MZEE MAJUTO KUPELEKWA NCHINI INDIA KWA MATIBABU

Na Cathbert Kajuna - Kajunason/MMG. 
Msanii mkongwe wa filamu za vichekesho nchini, King Majuto anatarajia kupelekwa nchini India kwa matibabu kutokana na tatizo linalomkabili. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, mara baada ya kutoka kumsalimia Mzee Majuto ambaye amelazwa katika hospitali ya Tumaini, Mwenyekiti wa Uzalendo Kwanza Steve Mengele 'Steve Nyerere' amesema kuwa uamuzi huo umekuja baada ya kuona mzee Majuto amekuwa akihangaika mara kwa mara kutafuta...

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

9 months ago

Zanzibar 24

Mzee Majuto kupelekwa India kimatibabu leo

Steve Nyerere ambaye amehusika katika kusaidia kuratibu zoezi la kumuwezesha Mzee Majuto kwenda nchini India kwa matibabu zaidi amesema kuwa leo Mei 1, 2018 Msanii huyo mkongwe nchini Mzee Majuto atapelekwa nchini India kwa ajili ya matibabu zaidi kufuatia matatizo aliyopata siku kadhaa zilizopita huku akiwataja watu ambao wamehusika katika kufanikisha jambo hilo na kusema ni pamoja na Rais Dkt. John Pombe Magufuli na Waziri wa Habari Dkt. Harrison Mwakyembe.

“Niseme ahsante...

 

3 years ago

Mwananchi

Dk Bisimba kupelekwa India kwa matibabu

Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Dk Hellen Kijo-Bisimba anatarajia kusafirishwa kwenda nchini India kwa ajili ya matibabu zaidi.

 

5 years ago

Mwananchi

Kisumo kupelekwa India kwa matibabu

Mwanasiasa mkongwe na kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Peter Kisumo ambaye amelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) akisumbuliwa na maradhi ya moyo na figo, amesema wiki hii atapelekwa nchini India kwa matibabu zaidi.

 

1 year ago

Malunde

LISSU KUPELEKWA NCHINI UBELGIJI KWA MATIBABU ZAIDI


Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema), Tundu Lissu ametoka Hospitali ya Nairobi nchini Kenya leo Jumamosi asubuhi kwenda nchini Ubelgiji kwa matibabu zaidi ya kuurejesha mwili wake katika hali yake ya kawaida.

Lissu ambaye pia ni Rais wa Chama cha Mawakili wa Tanzania (TLS) ataondoka saa 2.30 asubuhi ya leo Jumamosi na Ndege ya Shirika la Kenya akiambatana na mke wake, Alicia.

Lissu ametoka hospitalini hapo ikiwa baada ya matibabu aliyoyapata tangu Septemba 7 mwaka jana baada ya kushambuliwa...

 

9 months ago

Malunde

SERIKALI YABEBA JUKUMU LA MATIBABU YA MZEE MAJUTO

Waziri Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe amemtembelea msanii nguli wa filamu, Amri Athuman maarufu mzee Majuto na kueleza kuwa Serikali inabeba jukumu la matibabu yake.

Mzee Majuto alilazwa Aprili 23 baada ya kuzidiwa ghafla kutokana na kidonda cha operesheni ya henia aliyofanyiwa Julai mwaka jana jijini Tanga.

Akizungumza katika tukio hilo jana Aprili 28, 2018 Dk Mwakyembe amesema Serikali imeamua kumpeleka mzee Majuto nchini India kwa ajili ya matibabu zaidi.

"Kwa...

 

4 years ago

Dewji Blog

NHC yakabiliana na tatizo la moyo nchini kwa kusaidia matibabu ya watoto 53 nchini India

unnamed

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza wakati wa hafla fupi iliyofanyika leo Desemba 26, 2014 kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam ya kuwaaga jumla ya watoto 55 wenye matatizo ya ugonjwa wa Moyo kati ya 104, waliofadhiliwa na Lions Club ya jijini, kwa ajili ya kwenda kutibiwa nchini India. Watoto hao 55 wa awamu ya kwanza walionza kuondoka nchini jana.

Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) limechangia kiasi cha takribani shilingi...

 

9 months ago

Malunde

BONGO MOVIE KUMSAFIRISHA MZEE MAJUTO KWENDA INDIA KUTIBIWA

Wasanii wa Bongo Movie wakiongozwa na Steve Nyerere kwa Pamoja wamekwenda hospitali aliyolazwa muigizaji mkongwe mzee Majuto kwa lengo la kumuona na kumpa faraja katika kipindi hiki ambapo amelazwa katika hospitali hiyo.

Pamoja na kwenda hapo wamemkuta Mzee Majuto yupo kwenye hali nzuri huku akijitokeza mdau ambaye ni Kampuni ya ASAS aliyejitolea Ticket mbili kwaajili ya Mzee Majuto kwenda kutibiwa India.

Baada ya hapo Msanii Steve Nyerere alizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa'" Ni...

 

Share

Trending Now

Zinazosomwa Sasa

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani