CV(wasifu) zenye maelezo yao ya taaluma na vipaji mlivyonavyo na kuziwasilisha katika ofisi ya wilya ya umoja huo wa vijana ili hata nafasi za kazi zikitokea wilayani na kwingineko itakuwa rahisi kupata ajira serikalini na maeneo mengine,"amesema.
Makwiro amewaahidi vijana wilayani Kibiti kuwa kwa kumchagua yeye kuwa Mwenyekiti UVCCM Mkoa wa Pwani pamoja na wajumbe wa baraza kuu la mkoa huo atahakikisha anatumia rasirimali zake binafsi, akili zake kuhakikisha jumuiya hiyo ya vijana inatatua baadhi ya changamoto za vijana hao,"amesema.
Mjumbe wa Baraza Kuu la UVCCM Taifa Mkoa wa Pwani,Ramadhan Mlao amesema yupo bega kwa bega na Makwiro ili kutekeleza maagizo yaliyotolewa na Mwenyekiti wa umoja huo taifa, Kheri James kuwasaidia vijana kujikwamua kiuchumi.
Akizungumza kwa niaba ya wajumbe wa baraza la wilaya hiyo, Mwenyekiti UVCCM wa Kibiti,Juma Ndaluke amesema wamepokea maelekezo yote kutoka kwa viongozi hao wa Mkoa na ameahidi kuyatekeleza kwa jinsi watakavyojaliwa huku akisisitiza yeye na  wajumbe wake hawatowaangusha katika uboreshaji wa utendaji kazi wa umoja huo wa vijana.  Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Pwani, Charangwa Seleman Makwiro (katikati) akizungumza na wajumbe wa mkutano mkuu wa baraza la umoja wa vijana (UVCCM) Wilaya ya Kibiti mkoani Pwani. Kushoto ni Mjumbe wa Baraza Kuu UVCCM Taifa wa Mkoa wa Pwani,Ramadhan Mlao na Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Kibiti,Juma Ndaluke. Picha zote na Elisa Shunda   Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Pwani, Charangwa Seleman Makwiro (katikati) akimkabidhi Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Kibiti, Juma Ndaluke (wa pili kulia) kadi 200 na kanuni 100 kwa baada ya kuzungumza na wajumbe wa mkutano mkuu wa baraza la umoja wa vijana (UVCCM) Wilaya ya Kibiti mkoani Pwani. Wa kwanza kushoto ni Mjumbe wa Baraza Kuu UVCCM Taifa wa Mkoa wa Pwani ,Ramadhan Mlao.Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Kibiti, Juma Ndaluke akizungumza katika mkutano huo. Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Pwani, Charangwa Seleman Makwiro (katikati) akimkabidhi Yusuph Kimbe (kulia) kadi ya Umoja wa Vijana baada ya kujiunga.

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

3 months ago

Michuzi

VIJANA WA BAGAMAYO TEMBEENI KIFUA MBELE KUMSEMEA RAIS MAGUFULI -MWENYEKITI WA UVCCM MKOA WA PWANI


NA ELISA SHUNDA-BAGAMOYO.
WANACHAMA wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) wa Wilaya ya Bagamoyo wametakiwa kutembea kifua mbele huku wakijiamini na kuwaelezea vijana wenzao miradi mbalimbali mikubwa inayofanyika hapa nchini chini ya uongozi wa Mwenyekiti wa CCM Taifa na Rais,Dk.John Magufuli katika kutimiza malengo ya Tanzania ya Viwanda kwa kujenga barabara za juu (Fly Over),uboreshaji wa miundombinu,mradi wa umeme vijijini (REA),elimu bure shule za msingi na...

 

2 months ago

Michuzi

MWENYEKITI UVCCM MKOA PWANI AWATAKA VIJANA KUKITUMIKIA CHAMA KIPATE USHINDI WA KISHINDO MWAKA 2019/2020

NA ELISA SHUNDA,MAFIA .

VIONGOZI wanaounda Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wilayani Mafia wametakiwa kujitoa kwa nguvu,mali na rasilimali zao katika kukitumikia chama hicho na kuhakikisha kinafanya vizuri katika uchaguzi ujao wa serikali za mitaa mwakani na uchaguzi mkuu 2020 ili CCM katika wilaya hiyo kiibuke na ushindi wa kishindo.

Hayo yamesemwa na Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Pwani, Charangwa Selemani Makwiro wakati alipofanya...

 

4 weeks ago

Zanzibar 24

Mwenyekiti jumuiya ya vijana CUF atoa tahadhari kufuatia kutekwa kwa vijana 6 wa CUF Pemba

Mwenyekiti wa Jumuiya ya vijana ya Chama cha wananchi CUF Jimbo la Tumbe Nd. Mohd Nassor Suleiman amewataka wanachama na wananchi kuwa na tahadhari katika maeneo yao kufuatia kuripotiwa kutekwa vijana 6 wa CUF huko  Mtambwe hivi karibuni.

Akizungumza na vijana wa chama hicho huko katika ukumbi wa Bi Awena Hool Tumbe Wilaya ya Micheweni Mkoa Wa Kaskazini Pemba amesema nivyema kila mmoja kuwa na tahadhari kwani tukio hilo linaonesha taswira mbaya hasa kwa hali ya kisiasa ilivyo hapa...

 

2 years ago

Michuzi

Mwenyekiti wa CCM Shinyanga Awafuturisha Waislam Mkoa Wa Shinyanga,Sheikh Mkuu Apongeza,Askofu Atoa Neno Kwa Magufuli

Juni 29,2016 kumefanyika tukio muhimu mjini Shinyanga ambapo Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Shinyanga ndugu Erasto Kwilasa (pichani) amewaandalia chakula cha pamoja “futari” waumini wa dini ya kiislamu mkoa wa Shinyanga ikiwa ni sehemu ya kuutukuza mwezi mtukufu wa Ramadhani. Tukio hilo limefanyika leo jioni/usiku kuanzia  katika Ukumbi wa NSSF mjini Shinyanga na kuhudhuriwa na waumini na viongozi wa dini  wakiongozwa na Sheikh Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ismail Habibu Makusanya.

 

3 years ago

Habarileo

Mwenyekiti mstaafu UVCCM atoa somo

MWENYEKITI mstaafu wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) Dodoma Mjini, Robert Mwinje, amewahamasisha vijana kuwahoji wagombea wa nafasi mbalimbali katika Uchaguzi Mkuu ujao kama wana sera zitakazowasaidia vijana.

 

4 years ago

Dewji Blog

Jumuiya ya umoja wa vijana (UVCCM) yawaonya viongozi CCM mkoa kuacha kuwagawa vijana kwa maslahi yao

KATIBU

Katibu Mkuu wa UVCCM Wilaya ya Mkalama Florian Panga akizungumza kwenye kikao hicho.

Na Hillary Shoo, MKALAMA.

JUMUIYA ya Umoja wa Vijana (UVCCM) imewataka viongozi mbalimbali wa CCM Mkoa wa Singida kuacha kuwagawa vijana kwa maslahi yao binafsi kwani kufanya hivyo ni kuleta mpasuko na makundi miongoni mwao.

Changamoto hiyo imetolewa Wilayani hapa na Katibu Mkuu wa UVCCM Mkoa wa Singida, Ramadhani Kapeto wakati akifunga kambi ya vijana wa Wilaya ya Mkalama ya siku saba kwenye shule ya...

 

3 years ago

Michuzi

Makamu Mwenyekiti wa UVCCM achaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana Afrika Kanda ya Afrika Mashariki

 Makamu Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM),Mboni Mhita (katikati) akizungumza na waandishi (hawapo pichani) pamoja na baadhi ya vijana wa Mkoa wa Dar es salaam leo,juu ushindi wake alioupata katika Uchaguzi wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana Barani Afrika,ambapo yeye amechaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Umoja huo kwa upande wa Afrika Mashariki.Uchaguzi huo ulifanyika Mwishoni mwa mwezi uliopita katika Jiji la Johannesburg,nchini Afrika Kusini.Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa...

 

5 months ago

Malunde

MAGUFULI AWAPONDA UVCCM....APIGILIA MSUMARI RUSHWA ILIYOMPELEKA MAHABUSU MWENYEKITI WA UVCCM


Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk John Pombe Magufuli akisalimiana na baadhi ya wanachama wapya wa chama hicho.
****

RAIS John Magufuli amepigilia msumari kukamatwa kwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama cha Mapinduzi (UVCCM), Sadifa Juma Khamis akidaiwa kutoa rushwa akisema atashangaa kama atachaguliwa mwenyekiti anayewahonga fedha wamchague.
Sadifa ambaye pia ni mbunge wa Donge alikamatwa jana na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru)...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani