OBAMA AMWAGA CHOZI WAKATI AKIWAAGA WAMAREKANI

 Rais wa Marekani, Barack Obama amewaaga Wamarekani na ulimwengu mzima kwa ujumla ikiwa ni mara ya mwisho akiwa kama rais, katika hotuba iliyojaa hisia kubwa aliyoitoa mjini Chicago na kuwataka Wamarekani kuunganisha nguvu katika kuleta mabadiliko. Rais huyo ametokwa na machozi wakati akimshukuru mke wake Michelle Obama kwa namna alivyotoa mchango mkubwa katika utawala wake.
Akihitimisha utawala wake katika Ikulu ya Marekani, Obama amerejea katika mji ambao sasa ni nyumbani kwake wa Chicago ambako kampeni yake ya "ndio tunaweza" ilianzia hapo na leo akisema "ndio tumeweza".
Akiorodhesha mafanikio ya utawala wake kuanzia mkataba wa nyukilia na Iran hadi huduma ya bima ya afya, sehemu kubwa ya hotuba yake iliegemea katika kuwatia moyo wafuasi wake waloshtushwa na ushindi wa Donald Trump pamoja na kutathmini mafanikio aliyoyapata katika uongozi wake na mtazamo wake kuhusu wapi Marekani inaelekea .Obama amewataka Wamarekani kuamka, kupigania demokrasia lakini akaonya kuwa ubaguzi wa rangi na kukosekana kwa usawa bado ni kitisho kwa demokrasia. "Sisi sote bila ya kujali vyama, ni lazima turudi katika ujenzi wa taasisi ya demokrasia", amesema Obama.
"Hivyo sisi kama wananchi, lazima tuwe macho dhidi ya uchokozi wa nje, ni lazima tuilinde misingi yetu inayodhoofika inayotutambulisha sisi ni akina nani. Ndio maana katika kipindi cha miaka nane iliyopita nimefanya kazi ya kuweka mapambano dhidi ya ugaidi katika misingi ya kisheria.Ndio maana tumemaliza mateso, kufanya kazi kulifunga gereza la Guantanamo, na mageuzi ya sheria zetu zinazosimamia ufuatiliaji wa kulinda faragha na uhuru wa raia. Na ndio maana mimi nimekataa ubaguzi dhidi ya Waislamu Wamarekani", amenukuliwa rais huyo.
Miongoni mwa mafanikio mengine anayojisifia Obama ni pamoja na kuimarishwa kwa uchumi, kuhalilisha ndoa za jinisia moja, kufunguliwa kwa mahusiano ya kidiplomasia na Cuba na maenedeleo mengine.
Mke wake Michele Obama na makamu wa rais Joe Biden na mke wake Jill ambao rais amewaelezea kama "familia" wamehudhuria hafla hiyo.
Obama akifuta machozi machoni mwake amemshukuru mke wake Michelle akimuita ni rafiki yake mkubwa, mtoto wake Malia aliyekuwa akibubujikwa na machozi pamoja na Sasha ambaye hakuwepo. Akielezea mchango wa mke wake, Obama anasema,  "Michelle Lavaughn Robinson, msichana kutoka upande wa kusini, kwa miaka zaidi ya 20 iliyopita, umekuwa sio tu mke wangu na mama wa watoto wangu lakini rafiki yangu mkubwa.
Ulichukua jukumu ambalo hukuuliza na ukalifanya kuwa lako kwa neema , ujasiri, mipango na ucheshi mzuri. Uliifanya Ikulu kuwa sehemu ya kila mtu."
Anasema Marekani imekua bora na yenye nguvu duniani tangu alipokula kiapo kuiongoza nchi hiyo miaka nane iliyopita. Donald Trump atakayeapishwa Januari 20 anatarajiwa kuondoa baadhi ya yaliyofikiwa na karibu kiasi ya watu elfu 18 waliohudhuria hafla hiyo mjini Chicago walimshangilia rais huyo wakisema "miaka minne zaidi" na Obama akasema hawezi kufanya hivyo.
Obama katika hotuba yake ya mwisho ameepuka kumkosoa Trump moja kwa moja na kulaani mgawanyiko ambao umezikumba siasa za taifa hilo.Imeandikwa na Mtandao wa DW

Michuzi

Read more


Habari Zinazoendana

3 years ago

Vijimambo

BENJA MWAIPAJA AMWAGA CHOZI WAKATI WA MUMUAGA BALOZI LIBERATA MULAMULA


Benja Mwaipaja akionyesha kutokwa na chozi wakati Balozi Liberata Mulamula alipowaaga Watanzania nyumbani kwake Bethesda, Maryland siku ya Jumamosi Julai 25, 2015.

 

3 years ago

Vijimambo

Alichoongea JK wakati akiwaaga mabalozi wa Tanzania

Rais Jakaya Kikwete akiwahutubia mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi za nje wakati wa ufunguzi rasmi wa mkutano wa siku tatu ulioanza, Dar es Salaam juzi. Picha na Anthony Siame.
Dar es Salaam. Rais Jakaya Kikwete amewaaga rasmi mabalozi 36 wa Tanzania katika mataifa mbalimbali akiwaeleza kuwa hatakuwa madarakani baada ya Oktoba.Rais aliwaaga mabalozi hao jana wakati akifungua mkutano wa siku tatu utakaohitimishwa leo, ambao pamoja na mambo mengine, utajadili ‘Diplomasia ya Tanzania...

 

3 years ago

Dewji Blog

Vilio na majonzi Singida wakati MO akiwaaga wananchi wake!

IMG_7558

Mbunge wa Singida mjini, Mh. Mohammed Dewji akiwapungia wapiga kura wake kama ishara ya kuwaaga rasmi baada ya kutangaza kutogombea tena ubunge wa jimboni humo wakati wa mkutano mkubwa wa kuwasilisha taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM kwa miaka 10 ya kuwatumikia wananchi wa Singida.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).

Na Modewjiblog team, Singida

MBUNGE  wa Singida mjini na mfanyabiashara maarufu nchini, Mohammed Dewji  amesema hatagombea ubunge wa jimbo hilo tena baada ya...

 

2 years ago

Global Publishers

Penina amwaga chozi

Jennifer Raymond ‘Penina’ Jennifer Raymond ‘Penina’

Mwandishi wetu, Amani

MSANII wa Bongo Muvi anayefanya poa, Jennifer Raymond ‘Penina’ hivi karibuni alijikuta akitokwa na machozi baada ya kudaiwa kujiingiza katika biashara ya kujiuza nchini China.

Kwa mujibu wa chanzo cha kuaminika, Penina amekuwa na safari za China na Thailand na kwamba mambo yake kwa sasa ni supa.

penina“Yaani safari kwake haziishi, kama siyo China basi Thailand na inasemekana kuwa huko huwa anakwenda kujiuza na kupata fedha,” kilisema chanzo.

Baada...

 

1 year ago

Mwananchi

Roma amwaga chozi

Msanii wa Muziki wa kizazi kipya, Roma Mkatoliki amezungumza kwa hisia juu ya wasanii wenzake na watu wengine ambao wanahusisha kutekwa kwao na mchezo wa kiini macho.

 

3 years ago

GPL

Okwi amwaga chozi akisimulia

Kiungo mshambuliaji nyota wa Simba, Emmanuel Arnold Okwi. Musa Mateja na Martha Mboma
KIUNGO mshambuliaji nyota wa Simba, Emmanuel Arnold Okwi, ameshindwa kujizuia kumwaga machozi wakati akielezea tukio lake la kupigwa kiwiko ‘pepsi’ na beki Aggrey Morris kuwa ni la kikatili na lingeweza kumsababishia hata ulemavu kwa kuwa baada ya kuanguka alimmalizia kwa kumkita teke. Okwi, raia wa Uganda, ameliambia Championi Jumatano...

 

3 years ago

Bongo Movies

Dotnata Amwaga Chozi Lokesheni

Mwigizaji  mkongwe wa filamu za kibongo, Illuminata Posh maarufu kama Dotnata, amesema alitoa machozi wakati akirekodi sinema inayohusu unyanyasaji wanaofanyiwa watoto wadogo, hasa alipobaini ukweli kuwa wanakosa mtetezi hata wa kuweza kuhisi mateso wanayokutana nayo.

“Watoto wanapata mateso sana kutoka kwa jamii inayowazunguka, wakipoteza wazazi au familia ikifarakana, wanaoumia zaidi ni wao kwani huingia mitaani na kuwa ombaomba, wanajiingiza kwenye wizi, ukahaba na ushoga. Wanafanya haya...

 

11 months ago

Mwanaspoti

Bondia amwaga chozi ulingoni

MSONDO Ngoma waliwahi kuimba wimbo wa ‘Kilio cha Mtu Mzima’ kwa kudai ukiona mtu mzima analia, ujue kuna jambo.Hivi ndivyo ilivyokuwa  kwa bondia Abdallah Mohamed wa Magereza aliyewaacha hoi mashabiki wa ngumi alipoamua kuangua kilio ulingoni akidai apewe pointi na majaji.

 

2 years ago

Habarileo

Amwaga chozi akililia bajeti ya afya

MWAKILISHI wa Jimbo la Paje, Jaku Hashim Ayoub jana aliangua kilio ndani ya Baraza la Wawakilishi akilalamika bajeti ndogo iliyotengwa na serikali katika sekta ya afya.

 

Share

Trending Now

Stay updated, Sign up

Habari za Mikoani