Nafasi za kazi Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo

Tume ya Utumishi Serikalini inatangaza nafasi za kazi kwa ajili ya Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo kama ifuatavyo:-

1. Wahudumu Daraja la III “Nafasi 2” – Pemba na “Nafasi 1” – Unguja
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Sekondari na kupata cheti cha uhudumu kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

2. Afisa Michezo Msaidizi Daraja la III “Nafasi 1” – Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Stashahada ya Michezo au Utawala kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

3. Karani Masjala Daraja la III “Nafasi 1” – Pemba
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Stashahada katika fani ya Utunzaji Kumbukumbu ‘Record Management’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

4. Dereva Daraja la III “Nafasi 2” – Unguja
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Sekondari.
• Awe amepata mafunzo ya udereva kutoka katika Chuo cha mafunzo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

5. Walinzi Daraja la III “Nafasi 3” – Unguja
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Sekondari.
• Awe amepata mafunzo ya Ulinzi kutoka katika Chuo cha mafunzo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

6. Msimamizi wa Magofu Daraja la III “Nafasi 1” – Unguja
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu cheti katika fani ya ‘Teknolojia ya Habari na Mawasiliano na Uhasibu’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

7. Afisa Habari na Mawasiliano Msaidizi Daraja la III “Nafasi 3” – Unguja
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu Stashahada ya Kawaida katika fani ya ‘Habari na Mawasiliano’ kutoka katika Chuo kinachotambuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.

8. Customer Care Daraja la III “Nafasi 1” – Unguja
Sifa za Waombaji:
• Awe ni Mzanzibari.
• Awe amehitimu elimu ya Sekondari

Jinsi ya Kuomba:
• Barua za maombi ziandikwe kwa Mkono na zitumwe kwa anuani ifuatayo:-
KATIBU,
TUME YA UTUMISHI SERIKALINI,
S. L. P 1587 – ZANZIBAR.

• Muombaji anaombwa kuwasilisha ombi lake moja kwa moja katika Ofisi ya Tume ya Utumishi Serikalini iliyopo Jumba la Wananchi Forodhani Zanzibar wakati wa saa za kazi. Kwa waombaji walioko Pemba wanaombwa kuwasilisha maombi yao Ofisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Chake Chake Pemba.

Barua za Maombi ziambatanishwe na mambo yafuatayo:-
a) Kivuli cha Cheti cha kumalizia masomo
b) Kivuli cha Cheti cha mtihani wa Taifa (Elimu ya Sekondari)
c) Kivuli cha Cheti cha Kuzaliwa.
d) Kivuli cha Kitambulisho cha Mzanzibari.
e) Picha moja (1) ya Passport Size iliyopigwa karibuni.
f) Tarehe ya mwisho ya kupokea maombi ni tarehe 23 Mei, 2017 wakati wa saa za kazi.

The post Nafasi za kazi Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo appeared first on Zanzibar24.

Zanzibar 24

Read more


Habari Zinazoendana

6 months ago

Michuzi

DK.SHEIN AZUNGUMZA NA UONGOZI WA WIZARA YA HABARI,UTALII,UTAMADUNI NA MICHEZO

 Waziri wa Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo Mhe.Rashid Ali Juma  (katikati) alipokuwa akisoma taarifa yake katika   kikao cha siku moja cha  Utekelezaji wa Mpango kazi kwa kipindi cha robo ya kwanza Julai- Septemba 2017 cha  Uongozi wa Wizara  hiyo kilichofanyika leo katika ukumbi wa  Ikulu Mjini Unguja,chini ya Mwenyekiti wake Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein Baadhi ya Viongozi wa Idara mbali mbali zilizo chini ya Wizara...

 

9 months ago

Zanzibar 24

Orodha ya majina ya watu walioitwa wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na michezo

Tume ya Utumishi Serikalini inawatangazia vijana ambao wameomba nafasi ya kazi katika Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo kufika katika Ukumbi wa Idara ya Habari Maelezo (Rahaleo Zanzibar) saa 2:00 za asubuhi kwa ajili ya kufanyiwa usaili siku ya Ijumaa ya tarehe 14 Julai, 2017.

Wasailiwa wote wanaombwa wachukue vyeti vyao halisi vya kumalizia masomo, Cheti cha kuzaliwa pamoja na kitambulisho cha Mzanzibari Mkaazi.

WASAILIWA WENYEWE NI:

MSIMAMIZI WA MAGOFU DARAJA LA III
NO JINA...

 

2 years ago

Michuzi

KATIBU MKUU WIZARA YA HABARI UTALII UTAMADUNI NA MICHEZO ZANZIBAR AKABIDHIWA OFISI RASMI

 Katibu Mkuu Wizara ya Habari  Utalii Utamaduni na Michezo Omar Hassan Omar kushoto akikabithiwa nyaraka  na Katibu Mkuu Mstaafu Ali Mwinyikai katika makabidhiano ya Ofisi yaliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Habari Utalii Utamaduni na Michezo  Kikwajuni Mjini Unguja.Katibu Mkuu Wizara ya Habari  Utalii Utamaduni na Michezo Omar Hassan Omar kushoto na Katibu Mkuu Mstaafu Ali Mwinyikai wakitiliana saini katika makabidhiano ya Ofisi yaliofanyika katika ukumbi wa Wizara ya Habari...

 

11 months ago

Zanzibar 24

SMZ ina lengo la kufikia ajira laki 5 kupitia Wizara ya Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo ifikapo 2020

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania imejenga uwezo zaidi wa kukabiliana na vitendo vya  rushwa katika azma yake ya kujenga uchumi imara utakaostawisha Taifa kwa kuongeza Mapato kupitia Sekta ya Utalii sambamba na Ujenzi wa Viwanda vipya vya kudumu.
Kauli hiyo imetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi anayemuwakilisha Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli kwenye Jukwaa la Dunia la Uchumi { world Economy Forum } wakati akiwasilisha Muelekeo wa...

 

2 years ago

Dewji Blog

Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kuendelea kushirikiana na wadau katika kuendeleza Utamaduni

pinda

Waziri Mkuu mstaafu Mizengo Pinda (kushoto) akifungua kituo cha utamaduni wa China nchini Tanzania mapema hii leo jijini Dar es Salaam, katikati ni Katibu Mkuu Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Elisante Ole Gabriel na kulia ni Mkurugenzi wa Utamaduni toka Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Prof. Hermas Mwansoko.

pinda 2

Baadhi ya wanafunzi wa Kitanzania wanaojifunza lugha ya Kichina katika kituo cha Utamaduni wa China nchini Tanzania wakiimba nyimbo kwa lugha ya...

 

2 years ago

Dewji Blog

Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kuendelea kushirikiana na wajasiriamali wa kazi za Sanaa

9685-mkurugenzi

Kaimu Mkurugenzi Sanaa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi.Leah Kihimbi akiongea na wajasiriamali wa kazi za Sanaa wa Mikono Cultural Heritage Ltd walipomtembelea ofisini kwake jana jijini Dar es Salaam.Bi Leah aliwahaidi wasanii hao kufanya nao kazi kwa karibu na kuwapa ushirikiano mkubwa katika kazi zao.

9654-henry na eliawana utamaduni

Mwenyekiti wa kikundi cha wajasiriamali wa kazi za Sanaa Bw.Henry  Clemens akiishukuru serikali kwa kuonyesha nia ya kuwasaidia kwa kuanzisha Idara ya Sanaa na ivyo...

 

2 years ago

Michuzi

Wizara ya Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo kuendelea kushirikiana na wajasiriamali wa kazi za Sanaa

Mwenyekiti wa kikundi cha wajasiriamali wa kazi za Sanaa Bw.Henry Clemens akiishukuru serikali kwa kuonyesha nia ya kuwasaidia kwa kuanzisha Idara ya Sanaa na ivyo wataitumia kuimarisha kazi zao ili ziwanufaishe.Pembeni yake ni makamu mwenyekiti wa Kikundi icho Bw.Chief Eliewaha Shogholo Challi.Mwenyekiti wa kikundi cha wajasiriamali wa kazi za Sanaa Bw.Henry Clemens (kushoto) akimweleza jambo Kaimu Mkurugenzi wa Sanaa kutoka Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Bi Leah Kihimbi...

 

4 years ago

Michuzi

Timu ya Michezo ya Wizara ya Habari ,Vijana,Utamaduni na Michezo ya haswa kuwa mfano katika mashindano ya SHIMIWI

Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Bibi. Sihaba Nkinga akimkabidhi zawadi Mwanamichezo aliyeiletea Wizara ushindi katika mashindano ya SHIMIWI na Meimosi mwaka jana Bibi. Niuka Chande. Mchezaji huyo aliibuka mshindi katika michezo ya Draft na kurusha Tufe na kuiletea Wizara vikombe viwili. Kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Profesa Elisante Ole Gabriel na Mwenyekiti wa Timu ya Wizara Dkt. Margareth Mtaki.Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni...

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani