MWENYEKITI WA CUF TAIFA PROF.LIPUMBA AHIMIZA KUWEKEZA KWENYE SEKTA YA ELIMU

Na Jumbe Ismailly SINGIDA Jan,11,2018 Kuwekeza 

CHAMA Cha Wananchi (CUF) kimesema kuwa pamoja na serikali ya awamu ya tano kufuta ada katika shule za msingi hadi kidato cha nne,lakini sekta ya elimu bado haijawekeza ipasavyo kwenye sekta hiyo kutokana na changamoto mbali mbali zinazoendelea kuikabili sekta hiyo mpaka sasa.
Mwenyekiti wa CUF Taifa,Prof.Ibrahimu Lipumba aliyasema hayo kwenye mkutano wa kampeni za uchaguzi mdogo wa jimbo la Singida wakati wa kumnadi mgombea ubunge wa chama hicho,Delphina Mngazija uliofanyika katika Kijiji cha Ughandi,wilaya ya Singida vijijini.
Alifafanua kiongozi huyo wa kitaifa kwamba serikali inapowekeza kwenye sekta ya elimu kwa sasa ni lazima pia iwekeze kwenye matumizi ya kompyuta kwenye shule zilizopo na kuongeza kuwa elimu ya siku hizi inakwenda sambamba na mitandao ya kompyuta.
Kwa mujibu wa Prof.Lipumba nchi nyingi pamoja na nchi maskini zimewekeza mara tu watoto wanapoanza hujifunza pia kutumia kompyuta na kwamba matumizi ya kompyuta ni sawa kama vile kujifunza lugha.“Mtoto mdogo ni mwepesi kujifunza lugha kuliko mtu mzima,hata mtu mzima ukiwa na simu mwanao anaweza kujua kuitumia ile simu kuliko wewe mtu mzima.
Na kuongeza pia kuwa wataalamu wa mambo ya watoto wanasema kuwa mtoto anapokuwa ndani ya tumbo la mama yake na kwa miaka miwili ya kwanza ndizo zinazompa mtoto fursa ya kujenga maungo yake,ya kujenga ubongo wake,ya kujenga kinga ya mwili.”alisisitiza Prof.Lipumba.Prof.Lipumba hata hivyo alitumia fursa hiyo kuishauri serikali kuangalia uwezekano wa vituo vya afya vilivyopo kuwa na virutubisho muhimu na kwamba kutokana na taarifa za serikali kuna tatizo kubwa la akina mama wajawazito kutokuwa na damu ya kutosha.
“Kwa mujibu wa taarifa za serikali kuna tatizo kubwa la akina mama wajawazito kutokuwa na damu ya kutosha,hawana madini ya chuma ndani ya damu yao hii inasababisha watoto wasipate lishe bora na watoto wa Tanzania wamedumaa.”alibainisha Mwenyekiti huyo.
Naye Katibu wa CUF Mkoa wa Singida,Selemani Ntandu aliwatahadharisha wanachama wa CUF pamoja na wale wa CCM waishio katika Kijiji na kata ya Ughandi kwa ujumla kwamba endapo watamchagua mgombea wa CCM,Justine Monko wakae wakijua kwamba makao makuu ya wilaya hiyo yatahamishwa kwenda Kijiji cha Sagarumba badala ya Ilongero.
Aidha katibu huyo alisisitiza kwamba wananchi wa jimbo la Singida kaskazini wanahitaji huduma bora za kijamii zinaboreshwa na kuonyesha masikitiko yake kwamba hivi sasa miundombinu ya barabara kwenye maeneo mengi hairidhishi kabisa jambo ambalo halishughulikiwi na watu waliokabidhiwa dhamana ya utekelezaji wa ilani ya chama hicho.Mwenyekiti wa CUF Taifa,Prof.Ibrahimu Lipumba akiwasilimia wananchi pamoja na wanachama wa chama hicho katika Kijiji cha Ughandi,wilaya ya Singida vijijini alikwenda kumnadi mgombea ubunge wa chama hicha,Delphine Mngazija.Mwenyekiti wa Taifa wa CUF,Prof.Ibrahimu Lipumba akiwasisitiza wananchi wa vyama vyote vya siasa kumpigia kura mgombea wa chama hicho,Delphina Mngazija kwa kuwaonyesha mfano wa karatasi la kupigia kuraMwenyekitti wa CUF Taifa,Prof.Ibrahimu Lipumba akimnadi mgombea ubunge wa jimbo la Singida kaskazini,Delphina Mngazija kwenye mkutano wa kampeni uliofanyia katika Kijiji cha Ughandi,Singida vijijini.Mgombea ubunge wa CUF,Delphina Mngazija alipokuwa akiomba kura kwa wananchi wa kijiji na kata ya Ughandi kwa ujumla na kuwaahidi kwamba endapo wataampaa ridhaa ya kuwa mwakilishi wao atakwenda kupigania hadi kuondoa kero zinazowakabili wanawake wajawazito za kununua beseni,ndoo na mipira ya kujifungulia kwenye vituo vya kutolea huduma vuilivyopo kwenye maeneo yao.Baadhi ya wanafunzi wa shule ya msingi Ughandi wakimsikiliza mwenyekiti wa taifa wa CUF,Prof.Ibrahimu Lipumba alipokuwa nakiwahutubia wananchi wa Kijiji cha Ughandi kumuombea kura mgombea wa ubunge wa chama hicho ili aweze kuchagulia ifikapo jan,13,2018.(Picha zote Na Jumbe Ismailly)

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

1 year ago

Michuzi

PROF. MBARAWA AHIMIZA SEKTA BINAFSI KUWEKEZA NCHINI

Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa amewataka wadau wa Sekta binafsi kujitokeza na kushirikiana na Serikali katika uwekezaji wa ujenzi wa miradi ya usafirishaji nchini.
Aidha amewataka wadau hao kuendelea kufadhili utekelezaji wa miradi ya maendeleo iliyo chini ya sekta hiyo ili kuchochea fursa za maendeleo.

Hayo ameyasema wakati akifungua mkutano wa 10 wa mashauriano wa wadau wa Sekta ya Uchukuzi na usafirishaji uliofanyika jijini Dar es Salaam.

“Michango ya Sekta...

 

2 years ago

Bongo5

Prof Lipumba adai kuwa yeye bado ni mwenyekiti halali wa CUF

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi CUF, Prof Ibrahim Lipumba amesema yeye ndiye mwenyekiti halali wa chama hicho licha ya Baraza Kuu la chama hicho kutangaza kumsimamisha uanachama, yeye na wenzake 10.

Profesa-Ibrahim-Lipumba-640x559

Lipumba akiongea na kituo cha ITV amesema kikao kilichokaa jana visiwani Zanzibar na kufanya maamuzi ya kuwasimamisha uanachama, hakikuwa halali na kilikuwa nje ya katiba ya CUF, sababu mojawapo ikiwa ni kuwekwa kando kwa Naibu Katibu Mkuu Bara, Magdalena Sakaya.

“Hicho kikao hakikuwa...

 

2 years ago

Dewji Blog

Jaji Mutungi asisitiza kumtambua Prof. Lipumba kama mwenyekiti wa CUF

Msajili wa Vyama vya siasa Jaji Francis Mutungi, amesisitiza kwamba ana mtambua Prof. Ibrahim Lipumba kama mwenyekiti halali wa chama hicho na Maalim Seif Sharrif Hamad kama katibu mkuu wa chama hicho.

Akizungumza kwa simu na JAMVI LA HABARI kuhusiana na tuhuma za ofisi yake kuandika barua kumdhamini Prof. Lipumba kufungua akaunti na kuhusu taarifa inayosambaa mitandaoni juu ya Onyo la Mtatiro juu ya jambo hilo kwake msajili amesema mpaka sasa hamfahamu mtatiro kwa kuwa CUF ni chama kimoja...

 

1 year ago

Michuzi

Mwenyekiti wa CUF Prof.Ibrahim Lipumba akutana na Makamu wa rais Mhe. Samia Suluhu Hassan


 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba alipomtembelea ofisini kwake, Ikulu Jijini Dar es Salaam leo Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiwa kwenye picha ya pamoja na Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba mara baada ya kumaliza mazungumzo ofisini kwake, Ikulu Jijini Dar es Salaam leo.

 

2 years ago

Channelten

Wanachama wa CUF mkoani Mtwara wamepanga hili kwenye Mkutano wa Kumchagua Prof.Lipumba

lipumba

Wanachama wa chama cha wananchi CUF mkoani Mtwara wamewataka wajumbe wa mkutano mkuu wa CUF wanaotarajiwa kukutana August 21 mwaka huu kumkubalia aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho Prof. Ibrahimu Lipumba arejee kwenye nafasi yake ili kukiimarisha chama hicho.

Wamesema tangu Prof.Ibrahimu Lipumba atoke kwenye nafasi ya Mwenyekiti, chama hichi kimekuwa kikiyumba ambapo wamesema hakuna wa kusimamia na kukemea mambo mabaya yanayotokea ndani ya chama hicho.

Ni katika ufunguzi wa shina la chama...

 

1 year ago

Michuzi

CUF ya Maalim Seif kuiburuza CUF ya Prof.Lipumba mahakamani

Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii.
BODI ya Wadhamini ya Chama cha Wananchi (CUF ), imefungua kesi ya madai dhidi wanachama wake nane akiwemo Naibu Katibu Mkuu, Magdalena Sakaya
Kesi hiyo imefunguliwa leo katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ikitaka wanachama hao wasijihusishe na harakati  zozote za chama hicho.
Mbali ya Sakaya ambaye pia ni mbunge wa Kaliua mkoani Tabora, wadaiwa wengine ni Thomas Malima, mbunge wa Mtwara Mjini,Mafta Nachumu, Omar Mhina Masoud, Abdul Kambaya, Salama...

 

2 years ago

Global Publishers

CUF Wamkataa Prof. Lipumba

prof+LipumbaAliyekuwa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba. Wakati aliyekuwa Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba akitengua uamuzi wake wa kung’atuka kwenye wadhifa huo na kuomba kurejea, viongozi wa juu wa chama hicho wamepinga hatua hiyo wakisema katiba yao hairuhusu na kwamba anakwenda kukiua chama. Kauli za viongozi hao, zimekuja muda mfupi baada ya Profesa Lipumba kutangaza nia hiyo jana kwenye ofisi za makao makuu ya chama hicho, Buguruni huku akibainisha kuwa amefanya hivyo baada ya...

 

2 years ago

Mtanzania

Prof. Lipumba aivuruga CUF

Ibrahim_LipumbaNA EVANS MAGEGE

MWENENDO wa mambo ndani ya Chama cha Wananchi (CUF) sasa si shwari baada ya aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba, kutangaza nia ya kurejea kwenye wadhifa wake huo.

Tayari ndani ya CUF viongozi, wanachama na mashabiki wa chama hicho wamegawanyika kati ya wale wanaomuunga mkono na wanaompinga katika nia ya kuutaka tena wadhifa wa uenyekiti baada ya kujiuzulu Agosti 5, mwaka jana kwa kile alichoeleza kuwa ni kutoridhishwa na uamuzi wa vyama vya Umoja wa...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani