Nandy alivyouvaa uhusika katika Subalkheri Mpenzi

Ni jambo la kawaida kwa wasanii wa kike hapa kujipamba wakati wa kutengeneza video zao kwa mapambo ya kila aina ikiwamo vipodozi.

Hali hiyo inafanya wengine hata kusahaulika sura zao halisi, hasa pale wanapozidisha mapambo hiyo ikiwemo kubadili nywele zao kwa kuvaa za bandia.

Lakini kwa Nandy ambaye jina lake halisi Faustina Charles naona hali hiyo kaibadili katika video ya wimbo wake wa Kivuruge unaotesa kwa sasa.

Mbali na Kivuruge pia katika video ya wimbo wa Subalkheri, alioshirikishwa na Dogo Aslay nao ameonekana kuendelea na mwendo huo huo ambao hadi kufika mwanzoni mwa wiki hii ulikuwa na jumla ya watazamaji zaidi ya milioni.

Msanii huyo anayejiita African Princess, ukiangalia nyimbo hizo mbili zinaakisi jina lake kutokana na namna alivyojiweka Kiafrika zaidi.

Nandy aliyeanza kutambulika na kibao cha Nagusagusa, baadaye One Day, Wasikudanganye, kote humu hajaweza kutendea haki uhalisia wa maisha ya mwanamke wa kiafrika kama ilivyo kwa nyimbo hizo mbili.

Wimbo wake wa Kivuruge ulioonesha maisha halisi ya mwanamke wa Kiafrika na wa Kibongo kwa ujumla kuanzia nyumba anayoishi na mavazi yake.

Kwa wale wanaoishi Uswahilini, vazi la dera ndio mparo mkubwa sio kwa kushindia nyumbani tu, bali hata kutokea kitu ambacho Nandy kakionesha katika video hiyo.

Pia magauni ya mpira maarufu ‘Dar Combined’ yaani ukikatiza kona ya nyumba yako unaweza kuwakuta watu wengine sita wamevaa kama wewe na ukajiona ndio unakwenda na wakati.

Kingine kilichonesha Uafrika Princess ni Nandy kutopaka vipodozi vya aina yoyote katika video hiyo, kwani tumezoea kumuona akiwa na kucha ndefu za kubandika zikiwa zimekolezwa na rangi juu yake lakini kwa kivuruge hakuna hiki kitu.

Pia, suala la mwanamke kuchota maji kazi ambazo mwanamke wa Kiafrika ndizo hasa huzifanya achilia mbali wale waliovutiwa mabomba nyumbani kwao.

Jingine ni ile ya kubeba mfuko maarufu kwa jina la ‘Shangazi Kaja’ pale alipochosha na vituko vya mme wake vya kuwa na vimada. Mifuko hiyo ndio wengi huko Uswahilini wanaotumia kama mabegi yao ya kuhifadhia nguo.

Pia nyumba anayoishi Nandy, ndio familia nyingi za kibongo zenye maisha ya kawaida zinaishi, nyumba ambazo hata gari la wagonjwa au gari la zimamoto kupita ni kazi.

Ndani ya nyumba hiyo ya Nandy na mumewe kwenye korido kunaonekana kuwa na ndoo kibao za kuhifadhia maji, kwa wale waliopanga Uswahilini wanaelewa hii mambo, sasa ole wako ufumwe unachota maji ya mwenzako.

Mtaa ambao Nandy anaonekana kuishi, watu wapo busy na biashara zao za kuuza vitafunwa mbalimbali, mambo ambayo ni adimu kuyaona Uzunguni.

Tukija kwenye wimbo wa Subalkheri, Nandy kaendelea na utaratibu huo, amevaa nguo ambazo msichana wa Kitanzania anakuwa katika maisha ya kawaida hasa vijijini.

Katika video hiyo Nandy anaoneka akiwa amesuka mabutu yake mawili, hajapaka vipodozi usoni na hata maeneo ambayo yupo na mpenzi wake ni ya asili ambayo yanapatikana nchini kwetu hususani maeneo ya Pwani.

Kuna mahali anaonekana akiwa anagema nazi, zao linalopatikana maeneo ya Pwani, pia nyumba waliopo ya udongo inaakisi maisha ya Mwafrika na kuna wakati wanaonekana wakishiriki katika ngoma zinazochezwa huko Uswahilini kwetu na sio kwenye klabu kama ambavyo wanafanya wanamuziki wengine kwenye video zao.

Nandy afunguka ilivyokuwa ngumu kukubali

Akizungumza na mwananchi kuhusu hilo, Nandy anakiri kwamba awali ilikuwa ngumu kukubali kupigwa picha akiwa katika hali ile na kuongeza kwamba anashukuru wimbo huo umeweza kufanya vizuri kwani mpaka sasa umepata watazamaji zaidi ya milioni 1.9 kwenye mtandao wa Youtube.

Anasema ugumu zaidi ulikuja ukizingatia kwamba katika video zake nyingine amejipamba, lakini anashukuru kupitia kivuruge watu wameweza kumjua Nandy halisi ndio nani.

Kuhusu gharama anasema ilikuwa ni rahisi ukilinganisha na video alizozifanya huko nyuma kwani haifiki hata milioni mbili, kwa kati nyingine hadi tano zinafika.

Kwa upande wa mazingira aliyochukulia picha ambayo ni maeneo ya Mwananyamala, anasema anashukuru wananchi walimuheshimu na kuendelea na shughuli zao hali iliyoongeza uhalisia zaidi.

Mwanaspoti

Bongo Movies

Read more


Habari Zinazoendana

2 months ago

Zanzibar 24

Video ya nyimbo mpya Aslay na Nandy ‘Subalkheri Mpenzi’

Baada ya Nandy na Aslay kufanya vizuri na kolabo yao ya wimbo’Mahabuba’, hatimaye wawili hao wameachia video ya kolabo yao mpya ya wimbo, Subalkheri Mpenzi. Video ya wimbo huo imeandaliwa na director, Hanscana.

The post Video ya nyimbo mpya Aslay na Nandy ‘Subalkheri Mpenzi’ appeared first on Zanzibar24.

 

4 years ago

GPL

UHUSIKA WA WAZAZI HUSABABISHA MTOTO AWE GUMEGUME AU GUBEGUBE KATIKA MAPENZI -4

KWANZA tuwe tumeshakubaliana na ukweli kwamba mzazi ni kichocheo cha mtoto kuwa mhusika bora katika mapenzi, baada ya hapo tutakuwa na mawazo yanayoshabihiana kwamba gubegube au gumegume mara nyingi ni matokeo ya malezi mabaya. Tuendelee kutoka hapohapo, sasa ni muongozo kwako kuwa haina maana kuwa unaweza kusamehewa na kuachwa kama ulivyo eti kisa ndivyo ulivyolelewa. Nani atakukubali kama wewe ni mzigo usiobebeka? Tafakari...

 

4 years ago

GPL

UHUSIKA WA WAZAZI HUSABABISHA MTOTO AWE GUMEGUME AU GUBEGUBE KATIKA MAPENZI -5

KUTOKA mwanzo wa makala haya mpaka hapa tulipofikia, sina shaka utakuwa umeshatambua namna ambavyo uhusika wa wazazi unavyoweza kuwafanya watoto wao kuwa ama magubegube au magumegume katika mapenzi. Kutoka hapo, sasa tuhitimishe mambo machache kwa kupeana maelekezo ya kimsingi ambayo yanaweza kukusaidia katika maisha yako ya kimapenzi hata kama ulipata muongozo wa ovyo kutoka kwa wazazi wako. Haishindikani wewe kuwa bora hata...

 

1 year ago

Dewji Blog

PICHA: Ditto na Nandy walivyo’perform’ katika Tulia Marathon

Wanamuziki wawili wa muziki wa kizazi kipya (Bongo fleva) ambao pia ni mabalozi wa taasisi ya Tulia Trust, Ditto pamoja na Nandy ni baadhi ya watu ambao walipata nafasi ya kushiriki mashindano ya kukimbia ya Tulia (Tulia Marathon) yaliyofanyika jumamosi ya Machi, 11 katika uwanja wa Sokoine, Mbeya.

Baada ya mashindano kukamilika wasanii hao walitoa burudani kwa washiriki wa Tulia Marathon na hapa tumekuwekea baadhi ya picha wakati mastaa hao wakitoa burudani.

 

2 years ago

Bongo Movies

Mimi si Jambazi ni Uhusika Tu- Nkwabi

Nkwabi Juma mwigizaji nyota wa filamu ya C.P.U amefunguka kwa kusema kuwa yeye si Jambazi bali ni uhusika tu ambao umfanya acheze kama mtu mtata na jambazi liliokubuhu kutokana tu na watayarishaji kumchagua katika nafasi kama hizo lakini hajui hata kuiba kuku na amekuwa akimudu nafasi hizo kwa kufanya utafiti tu.

“Msanii mnzuri ni lazima huwe mbunifu na kuchagua character yako ambayo kila mtengeneza sinema akiandika muswada (script ) anakuona wewe ndio utakayoitendea haki na si mtu mwingine...

 

2 years ago

Bongo5

Video: Nicole azungumzia uhusika mkuu kwenye filamu ya Red Flag aliyofanya na Rammy Galis na Wanaijeria

Nicole Franklyn Sarakikya na Rammy Galis wameigiza kama mtu na girlfriend wake kwenye filamu iitwayo Red Flag iliyohusisha wasanii wa Nigeria pia.

12976203_1763105490588499_714244318_n

“Red Flag ni movie ambayo ina comedy kidogo na it’s a romantic comedy movie,” Nicole ameiambia Bongo5.

“Mimi nimecheza kama Vanessa, Vanessa kwenye movie ni main character. Rammy alikuwa Fred ambaye ndio alikuwa boyfriend wangu kimovie, alikuja Tanzania kutafuta girlfriend tukakutana. Kule Nigeria alienda kunitambulisha kwao,” ameongeza.

12479085_1718899638389618_123418846_n

“Ni...

 

2 years ago

Global Publishers

Diamond Platinumz ajiachia katika pozi tata na mpenzi wake

12661917_1060434517311695_7748402750095642070_n12670563_1060434543978359_5401264037533937997_n

Nasibu Abdul ‘Diamond Platinumz’ na Mpenzi wake, Zarinah Hassan ‘Mama Tiffah’ wakiwa katika pozi tata.

 

3 years ago

GPL

MPENZI WA ZAMANI WA MPENZI WAKO ANAPOKUWA KIRUSI HATARI!

Niwazi kila mmoja wetu ana historia katika maisha yake ya kimapenzi. Huenda mpaka sasa wewe msomaji ulishawahi kuwa na uhusiano na watu zaidi ya mmoja. Wala siyo ajabu! Yawezekana pia kati ya wale uliowahi kuwa nao wapo uliomwagana nao kwa shari lakini wapo pia ulioachana nao kiroho safi. Jambo ambalo leo nataka kulizungumzia ni hili la mtu kuendelea kuwa na mawasiliano na mpenzi wake wa zamani eti kwa sababu waliachana kwa...

 

3 years ago

Bongo5

New Video: Nandy Najiamini

Video mpya kutoka kwa mwanadada Nandy wimbo unaitwa “Najiamini” video imetaalishwa na kampuni ya Kokwa Production

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani